Tumwesige senior
JF-Expert Member
- Jan 28, 2013
- 6,978
- 12,641
Jamaa kaandika nondo tupu aisee
Hata Mimi nilikuwa mpinzani mkubwa wa chadema ila kwa sasa Sina cha kuwalaumu,hapa napanga kwenda kuchukua kadi yangu ya chadema Tena ile premium kabisa.Taifa linapaswa kuwa na viongozi imara na wenye ujasiri wa level ya Lissu.
Frankly speaking kinachofanywa na Lissu nikitendo cha ujasiri wa kiwangoo cha juu sana .
Niwe mkweli zamani sikuwahi kuielewa Chadema hata kwa kutania ila hii Chadema ya sasa nadhani wengi tumefanikiwa kuiona nuru iliyojoficha.
CCM kitabaki kuwa chama cha marehemu Babu yangu na siyo Mimi .
Mwamba amekohoa na sauti imesikika .
Hakuna ajuaye kesho, Mungu peke yake, na mwenye dhamana ya maisha yetu ni Mungu.Lissu utaozea humo humo ukonga kwa uchochezi wako wa machafuko ya nchi.
Pumbav onyesha uchawa wangu!Wewe uliyeko uraiani una mchango gani kwa taifa zaidi ya uchawa?
Ukisikia misimamo thabiti ndio hii sasa hakuna ku give up hata kama adui amekuwekea bunduki kichwani.BARUA KUTOKA GEREZA KUU LA UKONGA.
Samia Suluhu Hassan hakuchaguliwa na sio Rais halali wa nchi yetu:
Kwa mujibu wa Taarifa ya awali ya watazamaji wa uchaguzi kutoka umoja wa Africa (AU);
1. Taratibu za kisheria za uchaguzi zilizotumika zilikuwa "...kinyume na viwango vya kikanda, kibara na vya kimataifa"
2. Uchaguzi "haukuzingatia misingi ya umoja wa Africa, kanuni na wajibu wa sheria za kimataifa kuhusu chaguzi za kidemokrasia"
3. Mazingira yaliyozunguka uchaguzi kabla, wakati na baada ya siku ya Uchaguzi "....hayakuwezesha Uchaguzi kufanyika kwa amani na kukubalika kwa matokeo ya Uchaguzi huo."
Kwa mujibu wa kauli ya awali ya watazamaji wa jumuiya ya maendeleo kusini mwa Africa, yaani (SADC);
1. Kulikuwa na ukandamizaji wa vyombo vya habari na uhuru wa kutoa maoni kuliko katika chaguzi za nyuma.
2. Kulikuwa na "Idadi ndogo sana ya wapiga kura waliojitokeza katika vituo vyote vilivyoangaliwa na baadhi ya vituo havikuwa na wapiga kura kabisa"
3. "Katika maeneo mengi wapiga kura hawakuweza kutekeleza matakwa na utashi wao wa kidemokrasia"
4. Kwa ujumla Uchaguzi mkuu huu ".... haukufikia viwango vya kanuni na miongozo ya SADC, kuhusu Chaguzi za kidemokrasia ya mwaka 2021"
Na kwa mujibu wa kauli ya awali ya watazamaji kutoka jumuiya ya Africa Mashariki (EAC);
1. Watazamaji wa EAC hawakushuhudia majumuisho ya kitaifa ya matokeo ya uchaguzi kwasababu hawakujulishwa kilipokuwa kituo cha majumuisho ya kura kitaifa.
Kwa mujibu wa Seneta Jim Risch, Mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje ya Baraza la seneti ya Bunge la Marekani;
1. "Siku ya jumatano ya tarehe 29 Oktoba, watanzania walifanya uchaguzi uliotawaliwa na ukandamizaji wa kisiasa, utekaji na uchakachuaji uliofanya na vyombo vya Dola."
2. Uchaguzi wa Tanzania uliamuliwa muda mrefu kabla ya tarehe 29 Oktoba.
3. Kwasababu ya uchaguzi huu usioaminika, watanzania Waliingia barabarani ili kuonyesha kuchoshwa kwao na hasira zao
4. "Kwa bahati mbaya, badala ya kusikiliza wito wa kufanya mageuzi na kuendesha uchaguzi kwa uwazi, Serikali ya Tanzania ilijibu kwa kutumia mabavu na kusababisha vifo vya mamia na utekaji na ukamataji wa watu wengi zaidi.
Kwa mujibu wa Tafakuri ya Baraza la Maaskofu katoliki Tanzania (TEC) juu ya yaliyotokea siku na baada ya uchaguzi - 2025;
1. Uchaguzi wa Oktoba 29 umeliingiza Taifa katika hali ya "....mauaji, watu kujeruhiwa na kupotea...., uharibifu na upotevu wa Mali binafsi na za umma.
Aliyesababisha maafa yote na uharibifu wote huu ni Samia Suluhu Hassani, Serikali yake na chama chake cha CCM.
1. Tarehe 17 Februari, 1992, Tume ya Rais ya Mfumo wa cha Chama kimoja au vyama vingi vya siasa Tanzania, iliyoongozwa na Jaji Mkuu wa wakati huo, Marehemu Francis L. Nyalali, iliishauri serikali ".... kufanya uamuzi wa kukubali mageuzi na hivyo kuepuka kutumia nguvu za dola kupambana na watanzania wanaodai mageuzi."
2. Tume ya Nyalali ilitoa onyo "Matokeo ya kutumia nguvu ni kuvuruga amani na kuleta mabadiliko ya pupa katika hali ya woga."
3. Tume ya Nyalali ilipendekeza Ratiba ya mbadiliko ambayo kwayo Tume mpya ya Uchaguzi ingeundwa ndani ya miezi sita, katiba mpya ingepatikana kufikia September 1993 na uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi ungefanyika mwezi oktoba, 1995, chini ya katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi.
4. CCM ya Rais Ali Hassan Mwinyi ilikataa mapendekezo hayo ya tume ya Nyalali, na imeendelea kukataa mapendekezo ya katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi tangu wakati huo hadi sasa.
5. Baraza la maaskofu Katoliki limesema kwamba maafa ya Oktoba 29 yamesababishwa na "kukosekana kwa Demokrasia ya kweli ya namna ya kupata viongozi. Jambo hili limekuwa kilio cha muda mrefu cha Taifa...... chaguzi zinakosa ushindani, ukweli, uwazi, uhuru na kuaminika.
6. Tarehe 12 February, Mara baada ya kuchaguliwa mwenyekiti wa CHADEMA, nilirudia wito wetu wa muda mrefu wa kufanyika kwa mabadiliko ya msingi ya mfumo wa uchaguzi ili kuwezesha kufanyika kwa uchaguzi mkuu ulio huru, wa haki na wa kuaminika.
7. Majibu ya Samia Suluhu Hassan yalikuwa ni kesi ya Uhaini dhidi yangu, CHADEMA kuzuiliwa kushiriki Uchaguzi na kupigwa marufuku kufanya shughuli zote za kisiasa mpaka kesi ya mchongo iliyofunguliwa dhidi yetu itakapokwisha.
8. Maaskofu wa TEC wamesema kuwa "Wananchi wasiposikilizwa watazungumza kwa lugha wanayojua wao."
9. Bob Marley, mwimbaji wa regae na mpigania uhuru aliimba "Mlango mmoja ukifungwa mingine mingi inafunguliwa"!
10. John F. Kennedy, Rais wa 35 wa Marekani, aliuambia Mkutano wa Muungano kwa Maendeleo (Alliance for Progress) nchini Uruguay mwaka 1962 kwamba "Wale wanaofanya mageuzi yasiwezekane, wanafanya mapinduzi yasiepukike
11. Samia Suluhu Hassan na CCM wamekataa kuwasikiliza wananchi; Sasa wananchi wanazungumza lugha wanayoijua wao, yaani maandamano!
12. Samia Suluhu Hassan na CCM wamefunga mlango wa maridhiano na amani; sasa milango ya nguvu ya Umma imefunguliwa kila Mahali nchi nzima!!
13. Samia Suluhu Hassan na CCM wamefanya mageuzi ya amani yasiwezekane; sasa watafanya mapinduzi ya nguvu ya umma yasiepukike!!
14. Maaskofu wetu wametuambia ukweli. "Risasi hazijawahi kunyamazisha watu"!
15. Sasa Tujiandae ili kuhakikisha haki na kweli inatawala tena katika taifa letu;
16. Tujipange Upya ili kuhakikisha "Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama na wote waliohusika na mauaji ya wananchi wetu wanawajibika au kuwajibishwa..."
17. Tushikamane na kushirikiana ili kuwezesha mchakato wa katiba mpya yenye kujali haki, utu, usawa na ukweli kwa wote kuanza tena na kwa kushirikisha wadau wote!
18. Damu ya watu wote waliouawa au kujeruhiwa au walioumizwa wakati wakidai Demokrasia na haki kwa namna yeyote ile haijamwagika na haitamwagika bure. Damu yote hiyo na iwe wino utakaotuandikia Katiba Mpya itakayohakikisha ubinadamu wetu, na hali zetu na maisha yetu yanalindwa na kuthaminiwa.
POLENI SANA WATANZANIA KWA MAUMIVU YOTE MLIYOSABABISHIWA NA SAMIA SULUHU HASSAN NA CCM YAKE, KWA UOVU WOTE MLIOTENDEWA, NA KWA MASONONEKO YOTE MLIYOYAPATA
Mwenyezi Mungu aendelee kuwapa Faraja.
Tundu Antiphas Lissu
Gereza kuu la Ukonga.
25/11/2025.
Huyo Lissu ndo muhimili wa uovu (Pillar of Evil) , kwa hila zozote bila kujali damu za wenzi wake anataka afike kwenye hizo ndoto zakeNdio nimeanza kumuelewa alivyosema.tutakinukisha miezi zaidi ya mitano iliyopita