Barrick yatangaza rasmi kifo cha Acacia!. Acacia yakubali rasmi kununuliwa baada ya Barrick kuongeza dau!

Nimemsoma zito anasema moja ya masharti ya mkataba ni kufanya ''arbitration' na mahakama za kimataifa. Hii ni tofauti na sheria iliyolazimisha ''arbitration' kufanywa na mahakama za nyumbani

Barrick wapo sahihi, wanajua udhaifu wa nchi zinazoendelea. Wanajua Mahakama zetu si huru na kwamba shauri litaamuliwa kisiasa badala ya kisheria kwa mgongo wa ''Uzalendo''
Wamekataa na tumenywea a.k.a Kushindwa

Swali linalobaki kusumbua akili za watu ni, je ile sheria iliyokimbizwa usiku kwa njia za dharura ili 'arbitration'' zaifanywe hapa nchini itamhusu au husu shirika gani?

Yaani tutakuwa na sheria zinazohusu kampuni moja na kampuni nyingine tofauti

Tumeshindwa vibaya sana, na kisha kupokea kifuta machozi cha 0.157%! sad
 
Mkuu,haya masisiem vichwani ni zero kabisa!!

Wapinzani waliwaonya kuwa hiyo sheria haiwezekani wakabisha na sasa yametimia.
 
Mkuu Kuna tofauti Kati ya ""50/50 Profit Sharing na 50/50 Economic Benefits"". Tuwe na umakini kidogo kwenye issue hii.
Mbaya zaidi haijaelezewa vizuri kwa kina utakuwaje huo mgawanyo.
Mkuu ni kweli inatakiwa tuwe makini sana katika hili jambo.
Hoja zangu zote nimezijenga kulingana na uzi huu maana mleta uzi kasema kuwa profiti sharing itakuwa 50/50.

Nina maswali ya kumuuliza mleta uzi sema sasa sijajua ni nani maana nimesikia kuwa huu uzi umeunganishwa na uzi mwingine wa Pascal Mayalla

Pascal Mayalla hivi hii 50/50 ni profit sharing ama economic sharing maana hapa https://www.mining.com/barrick-tanzania-reach-proposal-settle-countrys-row-acacia/ naona wanasema ni economic sharing kutoka kwenye operations za Accacia
 
kama ndivyo ilivyo tumeumia. ngoja kwanza nitoke hapa kabisa maana hadi weekend yangu imeharibia
 

Watanzania wajuaji wanapata shida sana kwenye utawala huu. Kwanza kuwakolomea wawekezaji kama Barrick na kukaa nao mezani kuweka mambo sawa bila kuvurugwa, ni hatua kubwa inayohitaji kupongezwa. Tabia ya kuongeza upana wa magoli ni tabia ya watu walioshondwa.
Kampuni mpya itakayoundwa itakuwa na maslahi mapana kwetu na itabadili jinsi mining industry inavyofanya kazi Tanzania. Kuna graphite, cobalt, gold, copper na hata earth rare metals. Ili kuzivuna kama tutaendeleza ile mikataba kama ya Acacia, tutakuwa hatupati lolote.
Hili ni fundisho kuwa watanzania wako wengi na wana nguvu kuliko hao viongozi wachache wanaowauza kwa kutumia nafasi walizopewa kwenye nafasi za umma.
Hongera sana JPM kwa kuthubutu. Kuna kubwa waafrika watajifunza
 
Wameweka sawa mambo gani?! Nyofoa kipengele kimoja tu toka kwenye yale makubaliano kilochosema namna itakavyolipwa hiyo USD 190 Billion!
Kampuni mpya itakayoundwa itakuwa na maslahi mapana kwetu na itabadili jinsi mining industry inavyofanya kazi Tanzania.
Itabidili mining industry ki vipi?! Hivi umesoma ile ripoti au unaongea tu? Kwa mfano, hii issue chimbuko lake ni usafirishaji wa makinikia na si vinginevyo, na ndio maana kampuni zoooote ambazo hazizalishi makinikia yanayohitaji kusafirishwa, hazijaguswa!

Wakati issue imeanza kwenye kusafirisha makinikia na kuona wizi ndo unaanzia, makubaliano yanasema- Kumbe basi, ingawaje chanzo cha yote haya ni usafirishaji wa makinikia, makubaliano yanasema TMC itakuwa na UNFETTERED RIGHT TO EXPORT! What is Unfettered Right? Cambridge Dictionary wanasema "not limited by rules or any other controlling influence:" Mtandao wa Translegal una-define unfettered right kama "not influenced or limited by rules, regulations or any other outside influence. " there will be no obligation on the TMCs to construct beneficiation facilities in
country
"
Kuna graphite, cobalt, gold, copper na hata earth rare metals. Ili kuzivuna kama tutaendeleza ile mikataba kama ya Acacia, tutakuwa hatupati lolote.
Hizo rare metals utazipata vipi wakati makinikia itaendelea kusafirishwa nje?!
Hili ni fundisho kuwa watanzania wako wengi na wana nguvu kuliko hao viongozi wachache wanaowauza kwa kutumia nafasi walizopewa kwenye nafasi za umma.
Hongera sana JPM kwa kuthubutu. Kuna kubwa waafrika watajifunza
Mwakilishi mzuri wa Watanzania wengi manake mnachojua ni kushangilia tu bila kutafuta ukweli!
 
 


Kuna watu hawaoni kabisa kupata siti at a table 16% (maana yake watu kuangalia kila kitu kinachoendelea) kukaa nao kwenye meza kubwa. Kama jamaa aliyerudishwa TPDC, wenye exposure, waadilifu, waaminifu, wazalendo wa ukweli

50% of economic benefits sio haba hata kama zitajumuisha tozo zingine kama za barabara, royalty, capital gain tax local government taxes, import duties, skill development, bado ni big improvement ukilinganisha mikataba mingi ya madini iliyopita.

Hizi economics benefits inabidi ziwe defined vizuri, na labda kuwe na baseline. Otherwise zinaweza kuwa inflated, overestimated kupunguza pesa zinazoenda kwa JMT.

300M kwa miaka 7 ni kwa ajiri ya sustainability of the company ambapo sisi pia ni shareholders. Wakilipa zote ikafa kesho tutapata faida gani? Watalipa 100 Mn USD mwaka wa kwanza. Just over 33 kila mwaka baada ya hapo.

Faida zingine tutapata watu wetu serious management / business skills, engineers, wataalamu mbalimbali wataojua jinsi ya kusimamia migodi rasilimali zetu kwa huu wakati wetu wa wapigaji wengi wanaweza kupelekwa kwenye madini mengine kama Almas, Nishati makaa ya mawe,gas, solar, ,nuclearKilimo cha kisasa. Watu wetu watajifunza mengi.

Kwa miaka mitano, sita, 2009- 2015. Tembo walipungua kwa 60%. Wangekuwa wameisha leo. Simba, Twiga, Zebra ndege, miti, samaki, vilikuwa vinapotea kwa kasi ya ajabu. Mashamba, Ardhi yetu ilikuwa inauzwa kama njugu halafu wanaomba mikopo kupitia hizo asset, hawaziendelezi.

Sasa hapo si unaua utalii, uchumi, future ya Taifa, watoto wetu, vizazi vinavyokuja, Nchi.

Kulikuwa na viongozi hapo, usimimiaji wa rasilimia zetu uko wapi hapo?
.
 
Mambo mengine yanafurahisha sana, Unafurahia kuondoka kwa mbwa wakati mwenye mbwa bado yupo, akileta mbwa mwingine je.siku zote mbwa anatekeleza order za mmiliki wake.
 
Tueleze mchakato wa dividend ya 16% shares,

Hizo ndo issue za kujadili ili tujue tunanufaika au tunadanganywa na figure,

Karibu.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…