Paskali, Paskali, Paskali.
Wewe kama mwanafunzi wa Issa Gulamhussein Shivji, Profesa Nguli na Pan Aficanist wa kweli, unajua fika kuwa kilichokuwepo kati ya Acacia na Barrick ni mchezo wa dama wa kitoto.
Wajumbe wa Barrick kwenye Bodi ya Acacia ni asilimia 60, sasa hicho unachokiita sarakasi kinatoka wapi?
Barrick ndiye aliyetengeneza huu mchezo unaoitwa 'Acacia', ameucheza na kuibuka kidedea. Ataendelea kuvuna maliasili zetu, huku akinywa chai pale Magogoni, ndani ya Ikulu yetu.
Kizuri katika yote haya ni kwamba Rais Magufuli amesimama vyema na Act No. 7 of 2017, (Miscellaneous Amendment Act, 2017), ambayo kwa kiwango fulani, ambacho hakitoshi, (in my view) Nchi yetu Tanzania itanufaika, angalau, na rasilimali madini.
Ninachoeleza hapa ni kuwa hakukuwa na sakata la Barrick na Acacia, Bali lilikuwa sakata la Barrick na 'Barrick' kwa kuwa Acacia ni mali ya Barrick kwa asilimia zaidi ya sitini.