Tumeambiwa kuwa serikali inamiliki hisa 16 na mabeberu watamiliki hisa 84 lakini wakasema faida itakuwa 50/50! Kama ni hivyo kwa nini na hisa zisiwe 50/50? Nahisi kuna kitu hakiko wazi naomba kama kuna mtu mwenye ufafanuzi wa hili anisaidie
Utawezaje kujua mambo yako sawa au si sawa iwapo Rais Magufuli ameshindwa kufanya mikataba ya maliasili hii kuwa wazi?
Si bado inasainiwa gizani?
Hebu tujiulize, Mzee wa "HAPA KAZI TU" (Pombe) anasifiwa katika eneo hili kwa kufanya kitu gani hasa kipya ambacho hakikuwepo tangu enzi za mzee wa "UBINAFISISHAJI" (Mkapa) na kupokelewa na mwenzake mzee wa "ARI MPYA, KASI MPYA na NGUVU MPYA" (Kikwete) walichosahau kukifanya kama mkakati wao kuiba na kuiuza nchi kwa mikataba ya kisheria ya kimataifa??
Hizi awamu za CCM chini ya MKAPA (1995 - 2005) na KIKWETE (2005 - 2015) ndizo zilizosaini mikataba za kuiuza nchi hii rasmi......!!
Na tusidanganywe na mtu awaye yeyote kwa sababu mikataba hii masharti yake ni IRREVERSIBLE in anyway.....!!
Mikataba hii ina masharti ya mbele kwa mbele mpaka ukomo wake and not otherwise......
Labda kinachoweza kufanyika si kuivunja ama kuitengua bali kuyaomba majamaa kukaa nayo tena chini na ili ingalau wakubali kulegeza baadhi ya "clause" ili ingalau na sisi kama nchi tuambulie kitu kidogo....
Hakuna wa kubadilisha haya mambo, si Magufuli na hata akiingia ZITO KABWE na ACT yake ama TUNDU LISSU na CHADEMA yake.....
Absolutely, they all can't reverse anything.....!!
However, there is way forward to get through these problem by minimizing its consequences.....
MOSI; kilicho ndani ya uwezo wetu kama nchi ni kuwachukulia HATUA KALI wote kuanzia Mkapa & Co, Kikwete & Co na sasa Magufuli & Co ambao kwa TAMAA ZAO MBAYA waliiuza nchi yetu kwa vipande vya fedha.....
MBILI; Tusiingie mikataba mingine tena kwa mtindo waliotumia hawa wenzetu wasio WAZALENDO wa KWELI wa nchi hii mpaka kwa pamoja tukae chini na kurekebisha makosa haya.....
Hii ifanyike baada ya wale waliofanya makosa haya kwa makusudi kuwa Magerezani kwanza....
TATU; michakato yote ya mikataba ihusuyo uvunaji wa maliasili zetu iwe wazi (ingalau ipitie bungeni) kuanzia hatua ya negotiation hadi utiaji saini na implementation yake hatua kwa hatua......
NNE; Kufanyike mabadiliko makubwa ya KIKATIBA na KISHERIA kwa kuhakikisha kwamba mamlaka ya usimamizi wa rasrimali za nchi yanakuwa mikononi mwa wananchi wenyewe kupitia vyombo vyao vya uwakilishi na kamwe asiachiwe mtu mmoja aitwaye "Rais" ama "Waziri mwenye dhamana" bila ya kuwa na "checks" ili kuamua kwa niaba yetu....
TANO; mwekezaji yeyote ambaye atashindwa kukubaliana na utaratibu wetu juu ya mali yetu wenyewe, atupishe na maliasili yetu kama ni madini, wanyama, ardhi itabaki vivyo hivyo huku sisi wenyewe tukijenga uwezo wa kuivuna.....!!
SASA SWALI NI HILI;
Rais Magufuli Pombe amefanya hata moja tu kati ya hayo hapo juu??
Kwangu mimi sioni mwanga wowote, sioni na kwa kweli hakuna mabadiliko yoyote......!
Still mambo bado ni "business as usual??"
Ni kwa sababu CCM ni ileile yenye watu (kina John Pombe Magufuli, Change Andrew & Co) wenye vichwa na akili zilezile zilizotengeneza matatizo haya....!
Kwa hiyo ni ngumu sana ama haiwezekani kabisa mtu aliyetengeneza tatizo, akalilea kwa karibu miaka 69 umtegemee huyohuyo atatue tatizo hilo...
IMPOSSIBLE....!!!