Hili suala la sehemu za kujikwatua na kutanashitika zina athari siyo tu kwa ndoa bali hata kiafya.
Kuhusu athari katika ndoa, binafsi nadhani kila mahali kuna athari kama tutaangalia kwa undani.Ni mtu binafsi kujihadhari na mitego.Mara nyingi mchezo mchezo mtu hujikuta kwenye hatari.Kuanzia majumbani kuna wale wadada wasaidizi tumesikia nao huhatarisha ndoa, ukienda maofisini nako usiseme, kwenye sehemu za starehe nako si haba. Hata mitandaoni nako hivyo hivyo .Kwa hiyo hakuna palipo salama.Usalama utapatikana ahera peke yake.
Tukija kwenye suala la usafi, kwanza kitu ambacho nimekiona kwenye hizo barber shops - hao wanaofanya " facial scrub" hawana hata moja walijualo kwenye ufanyaji facial scrub.Ukitaka "facial" yauhakika nenda kwenye saloon zenye specialisation hii na huwa ni ghali siyo bei chee kam humo kwenye barber shops maana hii ni taaluma inayokaribiana na tiba kama siyo tiba.Inatakiwa isomewe ili mtu ajue hasa anafanya nini na kuzingatia taratibu za afya ya ngozi na mambo mengine kama mzio nk.kitu cha kusikitisha sana utaona hata mataulo wanayotumia wanayarudia na hata kufua hayafuliwi. Ukizingatia kuwa wanaume hunyolewa ndevu na wengine wana mapele na huenda mikwaruzo, mtu haoni anajihatarishia afya yake.Yuko radhi aka enjoy hizo huduma za kushikwa masikioni nk.
Kingine ni handling ya products za scrub.Kitaalamu au kiafya, haipaswi kuingiza vidole kuchota ile scrub bali inatakiwa ichotwe ama na spatula au kijiko maana ni kama uji fulani ambao huweza kuzalisha bacteria.Sasa mtu anapoingiza vidole tena ambavyo siyo sterile humo, bacteria wanajizalisha kwa wingi na matokeo yake huweza kuambukiza magonjwa. Yako mengi sana kwenye hii ishu lakini kwa leo naishia hapo.
Tip:
Ushauri kwa wale wasiokuwa na agenda tofauti zaidi ya kutaka usafi wa ngozi ya uso, nenda supermarket au duka la vipodozi, nunua products za ku scrub na ziko za kila aina - bei huanzia 3500/- hadi 30,000/= kutegemeana na unataka nini. Unapooga au kunawa uso, tumia . Au mwambie mkeo/ mpenzi wako akutengenezee home-made - changanya unga wa ulezi au hata oats na maziwa , sugua uso wako na kisha osha kwa maji ya uvuguvugu.Waweza pia kutumia limao au ndimu kutakatisha uso wako.