Barua kutoka chama cha wanaume wabahili

Barua kutoka chama cha wanaume wabahili

Chama chetu cha wanaume wabahili Tanzania ( chawawa)
Kinapenda kuwatangazia wanachama wake kuwa
Kesho kwetu sisi hakuna kitu kinachoitwa Valentine day .

Bali tutashinda tukiabudu kanisani na kusifu Muumba aliye juu.

Hii ikimaanisha mengi ikiwemo swala mtambuka la gharama na kufidia pesa za guest..
Kwani uchumi umebana

Mjulishe na mwenzio haraka upatapo ujumbe juu tuwaokoe wengine
Maana tumeskia koffi mopao atakuwepo huko dar .

Hivyo tunahofia wanachama wetu walioko huko kukiuka masharti ya chama ...

Imetolewa na makao makuu ya chama
Dodoma
Nikiwa stendi hapa mimi kama makamu mwenyekiti itifaki inazingatiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mr Slim tunaomba ufike ofisini na kadi ya chama kwa maelezo zaidi ili tuchunguze uhalisia wa tukio lilikuwaje
Nitafika mkuu, nipate hela ya mafuta hapa kwanza maana kuna ka hela kidogo nakasikilizia ninunulie wese
Ila kadi nilipoteza, nikaenda polisi kuchukua lost report wakataka nilipie, nikaona naingia kwenye jaribu la kukiuka miiko ya chama. ....hela ikaniuma nikaachana nao.
 
Kwa kuonyesha uchungu na kuendeleza sera ya KUNA HELA NAISIKILIZIA mpka kwa polisi😆😆 umekuwa huru
 
Kwa kuonyesha uchungu na kuendeleza sera ya KUNA HELA NAISIKILIZIA mpka kwa polisi😆😆 umekuwa huru
niliwasihi Sana waniandikie tu, sina pesa! Kuna hela naisikilizia ikiingia nitawafikiria, wakagoma mkuu nikaona isiwe shida nikaondoka lakini sio ku change 10,000/= langu
 
niliwasihi Sana waniandikie tu, sina pesa! Kuna hela naisikilizia ikiingia nitawafikiria, wakagoma mkuu nikaona isiwe shida nikaondoka lakini sio ku change 10,000/= langu
Najivunia kuwa na mwanachama kama wewe kwani unadumisha Sera yetu pendwa ya chama naunga mkono maamuzi ya ndugu katibu mkuu Mnyatiaji
 
Tunapenda kutoa taarifa kwa wanachama wote wa Umoja Wa Wanaume Bahili Tanzania (UWABATA).

Kuwa chama kipo imara na hadi sasa tumepokea taarifa mbalimbali kwa nchi nzima kuwa wanachama bado wapo ngangali kutimiza makubaliano ya kikao cha mwisho.

Hadi sasa kiasi kikubwa kilichotumika kwa wastani kwa kila Mwanachama ambaye atachakata papuchi leo ni shiling 750 tu.

Mchanganuo wa kiasi hicho nitauleta baadae.

Hivyo nasi uongozi wote unawatakiwa wanachama wote kuwa na shughuli njema huku mkiilinda katiba yetu ya UWABATA.

Msemaji wa Umoja Wa Wanaume Bahili Tanzania (UWABATA)
Nikiwa kama mwenyekiti naheshimu kazi yako ya ndugu msemaji bwana Kichwa Kichafu
 
Ada ilipwe kwa muda stahiki,au wajuba wanafanya ubahili hata kwenye ada? yaani ubahili unaanza sisi kwa sisi!!
Ndugu muweka hazina kwa sasa ni lazima uhamie makao makuu ya chama Dodoma kwani huku wajumbe wengi wameleta Sera yao mpka kwenye mambo muhimu ya ada kitu ambacho ni kinyume na katiba
 
Sisi ambao tukisema "I love you" tunajibiwa "Thank you" ratiba yetu ya leo hii hapa..

  1. Soton vs Wolves
  2. Westbrom vs Man united
  3. Arsenal vs Leeds
  4. Everton vs Fulham.
Game nzuri, nataka nikaangalie sehemu na wana sema nimekwama dukani kwa Mangi lisaa la pili sasa, namdai chenji yangu Tsh 100/= ,sasa hana na siwezi iacha mpaka aipate, bora nichelewe kuangalia mechi
 
Game nzuri, nataka nikaangalie sehemu na wana sema nimekwama dukani kwa Mangi lisaa la pili sasa, namdai chenji yangu Tsh 100/= ,sasa hana na siwezi iacha mpaka aipate, bora nichelewe kuangalia mechi
Ndugu mjumbe wewe kwa sasa utakuwa kitengo cha propaganda za kueneza chama kwani unafanya kazi ipasavyo

Nikiwa kama mwenyekiti Leo asubuhi nilinunua vitumbua kwa mama sikitu na namdai shng hamsinj mpka sasa sijaondoka nasubir chenchi na vitumbua mkononi
Kidumu chama
 
Nimepokea kwa mikono miwili huu wadhifa Ndugu.
Hiyo hamsini, usiondoke mpaka amekupa mkuu. Hela ngumu sana, usituangushe
 
Pia mwanachama wetu mmoja anakaribia kuvunja itifaki kwani nimepokea malalamiko Leo asubuhi

Anataka kufunga ndoa hivyo amepanga kupeleka mahari shilingi 5000 na kiroba cha matikiti
Kitu ambacho ni kinyume na matakwa na katiba ya chama kwani ni vitu Vinci sana alipaswa kupeleka matembele ya 300 kisha apewe mkewe ..

Naomba swala hill ndugu ushughulikie kesho kwani kama mwenyekiti Nina majukumu mengi Mnyatiaji
 
Back
Top Bottom