Barrick vs Tanzania: Tukubali tu kwamba tumezidiwa ujanja na Wazungu

Barrick vs Tanzania: Tukubali tu kwamba tumezidiwa ujanja na Wazungu

Hapa vipi? "...kinachopatikana Tanzania ni kama 16% ya value ya Barrick worldwide, that is why Twinga wapo 50-50 percentagewise. Natumaini unaweza kuwa umeambulia kitu."

Imebidi nikachekee mbali!
 
Ona unakoelekea sasa. Yaan nyie sio vigumu kujua ujinga wenu, unaongelea vyama sisi tunaongelea mkataba huu mpya, this is new ccm yenye mabadiliko. Ccm ya enzi za ujima hatutaki kusikia
Waliosaini mkataba wa 3% ni viongozi wa chama kipi?
Mwaka 1991 Lisu aliwekwa ndani na serikali ya CCM akiwa anapinga hiyo 3%. Alikuwa anataka mapato ya madini yagawanywe 50 kwa 50. Alipigwa sana na akasekwa ndani.
Acheni ufala wenu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi huwa sisomi comment za huyu chizi
Kutoka Mezani kwa Zitto Kabwe,

**********

MAKUBALIANO YA SERIKALI NA BARRICK GOLD CHANGA LA MACHO.
__________________

Jana, Julai 19, 2019 Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Barrick Gold Corporation imetoa Taarifa kwa Umma ya kuinunua Kampuni yake tanzu ya Acacia Mining Plc kwa jumla ya Dola za Marekani Milioni 428. Baada ya malumbano ya takribani miezi 5 Barrick na Acacia wamekubaliana juu ya thamani ya Kampuni ya Acacia kuwa ni Dola za Marekani milioni 951 (wastani wa TZS 2.2 Trilioni).

Itakumbukwa kuwa kabla ya sakata la Makanikia la Mwezi Machi mwaka 2017, Kampuni ya Acacia ilikuwa na thamani ya Dola za Marekani Milioni 4,400 (wastani wa TZS 10 Trilioni). Kwa mujibu wa kanuni za Masoko ya Hisa na Mitaji, taarifa za manunuzi ya makampuni huwekwa wazi pamoja na nyaraka nyengine zote husika.

Kwa Watanzania nyaraka muhimu katika mauziano haya ya Acacia, ni ile ya Makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick katika kumaliza mgogoro wa Makanikia na masuala ya Kodi. Nyaraka hiyo (ambayo Serikali imekuwa ikiificha baada ya Majadiliano yaliyofanywa na Prof. Palamagamba Kabudi) sasa imewekwa wazi kama Kiambatanisho namba 4 cha nyaraka za manunuzi ya Acacia.

Nyaraka hizo zinaonyesha kuwa Serikali ya Tanzania imeingia makubaliano na Barrick Gold Corporation mnamo tarehe 19 Mei, 2019. Makubaliano hayo ni MABAYA, ya HOVYO, yasiyo ya KIZALENDO na yanayoumiza nchi kuliko makubaliano yaliyokuwepo kwa Mujibu wa sheria ya Madini ya mwaka 2010. Kwa ufupi tu ni kuwa Rais John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Palamagamba Kabudi WAMEUZA nchi kwa vipande vya dhahabu. Nitaeleza kama ifuatavyo.

Kiambatanisho namba 4 kimeweka muhtasari wa kinachoitwa ‘Material Terms’ katika Makubaliano ya awali kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick Gold ambayo yamesainiwa (INITIALED) mwezi Mei mwaka huu. Kimsingi Barrick imelazimishwa na kanuni za masoko ya mitaji kuweka wazi makubaliano hayo. Ni masikitiko makubwa kuwa Serikali yetu haijathubutu hata kuliambia Bunge kuwa kuna makubaliano ya namna hiyo wakati wa Bunge la Bajeti, imesaini kwa siri kama ulivyosainiwa mkataba wa Buzwagi.

Ikumbukwe kuwa makubaliano hayo yamesainiwa wakati Bunge likiwa linaendelea na mkutano wake jijini Dodoma. Sisi kama wawakilishi wa Wananchi imebidi kusubiri masoko ya mitaji ya ‘MABEBERU’ wa London yaweke wazi masuala yanayohusu nchi yetu. Hii ni dharau kubwa ambayo Serikali ya Rais Magufuli imefanya kwa Wananchi na kwa Bunge. Sasa tutazame ni nini Serikali yetu imekubaliana na Barrick Gold katika maeneo matano tu.

1. Dola Milioni 300 za kumaliza mgogoro KIINI MACHO

Serikali imekubaliana na Barrick kuwa italipwa Dola milioni 300 (wastani wa TZS 700 Bilioni) kama malipo ya kumaliza mgogoro wote (full, final and complete settlement) na SIO kishika uchumba kama Serikali ilivyoeleza umma. Barrick watalipa fedha hizi kwa muda wa MIAKA 7 na zitakuwa ni baada ya kuondoa madai yote ya kodi ambayo Acacia inaidai Tanzania.

Itakumbukwa kuwa Acacia Group ina madai ya marejesho ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT refunds) inayofikia takribani Dola za Marekani milioni 240 (wastani wa 552 Bilioni). Hivyo katika malipo ya Dola za Marekani Milioni 300, zitakazobakia baada ya kutoa madai ya VAT refunds ni Dola Milioni 60 (wastani wa 138 Bilioni) tu. Kama tutakavyoona katika hoja ya pili hapa chini hata hizi Dola za Marekani Milioni 60 kimsingi hazitatolewa.

2. Barrick Gold Wamesamehewa Kodi ya Ongezeko la Mtaji USD 85.6M

Serikali ya Tanzania imetoa misamaha mbalimbali ya Kodi kwa Kampuni ya Barrick Gold katika makubaliano yaliyoingiwa ikiwemo kodi ya ‘Capital Gains’ ambayo inatokana na mauzo ya hisa za Acacia kwa Barrick. Itakumbukwa kuwa mwaka 2012 Bunge lilitunga sheria ya kutoa Kodi ya Ongezeko la Mtaji kwa mauzo ya mali zilizopo Tanzania ili kudhibiti ukwepaji wa Kodi.

Barrick inainunua Acacia kwa Hisa ambazo Barrick haikuwa inamiliki ambazo zimepewa thamani ya Dola Milioni 428. Capital Gains Tax ya 20% ilipaswa kulipwa lakini Rais Magufuli na Profesa Kabudi wametoa ‘waiver’ (Msamaha) na kupoteza Mapato halali na ya kisheria kwa nchi yetu ya Dola Milioni 85.6 (wastani wa TZS 200 Bilioni). Tukirejea hoja ya kwanza hapo juu utaona kuwa sio tu Tanzania kiuhalisia haitapata Dola Milioni 300, bali pia tunaipa zawadi Barrick ya Dola Milioni 25.6 (wastani wa TZS 59 Bilioni) za ziada.

3. Tanzania kupewa Hisa 16% za daraja B lakini Watanzania kunyimwa umiliki wa 30% kupitia Soko la Hisa la DSE

Ni kweli kuwa Serikali itapewa hisa za bure 16% kwenye Kampuni tanzu zote za Acacia hapa nchini kama tulivyoambiwa na Serikali. Lakini hisa hizo ni za Daraja la B ambazo ni hisa dhaifu kulinganisha na zile za Daraja la kwanza. Hisa hizo haziruhusiwi kuuzwa, hazina kura kwa masuala fulani fulani ya Kampuni na huwezi hata kuziweka kama dhamana ya mikopo. Hata mgawo wa gawio hisa hizi hupata baada ya wale wa daraja A kulipwa kwa ukamilifu.

Licha ya makubaliano haya ya hovyo na yasiyo na tija, Serikali yetu imetoa ‘waiver’ (msamaha) kwa Barrick kutoorodhesha hisa kwenye Soko la Hisa la Tanzania. Sheria ya Madini ya mwaka 2010 (Wakati wa Waziri William Ngeleja) na Kanuni zake iliweka sharti kwamba ni lazima makampuni ya madini yauze 30% ya hisa kwa Watanzania kwenye soko la Hisa la Tanzania.

Makubaliano ya Mei 2019 kati ya Barrick na Serikali ya Tanzania yametoa msamaha kwa Barrick kutekeleza sharti hilo la kisheria. Uamuzi huu unavunja sheria za nchi, ni hujuma kwa Watanzania kumiliki maliasili zao na ni ukosefu wa maarifa ya kiuchumi kwa kiwango kisichomithilika wala kuvumilika.

4. Bunge lafungwa mikono kubadili sheria yeyote

Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick wamekubaliana kuwa baada ya mkataba wao kukamilika Bunge la Tanzania haliwezi kutunga sheria yeyote ambayo itabadili makubaliano hayo na kodi zote zilizokuwa zinafanya kazi wakati wa kuingia makubaliano hazitaweza kubadilishwa kipindi chote ambacho Barrick watakuwa wanafanya kazi Tanzania (fiscal stabilisation).

Makubaliano ya namna hii ndiyo kitu kilicholeta Buzwagi mwaka 2007 ambapo Serikali za Rais Mkapa na Rais Kikwete ziliingia mikataba ya kulifunga Bunge kutimiza majukumu yake ya kikatiba kama Dola (sovereign). Sheria ya Madini yam waka 2010 iliondoa sharti hili kufuatia mapendekezo ya Kamati ya Bomani. Rais Magufuli na Waziri Kabudi wameturudisha kwenye unyonyaji wa kihayawani kabisa.

5. Barrick wameruhusiwa kufungua kesi ughaibuni kinyume na Sheria

Kwa mujibu wa sheria mpya za madini za mwaka 2017 makampuni yamezuiliwa kufungua mashauri yake nje ya Tanzania. Migogoro yote inapaswa kushughulikiwa na mahakama za ndani ya nchi. Serikali ya Tanzania imekubaliana na Barrick kuwa migogoro itafanyika kwa mujibu wa kanuni za UNICITRAL na Rais wa Kituo cha usuluhishi wa migogoro cha Singapore ndio atateua wasuluhishi ambao hapatakuwa na Mtanzania.

Serikali mara zote iliambiwa kuwa mabadiliko ya sheria kuhusu ‘arbitration’ hayakuwa halisi na ni ulaghai. Serikali yenyewe imekuwa ya kwanza kuvunja sheria yake yenyewe kwa kuingia makubaliano na Barrick Gold kuwa Mahakama zetu hazitahusika na kutatua mgogoro wowote kati ya Barrick na Tanzania.

Tanzania Imekosa Shilingi Trilioni 2 kwa Sababu ya Viongozi Kukosa Maarifa

Siku za mwanzo kabisa za mgogoro wa Makanikia nilieleza kuwa Serikali ya Rais Magufuli haina Maarifa ya kuwezesha nchi kupata ushindi katika suala hili, watu wengi walinitukana, lakini leo imedhihirika hivyo.

Wakati ule nilitoa mfano kuwa Acacia ilipotaka kununuliwa na Kampuni nyengine ya Canada kwa thamani ya Dola za Marekani 4.4 Bilioni (wastani wa TZS 10 Trilioni), Tanzania ingefaidika sana kwa kupata Kodi ya Ongezeko la Mtaji ya Dola za Marekani 880 Milioni (wastani wa TZS 2 Trilioni), Serikali haikufanya subira na ikazuia Makanikia na mpango ule wa Acacia kununuliwa ukavubjika.

Leo Serikali yetu imekwenda kuingia MAKUBALIANO YA AIBU kabisa ambayo kiuhalisia tunaishia kufuta kesi za Kodi ya Dola za Marekani 190 Bilioni (wastani wa TZS 400 Trilioni) na tunawalipa Barrick fedha badala ya sisi kupata Fedha. Ni jambo la fedheha mno, wanaojigamba kuwa ni wazalendo leo wametuuza.

Ingekuwa nchi nyengine, Makubaliano haya ya KIMANGUNGO kati ya Serikali ya Rais Magufuli na Kampuni ya Barrick, ingetosha kuiondoa Serikali madarakani. Rais John Magufuli na Waziri Palamagamba Kabudi wameuza nchi yetu kwa kipande cha dhahabu. Wamelihujumu Taifa.

Kabwe Z.Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Vuga, Zanzibar
Julai 20, 2019

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Good question!
Barick anaweke pesa zake!! Sisi hatuweki hata sh 100.Barrick atalipa kodi na kodi hyo itaenda kwenye Serikal ya Tanzania.Hizo 16% ni insoluble yaani hata kama barrick akaongeza investment yake hisa zetu hazipungui.Na pesa anayowekeza ni trilions of money! So tukitaka share 50% inabid na sisi tununue hizo hisa.lkn hiz tulizonazo n za bure kabisa
 
Hakuna ufafanuzi wowote uliotoa. FYI yaani umezidi kuchanganya mambo zaidi.

Tunafahamu kuwa faida ya biashara yoyote hugawanywa kutokana na kiwango cha uwekezaji ( hisa) katika kampuni. Sasa iweje mwenye 84% na 16% wagawane faida 50/50. Kwa nink umiliki wa kampuni usiwe pia 50/50?
Mkuu tofautisha dividend na benefit, bus linapofika msamvu unanunua karanga maji soda, lisingesimama wasingeuza hayo maji, huyo muuza maji na karanga amepata benefit yaani kafaidika na uwepo wa bus stand, umeelewa?
 
1. Hakuna kubadili sheria ya madini mpaka Barrick waondoke nchini.

2. Hakuna kuishtaki Barrick mahakama za ndani.

3. Barrick haitajisajili ndani ya DSE.

4. Hakuna Mtanzania atakayeweza kununua hisa kwenye kampuni.

5. Serikali itapata share ya net profit na net loss kwa 50%.

Kwa mkataba huu tumepakatwa na hatuna pa kutokea uzalendo kweli ndio huu?

Kabudi Mungu anakuona
Mkuu, hivi hapo nilipo weka red color walipaona kweli hao Viongozi wa Nchi hii ??
 
Nimekuambia hata kwenye ule uzi mwingine kusainiwa mkataba sio jambo geni, tija ya kilichosainiwa ndio muhimu. Yeye ww akili yako yote ni kwenye hilo igizo la kusainiwa na wala sio kilichoko ndani ya mkataba.
Mkuu ni swala la muda tu, tusubiri tuone hizi ngonjera zinatupeleka wapi...
 
Asilimia hizo ni share holding, ie 16% ya shares zote za Barrick na wao Barick wanamiliki 84%.(In actual fact hizo 84% wanaweza wasizimiliki wao Barrick kwa sababu kila mtu ana uhuru wa kununua shares kwenye stock exchange worldwide ie From Hong Kong, Tokyo, Melbourne, London, Paris, New York au Toronto etc. Kampuni huwa na shares 100 percent ambazo zinajulikana, sifahamu Barrick wana kiasi gani cha shares, usichanganye number of shares na percentage. (FYI shares za Barrick ni worldwide wana chimba Gold kila mahali ulimwenguni na makadirio yao kipato kinachopatikana Tanzania ni kama 16% ya value ya Barrick worldwide, that is why Twinga wapo 50-50 percentagewise. Natumaini unaweza kuwa umeambulia kitu.

Mkuu samahani naona kama kuna vitu unachanganya au ni mimi labda sijaelewa..

Barrick sio mtu bali ni kampuni inayomilikiwa na share holders wengi world wide.. 84% shares ndani ya Twiga yenye migodi mitatu inabaki kuwa moja ya Asset za Barrick na hili sio hapa tu nchi nyinginezo kama Mali Barrick amefanya the same kama hapa.

Hiyo 50-50 percentage wise inahitaji more clarification iweze kueleweka, fahamu pia Tanzania anamiliki ardhi kama mtaji na Barrick yeye amefanya investment kuanzia exploralation, Construction na Operations na huko kote ameweka fedha na Tanzania hana alichowekeza zaidi ya ardhi, how huyu Tanzania anapata 50/50? naomba kueleweshwa kidogo..
 
HUYU ZITO TUMNYANG" ANYE URAIA, HIZO NONDO ZAKE NI HATARI SANA NA ZA KICHOCHEZI..
 
Nimekuambia hata kwenye ule uzi mwingine kusainiwa mkataba sio jambo geni, tija ya kilichosainiwa ndio muhimu. Yeye ww akili yako yote ni kwenye hilo igizo la kusainiwa na wala sio kilichoko ndani ya mkataba.
Kweli wewe ni vuvuzela huchelewi kubadirisha gia angani!!
 
Ona unakoelekea sasa. Yaan nyie sio vigumu kujua ujinga wenu, unaongelea vyama sisi tunaongelea mkataba huu mpya, this is new ccm yenye mabadiliko. Ccm ya enzi za ujima hatutaki kusikia

Sent using Jamii Forums mobile app
CCM ni Ile ile hilo halina ubishi acha kujifanya mwendawazimu.
Hao wana ccm walioingia hiyo mikataba ya kijima wachukuliwe hatua za kisheria basi
 
1. Hakuna kubadili sheria ya madini mpaka Barrick waondoke nchini.

2. Hakuna kuishtaki Barrick mahakama za ndani.

3. Barrick haitajisajili ndani ya DSE.

4. Hakuna Mtanzania atakayeweza kununua hisa kwenye kampuni.

5. Serikali itapata share ya net profit na net loss kwa 50%.

Kwa mkataba huu tumepakatwa na hatuna pa kutokea uzalendo kweli ndio huu?

Kabudi Mungu anakuona
Pia jamaa wamebaki na tril 495 zao pamoja na kishika uchumba tulichodanganywa!
 
1. Toa ushahidi ulionao.
2. Barrick ni shareholder wa kampuni ya Twiga pamoja na TZ Government.
3. Twiga watajisajili DSE
4. Unaweza kununua shares za Twiga DSE au Barrrick LSE, CNSX au NSE popote unaponunua its value will be the same. (ie determined by the market)
5. Usitegemee kupata faida wakati hakuna uzalishaji.
Kwenye hiyo kampuni ya Twiga majority shareholder ni nani?
 
Hakuna ufafanuzi wowote uliotoa. FYI yaani umezidi kuchanganya mambo zaidi.

Tunafahamu kuwa faida ya biashara yoyote hugawanywa kutokana na kiwango cha uwekezaji ( hisa) katika kampuni. Sasa iweje mwenye 84% na 16% wagawane faida 50/50. Kwa nink umiliki wa kampuni usiwe pia 50/50?
Siyo lazima mgawanyo wa faida ulingane na asilimia za umiliki wa kampuni........Hivi vitu vinajitegemea!
 
Back
Top Bottom