Barcelona wadaiwa kuhamia EPL, Wenger aanza kuhanya

Barcelona wadaiwa kuhamia EPL, Wenger aanza kuhanya

Hivi timu inaweza kuhama kama taifa moja kwenda jingine (ligi moja hadi nyingine) kama kuhamisha kontena? Tujuzane hapa.
Jumbo lao linadai Uhuru kutoka Spain liwe taifa huru
 
Yanga anaweza kuhamia nchi yoyote east africa na akapokelewa.nnavyojua

Lakini kwa ulaya tunadanganyana tu,hicho ki2 hakipo.
mbona celtic iliapply kujiunga EPL? Hta barcelona ilianzia Fc basel ?? ni rahisi tu unaisajili upya uingereza kma kampuni mpya unaanzia tokea non league mpaka upande hadi EPL ssa kwa mazingira hayo lazma ukubaliwe tu
 

Kocha Arsene Wenger wa Arsenal, amesema kama FC Barcelona watakuwa ‘siriaz’ na uamuzi wao wa kuhama La Liga na kucheza Premier League litakuwa jambo zuri lakini wataongeza ugumu kwa kiasi kikubwa.

Barcelona wameonyesha nia ya kujiunga na Premier League kutokana na hali ya kisiasa inayoendelea nchini humo hasa wao wakionyesha kuunga mkono upande wa Catalonia.
“Sidhani kama wamefikia siriaz kiasi hivyo na kwenda wanataka kuhamia EPL.

“Lakini kama ni kweli basi ugumu utakuwa kwa kila mmoja wetu kwa kuwa tunawajua Barcelona na uwezo wao,” alisema Wenger.

Kwa hisani ya salehe Jembe
Wajiunge under what basis??
 
EPL ina timu 20 je huyo barca anaingia kuchukua nafasi ya nani?
Kama Barca anataka kuja epl itambidi ainzie kule ligi za vitongoji then apande league two, one, Championship ndo atue EPL
Hapa atapewa favour kutokana na hali ya nchini kwao, atajiunga moja kwa moja ligi kuu
Ikwa ndivyo, timu zitakazoshuka daraja msimu ujao zitakuwa 4
 
EPL ina timu 20 je huyo barca anaingia kuchukua nafasi ya nani?
Kama Barca anataka kuja epl itambidi ainzie kule ligi za vitongoji then apande league two, one, Championship ndo atue EPL
Its very simple, inakuja nunuliwa weak team iliyopo ligi kuu, inasajili wachezaji hao hao waliotoka barcelona, kocha aliyetoka barcelona, challenge itakuwa in one match line up lazima awe na 5 british nationals kwa pitch, ambao atawanunua pia toka kwa club kubwa hapo hapo epl.
 
upload_2017-10-3_9-42-13.jpeg

London, England.Baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Brighton and Hove Albion, kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema ujio wa Barcelona katika Ligi Kuu England itaongeza ugumu kwa kila timu.

Akizungumzia hilo kutokana na hali ya kisiasa ilivyokuwa kwa sasa Catalonia, na kumekuwa na tetesi kuwa ni wapi Barcelona itacheza kama wakiondolewa kushiriki La Liga.

Wenger aliuliza kuhusu mtazamo wake iwapo timu hiyo itapendelea kucheza katika Ligi Kuu England.

"Najaribu kujifunza kwa kinachotokea Catalan," alisema Wenger.

"Kama Barcelona wanataka kujiunga na Ligi Kuu England, itafanya mambo kuwa magumu kwa kila mmoja wetu.

"Lakini siamini kama watafikia hatua hiyo.

"Ni jambo linalovutia na linatokea katika michezo hasa Barcelona ambayo imekuwa ni timu ya kisiasa zaidi."

Wakati alipoulizwa tena kama yuko tayari kuwakaribisha Barcelona katika Ligi Kuu England, Mfaransa huyo alidai kuwa wanatakiwa kuangalia timu zilizokuwa karibu na nyumbani kwao kwanza kama wanampango huo.

"Nafikiri itakuwa vizuri kuwaona jinsi watakavyopambana katika Ligi Daraja la kwanza," aliongeza.

"Hapa tuna idadi ya timu za kutosha 20, lakini kama wanataka kuongeza kufikia 24, tulitakiwa kwanza tukaribishe klabu kutoka Scotland kabla ya kwenda Hispania."
 
Ha ha ha ha ha ha ha eti haamini kama Barca watafikia hatua hiyo.
 
waje tu epl wakutane na miziki ya burnley stoke na wengineo
 
Back
Top Bottom