Barua kutoka kwa mume wa Florah Mbasha kwenda kwa mchungaji Gwajima

Barua kutoka kwa mume wa Florah Mbasha kwenda kwa mchungaji Gwajima

Flora sijui kama Ni member WA jamiiforums ILA nitoe ushauri WA bure kwako, kwa na mumeo muyamalize hata kama Ni kupeana talaka mpeane kwa amani kulinda heshima zenu, vinginevyo sitashangaa Flora ukiimba taarab ndani ya muda mfupi ujao kwani hakuna atayesiiliza nyimbo zako za injili tena.....sisemi kama wewe ndiye kwenye kosa ILA ninachojua ukikosea ku'handle' hizi issue za ndoa kwa hekima na busara hasa wewe mwanamke mwenzangu madhara yake Ni mabaya Sana......hasa kwako Flora....kufuta mfumo dume Ni kazi Sana....through experience women are always victims...tumia busara mdogo wangu hata mambo myamalize wenyewe kwa usalama.......
Nilishawahi kuandika katika uzi mmoja humu, naomba nirudie tena: Mwanadamu anayeweza kuinusuru huduma ya nyimbo ya flora hasa ya majukwaani, ni Imma tu. Flora hawezi tena kupanda jukwaani bila imma akitegemea kuimba bila kuhojiwa na mashabiki; 'Imma yuko wapi?'
 
ifike hatua serikali iweke utaratibu wa kuanzisha kanisa kwani siku hizi mtu akilala na mke wake wanashauliana ujinga kesho mtu anaanzisha kanisa, hawa akina gwajima huu ujasiri wameupata wapi, na kweli ndoa nyingi zimevunjika lisa huu ulokole, famila nyingi zimekuwa maskini kisa huu ulokole...serikali ingilia kati okoa jahazi
 
Kweli Emanuel Mbasha umekwisha kabisa kabisa. Unadhani kuanika nguo zako za ndani kwenye kioo cha dala dala ndio zitakauka upesi? Huo sio msaada bali wajiletea aibu juu ya kichwa chako mwenyewe. Yupo muimbaji mmoja wa Bongo fleva aliimba akasema "Kuchapiwa ni siri ya ndani" weye sio wa kwanza kunyang'anywa mke.
Malalamiko yako kuwa ukifungwa watoto watapata taabu hayo ni mawazo finyu saana. Kulalamika kwako kuwa Flora kaupata utajiri wa haraka nayo yaonesha ulivyoshindwa kumtunza wenzako wakaonesha kuwa hukumstahili. Ulikuwa unamvua nguo bureee ati ni mali yako, wenzako wakamfungua macho kuwa anastahili kutuzwa, kila siku anapewa mamilioni. Weye unapoenda kuchunguza ati zimetoka wapi, nani kazideposit ni ili iweje?
Emanuel, usipojiangalia, siku si nyingi utaokota makopo. Wadhani unapambana na Gwajima kumbe wajitia wendawazimu mwenyewe.
Ushauri wangu; Mwachie Mungu yule uliyesema alikuokoa. Yeye ndiye atakupa uwezo wa kumsahau Flora na maisha yataenda mbele tuu. Si lazima ule jasho la mkeo. Jitafutie taratibu, utapata tu kwani rizki hugawa na Mungu si Gwajima wala Flora.
Huoni ajabu, wote wawili wamekudharau wala hakuna anaye bishana na weye humu JF?? Pole Bro. Angalia mbele, mlilie huyo shem, akuhurumie tuuu usiende Segerea. Ninavyomfaham yule ni mama huruma tu ukimtumia ujumbe mzuri, atakusamehe na kesi itafutwa.
Kama miye ni weye, huo ukoo ningeusahau kabisa mpaka hata mkoa wao nisingelifika huko tena. Kwa heri acha kulalama humu JF unajiaibisha sana. Yaonesha bila Flora hata ch.oo huendi
Kuna watu mna roho mbaya dah..!!
 
Emmanuel Mbasha. Mungu atakushindia. Mungu atapigana nao na mashimo waliokuchimbia wataanguka wao. Soma Zab: 35 na zab: 140. Pia kumb. 28:13. Ndiyo maana nashauri wakristo wote msibabaike na haya makanisa wanaita eti ya kiroho. Ni upuuzi mtupu. Bakini makanisa yenu ya asili ila kama unapenda semina za hawa watu nenda tu maana zinatumia biblia. Mimi nahudhuria sana semina za baadhi ya watumishi ila kanisani kwangu sitoki. TB Joshua anasema unaomba ndani ya kanisa lako cha msingi simamia neno la Mungu.
 
Mwandishi unafaa kuandika riwaya za magazeti safi sana
 
Inauma sana ninevaa viatu vya mbasha dah....sina lakuongeza ila gwajima Hauta uona Ufalme wa mungu km kweli unahusika
 
bongolala unge acknowledge source bold mbona keshatuwekea hii kitu siku mingi
 
Wewe ni Flora au ndugu wa upande wa akina Flora

Mwiyuzi;
Mtu angekwambia huyo Flora niliwahi kumwona siku 3 tu alipokuja kwenye mkutano tuliokuwa tumeuandaa utashangaa. Huyo Mbasha hata kumtia machoni hivi sijawahi.
Hapa niko kiroho zaidi kuliko kimwili. Mbasha ameamua kumvua Roho akapambana kimwili. Bila Roho wa Mungu, hutashinda. Anajitapa kuwa atashinda, yetu yawe macho, atazidi kujiaibisha mpaka aogope kwenda uani kujisaidia. Usijaribu kumpinga shetani kimwili. Lakini kwa kuwa tayari alishauacha wokovu na kujiona kuwa yeye ni yeye kama mwanamume, kitu ambacho nadhani ni porojo tuu, amrudie Mungu na kumlilia kwa dhati. Mungu amsamehe na kumpigania.
Mwiyuzi, mimi si lolote wala chochote katika utumishi, lakini, ukiisha fikia mahali pa kumwita mtumishi yeyote wa Mungu ukamwita kuwa ni Shetani, weye utakuwa una tatizo. Mwambie Mbasha kwamba, kama ni ushetani yeye ndo ameuanza. Kuchapiwa mke, hakukupi nafasi ya kuja kumwanika humu JF tena kwa mijitusi ya wazi.
Neno la Mungu linasema; Maneno yenu yakolee munyu. Mdomo wa Mbasha umekwisha munyu. Sijui utatiwa nini tena hata ukolee.
Mnaomshabikia, mnamharibu zaidi. Mfundisheni amwamini Mungu wa kweli ili ampiganie. Atumie muda wake zaidi kumwomba Mungu aihuishe tena ndoa yake. Wapo wenzako wanaodhani kuwa haiwezekani, No no nooo. Kwa mwanadamu hiyo haiwezekani bali kwa Mungu, yoooote yawezekana. Tena watapendana sana na kuilea hiyo familia anayo ililia.
Asiwatukane watumishi wa Mungu na kuidharau miujiza na kuiita ati ni mazingaombwe. Kama hiyo ni mazingaombwe tu yakamnyang'anya mke na watoto, tena yanataka kumtia ndani Segerea akanyee ndoo mvua 30 kwa kama mbakaji; basi sitaki kuiona miujiza kwani itamhamisha dunia hii. Someni taratibu huu uzi, simkingii kifua Flora wala huyo mliyemwona kuwa mwanamazingaombwe. Mimi nawaona kama watu walio kengeuka na kwangu zaidi sana ni huyo Mbasha. Moto woote anauwasha yeye.
Usiniite Flora, miye ni kidume na nina mke mmoja na wajukuu tele. Ni mawazo yangu tuuu
 
Kuna watu mna roho mbaya dah..!!

Dr. Mo;
kama nani? Ni roho mbaya Daktari wangu au moyo mbaya? Kwenye aveta nakuona unaupima moyo si roho. Samahani tu bure. dah!
Sijui sikuelewi au??
 
mbona Flora wa kawaida sana jamani? wanaume na sisi tunapendaga vitu vya ajabu ajabu sana yaani tupo kama NZI kufata uchafu jalalani

blessings;
Weye kwa vile hutamani vya watu ndo maana unaona hivyo. Flora ukimwita wa kawaida utamwonea kwani hujamwonja, ila Mbasha amefikia mahali pa kuchanganya mambo. Akimwota na kumkumbuka anaona hakuna mtu wa kumpiku.
Analalamika mpaka anasema kwa kuweweseka.
Mwambieni tu kuwa watu wanamwona wa kawaida sana tu si wa kuwavuruga akili kiasi hicho. Ndo maana Flora mwenyewe wala hamjibu, Gwajima ndo kabisa kakaa kimya naye anamshangaa Mbasha ka weye unavyo mshangaa. Nani akagombee makitu hayo, watu tupo kwenda mbinguni weye upo kwenye uroda. Wapi na wapi???
 
Panapofuka Moshi lazima Ndimi za Moto zionekane, Waswahili wanapenda kusemaa, Lisemwalo lipo, na kama halipo basi laja.

Hatupaswi kuyafumbia macho haya yanayoendela kati ya hii Ndoa ya Bw.Mbasha/Mkewe na anayetuhumiwa kuharibu ndoa yao. Kama ushahidi upo wa Kutosha, Naona ni Muda Muafaka wa kuuweka wazi ili sisi Waumini wa huyu Nabii tukajua kama tunaongozwa na Roho wa Mungu au Roho wa Peponi. Tena Ndugu Mbasha ameenda Mbali zaidi akadai kuwa Huyu Mtuhumiwa wake #1 ,mijihela yake ni ya Sembe. Amenifumbua macho na kunikumbusha kipindi kile Viongozi wa serikali walipotoa Tamko/Madai kuwa baadhi ya Makanisa na viongozi wao Wanajihusisha na Mambo ya Sembe(Cardinal Pengo akaomba Serikali Ianike Majina ya hayo makanisa na Viongozi Wao, Lakini serikali haikutaka kufanya hivyo).

Aiseeee, Kama ndo hivi Mbona tutachomwa wengi kwa kukosa Maarifa kama Maandiko yanenavyo!? Umetimia wasaa wa kujaribu kila Roho lakini tusiziamini kila roho zinazotaja Jina la bwana kwani walio wengi ndo wale Manabii Fake.

MUNGU Tunusuru, na utupe Macho ya Rohoni tuweze kuzing'amua hizi Roho mbaya zinazotaka kutupeleka Motoni.
 
Mwiyuzi;
Mtu angekwambia huyo Flora niliwahi kumwona siku 3 tu alipokuja kwenye mkutano tuliokuwa tumeuandaa utashangaa. Huyo Mbasha hata kumtia machoni hivi sijawahi.
Hapa niko kiroho zaidi kuliko kimwili. Mbasha ameamua kumvua Roho akapambana kimwili. Bila Roho wa Mungu, hutashinda. Anajitapa kuwa atashinda, yetu yawe macho, atazidi kujiaibisha mpaka aogope kwenda uani kujisaidia. Usijaribu kumpinga shetani kimwili. Lakini kwa kuwa tayari alishauacha wokovu na kujiona kuwa yeye ni yeye kama mwanamume, kitu ambacho nadhani ni porojo tuu, amrudie Mungu na kumlilia kwa dhati. Mungu amsamehe na kumpigania.
Mwiyuzi, mimi si lolote wala chochote katika utumishi, lakini, ukiisha fikia mahali pa kumwita mtumishi yeyote wa Mungu ukamwita kuwa ni Shetani, weye utakuwa una tatizo. Mwambie Mbasha kwamba, kama ni ushetani yeye ndo ameuanza. Kuchapiwa mke, hakukupi nafasi ya kuja kumwanika humu JF tena kwa mijitusi ya wazi.
Neno la Mungu linasema; Maneno yenu yakolee munyu. Mdomo wa Mbasha umekwisha munyu. Sijui utatiwa nini tena hata ukolee.
Mnaomshabikia, mnamharibu zaidi. Mfundisheni amwamini Mungu wa kweli ili ampiganie. Atumie muda wake zaidi kumwomba Mungu aihuishe tena ndoa yake. Wapo wenzako wanaodhani kuwa haiwezekani, No no nooo. Kwa mwanadamu hiyo haiwezekani bali kwa Mungu, yoooote yawezekana. Tena watapendana sana na kuilea hiyo familia anayo ililia.
Asiwatukane watumishi wa Mungu na kuidharau miujiza na kuiita ati ni mazingaombwe. Kama hiyo ni mazingaombwe tu yakamnyang'anya mke na watoto, tena yanataka kumtia ndani Segerea akanyee ndoo mvua 30 kwa kama mbakaji; basi sitaki kuiona miujiza kwani itamhamisha dunia hii. Someni taratibu huu uzi, simkingii kifua Flora wala huyo mliyemwona kuwa mwanamazingaombwe. Mimi nawaona kama watu walio kengeuka na kwangu zaidi sana ni huyo Mbasha. Moto woote anauwasha yeye.
Usiniite Flora, miye ni kidume na nina mke mmoja na wajukuu tele. Ni mawazo yangu tuuu

Ila muumini wa baba gwaji.. au sio
 
Hivi nyinyi mkishaokoka akili za kufanya reasoning ndo huwa mnazitupa kabisa.yani mtu achapiwe mkewe apewe na kesi ya ubakaji na achafuliwe magazetini alafu bado awe mpole?kisa huyo aliemfanyia hayo ni mtumishi wa mungu? Si ufa.l.a huo.kwani huyo mtumishi wa mungu sio binadamu.hebu weye ufanyiwe hivyo afu ndo uone utajiskiaje.u have to walk in his shoes first.alaa
 
Ila muumini wa baba gwaji.. au sio

CSC;
Tatizo la watu wengi ni kutokulielewa neno la Mungu tu. Yule, anasema ni Mtumishi wa Mungu aliye hai. Kama ni hivyo Mungu aweza kumtumia kwa wakati wa mema au akamtumia kwa wakati mbaya pia. Je kama weye walisoma neno la Mungu, Yehu alikuwa mtumishi wa Mungu au wa shetani? Mungu ninaye mwamini hahitaji kusaidiwa na wanadamu kumchagulia mtumishi halali na mwovu. Alisema; Acha magugu yakue pamoja na ngano, tusijeng'oa ngano pia.
We are not here to condemn anyone. Sisi ni nani hata tumjue mwovu na mwema katika dunia hii iliyo lewa mvinyo wa kukimbilia miujiza tuuu?? Hata manyaunyau alipata wafuasi kule Temeke. Tena wakamkingia kifua kuwa anawatambulisha wachawi kwa kunywa damu ya paka.
 
Hivi nyinyi mkishaokoka akili za kufanya reasoning ndo huwa mnazitupa kabisa.yani mtu achapiwe mkewe apewe na kesi ya ubakaji na achafuliwe magazetini alafu bado awe mpole?kisa huyo aliemfanyia hayo ni mtumishi wa mungu? Si ufa.l.a huo.kwani huyo mtumishi wa mungu sio binadamu.hebu weye ufanyiwe hivyo afu ndo uone utajiskiaje.u have to walk in his shoes first.alaa

loban;
Nimefurahi sana kwa sababu sasa naamini unamwunga mkono Flora kuwa alifanya sawa sawa kabisa. Uibiwe mume tena mume mwizi wa nyumbani mwake mwenyewe. Ungelimfanyaje? Vaa weye viatu vya Flora. Alaa!
Flora alifanyiwa uovu usioonekana, alilambiwa mdogo wake walioshiriki ziwa moja na mume aliyekuwa anamwamini halafu mume huyo huyo paka shume akamwandika magazetini. Tena baada ya kumnyima ada ya mtoto wao wala si wa kufikia.
Akaenda kutafuta msaada, akaupata kwa sababu ya huruma za watu. Dume likaona kuwa kwa kuwa mkewe kapewa msaada, sasa hawezi kumkunja twna atakavyo. Ndo akaanza maneno kwenye vyombo vya habari. Kila kukicha, nimechapiwaaaa, nimechapiwaaaa!
Kwani yeye ndo wa kwanza kuchapiwa??? Mbasha wako ana lake jambo. Hata akane namna gani, kama alimlamba mdogo wake Flora, atafute njia ya kumalizana naye kabla hawajafikishana kwa Pilato. Mvua 30 zamngojea Segerea na hilo sio tishio ndo ukweli wenyewe huo. Sorry I have no other words to put it.
Asijifanye Kigogo akimtishia Gwajima. Atamwacha mkewe alifaidiwa, na hasira aliyo nayo mkewe, sijui ka atamaliza mwezi akijikunyata mwenyewe.
Mwambieni enyi washauri wake; Neno samahani mbona la kawaida tuuuu:hail:
 
"Mchungaji ...yapata kama wiki mbili zilizopita nilihoji kupitia vyombo vya habari juu ya ‘utajiri' wa ghafla wa mkewangu Mara baada ya mgogoro kutokea kati yangu na yeye, bila kupoteza muda mkewangu akanijibu kupitia gazeti moja la udaku kuwa amechangiwa fedha kiasi cha milioni 9 na waumini kanisani kwakoMchungaji, naomba uelewe kuwa nafahamu juu ya mipango yote mnayoipanga kuliko unavyodhani!! Kwanza ni kweli kuwa mlipitisha harambee ya kumchangia mkewangu, lakini kiwango kilichopatikana kilikuwa ni milioni 2 na laki tatu na si milioni tisa kama mlivyotangaza!! Lakini mlitangaza uongo huo makusudi iwe rahisi kutimiza malengo yenu ya kidhalimu mliyoyapanga juu yangu!!Mnamo tarehe 3 mwezi juni mwaka huu, mlifungua akaunti mpya kwa jina la mkewangu katika benki ya crdb morogoro, na siku nne baadae mkewangu aliingiziwa fedha kiasi cha milioni 18 kutoka akaunti ya MWANAMAPINDUZI FOUNDATION ambayo hyo accnt ipo nmb mwanza! Ambapo asasi hii inamilikiwa na mchungaji wako msaidizi Maximilian Machumu pamoja na mbunge wa viti maalumu kutoka mikoa ya kaskazini!
Nashukuru kama ulimpa fedha hizi kwa nia ya kumsaidia, lakini hofu yangu ni kuwa kwanini kitendo hiki kifanyike kwa kificho?? Kwanini mtumie njia za siri ambazo si rahisi watu kujua kama mmempa fedha??
Pia napatwa na mashaka zaidi kwani siku moja baada ya fedha hizi kuingizwa taarifa ya benki inaonyesha kuwa kiasi cha milioni sita cash zilitolewa na siku hiyo hiyo wapo waandishi watatu wa magazeti ya udaku ambao wanaonekana waliingiziwa fedha kiasi cha milioni moja kila mtu na aliyedeposit hizo fedha ni moja ya viongozi wako hapo kanisani!! Kuna nini hapo??
Mchungaji, naomba tusizunguke mbuyu! Ni dhahiri shahiri kuwa umekuwa na uhusiano wenye utata na mkewangu kwa muda mrefu sasa!
Binafsi nilianza kupata wasiwasi mwaka jana mwezi desemba tulipoenda katika mkutano wako wa injili pale morogoro! Mimi na mkewangu tulifikia hoteli ya kingsway msamvu na wewe ulifikia Nashera Hotel maeneo ya forest hill!!
Baada ya siku tatu za mahubiri mkutano wako ulipigwa marufuku na serikali kwasababu ya maneno yakichochezi uliyokuwa unahubiri, hvyo ikatulazimu waimbaji wote turejee dar es salaam!!
Lakini uliniomba mkewangu abaki na wewe kwani ulipanga uwe unawafanyia watu maombi pale kanisani kwako kihonda kwa muda wa siku nne!! Nilikubali na nikamuacha mkewangu nyumbani kwa dada yako pale mazimbu!! Lakini kesho yake dada yako alisafiri kwenda mwanza na ikabidi mkewangu arudi hotelini kingsway!!
Kwaa taarifa nilizonazo na nimezithibitisha kupitia wahudumu wa pale hotelini ni kuwa mkewangu hakuwahi kulala pale hata siku moja ingawa chumba kililipiwa kwa siku zote zile!! Unaweza kunijibu alikuwa analala wapi?? Je unaweza kunieleza kwanini mkewangu alikuwa analetwa nashera hoteli na taxi kila siku usiku!! Sibahatishi katika hili kwani hata namba ya dereva taxi ninayo!!
Yote haya nilivumilia, na hapa kati kati kuna mengi sana yametokea lakini nikajifanya mjinga nikajishusha nikavumilia kwa lengo la kulinda ndoa yangu isiharibike lakini naona wenzangu hambadiliki wala hamjishitukii sana sana mapenzi ndio yanzidi kuwa motomoto kati yenu!! Ulikuwa unategemea nivumilie mpaka lini, nijishushe kiasi gani, niwe mjinga kiasi gani Nilikuvumilia sana mchungaji lakini sasa imefika point hapana, imetosha lazima nikuondelee uvivu watanzania na dunia ikufahamu jinsi ulivyo na kitendo ulichonifanyaia na unataka kuniziba mdomo kwa kunitishia jela miaka 30!!!
Wewe ni mpuuzi na shetani anaishi ndani yako... na nataka nikuahidi kitu kimoja kuwa NITAKUSHINDA! Najua utanisumbua sana kutokana na hela zako but at the end, I will be the last man standing!! Narudia tena, nitakushinda.!!
Bila kusahau naomba niongee na wewe pia mkewangu, hivi ni nini kilichokukuta ndani ya moyo wako How did we get here?? Je ni fedha zilizokufanya ukengeuke kiasi hicho au kuna kingine?? Kama unanichukia mimi kiasi hiki je, uwahurumii hata watoto wetu?? Mbona tunawatengenezea mikosi wakiwa wadogo hivi?? Hivi unadhani watoto wanajisikiaje watakaposikia kuwa baba ameenda jela kwa kosa la kubaka lakini aliyechongesha muvi yote hiyo ni mama?? Hivi kisaikolojia hawa watoto watakuwaje Si watakuwa huku wanatuchukia sisi wote wawili kwa aibu na mikosi hii tunayowatengenezea Kwanini tunataka kuwataabisha watoto kwa dhambi ambayo hawajaitenda
Yes nafahamu nimekukosea mengi and am very sory for that, lakini basi embu kumbuka mkewangu nimekuvumilia mambo mangapi mkewangu, kumbuka makosa mazito uliyonifanyia lakini nikakusamehe ni sijamsimulia hata ndugu yako ama ndugu yangu ili kulinda heshima yako!! Kumbuka jinsi tulivyopogana na changamoto mbalimbali mpaka leo hii umefikia kuwa moja ya icons wa muziki wa injili hapa nchini?? Kumbuka shida, manyanyaso, dhuluma, kuchekwa na kudharauliwa ambako tumepitia mpaka leo hii tuko hapa!!!
Mkewangu, kwa miaka yote hii nimekubali nionekane bushoke tu huku watu hawajui kuwa mimi ndiye ninayechora ramani ya kila ishu yako!! Mimi ndiye nimekuwa nafatilia na kufanikisha kila kitu chako from scratch!!!
Lakini nimekubali jamii inione bushoke kwani nilikuwa najua nini mimi na wewe tunatengeneza kwa maisha yetu ya sasa na baadae!!! Nini kilichokubadilisha mkewangu Fedha Au huyo mchungaji mwanamazingaombwe
Hivi kweli kabisa umefikia hatua ya kulipa waandishi wa habari ili wanikandamize nionekane sifai katika jamii Ni nini kilichokuoata mkewangu??
Naomba uelewe kuwa binafsi siogopi kwenda jela kwasababu ya hiyo muvi mliyonizushia, kwani ni bora nikakae jela kuliko kuishi huru huku mkininyanyasa kiasi cha kuondoa utu wangu kama bidamu, lakini kinachoniuma ni familia yetu!! Kwanini watoto wateseke kwa sababu ya tamaa zetu binafsi!! Nikifikiria hilo naumia sana!
Najua kwa sasa inaonekana kama vile ni impossible kwa mimi na wewe kurudiana tena, lakini binafsi naamini tunaweza!! Najua haitakuwa rahisi kwani tumeharibu mno, lakini ni heri ya kujaribu kuliko kuendelea kufanya huu upuuzi tunoufanya sasa!!
Kumbuka hiki tunachokifanya sasa hatujajipaka matope sisi tu pekee, bali mziki wote wa injili Tanzania, na tusipotubu tukajirudi Mungu atatuhukumu kwa dhambi hii!!

Kumbuka kuwa hakuna kati yenu atakayeshinda katika hii vita, vyombo vya habari pekee ndivyo vitakavyo nufaika lakini mimi, wewe na mchungaji wote tuta loose!!

Mwisho nimalizie na wewe mchungaji, tulipokutana mara ya kwanza nilikuchukulia kama kaka na kama mlezi wetu wa kiroho!! Lakini umegeuka shetani mwenye pembe saba, umeparaganyisha familia yangu, umeleta maumivu makali kwenye ukoo!!
Nakuonya tena kwa mara nyingine, muache mkewangu!! Huyo ni mkewangu, nilimtolea mahali mimi mwenyewe na wazazi wake waliniamini na kunikabidhi!!! Nasema niachie mkewangu!!
Wewe ni nyoka, imefika time watanzania wakujue ukweli wako wewe mbwa mwitu mkali uliyevaa ngozi ya kondoo!!!
Umedanganya watu vya kutosha na umefarakanisha ndoa nyingi sana kwa sababu ya kiburi cha pesa zako chafu za sembe!! Umeudhalilisha ulokole kiasi cha kutosha imefika time tuwaeleze watanzania ukweli na wakufahamu kuwa wewe ni nyoka!!
Sitakubali kuona ukiendelea kuitesa familia yangu, nitapambana na nitakushinda!!! Siogopi fedha zako wala connection ulizonazo, ni bora nife nikiwa nimesimama kuliko kuishi nimepiga magoti!
Nitapambana na wewe mpaka mwisho ili historia isomeke vizuri ili hata wanangu wakiwa wakubwa wajue kuwa baba yao sikuwa lofa kiasi cha kupiga magoti na kuelekeza shingo kibla kuruhusu mdhalimu kama wewe uichinje familia yangu, bali licha ya umasikini wangu nilisimama kiume na kupigana kutetea familia yangu!!!
Narudia tena mchungaji, nitapambana na nitakushinda..​

Back
Top Bottom