Mwiyuzi;
Mtu angekwambia huyo Flora niliwahi kumwona siku 3 tu alipokuja kwenye mkutano tuliokuwa tumeuandaa utashangaa. Huyo Mbasha hata kumtia machoni hivi sijawahi.
Hapa niko kiroho zaidi kuliko kimwili. Mbasha ameamua kumvua Roho akapambana kimwili. Bila Roho wa Mungu, hutashinda. Anajitapa kuwa atashinda, yetu yawe macho, atazidi kujiaibisha mpaka aogope kwenda uani kujisaidia. Usijaribu kumpinga shetani kimwili. Lakini kwa kuwa tayari alishauacha wokovu na kujiona kuwa yeye ni yeye kama mwanamume, kitu ambacho nadhani ni porojo tuu, amrudie Mungu na kumlilia kwa dhati. Mungu amsamehe na kumpigania.
Mwiyuzi, mimi si lolote wala chochote katika utumishi, lakini, ukiisha fikia mahali pa kumwita mtumishi yeyote wa Mungu ukamwita kuwa ni Shetani, weye utakuwa una tatizo. Mwambie Mbasha kwamba, kama ni ushetani yeye ndo ameuanza. Kuchapiwa mke, hakukupi nafasi ya kuja kumwanika humu JF tena kwa mijitusi ya wazi.
Neno la Mungu linasema; Maneno yenu yakolee munyu. Mdomo wa Mbasha umekwisha munyu. Sijui utatiwa nini tena hata ukolee.
Mnaomshabikia, mnamharibu zaidi. Mfundisheni amwamini Mungu wa kweli ili ampiganie. Atumie muda wake zaidi kumwomba Mungu aihuishe tena ndoa yake. Wapo wenzako wanaodhani kuwa haiwezekani, No no nooo. Kwa mwanadamu hiyo haiwezekani bali kwa Mungu, yoooote yawezekana. Tena watapendana sana na kuilea hiyo familia anayo ililia.
Asiwatukane watumishi wa Mungu na kuidharau miujiza na kuiita ati ni mazingaombwe. Kama hiyo ni mazingaombwe tu yakamnyang'anya mke na watoto, tena yanataka kumtia ndani Segerea akanyee ndoo mvua 30 kwa kama mbakaji; basi sitaki kuiona miujiza kwani itamhamisha dunia hii. Someni taratibu huu uzi, simkingii kifua Flora wala huyo mliyemwona kuwa mwanamazingaombwe. Mimi nawaona kama watu walio kengeuka na kwangu zaidi sana ni huyo Mbasha. Moto woote anauwasha yeye.
Usiniite Flora, miye ni kidume na nina mke mmoja na wajukuu tele. Ni mawazo yangu tuuu