Wewe ni mtaalam wa masuala ya uchumi, naomba utueleweshe hiki kitu vizuri maana baada ya vurugu zote sikutgemea wataishia kwenye
- Umiliki wa hisa GoT 16% vs Mabeberu 84%, hapo mabeberu wana sauti ya nini kifanyike na wapi na lini na kwa namna gani
- Hiyo net faida unayosema 50/50 kumbuka gharama za uendeshaji na utaalam vipo kwenye mikono ya mabeberu, wao ndio watatangaza nini faida
- Makinikia sasa ruksa kuondoka, hivyo hapo wanarudi kwenye yale yale
- Pia kuna zile dola bilioni 150 ambazo walikua wamesema watalipwa, yaani hela ndefu sana hizo, ila nimeona wameishia kwenye milioni 300