Barrick yatangaza rasmi kifo cha Acacia!. Acacia yakubali rasmi kununuliwa baada ya Barrick kuongeza dau!

Funguka,sababu zako?
1. Kukubali 300M ni kujenga uhalali kuwa Acacia hawakutenda dhambi.
Kwamba, hata kwenye meza tumeona halali yetu ni $ 300 M

2. Tukijenga uhalali wa Acacia kutotenda dhambi tunajenga uhalali mwingine kwamba madai ya $ 193 B hayakuwa ya kweli. Tukifika hapo tunabaki njia panda...

3. Ikiwa tulikataa pesa za Millenium kwa mabilioni seuse hizi bilioni chache!
 
Wewe ungepata deal gani? Nzuri zaidi?

Kwahiyo unasema tungekataa deals zote, Wewe unaweza kufanya deal zote za Tanzania. Kukataa deal zote.

Tutapata wapi pesa kuwasaidia wananchi wetu.
 
Wewe ungepata deal gani? Nzuri zaidi?

Qqqqqqqq1qqqqqqqKwahiyo unasema tungekataa deals zote, Unaweza kufanya deal zote za Tanzania.

Tutapata wapi pesa kuwasaidia wananchi wetu.
Ningekataa deal. Inawajengea Uhalali Acacia na kuondoa uhalali wa madai 93B

Nyerere hakuchimba madini, aliyaacha ili tuchimbe.

Pesa ya Acacia haiendeshi nchi. Kama ni hivyo kwanini tulikataa pesa za millemium kwa kusema ''wanatudhalilisha''. Pesa za kuwasaidia watu wetu tumezipata wapi!

Hatuwezi kupewa ''peremende'' tukubali tu na kujiondolea uhalali wa madini yetu
Tukikubali peremende tukubali pia kuwa madai yetu ya 193B hayakuwa ya kweli

Laiti yangekuwa ya kweli kwanini tukubali 0.157% yaani less than 0.5%
Well, huko si kujidhalilisha kama kule tulikokataa kwa millenium

Hayo madini hayaozi yangebaki ardhini, tukaa chini, tukazungumza kwa uwazi, tukawatafuta wachawi, tukufungua tunguri zao, halafu tukasonga mbele kwa nguvu za dona na si peremende
 
Kuna kitu kinaitwa negotiatian tactics.
 
Mkuu assets za Acacia Tanzania ni muhimu sana kwa Barrick Gold. Pia makubaliano haya yanatokana na pressure inayowekwa kwa Acacia na serikali ya JMT.

Kusitishwa kutumia tailing storage facilities on North Mara, na kusema hatuongei na nyinyi tena. Unaweza kusoma zaidi hapa chini.

Share zimepanda zaidi ya 20% baada ya hii habari ya makubaliano kati ya Acacia na Barrick.

Nafahamu, na ndio maana nikasema tusije siku ya siku tukaambiwa Barrick wamenunua assets za Acacia peke yake na sio liabilities! Au Kiongozi hujawahi kusikia kampuni inanunua another company's assets but not liabilities?! Suala la kupanda bei ya share hilo nilishatarajia, kwa sababu hata wsakati hili sakata linaanza, bei ya shares ilishuka haraka sana lakini walipofikia yale makubaliano ya awali kabisa, shares zikaanza kupanda. Basically, kwa wenzetu that's how the stock markets work. News zinashusha na kupandisha bei ya stocks
 
Hi hivi mkuu, Barrick wakifikia muafaka na serikali ya JMT, assets zao zita double, probably triple in value.

Wawekezaji watafurahi sana. Hizi assets hazipatikana kila sehemu duniani.

How stock markets works, i know it for over 15 years.
 
Kuna kitu kinaitwa negotiatian tactics.
Ni kwamba, katika hili hakuna tactics zozote, tumeshindwa. Kwa 0.157% !

Nitakupa mfano mmoja rahisi uelewe ninaongelea nini

Siku za nyuma sana rafiki yangu mmoja anaishi ughaibuni alikamatwa na Polisi kwa kuendesha gari juu ya kiwango.

Rafiki yangu akaamua kwenda mahakamani kupinga kosa hilo kwani lingemuathiri katika leseni yake ya kuendesha magari makubwa

Baada ya kesi kuunguruma mahakamani, hakimu akatoa hukumu ya kumtaka yule bwana alipe faini ya dola 50 tu kwani kosa lenyewe halikupaswa kumfanya apoteze point katika leseni

Rafiki yangu akatoka mahakamani akiwa na furaha sana, kalipa dola 50 tu.

Baada ya wiki moja akapata barua kutoka insurance company kwamba wana taarifa za yeye kuendesha hovyo ''reckless' na kwamba bima yake itaongezeka kwa dola 10 kwa mwezi

Maana yake ni kuwa bima itaongezeka kwa dola 120 kwa mwaka, na rekodi itafutika baada ya miaka 3 ya uendeshaji hovyo

Hii maana yake ni kuwa rafiki yangu alidhani amepata deal, kumbe ilikuwa deal mbovu sana iliyomtia matatani zaidi. Dola 50 zimemgharimu kwa rekodi yake na Bima

Ndiyo maana nasema, kukubali 300M kwa kisingizio cha pesa za kusaidia wananchi ni bad deal, in fact ni shoddy. Huko kunaondoa uhalali wa $ 193 Bilioni tulizodai.

Unaweka rekodi yetu vibaya mbele ya dunia.
Kwamba, siku tukisema Barrick wanatuibia, dunia itasema ''ndiyo zao hizo''

Wanatunga namba kama ilivyokuwa kwa Acacia,wape pipi watatulia

Kumbe tungeacha isingetuathiri kwani Acacia walishafanya yao siku nyingi kwa ujinga wetu

Umenielewa?
 
Ni kwamba, katika hili hakuna tactics zozote, tumeshindwa. Kwa 0.157% !

Nitakupa mfano mmoja rahisi uelewe ninaongelea nini

Siku za nyuma sana rafiki yangu mmoja anaishi ugahibuni alikamatwa na Polisi kwa kuendesha gari juu ya kiwango. Rafiki yangu akaamua kwenda mahakamani kupinga kosa hilo kwani lingemuathiri katika leseni yake ya kuendesha magari makubwa

Baada ya kesi kuunguruma mahakamani, hakimu akatoa hukumu ya kumtaka yule bwana alipe faini ya dola 50 tu kwani kosa lenyewe halikupaswa kumfanya apoteze point katika leseni

Rafiki yangu akatoka mahakamani akiwa na furaha sana, kalipa dola 50 tu.
Baada ya wiki moja akapata barua kutoka insurance company kwamba wana taarifa za yeye kuendesha hovyo ''reckless' na kwamba bima yake itaongezeka kwa dola 10 kwa mwezi

Maana yake ni kuwa bima itaongezeka kwa dola 120 kwa mwaka, na rekodi itafutika baada ya miaka 3 ya uendeshaji hovyo

Hii maana yake ni kuwa rafiki yangu alidhani amepata deal, kumbe ilikuwa deal mbovu sana iliyomtia matatani zaidi. Dola 50 zimemgharimu kwa rekodi yake na Bima

Ndiyo maana nasema, kukubali 300M kwa kisingizio cha pesa za kusaidia wananchi ni bad deal, in fact ni shoddy. Huko kunaondoa uhalali wa $ 193 Bilioni tulizodai. Unaweka rekodi yetu vibaya mbele ya dunia. Kwamba, siku tukisema Barrick wanatuibia dunia itasema ''ndiyo zao hizo''
Wanatunga namba kama ilivyokuwa kwa Acacia

Kumbe tungeacha isingtuathiri kwani Acacia walishafanya yao siku nyingi kwa ujinga wetu

Umenielewa?

Umeeweleka vizuri, kwa kile utachotaka kukisema. Ila you are wrong. Acacia, Barrick, Escrow, ni udhaifu wa serikali iliyopita, zilizopita.

Magufuli anaweka misingi ya uwajibikaji. Kuhoji, umakini, kufanya vitu haraka. (Tatizo ana haraka sana, kuchangisha anataka hapo hapo, ila ni bora kuliko wapiga dili).

Kufanya record yetu iwe nzuri duniani, ni jambo jema au baya?

Wewe ungetaka kupata kiasi gani? kwa masharti gani kutoka Barrick? Zingatia soon they ll be the biģgest company in mining industry. Mdau muhimu.

Magufuli anawaambia hii ni Tanzania mpya. No messing about, Tumpinge hata kwa hili?
 
Wewe ungepata deal gani? Nzuri zaidi?

Kwahiyo unasema tungekataa deals zote, Wewe unaweza kufanya deal zote za Tanzania. Kukataa deal zote.

Tutapata wapi pesa kuwasaidia wananchi wetu.
Man, ni vile tu mashabiki wa CCM na Magufuli wanaleta siasa kwenye serious issues na ndio maana hapa unaona wanatamba kwamba eti Tundu Lissu hivi, Tundu Lissu vile! Amini usiamini, ungefuatwa ushauri wa TL tungepata pakubwa zaidi kuliko ilivyo! Ushauri wa TL ingawaje watu waliupotosha ilikuwa kama tunataka kuwabana hawa jamaa lazima kwanza tujitoe MiGA ili wasiwe na kwa kukimbilia! Hizi dana dana mara hivi, mara vile na kwavile wanajua wana mbadala! Nashangaa kusikia watu wanakejeli mbona hawaendi basi huko MiGA! Sasa waende MiGa wakafanye nini? Mwaka wa 3 huu sasa, tunapita huku, tunatokea kule na hawajatoa hata senti 5 halafu watu wanakejeli mbona hawaendi basi huko MIGA! Suala la Barrick kuchukua shares za Acaccia sio hoja kwa sababu wao kuchukua shares haimaanishi ndo basi tena hivi sasa kila kitu kitakuwa level! Barrick na Acacia ni wale wale, and all this time the guys were playing delaying techniques! Na wanafanya yote haya kwa sababu wanajua tukivuka mipaka wanapo pa kukimbilia; huko huko MIGA ambako watu wanakejeli! Na kuzihofia hizo hizo MIGA ndio maana unakuta JPM anakuwa mpole!

Lissu alisema kwamba hawa jamaa ukitaka kuwabana ni lazima ukate matawi wanayoshikilia wanapotaka kudondoka, na matawi hayo ni kwa Tanzania kujitoa MIGA hata kama tungeshambuliwa! Mataifa yote yaliyotaka kupambana na hawa watu walikuwa wanajitoa kwanza MIGA kwa sababu MIGA inawabeba sana Investors. Na Lissu akaendelea kwamba, tukiwafanyia roho mbaya, hawa jamaa watatushitaki! Hapa Team Magufuli ndo wameshindwa kuelewa! Si kwamba Acacia wangetupeleka MIGA bali endapo tungewafanyia umafia kwenye kudai chetu wangetupeleka MIGA! Kwa mfano, tungewaambia mmetuibia sana, but now enough is enough! So, either lipeni pesa zetu or pack your bags ONLY and GO! Kwa maana nyingine kutaifisha mgodi na assets zao! Au tungeamua kupiga mnada assets zao including migodi! Hapo jamaa lazima wangeenda MIGA na huko tungeshindwa tu! Lakini kama unajitoa kwanza, ukitaifisha hawana kwa kwenda kulia lia zaidi ya kwenye mahakama zetu wenyewe!

Kwahiyo kama alivyosema Pascal Mayalla hapo juu kwamba "Kwa kuanzia tutalipwa dola milioni 300 zilizokuwa ni kishika uchumba, lakini sasa sio kishika uchumba tena bali ni kifuta machozi cha kusamehe lile deni kubwa la kodi la dola bilioni 190" And trust me, wala tusitarajie hiyo USD 300 kulipwa kwa mkupuo mmoja! Na wala hawaitangia mfukoni mwao kulipa hiyo USD 300M. Isitoshe wataitumia hiyo USD 300M kama fimbo ya kutulazimisha makinikia yaruhusiwe kusafirishwa! Yakiruhusiwa, hiyo USD 300M itatoka hapo hapo kwenye makinikia na hata pesa ya kufidia gharama za shares za Acacia's minority shareholders zitatoka hapo hapo kwenye makinikia! Makinikia ambayo, endapo tungeanza kujitoa MIGA, tungekuwa na uwezo wa kuyataifisha na kuyafanya yetu au kuyapiga mnada lakini hivi sasa ubavu huo hatuna, na tukifanya hivyo, jamaa wanaenda MIGA ambako watu kwa kutojua tu wanakejeli! Na huko lazima watushinde tu!

So, ingawaje watu wanafunga vibwebwe lakini kimsingi Barrick 3, Tanzania 1. Sio Barrick wala Accacia aliyeumia kwa uamuzi huu! Wangeumia endapo tungetaifisha, na ubavu huo HATUNA! Lakini kubwa zaidi, hata kama sio kujitoa MIGA, Magu angeshughulikia hili suala in a smart way na sio kama alivyoshughulikia, ambapo hata kama ni kwa mahakama za Tanzania, labda Jaji awe Magu, wazee wa baraza wawe akina Bashite ndipo madai yetu yangeonekana relevant!
 
Umeeweleka vizuri, kwa kile utachotaka kukisema. Ila you are wrong. Acacia, Barrick, Escrow, ni udhaifu wa serikali iliyopita, zilizopita.

Magufuli anaweka misingi ya uwajibikaji. Kuhoji, umakini, kufanya vitu haraka. (Tatizo ana haraka sana, kuchangisha anataka hapo hapo, ila ni bora kuliko wapiga dili).
Yaani kabisa huoni tatizo la JPM Administration katika kushughulikia hili suala?! Wallah Watanzania tutakuwa tumerogwa!

Labda nikuulize swali moja! Ripoti ya Pili inasema Acacia tunawadai USD 190 Billion! Hivi unaamini kuna mahakama yoyote huru duniani inayoweza kuamua in favor of Tanzania kama tunashitaki kutolipwa USD 190 Billioni zetu?! Na kama unaamini, kwa grounds zipi?!

Halafu unasema Acacia, Barrick, Escrow ni udhaifu wa serikali zilizopita! Hivi unaamini kabisa kwamba kampuni iliyokuwa inaiba Tanzania hii angalau kwenye sekta ya madini ni Acacia peke yake?! Yaani unataka kutuambia wengine wooooooote ni malaika, isipokuwa Acacia? Deep inside your heart, unaamini hicho kitu kwamba akina Geita Mine wote walikuwa wanatulipa tunavyostahiki!!
 
Man, ni vile tu mashabiki wa CCM na Magufuli wanaleta siasa kwenye serious issues na ndio maana hapa unaona wanatamba kwamba eti Tundu Lissu hivi, Tundu Lissu vile! Amini usiamini, ungefuatwa ushauri wa TL tungepata pakubwa zaidi kuliko ilivyo! Ushauri wa TL ingawaje watu waliupotosha ilikuwa kama tunataka kuwabana hawa jamaa lazima kwanza tujitoe MiGA ili wasiwe na kwa kukimbilia! Hizi dana dana mara hivi, mara vile na kwavile wanajua wana mbadala! Nashangaa kusikia watu wanakejeli mbona hawaendi basi huko MiGA! Sasa waende MiGa wakafanye nini? Mwaka wa 3 huu sasa, tunapita huku, tunatokea kule na hawajatoa hata senti 5 halafu watu wanakejeli mbona hawaendi basi huko MIGA! Suala la Barrick kuchukua shares za Acaccia sio hoja kwa sababu wao kuchukua shares haimaanishi ndo basi tena hivi sasa kila kitu kitakuwa level! Barrick na Acacia ni wale wale, and all this time the guys were playing delaying techniques! Na wanafanya yote haya kwa sababu wanajua tukivuka mipaka wanapo pa kukimbilia; huko huko MIGA ambako watu wanakejeli! Na kuzihofia hizo hizo MIGA ndio maana unakuta JPM anakuwa mpole!

Lissu alisema kwamba hawa jamaa ukitaka kuwabana ni lazima ukate matawi wanayoshikilia wanapotaka kudondoka, na matawi hayo ni kwa Tanzania kujitoa MIGA hata kama tungeshambuliwa! Mataifa yote yaliyotaka kupambana na hawa watu walikuwa wanajitoa kwanza MIGA kwa sababu MIGA inawabeba sana Investors. Na Lissu akaendelea kwamba, tukiwafanyia roho mbaya, hawa jamaa watatushitaki! Hapa Team Magufuli ndo wameshindwa kuelewa! Si kwamba Acacia wangetupeleka MIGA bali endapo tungewafanyia umafia kwenye kudai chetu wangetupeleka MIGA! Kwa mfano, tungewaambia mmetuibia sana, but now enough is enough! So, either lipeni pesa zetu or pack your bags ONLY and GO! Kwa maana nyingine kutaifisha mgodi na assets zao! Au tungeamua kupiga mnada assets zao including migodi! Hapo jamaa lazima wangeenda MIGA na huko tungeshindwa tu! Lakini kama unajitoa kwanza, ukitaifisha hawana kwa kwenda kulia lia zaidi ya kwenye mahakama zetu wenyewe!

Kwahiyo kama alivyosema Pascal Mayalla hapo juu kwamba "Kwa kuanzia tutalipwa dola milioni 300 zilizokuwa ni kishika uchumba, lakini sasa sio kishika uchumba tena bali ni kifuta machozi cha kusamehe lile deni kubwa la kodi la dola bilioni 190" And trust me, wala tusitarajie hiyo USD 300 kulipwa kwa mkupuo mmoja! Na wala hawaitangia mfukoni mwao kulipa hiyo USD 300M. Isitoshe wataitumia hiyo USD 300M kama fimbo ya kutulazimisha makinikia yaruhusiwe kusafirishwa! Yakiruhusiwa, hiyo USD 300M itatoka hapo hapo kwenye makinikia na hata pesa ya kufidia gharama za shares za Acacia's minority shareholders zitatoka hapo hapo kwenye makinikia! Makinikia ambayo, endapo tungeanza kujitoa MIGA, tungekuwa na uwezo wa kuyataifisha na kuyafanya yetu au kuyapiga mnada lakini hivi sasa ubavu huo hatuna, na tukifanya hivyo, jamaa wanaenda MIGA ambako watu kwa kutojua tu wanakejeli! Na huko lazima watushinde tu!

So, ingawaje watu wanafunga vibwebwe lakini kimsingi Barrick 3, Tanzania 1. Sio Barrick wala Accacia aliyeumia kwa uamuzi huu! Wangeumia endapo tungetaifisha, na ubavu huo HATUNA!

Dunia ilivyo ndivyo ilivyo. Tukiweza tubadili sheria, unajua maana ya kujitoa MIGA, kuhusu biashara ya madini? Tutadili na wahuni tu.

Iko hivi. Tanzania ni iwe na masoko ya ndani ya kutosha, watu waje wapangishe hotels, wale chakula, wapande taxi, wafanye utalii, wazunguke kidogo. Wanunue Tanzanite, dhahabu, almas, madini ya aina yote. Pesa itazunguzuka.
 
Umeeweleka vizuri, kwa kile utachotaka kukisema. Ila you are wrong. Acacia, Barrick, Escrow, ni udhaifu wa serikali iliyopita, zilizopita.

Magufuli anaweka misingi ya uwajibikaji. Kuhoji, umakini, kufanya vitu haraka. (Tatizo ana haraka sana, kuchangisha anataka hapo hapo, ila ni bora kuliko wapiga dili).

Kufanya record yetu iwe nzuri duniani, ni jambo jema au baya?

Wewe ungetaka kupata kiasi gani? kwa masharti gani?
Mimi nikiwa mtaalam kwenye sekta hii, nikiwa naifahamu vizuri migodi karibu yote ya Barrick ya Tanzania na sehemu nyingine Duniani, sioni mahali popote ambapo utasema serikali imefanya chochote kikubwa cha maana kwenye madini, iwe ni katika kuongeza mapato kwa serikali au hata kuboresha sekta yenyewe.

Kwanza imeshindwa kuthibitisha kuwa tulikuwa tunaibiwa. Dola milioni 300 tumeomba tupewe kama msaada, na tutakayopewa ni milioni 120 tu kwa sababu dola milioni 180 serikali ilikuwa inadaiwa na Acacia.

Serikali iliwadanganya watu kuwa tulikuwa tunaidia Acacia dola bilioni 190, tukaonekana na Dunia nzima kuwa ni Nchi ya Wajinga, kilichokuja kudhihirika ni kuwa Serikali haiidai chochote Acacia bali yenyewe ndiyo inayodaiwa dola milioni 180.

Katika mapato yajayo ndiyo tumeshindwa zaidi. Uchimbaji Bulyanhulu umesimamishwa moja kwa moja, sasa wanafanya treatment ya tailings tu. Wakimaliza ndiyo mwisho. Na siyo rahisi kumpata mwekezaji mwingine kuendesha mgodi huo ulio kilometa 2 chini ya ardhi kwa sasa, ukihitaji teknolojia ya juu na ya pekee, ambayo hatuna, na wala hategemewi mchina yeyote kugusa pale.

Buzwagi hakuna uchimbaji. Wanafanya processing ya stockpile ya ore, baada ya hapo mgodi unafungwa.

Tulawaka umekwishafungwa.

Processing ya ore concentrate Bulyanhulu na Buzwagi, imefutwa. North Mara - Gokona underground umekwishawarudishia Acacia capital investment yao na faida, na hawana pressure hata ukifungwa japo bado production ni nzuri sana.

Barrick na Acacia wamefanikiwa kwa 100% kwenye ground, kama walivyokuwa wamepanga. In today's business, the most profitable business is selling trust. Barrick waliitereresha trust ya investors kutokana na kuwa na matatizo na serikali ya Tanzania, sasa wameirudisha, na hisa zitapanda sana lakini kwa bahati mbaya serikali haitaweza kufaidika na trust business because it is not trading in that. Wanategemea zaidi commodity business.

Serikali ilichofanikiwa sana kwenye hili ni kutengeneza political popularity, hasa miongoni mwa watu wenye uelewa mdogo kwenye sekta hii na biashara za kimataifa kwa ujumla.

Serikali pia imefanikiwa katika moral satisfaction. Kuna namba nzuri kwenye makaratasi hata kama kwenye uhalisia, mapato yameshuka na yataendelea kushuka. Hata ukaongeza kodi maradufu, wakati wazalishaji wanafunga, kodi hizo zitaongeza nini?

Kutokana na kodi kuongezeka zaidi, all marginal projects will never get developed, na cutoff grades kwenye migodi yote zimebadilishwa, na hivyo kusababisha ile ore ambayo mara ya kwanza ingeweza kuchimbwa, sasa itaachwa ardhini.

Serikali ilihitaji sana ushauri wa wataalam kuliko kumtegemea Kabudi pekee yake ambaye kwa sasa, kwa kiasi kikubwa amekuwa na mchango wa pekee katika kuua sekta ya madini kwa kupitia ile sheria yake mpya.
 
Hi hivi mkuu, Barrick wakifikia muafaka na serikali ya JMT, assets zao zita double, probably triple in value.

Wawekezaji watafurahi sana. Hizi assets hazipatikana kila sehemu duniani.

How stock markets works, i know it for over 15 years.
Sasa kama unajua for over 15 years basi usingeona ni issue kwa sababu hiyo ni taarifa tu! Kwamba wakifikia muafaka na serikali, muafaka upi?! Kama wa kulipa USD 190, hilo halitatokea na likitokea, Investors watakimbia kwa sababu hakuna atakayekubali kuweka pesa kwenye kampuni inayodaiwa zaidi ya mara 50 ya Market Cap yake yenyewe! That being said, suala la kwamba assets zake zita-double au ku-tripple; HAIWEZEKANI!

Na hizo assets unazosema hazipatikani kila sehemu duniani ni assets zipi?! Hivi Kiongozi unafahamu kwamba Barrick Gold inaundwa na kampuni takribani 7 including Acacia; na Acacia sio top gold producer within Barrick?
 
Yaani kabisa huoni tatizo la JPM Administration katika kushughulikia hili suala?! Wallah Watanzania tutakuwa tumerogwa!

Labda nikuulize swali moja! Ripoti ya Pili inasema Acacia tunawadai USD 190 Billion! Hivi unaamini kuna mahakama yoyote huru duniani inayoweza kuamua in favor of Tanzania kama tunashitaki kutolipwa USD 190 Billioni zetu?! Na kama unaamini, kwa grounds zipi?!

Halafu unasema Acacia, Barrick, Escrow ni udhaifu wa serikali zilizopita! Hivi unaamini kabisa kwamba kampuni iliyokuwa inaiba Tanzania hii angalau kwenye sekta ya madini ni Acacia peke yake?! Yaani unataka kutuambia wengine wooooooote ni malaika, isipokuwa Acacia? Deep inside your heart, unaamini hicho kitu kwamba akina Geita Mine wote walikuwa wanatulipa tunavyostahiki!!

Mkuu naona unaweweseka kidogo. Obvious Acacia, Barrick hawawezi kulipa 190 bn USD. Nimekwambia ni negotiation tactics in order to get the best deal possible.

Hatujawahi kulipwa our fair share, stahiki zetu. Wengi walikuwa wapigaji ndani ya serikali, CCM.

This is game changer, send out the message, we are in different era. This is what Magufuli is doing, at least try, trying to do.

Kwa sekta zote Tanzania.
 
Dunia ilivyo ndivyo ilivyo. Tukiweza tubadili sheria, unajua maana ya kujitoa MIGA, kuhusu biashara ya madini? Tutadili na wahuni tu.

Iko hivi. Tanzania ni iwe na masoko ya ndani ya kutosha, watu waje wapangishe hotels, wale chakula, wapande taxi, wafanye utalii, wazunguke kidogo. Wanunue Tanzanite, dhahabu, almas, madini ya aina yote. Pesa itazunguzuka.
No any business in Tanzania is worth USD 190 Billion! Unganisha kampuni zoooooooote, za ndani na nje zilizopo Tanzania lakini bado TOTAL ASSETS zake hazitafika hata robo ya hiyo USD 190 Billion! Sasa kama kujitoa kunaweza kuleta USD 190 Billion zetu, who cares hayo mengine?! Au kwavile unajua suala la kudai USD 190 Billion ni KIROJA cha Kamati ya Mrosso?!

Na kujitoa MIGA haimaanishi kwamba foreign companies hazitakuja tena Tanzania bali zitakuja at their own risk kwa sababu hapatakuwa na "independent" body ya kuweza kuwatetea in case of anything, lakini pia haimaanishi hazitatetewa moja kwa moja kwa sababu bado watakuwa na option ya kupeleka malalamiko yao kwenye mahakama zetu!

Kama mahakama zetu unaamini zipo huru, kwanini waogope kuja kwa sababu tu hatupo MIGA?! Lakini kubwa zaidi, kujitoa MIGA ni technique tu ya kuwatisha wezi aina ya Acacia! Jeuri ya Acacia yote ni kwa sababu walijua wana pa kukimbilia!
 
Mimi nikiwa mtaalam kwenye sekta hii, nikiwa naifahamu vizuri migodi karibu yote ya Barrick ya Tanzania na sehemu nyingine Duniani, sioni mahali popote ambapo utasema serikali imefanya chochote kikubwa cha maana kwenye madini, iwe ni katika kuongeza mapato kwa serikali au hata kuboresha sekta yenyewe.

Kwanza imeshindwa kuthibitisha kuwa tulikuwa tunaibiwa. Dola milioni 300 tumeomba tupewe kama msaada, na tutakayopewa ni milioni 120 tu kwa sababu dola milioni 180 serikali ilikuwa inadaiwa na Acacia.

Serikali iliwadanganya watu kuwa tulikuwa tunaidia Acacia dola bilioni 190, tukaonekana na Dunia nzima kuwa ni Nchi ya Wajinga, kilichokuja kudhihirika ni kuwa Serikali haiidai chochote Acacia bali yenyewe ndiyo inayodaiwa dola milioni 180.

Katika mapato yajayo ndiyo tumeshindwa zaidi. Uchimbaji Bulyanhulu umesimamishwa moja kwa moja, sasa wanafanya treatment ya tailings tu. Wakimaliza ndiyo mwisho. Na siyo rahisi kumpata mwekezaji mwingine kuendesha mgodi huo ulio kilometa 2 chini ya ardhi kwa sasa, ukihitaji teknolojia ya juu na ya pekee, ambayo hatuna, na wala hategemewi mchina yeyote kugusa pale.

Buzwagi hakuna uchimbaji. Wanafanya processing ya stockpile ya ore, baada ya hapo mgodi unafungwa.

Tulawaka umekwishafungwa.

Processing ya ore concentrate Bulyanhulu na Buzwagi, imefutwa. North Mara - Gokona underground umekwishawarudishia Acacia capital investment yao na faida, na hawana pressure hata ukifungwa japo bado production ni nzuri sana.

Barrick na Acacia wamefanikiwa kwa 100% kwenye ground, kama walivyokuwa wamepanga. In today's business, the most profitable business is selling trust. Barrick waliitereresha trust ya investors kutokana na kuwa na matatizo na serikali ya Tanzania, sasa wameirudisha, na hisa zitapanda sana lakini kwa bahati mbaya serikali haitaweza kufaidika na trust business because it is not trading in that. Wanategemea zaidi commodity business.

Serikali ilichofanikiwa sana kwenye hili ni kutengeneza political popularity, hasa miongoni mwa watu wenye uelewa mdogo kwenye sekta hii na biashara za kimataifa kwa ujumla.

Serikali pia imefanikiwa katika moral satisfaction. Kuna namba nzuri kwenye makaratasi hata kama kwenye uhalisia, mapato yameshuka na yataendelea kushuka. Hata ukaongeza kodi maradufu, wakati wazalishaji wanafunga, kodi hizo zitaongeza nini?

Kutokana na kodi kuongezeka zaidi, all marginal projects will never get developed, na cutoff grades kwenye migodi yote zimebadilishwa, na hivyo kusababisha ile ore ambayo mara ya kwanza ingeweza kuchimbwa, sasa itaachwa ardhini.

Serikali ilihitaji sana ushauri wa wataalam kuliko kumtegemea Kabudi pekee yake ambaye kwa sasa, kwa kiasi kikubwa amekuwa na mchango wa pekee katika kuua sekta ya madini kwa kupitia ile sheria yake mpya.

Nyie watalaamu mchangie. Msiyumbishwe. Mawazo yenu yanaweza kusikilizwa, kutosisikizwa. Ila tuone mchango wenu, omba kuongea na wizara, waziri husika.
 
Mkuu naona unaweweseka kidogo. Obvious Acacia, Barrick hawawezi kulipa 190 bn USD. Nimekwambia ni negotiation tactics in order to get the best deal possible.

Hatujawahi kulipwa our fair share, stahiki zetu. Wengi walikuwa wapigaji ndani ya serikali, CCM.

This is game changer, send out the message, we are in different era. This is what Magufuli is doing, at least try, trying to do.

Kwa sekta zote Tanzania.
Our best deals zipi zaidi ya USD 300M?! Mengine yote yapo kisheria and have nothing to do with negotiation. Kwa mfano, 16% ipo kwenye sheria iliyotungwa mwaka jana, kwahiyo hakuna cha negotiotion hapo! 50/50 tayari imeshaafikiwa! Suala la kodi na mrahaba lipo kisheria! Sasa hiyo negotiation technique ni kwa ajili ya kupata nini kama sio USD190 Billion na ile USD 300M?! Na kama nilivyosema, Acacia hawatalipa hiyo USD 300M bila Magu kuruhusu makinikia kusafirishwa! Na kama ni kulipa b4, basi ni just a small portion kuonesha willingness to pay huku large portion ikisubiria kuhakikishiwa kusafirisha makinikia!!
 
Wanabodi wengine ni wa ajabu sana, mtoto kakubali yaishe kwa baba yake na mvutano umekwisha sasa watu ndio wanafukua kaburi la siasa za MIGA.

Acadia na MIGA are now irrelevant topics,
waacheni Barrick na GoT waendelee na mpango kazi wao.
 
Nyie watalaamu mchangie. Msiyumbishwe. Mawazo yenu yanaweza kusikilizwa, kutosisikizwa. Ila tuone mchango wenu, omba kuongea na wizara, waziri husika.
Nyie watu huwa hamtaki kusikiliza maneno ya wataalamu bali mnapenda kusikiliza maneno ya wanasiasa!! Na kama alivyosema Bams, kwenye hii issue Barrick/Accacia ndio washindi!
 
Back
Top Bottom