Barrick vs Tanzania: Tukubali tu kwamba tumezidiwa ujanja na Wazungu

Barrick vs Tanzania: Tukubali tu kwamba tumezidiwa ujanja na Wazungu

1. Hakuna kubadili sheria ya madini mpaka Barrick waondoke nchini.

2. Hakuna kuishtaki Barrick mahakama za ndani.

3. Barrick haitajisajili ndani ya DSE.

4. Hakuna Mtanzania atakayeweza kununua hisa kwenye kampuni.

5. Serikali itapata share ya net profit na net loss kwa 50%.

Kwa mkataba huu tumepakatwa na hatuna pa kutokea uzalendo kweli ndio huu?

Kabudi Mungu anakuona
Watu wa kulalamika Kila wakati...wewe ulitaka mkataba uweje?
 
Mkuu Stuxnet mi nachoona hapa hiyo ecomic benefit ina include all labour force, operating costs etc yaani ni profit before tax siyo net profit after deduction of all expenses inccured per annum.
Barrick ni multinational coy kwenye sector ya madini ni wabobevu, hivyo kwenye mkataba huu tusitegemee win win situation.
Akina Kabudi na Jiwe waache wakenue meno tu ila the effect is ahead of us.
Muda ni mwalimu mzuri tusubiri tutajionea!
 
..Barrick amepata 84%.

..sisi tumepata 16%.

..sasa kwanini tujione tumeshinda?

..Je, kushangilia 16% siyo kujidharau sisi wenyewe?

..Na kama madai yetu ya mwanzo yalikuwa usd 191 billion, kusaini makubaliano haya siyo kusalimu amri kwa kampuni ya mabeberu?
 
..Barrick amepata 84%.

..sisi tumepata 16%.

..sasa kwanini tujione tumeshinda?

..Je, kushangilia 16% siyo kujidharau sisi wenyewe?

..Na kama madai yetu ya mwanzo yalikuwa usd 191 billion, kusaini makubaliano haya siyo kusalimu amri kwa kampuni ya mabeberu?
Magufuli amempa kilema bure Tundu Lissu kwa kuwa kwenye hiyo deal ya Twiga/Barrick hakuna kitu chochote ambacho tuna gain kama Taifa. Aliyo tahadharisha Tundu Lissu bado yanaishi.

Makusudi ya Mungu kumnusuri Tundu Lissu dhidi ya risasi 16 siyo kitu cha kuchukulia kirahisi. Itakuja Serikali nyingine itayaweka wazi mauchafu ya Magufuri kuficha. Hususan hili la kumpiga mzalendo wa kweli Lissu risasi akìtetea ukweli
 
Asilimia hizo ni share holding, ie 16% ya shares zote za Barrick na wao Barick wanamiliki 84%.(In actual fact hizo 84% wanaweza wasizimiliki wao Barrick kwa sababu kila mtu ana uhuru wa kununua shares kwenye stock exchange worldwide ie From Hong Kong, Tokyo, Melbourne, London, Paris, New York au Toronto etc.

Kampuni huwa na shares 100 percent ambazo zinajulikana, sifahamu Barrick wana kiasi gani cha shares, usichanganye number of shares na percentage. (FYI shares za Barrick ni worldwide wana chimba Gold kila mahali ulimwenguni na makadirio yao kipato kinachopatikana Tanzania ni kama 16% ya value ya Barrick worldwide, that is why Twinga wapo 50-50 percentagewise. Natumaini unaweza kuwa umeambulia kitu.
Hili suala la kugawana faida na hasara tuliangalie vizuri vinginevyo share zetu zitaoshia kulipa hasara
 
Back
Top Bottom