Samcezar
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 13,095
- 22,731
Kuna dogo juzi hapa niliona katika taarifa ya habari ITV kaja kuchukuliwa na sungusungu kwao kwa wazazi wake.Tatizo kubwa la Dar hivi vitoto tunavifuga wenyewe, wala hakuna sababu nyingine na tusiwalaumu Polisi.
Tuko nao mitaani na tunawajuwa na hatuchukui hatua stahiki kukomesha tabia hizi.
Walimuomba wakaondoka nae wakidai wanahitaji kumhoji na kuongea nae kuna jambo wanahitaji kuongea nae.
Walipotoka nae hawakurejea nae tena hadi kesho yake alipokutwa mtaroni akiwa mahututi kwa kichapo kizito alichopewa bila majeraha na alipopelekwa kituoni alifia njiani mwili ukapelekwa monchwari.
Nikawazia tu huyu atakuwa ni wale madogo watukutu wanaotest uhuni sungusungu wameamua kumalizana nae kimya kimya. Hakutakuwa na kesi. Mwizi huwa anajulikana sana na karibu kila mtu hapo mtaani.
Wazazi wanatetea watoto wao na aibu ya ujirani mwema ndio hufanya hawa madogo kuwa na viburi vya kuendelea kufanya ugaidi.
But dawa yao imepatikana.