Nikiri kwanza, kwamba mimi sio mwanasheria. Halafu swali langu ni kuhusu ufafanuzi wa jumla wa sheria zetu.
Swali: Hivi kama kisheria ardhi ya Tanzania ni mali ya Serikali, madini yaliyomo ardhini pamoja na gesi, mafuta nk ni mali ya Serikali pia au sivyo?
Kama ni mali yetu mbona sijasikia yakitajwa kuwa mtaji wetu katika mikataba ya ubia na wawekezaji?
Pili; Nini kinafanyika mwekezaji mpya anapopewa eneo la kutafuta na kuchimba madini anamilikishwa ardhi tu au na madini yaliyomo?
Nauliza hivi kwasababu kwa sheria za nchi Mtanzania anaruhusiwa kumiliki ardhi tu lakini sio madini yaliyomo ardhini kwake. Serikali nayo haisemi wazi kama inamiliki ardhi na madini! Lakini tunaambiwa sisi ni matajiri!
Utajiri wetu ni upi kama haturuhusiwi kumiliki ardhi na madini yaliyomo ardhini?
Halafu Serikali nayo inapompa mwekezaji mpya eneo la kutafuta na kuchimba madini, inasarenda ardhi na hayo madini jumla jumla kwa mwekezaji au vipi?
Maoni yangu:
Sera yetu ya umiliki wa ardhi kwa sisi wananchi inatunyima fursa za kuitumia ardhi kikamilifu kama mtaji.
Tumpe mwananchi 'free hold' ili itambulike kwamba ardhi na kilichomo ni mali yake.
Vinginevyo Mtanzania atabaki masikini milele wakati nchi yake ni "TAJIRI" masikini.
Unaweza "kumiliki ardhi" na majumba ya kifahari Tanzania lakini siku yoyote unaweza kupokonywa na Serikali kwa kisingizio cha 'eminent domain' na kuishia kupewa fidia ya majengo au mazao yako tu, sio ardhi!
Tafsiri yake ni kama vile ardhi haina thamani, ambayo sio kweli.
Ardhi ina thamani, iwe mjini au kijijini, iwe na madini au haina.
Tukiendelea na sera ya kinafiki kwamba ardhi haina thamani tunaitangazia dunia umasikini wa Watanzania.
Haya ni MAONI yangu tu. Kuna watu ukitoa maoni wanasema umewapinga kwahiyo ni adui yao! Binadamu gani asiye na maoni?
Maendeleo yatakujaje kama hamtaki kusikiliza MAONI ya wenzenu?
Sent using
Jamii Forums mobile app