Barcelona na Real Madrid ni Timu za wanachama kunachosumbua Simba na Yanga ni umasikini na ukosefu wa mipango thabiti

Barcelona na Real Madrid ni Timu za wanachama kunachosumbua Simba na Yanga ni umasikini na ukosefu wa mipango thabiti

Nehemia Kilave

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2022
Posts
1,414
Reaction score
3,118
Simba na Yanga ni timu kubwa zisizo na vyanzo vya mapato vinavyoeleweka hii ni kutokana na ukosefu wa mipango ya kueleweka , lakini pia kuwa na viongozi wabovu .

Ingawa na siasa inachangia pia , mikataba inatekelezwa kimaneno hakuna vitendo .

Hatumuelewi Mzee Magoma sababu ya umasikini wa Timu hizi mbili unajiuliza akiondoka Mo tutatoa hela wapi au akiondoka GSM timu itaendaje .

Timu hazina viwanja , hazina katiba za kueleweka, mauzo ya jezi /vifaa ndio tumeanza kufuatilia

Kuna haja ya wanachama kuwa wakali kwa viongozi timu ziwe na malengo ,mfadhili akitokea cha kwanza ajenge Uwanja na mambo mengine ya kimaendeleo.

Wakina Mo na GSM wanapata faida kubwa ya kimatangazo na urahisi wa kutanua biashara zao kupitia hizi timu ni lazima wawekeze vitu ambavyo wakiondoka vitabaki kwenye timu .
Bila hivi migogoro kwenye hizi club haitaisha ,mbona Barca na Madrid wanaweza ? Huku nao ni timu za wanachama .
 
Acheni uongo,
Wanachama wa bongo hawajui wajibu wao,
Wanachama wa bongo hawanunui jersey og,
Hawaendi uwanjani,
Hawalipii App
Hawalipii kadi za uanachama,

Ndio hawa hawa unalinganisha na wa madrid ? Au Barca ? Ambao kila match ni sold out ? Ambako jersey zinauzwa mpaka zinaagizwa tena kiwandani?

Shida sio mfumo, shida wabongo hatuko responsible
 
Sio kweli kuna wanachama wengi wako serious sana na timu lakini pia Timu hazijafanya juhudi kubwa kuwatafuta
 
Sio kweli kuna wanachama wengi wako serious sana na timu lakini pia Timu hazijafanya juhudi kubwa kuwatafuta
Yan mtu upo serious na team yako ila hujalipia app au hununui jersey og ?
Userious wako uko wapi?

wanachama wa hizi team miaka nenda miaka rudi wamekuwa wakikwepa kuchangia maendeleo,

Nambie na suala la mahudhurio hafifu viwanjani?

Yanga Vs Al ahly walishindwa jaza mkapa, unasema napo club haikuwatafuta wanachama ?

Usikae ukawadhamin wanachama wa hizi team, ni watu wapenda kelele ila sio majukumu,

Walikuwa na hizo team miaka zaidi ya 80 wamefanya nn?
 
Acheni uongo,
Wanachama wa bongo hawajui wajibu wao,
Wanachama wa bongo hawanunui jersey og,
Hawaendi uwanjani,
Hawalipii App
Hawalipii kadi za uanachama,

Ndio hawa hawa unalinganisha na wa madrid ? Au Barca ? Ambao kila match ni sold out ? Ambako jersey zinauzwa mpaka zinaagizwa tena kiwandani?

Shida sio mfumo, shida wabongo hatuko responsible
Ishu hapo ni purchasing power kibongobongo ni ndogo sana.washabiki wengi wa hizi timu ni maskini wa kutupwa tofauti na wenzetu wa ulaya ambao kwa hela sio inshu sana
 
Ishu hapo ni purchasing power kibongobongo ni ndogo sana.washabiki wengi wa hizi timu ni maskini wa kutupwa tofauti na wenzetu wa ulaya ambao kwa hela sio inshu sana
Sio umaskin wa kutupwa mkuu,,

Ndio washindwe lipa buku 2 ya app kwa mwezi?
Ndio washindwe kwenda hata game tatu kwa msimu za kiingilio cha 3K ?
 
Sio umaskin wa kutupwa mkuu,,

Ndio washindwe lipa buku 2 ya app kwa mwezi?
Ndio washindwe kwenda hata game tatu kwa msimu za kiingilio cha 3K ?
Hivi unaujua imaskini wa kutupwa mkuu...
Habari za timu yake tu hana sehemu ya kizipata zaidi kwenda kijiweni asubiri mdosi mmoja anujua gazeti kijiwe kizima kisome waanze kubishana..

Mzee ni mashabiki wachache wenye ubavu wa kununua jezi og za timu, kwenda uwanjani mara kwa mara, kulipia kadi au app(smartphones zenyewe wengi hawana)
 
Sio umaskin wa kutupwa mkuu,,

Ndio washindwe lipa buku 2 ya app kwa mwezi?
Ndio washindwe kwenda hata game tatu kwa msimu za kiingilio cha 3K ?
Mkuu unaonekana haujatembea, au ni mgeni na maisha ya dhiki. Kuna watu milo miwili akila ni bahati nasibu. Kuna watu vocha tu kuweka kwenye simu ni baada ya mwezi kutokana na hali duni za kimaisha. Halafu kwenye hawa mashabiki wamegawanyika katika makundi matatu kuna mashabiki wanachama ambao hawa wapo tayari kulipa ada, kununua jezi, na kuingia viwanjani. Ila wapo mashabiki ambao sio wanachama ila jezi wananunua na viwanjani wanaingia na kundi la tatu ni mashabiki ambao wao hawajachizika kivile, wao ni kuangalia mechi kupitia TV tu hajawahi kukanyaga uwanjani hata mechi moja. Tusiseme tu kuwa hizi timu zina mashabiki wengi bali angalieni na aina ya hao mashabiki wenyewe.
 
Hivi unaujua imaskini wa kutupwa mkuu...
Habari za timu yake tu hana sehemu ya kizipata zaidi kwenda kijiweni asubiri mdosi mmoja anujua gazeti kijiwe kizima kisome waanze kubishana..

Mzee ni mashabiki wachache wenye ubavu wa kununua jezi og za timu, kwenda uwanjani mara kwa mara, kulipia kadi au app(smartphones zenyewe wengi hawana)
Mkuu, mm nakubali wapo,
Ila hata hao wachache hawapo
App ya mange ina subscribers na downloads nying kuliko app ya simba na yanga kwa umoja wao,
Yan jumlisha subscribers wa Yanga app na Simba App bado hutafikia wa Mange, hata nusu,

Kwa hio utaona suala la hela sio kweli, ni vipaumbele tu, na kutopenda kuwajibika,
 
Acheni uongo,
Wanachama wa bongo hawajui wajibu wao,
Wanachama wa bongo hawanunui jersey og,
Hawaendi uwanjani,
Hawalipii App
Hawalipii kadi za uanachama,

Ndio hawa hawa unalinganisha na wa madrid ? Au Barca ? Ambao kila match ni sold out ? Ambako jersey zinauzwa mpaka zinaagizwa tena kiwandani?

Shida sio mfumo, shida wabongo hatuko responsible
Jamaa anafikiri na huko Real madrid kuna akina magoma na mzee mangungo ambao wameshika nafasi za uongozi kwa sababu tu ni wadau wa timu kwa miaka mingi licha ya kutokuwa na shule yoyote.
 
Back
Top Bottom