Barrick yatangaza rasmi kifo cha Acacia!. Acacia yakubali rasmi kununuliwa baada ya Barrick kuongeza dau!

Barrick yatangaza rasmi kifo cha Acacia!. Acacia yakubali rasmi kununuliwa baada ya Barrick kuongeza dau!

Kwa kuanzia tutalipwa dola milioni 300 zilizokuwa ni kishika uchumba, lakini sasa sio kishika uchumba tena bali ni kifuta machozi cha kusamehe lile deni kubwa la kodi la dola bilioni 190.
Mbona huo msamaha ni mkubwa sana? Naufananisha na ule wa kuwafutia mashtaka baadhi ya watuhumiwa wa uhujumu uchumi
 
Kwa vip? Walichoshinda ni nini?

..wanailipa serekali usd 300 million badala ya usd 190 billion ambazo ripoti zilisema tunawadai.

..kiwango hicho ni sawa na 0.157 % ya deni lote.

..vilevile itachukua miaka 600+ kumaliza deni la 190 billion kwa malipo ya 300 million kila mwaka bila riba.

..Hii siyo mazingira ya win-win, bali ni WIN-LOSS.
 
JokaKuu, heshima yako mkuu. TRA sijui kuna watu wa aina gani. Hiyo kodi waliitoa wapi? Tatizo la kuokota okota watu wenye vyeti na kufikiri wamesoma. Kusoma ni Zaidi ya kuwa na vyeti,
 
..wanailipa serekali usd 300 million badala ya usd 190 billion ambazo ripoti zilisema tunawadai.

..kiwango hicho ni sawa na 0.157 % ya deni lote.

..vilevile itachukua miaka 600+ kumaliza deni la 190 billion kwa malipo ya 300 million kila mwaka bila riba.

..Hii siyo mazingira ya win-win, bali ni WIN-LOSS.

Mgombea wenu Ngoyai angekuwa Ikulu tungelipwa ngapi labda!
 
Mgombea wenu Ngoyai angekuwa Ikulu tungelipwa ngapi labda!

..hicho ni kisingizio tu.

..Ngoyai hayuko Ikulu.

..tuwahoji waliofikia makubaliano haya.

..toka usd 190 billion mpaka usd 300 million kuna tofauti kubwa sana.

..Is this win-win or win-loss?
 
..hicho ni kisingizio tu.

..Ngoyai hayuko Ikulu.

..tuwahoji waliofikia makubaliano haya.

..toka usd 190 billion mpaka usd 300 million kuna tofauti kubwa sana.

..Is this win-win or win-loss?
Nafahamu hayuko Ikulu, ndiyo maana nikauliza angekuwa Ikulu na timu yake ya kina Mwapachu tungelipwa kiasi gani mkuu?!
 
Wanabodi,
Hatimaye huu mtanange wa Acacia kununuliwa na Barrick, hatimaye umefika mwisho leo, kwa Barrick kutoa tangazo la kuinunua Acacia, na Acacia kutoa tango la kukubali kununuliwa na Barrick.

Tangazo la Barrick la Kifo cha Acacia ni Hili
PRESS RELEASES
Recommended Final Offer For Acacia Mining Plc By Barrick Gold Corporation – July 19, 2019

Tangazo la Acacia kukubali kununuliwa na Barrick ni hili

Hii maana yake ni
  1. Sasa mgogoro wa Acacia na serikali yetu, umemalizika rasmi kwa sababu sasa Acacia doesnt exist anymore.
  2. Migodi yote mitatu iliyokuwa chini ya Acacia, sasa itakuwa chini ya Barrick
  3. Yale makubaliano ya serikali yetu sasa yatatekelezwa.
  4. Kwa kuanzia tutalipwa dola milioni 300 zilizokuwa ni kishika uchumba, lakini sasa sio kishika uchumba tena bali ni kifuta machozi cha kusamehe lile deni kubwa la kodi la dola bilioni 190.
  5. Barrick ataunda kampuni mpya ya ubia na Tanzania kuchukuwa shughuli za Acacia
  6. Kwenye hiyo kampuni mpya, serikali ya Tanzania itakuwa na shares asilimia 16%.
  7. Bodi ya hiyo kampuni mpya itakuwa na Watanzania.
  8. Makao Makuu yatakuwa Tanzania
  9. Menejiment itakuwa na Watanzania.
  10. Tutagawana manufaa ya kiuchumi pasu kwa pasu, yaani 50/50.(NB.Manufaa ya kiuchumi ni economic benefits na sio faida profits)
Huu ndio utakuwa ushindi wa kwanza wa kishindo wa rais Magufuli na awamu ya Tano kwa kuanza rasmi utekelezaji wa kwanza wa sheria mpya ya madini.
Hongera Kabudi, Hongera Magufuli, Hongera Watanzania, ila kwenye makinikia, bado kuna lakini!.
Leo tupongezane kwanza, lakini tuzijadili baada ya kusainiwa makubaliano yenyewe!.
Paskali
Vipi kuhusu financial transactions?! Zitapitia kwenye benki zetu au?!
 
Mkuu Paskali kuna Nondo iko kwenye page ya FB ya ZITO KABWE, ni vyema ukaianzishia uzi hiyo nondo wadau waijadili hiyo nondo..

Ukiisoma hiyo nondo aisee ni aibu kifupi Barrick wametupiga kuanzia kwenye hizo dola milioni 300 mpaka kwenye 16% shares.. Yapo mengi sana mkuu kwenye hiyo nondo..

Kwa heshima yako kwenye ifuatiliaji wa suala hili nivyema ukaileta ile nondo jamvini ikawa na uzi wake bila mods kuunganisha ni kwa maslahi mapana ya nchi..ZZK ni hatari sana kwa kuchimba data kuliko wengi tunaomeza kama kasuku..
 
Madini tusteng yatasafirishwa kwa njia ya reli kwenda nje ya nchi, na makinikia kutoka tanzania kwenda rwanda na bidhaa mbalimbali kama makontena yaliyobeba mizigo ya rwanda.
Unaongea mambo kirahisi mno! Hayo madini tusteng itakayosafirishwa kwa reli ni madini tusteng ipi?! Na hayo makinikia yatakayotoka Tanzania kwenda Rwanda ni makinikia yapi na yanaenda Rwanda kufanya nini?
 
Mkuu Paskali kuna Nondo iko kwenye page ya FB ya ZITO KABWE, ni vyema ukaianzishia uzi hiyo nondo wadau waijadili hiyo nondo..
Ukiisoma hiyo nondo aisee ni aibu kifupi Barrick wametupiga kuanzia kwenye hizo dola milioni 300 mpaka kwenye 16% shares.. Yapo mengi sana mkuu kwenye hiyo nondo..
Kwa heshima yako kwenye ifuatiliaji wa suala hili nivyema ukaileta ile nondo jamvini ikawa na uzi wake bila mods kuunganisha ni kwa maslahi mapana ya nchi..ZZK ni hatari sana kwa kuchimba data kuliko wengi tunaomeza kama kasuku..
Na iletwe, ijadiliwe, ZZK naye aminia, wenye uwezo watapambana nayo...
 
Barick Gold imeungana na Rand Gold ya Africa kusini hivyo wataunda menejiment mpya na serikali itajichukulia 16% asilimia. Hivyo Acacia hatambuliki tena anaetambulika ni Rand Gold na Barick na ninadhani kisheria huwa huwa ubia ukiwepo hawachimbi wao bali inatengenezwa kampuni ya kuchimba kuweka Transparence.
Kwani hao Barrick na Rand Gold wameungana leo wakati waliungana tangia mwaka jana, na officially wapo pamoja tangia January! The problem hufahamu muundo wa Barrick! Barrick Gold ni kampuni mama, na ndani yake kuna kampuni takribani 7 including Acacia!
 
Bado mambo mengi ya kuchunguza hawa wazungu hawajawahi kuwa mazuzu. Yaani jiwe awe mshindi kwa wazi hivi. Lazima kuna maeneo tumepiga mpira nje tena mbali sana. Naingia kusoma taarifa ambazo nchi yetu imetuficha na bila kutangaza
 
Kwa vip? Walichoshinda ni nini?
Kwa sababu tunachoshangilia hakipo na hakiwezi kutokea! Kwanza zile USD 190Billion ndo zimekufa Kibudu! Kwenye moja ya posts zangu hapo juu nilisema kilichobaki kupata hapo ni zile USD 300M, na katu hawatalipa kwa mkupuo! Bahati mzuri, hatimae Zitto amelieleza hilo kwa undani zaidi kwamba kumbe tutalipwa kwa miaka 7, na sio tena USD 300M kwa sababu Acacia wanatudai!

Na kama nilivyosema awali, hata haya makubaliano yanai-favor zaidi Barrick kwa sababu, hata hiyo USD 300Million wataitumia kama fimbo ya kulazimisha serikali iachie makinikia ndipo ianze kulipa!

Sasa tukiachilia mbali haya aliyolete Zitto hivi sasa, huoni ni namna gani Barrick walivyoshinda? Tena watakuwa wameshinda huku waki-restore the company image!
 
Mkuu Paskali kuna Nondo iko kwenye page ya FB ya ZITO KABWE, ni vyema ukaianzishia uzi hiyo nondo wadau waijadili hiyo nondo..

Ukiisoma hiyo nondo aisee ni aibu kifupi Barrick wametupiga kuanzia kwenye hizo dola milioni 300 mpaka kwenye 16% shares.. Yapo mengi sana mkuu kwenye hiyo nondo..

Kwa heshima yako kwenye ifuatiliaji wa suala hili nivyema ukaileta ile nondo jamvini ikawa na uzi wake bila mods kuunganisha ni kwa maslahi mapana ya nchi..ZZK ni hatari sana kwa kuchimba data kuliko wengi tunaomeza kama kasuku..
Unajua ripoti aliyoiachambua Zitto kuna mtu alinipatia asubuhi ya leo! Nikaisoma nusu, nikaona itakuwa fake kwa sababu hata logo ya Acacia au Barrick hainayo! Niliona ni fake kwa sababu sikutaka kuamini nilichokuwa nasoma! Saa chache zilizopita nilipoenda tena kwenye website ya Acacia, nikaikuta kama ilivyo, na wala sio fake kama ambavyo nilidhani hapo kabla!
 
Mkuu Paskali kuna Nondo iko kwenye page ya FB ya ZITO KABWE, ni vyema ukaianzishia uzi hiyo nondo wadau waijadili hiyo nondo..

Ukiisoma hiyo nondo aisee ni aibu kifupi Barrick wametupiga kuanzia kwenye hizo dola milioni 300 mpaka kwenye 16% shares.. Yapo mengi sana mkuu kwenye hiyo nondo..

Kwa heshima yako kwenye ifuatiliaji wa suala hili nivyema ukaileta ile nondo jamvini ikawa na uzi wake bila mods kuunganisha ni kwa maslahi mapana ya nchi..ZZK ni hatari sana kwa kuchimba data kuliko wengi tunaomeza kama kasuku..
Aliona hizo nondo ila akaona aibu kuzileta hapa mtandaoni.
 
Back
Top Bottom