Barrick na Tanzania waunda Kampuni ya ubia iitwayo Twiga Minerals na Serikali itamiliki asilimia 16

Barrick na Tanzania waunda Kampuni ya ubia iitwayo Twiga Minerals na Serikali itamiliki asilimia 16

Kwa uelewa wa maandishi kama yatakuwa hivyo ni kuwa Sheria ya madini 2010 na marekebisho yake 2017 inaeleza kuwa kwa Mgodi wowote unaoanza serikali itakuwa na hisa bure(Free) 16% na Mwekezaji 84% hii ni kuwa uendeshaji na shughuli zote zitakuwa za muwekezaji bila serikali kuweka chochote, ila serikali inauhuru wa kuongeza umiliki mpaka 50%, na hii 50/50 ni mgawanyo wa faida baada ya kutoa gharama za uendeshaji. Kama itafanyika hivyo kweli itakuwa faida kwa nchi
Kwa uelewa wangu mdogo mgao wa faida inapaswa kuwiana idadi ya hisa, iko hivyo duniani kote ndio maana nahisi kuna kitu hakiko sawa
 
Kwa jinsi ambavyo nimeelewa ni kwamba kampuni itakapokuwa inafanya kazi mwekezaji lazima awe anarudisha kwenye capital yake aliyoinvest, yeye atakuwa amewekeza katika mitambo na ujenzi wa infrastructure achilia mbali man power, sisi mtaji wetu ni ardhi na madini. Katika exploration ya madini walishakadiria kiasi kilichopo na possible extraction kwa mwaka. Kwa mkadirio huo wameshaproject mpaka kipindi mgodi utakuwa exhausted.
Kwa hiyo sasa watakapokuwa wanaanza kazi tu watakapo kuwa wanarudisha capital invested amount itakayokuwa inarudishwa itagawanywa kwa mgawanyo huu Barick 86% na Tanzania 16%. Kama kutakuwa na net profit basi hiyo itagawanywa 50 kwa 50.
Faida ya haya makubaliano ni kwamba hata kama hakutakuwa na net profit basi anaporudisha kwenye capital yake na kwetu kwenye ardhi tupate walao 16% ya kila atakachokuwa anarudisha kwenye mtaji wake.
Tofauti na zamani mwekezaji anakuja anapewa grace period ya miaka mitano kwa madai kwamba anarudisha capital aliyoinvest ikiisha miaka mitano anajifanya anaondoka anakuja mwingine naye anaanza hivyo hivyo.
Sasa hivi apate faida au asipate lazima nasi tupate 16% ya kiasi anachorudisha kwenye capital yake. 50/50 inatumika kwenye kugawana faida halisi.
Kumbuka kwa sasa hata serikali itakuwa na watu wake kwenye management.
 
4% to 16% unaona ni hatua kubwa sana? Kivipi ni hatua kubwa?

Madini ni yenu mnanyanyaswa then unajisifia kwamba ni hatua kubwa hiyo.

Kwanini Tanzania asimiliki asilimia 50 ya hisa na 50 zingine apewe Barrick?
Suala kusema kwamba hamna capital or teknolojia hizo ni lame arguments na ni ugonjwa mbaya sana kwenu nyie maana bila kujiongeza mtazidi kuonewa tu.
Tanzania ina migodi mingi ila bado umasikini unawasumbua sana.

Kwanini msibinafsishe hata migodi miwili tu kwa masharti kwamba wawape mashines za kila aina za kuchiba na kuchakata madini hapa hapa Tanzania?

Kinachonishangaza, kwa makelele yote yale nilitegemea wataibuka na la maana, kwanza hapo ujue Barrick tayari wameashiria lazima gharama zilipwe za kuresha kampuni ikae vizuri maana wamecheleweshwa kwa muda mrefu.
 
4% from where? GoT had 0% shares with exeptions of individuals who had shares in Acacia that have just been bought out!
 
Ngoja niendelee kusoma majibu nipate mwanga.

Ninyi msio na majibu ila mnamshambulia mleta mada mnaboa.
 
Unaweza kuta hiyo faida inayosemwa itapatika baada ya miaka 20, humu katikati watakwambia tunarudisha hela yetu ya uwekezaji.
Wanaporudisha hela yao kiasi wanachorudisha sisi tunatakiwa tupate 16% kama wadau wa ardhi yenye madini.
 
Tumeambiwa kuwa serikali inamiliki hisa 16 na mabeberu watamiliki hisa 84 lakini wakasema faida itakuwa 50/50! Kama ni hivyo kwa nini na hisa zisiwe 50/50? Nahisi kuna kitu hakiko wazi naomba kama kuna mtu mwenye ufafanuzi wa hili anisaidie

Sijawahi Kumuelewa Profesa Kabudi na tokea aseme mwenyewe kuwa aliokotwa Jalalani basi nikimwona anazungumza huwa naliona Jalala tu na siyo Maelezo yake. Huku mnasema hisa zao ni 84% na Sisi Watanzania zetu ni 16% halafu hapo hapo tena mnasema kuwa Faida tutagawana pasu kwa pasu. Hivi hii inaingia Akilini Kweli? Acheni kutufanya Watanzania wote labda ni ' Mapopoma ' kama mlivyo baadhi yenu. Mleta Mada ( Uzi ) yupo sahihi, namuunga Mkono na ana Hoja Kubwa, ya maana na ya msingi kabisa.
 
Unaweza kuta hiyo faida inayosemwa itapatika baada ya miaka 20, humu katikati watakwambia tunarudisha hela yetu ya uwekezaji.
Huenda kuta? Zito anawaharibu vijana kwa kweli..wamekua ni watu wa kupuyanga na watoa utabiri
 
Tumeambiwa kuwa serikali inamiliki hisa 16 na mabeberu watamiliki hisa 84 lakini wakasema faida itakuwa 50/50! Kama ni hivyo kwa nini na hisa zisiwe 50/50? Nahisi kuna kitu hakiko wazi naomba kama kuna mtu mwenye ufafanuzi wa hili anisaidie
Gulwa wakiweza kukuelewesha unitagi
 
Sijawahi Kumuelewa Profesa Kabudi na tokea aseme mwenyewe kuwa aliokotwa Jalalani basi nikimwona anazungumza huwa naliona Jalala tu na siyo Maelezo yake. Huku mnasema hisa zao ni 84% na Sisi Watanzania zetu ni 16% halafu hapo hapo tena mnasema kuwa Faida tutagawana pasu kwa pasu. Hivi hii inaingia Akilini Kweli? Acheni kutufanya Watanzania wote labda ni ' Mapopoma ' kama mlivyo baadhi yenu. Mleta Mada ( Uzi ) yupo sahihi, namuunga Mkono na ana Hoja Kubwa, ya maana na ya msingi kabisa.
Mkuu soma post ya 23 ya uzi huu usipoelewa unalako jambo.
 
Kwa uelewa wangu mdogo mgao wa faida inapaswa kuwiana idadi ya hisa, iko hivyo duniani kote ndio maana nahisi kuna kitu hakiko sawa

Hapana haiwezekani kwa mchakato huu wa 16% kwa 84% maana hii 16% ni free Interest, na hii ni kwasababu ya ardhi ni ya serikali maanake itaipa uhuru wa kuingia vikao na kuwa na cha kuongea kwa kampuni sababu naye anaumiliki huo wa 16%, na indapo mgodi utauzwa serikali hapo ina udhamani wa 16% ya mauzo hayo bila kuongeza chochote, endapo itapenda kuongeza umiliki mpaka 50% maana yake itatakiwa kuwekeza hela za uendeshaji kwa 34% maana 16% hiyo ni free.
Ila ule mgawanyo wa faida baada ya kutoa gharama za uendeshaji ndo 50/50.
Ila kwenye hiyo mabadiliko ya sheria yanaeleza kwa migodi inayoanza sasa kwa hii iliyokuwepo iliyokuwa na MDA's tayari haiguswi, ila kwa maelezo yaliyotolewa na waziri ni kuwa wamekubaliana huenda ikaifuta hiyo mikataba ya awali MDA's (Mining Development Agrements). Ikiwa hivyo vipi kwa Migodi ya GGM-Geita, Shanta-Chunya nao hii 16% by 84% inawahusu kwa sasa? Hili nalo anayejua atatudadavulia tujifunze zaidi
 
Cc😡p.mayalla plies msaada hapa
Tumeambiwa kuwa serikali inamiliki hisa 16 na mabeberu watamiliki hisa 84 lakini wakasema faida itakuwa 50/50! Kama ni hivyo kwa nini na hisa zisiwe 50/50? Nahisi kuna kitu hakiko wazi naomba kama kuna mtu mwenye ufafanuzi wa hili anisaidie
 
Unapoandika tumeuziwa mbuzi kwenye gunia maana yake una uhakika... Wenzako hua wanaandika "tetesi" hujachelewa unaweza kubadili kichwa cha habari.
Vijana wa Zitto mnafundishwa kutukana tu
Mkuu, uwe unasoma vyema. Mleta mada ameuliza swali. Saidia kutoa majibu na uache kando mabishano. Kama huna majibu, baki kimya.
 
Kinachonishangaza, kwa makelele yote yale nilitegemea wataibuka na la maana, kwanza hapo ujue Barrick tayari wameashiria lazima gharama zilipwe za kuresha kampuni ikae vizuri maana wamecheleweshwa kwa muda mrefu.
Exactly. Kwa makelele huwa wanaongoza ila linapokuja la msingi na limewekwa mezani kujadiliwa huwa wanapoteza confidence na kukubali mambo ya ajabu.perhaps language is still a problem. If you don't fathom it well, you won't say anything but ending up saying Yes, yes, no, no, etc.
 
Back
Top Bottom