Barua kwako Rais Samia Suluhu Hassan

Barua kwako Rais Samia Suluhu Hassan

Hizo ni fikra zako tuh ndug yangu
Take easy ndugu yangu, tujadiliane but kwa upole na hekima. Tuna matatizo mengi ya kimfumo ambayo zaidi yako kwenye ubinafsi na unafiki na tunasahau kuwa sisi ni watu kwanza na hizi dini tumeletewa kutoka ulaya na uarabuni. Jambo la msingi ni utu(ubuntu) na si kutazama hizo dini za kuletewa. Yatupasa tupendane kama watu tu and nothing else.
 
The big show,Ritz na Faizafoxy (demu wa kariakoo) watakuwa active sana humu awamu hii
Walikuwa busy kumtetea jk awamu ya nne kwa jema na baya
Wakaambiana wapotee awamu ya mwendazake,they kept a low profile
Sasa wameibuka kwa kasi kama mashujaa wa dini
Sina dini ila wakristo mna midomo sana
Kiongozi muislam akiteua waislam 4 na wakristo 6 mnamuita mdini
Kiongozi mkristo akiteua wakristo 10 na waislam o hamumuiti mdini
Mnajifanya nyinyi ndio mnastahili..sijui nani kawaroga
 
Mkuu The hitman,

Nakushukuru Sana,unajua hawa ndugu zetu KWA miaka Mingi Sana wamekuwa na kasumba hii ya kulalamika na kujenga taharuki,wanashindwa kuelewa kuwa zama zinabadirika na maisha pia,

Katika zama kama hizi hauwez tena kufanya mambo kisha yakawa siri yasijulikane,hawataki kukubali ukweli shida yao
Yeah that's very true
 
Madam President,naomba nikusalimie kwa salam ambayo umeipendelea Sana wewe mwenyewe kuwa NAKUSALIM KWA JINA LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,NA KAZ IENDELEE.

First and foremost,naomba nichukue nafas hii kukupa pole zangu nyingi sana KWA kifo cha aliekuwa RAIS wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Hayati John Joseph Magufuli, pole Sana Madam President, hakika hayakuwa haya maisha ya dunian, ila ni kitu Cha kupita tuh, na mbora miongon mwetu kwenye macho ya Mwenyezmungu ni yule ambae ni mchamungu.

Nakupa pole na kukuombea Sana,kwani umepokea kijiti Cha uongoz katika kipindi kigumu Sana, ambacho Taifa lilikuwa kwenye mtanziko, na mgawanyiko mkubwa Sana ambao kila mwananchi mwenye uelewa amekuwa anauona, siyo wafanyabiashara, wafanyakaz, wakulima na hata wajasariamali wakubwa na wadogo,bila kusahau wanasiasa na vyombo vya habari.

Pamoja na changamoto zilizopo mbele yako Wananchi wenye nia njema na Taifa hili tupo pamoja nawewe na siku zote tutakuombea KWA Mola akusimamie katika shughuli zako za kuliongoza Taifa.

Leo,nitaenda kwenye kipengele nyeti Sana,ambacho kinakuhusu wewe kuunda serikali yako madam president.

Nakupa pole Sana,katika mtihan mkubwa ambao utakutana nao ni jicho la waz waz la kuangaliwa KWA UDINI katika uteuzi wako,mama hii ni cancer ambayo sidhan kama utafanikiwa kuipata tiba yake zaid zaid ya kupiga moyo konde,kusimama kwenye haki,usawa na kuangalia weledi wa nani unamuhitaj katika kujenga serikali yako.

Kipindi ambacho Mh Jakaya Kikwete akiwa MADARAKANI,pamoja na kwamba kwenye serikali yake alikuwa fair kwenye teuzi zake na kuunda serikali yake,hakuachwa salama kuandamwa KWA waraka mbali mbali kumtuhum kuwa amekuwa akifanya teuzi zake KWA upendeleo wa kiiman,pamoja na ukweli kwamba katika teuzi hizo nafas nyingi alizitoa KWA haki na kuwapa nafasi nyingi ndug zetu hawa hawa christians bado ilionekana kuwa ana elements za udini.

Hali kama hiyo ya malalamiko hatukuiona Kabisa kutoka kwao katika utawala wa mkapa wala Magufuli pamoja na kwamba ukweli upo waz kuwa walipewa Sana wao nafas,hukuwahi kuwaskia waislam wakilalamika kuhusu teuzi hizo,na hata pale inapotokea baadhi wakihoji majibu yanayokuja ni kwamba waislam mtulie na hamna elimu,hiyo ni kasumba ambayo imejengeka kwa muda mrefu Sana, na haijengi kama Taifa.

Last week, ulifanya uteuzi ambao katika uteuzi huo yalionekana majina ya waislam kama wanne katika watu nane nadhan uliowateua ikazuka taharuki kwenye mitandao ya jamii, instagram, Twitter na hata huku JamiiForum kuwa eti awamu hii wavaa makubazi na barakashia ni awam yao, maneno ya chuki na kuudhi kabisa, na unaweza dhan huyo anaetoa mada kama hizo ni minority lakin amin kwamba anawakilisha views za wengi Sana ambao hawana tuh ujasir wa kusimama na kuongea chuki kama hizo.

Unafanya Tena uteuzi juz hapa,katika teuzi hizo hakuna jina hata moja la Muislam,wao wote wapo kimya Na hakuna taharuki yoyote iliyozuka na hujaskia malalamiko yoyote hata kutoka kwa waislam, siyo kama waislam hatuoni hilo,tunaona ila tunaingiwa na hali ya iman na kuchukulia kuwa kasumba ambayo hata tufanye nini hawa ndugu zetu hawawez kuiondoa fikran mwao,nadhan ni kasumba ambayo imegongwa muhuri ndani ya mioyo yao na wao nahis wanarithisha kizaz baada ya kizaz, it's sad.

Katika kukupa pole juu ya hilo rai yetu ni kukuomba,kwanza Simama kwenye haki,usiangalie udini,usiangalie ukanda wala ukabila,

Mkristo akiwa na qualifications na ukaridhika nae mpe nafas kwani huyo ni mtanzania, Muislam akiwa na qualifications na ukaridhika nae mpe nafas kwani huyo ni mtanzania pia.

Pamoja na kwamba ndan ya hii serikali wamejaa wao ila wakionekana waislam kadhaa tuh sehemu flan utaskia taasisi flan kuna udini, neno hilo udini limewekwa hapo Ili kukandamiza haki za watanzania hawa ambao ni Waislam wasionekane kwa namna yeyote katika hizo positions za uteuzi na utumishi hususan katika sekta ya umma.

Madam president, kuwa huru kumchagua team yako, hata kama wapo waislam wengi ambao unaona wako smart na competent kufanya nao kazi, usiache kuwapa nafas eti kwa kuhofia kuwa watapiga kelele za udini, hawa hawakuanza leo na hawatokuja kumaliza leo, ni muda SASA umefika kujifunza kuish nao kama walivyo na hiyo kasumba yao.

VYOVYOTE VILE IWAVYO MADAM PRESIDENT, WE SHALL STAND BEHIND YOU, KWA HILA NA CHUKI WATAZAOZIANZISHA KATIKA KUKUONDOA KWENYE MSTARI WA WEWE KUTENDA HAKI NA KUONGOZA TAIFA HILI.

RAMADHAAN KAREEM MADAM PRESIDENT.
Takhbiiiiiiiirrrr !!!
 
The big show,Ritz na Faizafoxy (demu wa kariakoo) watakuwa active sana humu awamu hii
Walikuwa busy kumtetea jk awamu ya nne kwa jema na baya
Wakaambiana wapotee awamu ya mwendazake,they kept a low profile
Sasa wameibuka kwa kasi kama mashujaa wa dini
Sina dini ila wakristo mna midomo sana
Kiongozi muislam akiteua waislam 4 na wakristo 6 mnamuita mdini
Kiongozi mkristo akiteua wakristo 10 na waislam o hamumuiti mdini
Mnajifanya nyingi ndio mnastahili..sijui nani kawaroga
Hivi huyo FaizaFoxy anajua kwamba ikulu ya sasa hakuna kupikwa Kitimoto ?
 
Asante sana mkuu, uzi umetulia na umejaa busara zote, waislam na wakristo na wapagani tunaunganishwa na kitu kimoja tu, haki na amani, tuzingatie haki tupate amani
ni hayo tu
 
Asante sana mkuu, uzi umetulia na umejaa busara zote, waislam na wakristo na wapagani tunaunganishwa na kitu kimoja tu, haki na amani, tuzingatie haki tupate amani
ni hayo tu

Thanks Mkuu,

Nice compliment,nia yetu siyo kupalilia chuki,but nia yetu ni kukemea chuki na kuweka mambo sawa,as long as sote ni Watanzania basi haina haja ya kuangalia a KWA macho ya udini na chuki, especially KWA huyu mama ndiyo kwanza kachukua hatam ya uongoz,tumpe ushirikiano atuongoze sote bila upendeleo
 
Anajua ndo maana yupo active now..i like it though..
Waislam kama faizafoxy,na bigshow ni watu wa haki
Ritz ni kama haeleweki kwenye uislam wake

Mkuu nyabhingi,

Bila haki na usawa amani hawezi kuwepo,

Na siku zote kama unaona hujatendewa haki na ukawa una hoja nasi njoo na evidence,sisi tuna evidence kuwa Magufuli kwenye baraza la mawazir alikuwa na mawazir 24 waislam walikuwa wanne tuh,na manaibu wazir walikuwa 16 na waislam walikuwa 10 tuh,je uliwahi kutuskia waislam tukilalamikia kuwa kuna udini,tulimpa nafas aongoze nchi,madam msaidiz wake mkuu vice president alikuwa Muislam na wazir mkuu akwa Muislam tukaona wacha wafanye kazi,ila SASA hawa ndug zetu mama Hana hata miez miwili wanaanza complain ya udini kwake kweli??

Siyo sawa,haiwez kuwa sawa...

Na sisi lazima tutatoka mafichoni tuh
 
Please please let the President rule the Country, mweche ateue aonavyo inafaa, dini haijawahi kuwa kigezo cha weledi katika kazi let her make her choice bila kigugumizi chochote period. Tutampima kwa utekelezaji wa ilani na kufikia mpango wa maendeleo wa kitaifa.
 
Umeongea point, utaweza kumtambua Muislam au mkristo kwanza KWA JINA lake, baada ya hapo ndipo utaujua uhakika wake kuwa ni muumin kweli wa hiyo dini au la, that's why hawa ndug zetu walipoona majina tuh yenye muelekeo wa arabic kwenye huo uteuzi wakaconclude kuwa ni Waislam wameanza kupendelewa.
Kutoka Passive resistance juu ya gesi mpaka kumpangia namna ya kufanya kazi Rais wetu. Maajabu.

Tatizo ninaloliona kwa baadhi yenu na wewe Mkuu ukiwemo, silika zenu za "mfumo dume". Yaani kwa silika hizi nadhani mnafikiria mwanamke hana uwezo wa kufanya kazi kwa juhudi, hekima, busara , haki na nguvu kubwa kusimamia wajibu aliopewa katika sehemu husika. Hili, kama kweli silika zinawatuma hivyo, hili ni kosa kubwa mnalifanya. Mjisahihishe.

Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano Tanzania anao uwezo wa kufanya kazi kwa juhudi, hekima, busara, haki, nguvu, nia, na mengine kama haya kuliongoza taifa la Tanzania kustawi katika nyanja zote. Tujiepushe na kutoa maelezo yanayotaka kufifisha sifa sahihi alizonazo rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan.

Nimebaki nikiwa TUJITEGEMEE.
 
Umeielewa lakin hoja yangu hapo juu au,hebu tulia usome vizur
 
Thanks Mkuu,

Nice compliment,nia yetu siyo kupalilia chuki,but nia yetu ni kukemea chuki na kuweka mambo sawa,as long as sote ni Watanzania basi haina haja ya kuangalia a KWA macho ya udini na chuki, especially KWA huyu mama ndiyo kwanza kachukua hatam ya uongoz,tumpe ushirikiano atuongoze sote bila upendeleo
Mungu ana makusudi na sisi,
katika Wimbi kubwa la CORONA tumepata Raisi ambaye alinusurika kufa kwa COVID hivyo anajua hatari ya ugonjwa ule, hivyo hawezi leta masihara kwa watu anaowaongoza maana yeye anajua nini kimemtibu ni huduma bora za kiafya sio nyungu wala malimao.
kwa hali ya kawaida tulifikiri ni lini tungepata Raisi kutoka Zanzibar au Mwanamke ila Mungu kafanya yatokee,
Kwa kipindi kirefu tumeongozwa na viongozi wanaona mawazo yao ni muhimu kuliko ya wengine, lakini leo hii viongozi wale wameanza kujirekebisha,
Ubabe, vitisho na uongo vilianza kupewa heshima kubwa ila naamini mwisho wake ilibidi ufike.
huwa nikisikiliza hotuba baadhi naumia sana, inakuwaje wananchi muwapeleke kwenye Uchaguzi ambao mtaenda kufanya hujuma, kwa nini pesa ipotee? kwa nini watu wanaolipa kodi muwaambie hatuleti maji kisa mmetumia haki yenu kuchagua mtu mnayemtaka? ilhali maji yale wataenda kulipa bili? wataenda kuboresha afya zao kuepuka magonjwa kama kipindupindu? kwa nini kiongozi unaruhusu nafsi yako kuwa na mawazo ya kishetani?
una itisha uchaguzi unawanyima mawakala viapo , wanadai haki yao unawapiga unaua watu, then unawaweka ndani waliokuwa wanataka haki ambayo ungewapa yasingetokea maafa.
mtu kama anafanya mazuri asitumie mazuri yake kufanyia ubaya wenzake.
Leo hii damu za Wazanzibari zikiwalilia kwa madhila waliyofanyiwa kwenye Uchaguzi , Mungu akasikia kilio cha yule bibi Mzanzibari aliyefanyiwa ukatili, Askari wetu wataishi maisha magumu sana.
 
Asante mkuu,

Badala ya kuwa mfariji mkuu,alikuwa sometimes ni mtesi mkuu,

Watu wakapata maafa ya tetemeko kagera,nyumba zimebomoka,hawana makaz,hawana chakula,hawana majina hawana mavazi na kadhalika,

Unahamasisha wananchi wenzao tuwachangie na tunawachangie kwenye account kuu ya maafa,badala ya kuwapeleka misaada unaenda kuwasimanga kuwa hupeleki chakula,na kwamba we hukupeleka tetemeko,kama hawatafanya kaz na wafe,ule haukuwa uti hata kidogo,

Kuna mengi ya kukera lakin lipo jambo kubwa tumejifunza ya kuwa ukipata nafas ya kuongoza basi jaribu kuwa na roho ya utu na kujali,ubabe na ujeuri hauna mwisho mwema always
 
Ofcoz I am a Muslim that's why unaniita mdini,ushawahi sikia mkristo anaitwa mdini?

Si ndiyo KWA maana hata madam president SAMIA mnaanza kumtazama KWA jicho la udini now,but Magufuli hamkumtazama KWA jicho la udini kipindi kile,yes I know Mimi ni mdin,and I am proud of that
Wow!
 
THE BIG SHOW
Hongera sana kwa uzi wa maana, uzi wenye kuhimiza haki.

Kwa kweli kila Mtanzania kwa mujibu wa vigezo ana haki ya kutobaguliwa katika kuitumikia serikali

Kama tunaona kila wakati teuzi zinalalia watu wa ukanda mmoja au kabila moja basi tuna haki ya kuweka question mark.

Na pia kama tunaona kila wakati teuzi zinalalia kwa wingi kwa watu wa dini moja wakati hii nchi ina mchanganyiko wa watu wa dini mbalimbali ambao nao wana vigezo, Pia tuna haki ya kuweka question mark

Uongo mbaya serikali ya Magufuli iliwaweka kando sana Waislamu kwenye teuzi, Waislamu walikuwa wanayaona haya, hawakupendezwa nayo, mwanzo walisema, lakini baadae wakamuacha tu waone mwisho wa udini wake ni nini!

Sasa Samia atende haki kwa Watanzania wote, Tunataka kuona Watu wenye vigezo, Waislamu kwa Wakiristo na kana kuna wasio na dini nao wapate fursa ya kuitumikia nchi.

Tunataka kuona wanawake kwa wanaume, Wazanzibari kwa Watanganyika wote wanapata fursa

Hatumaanishi abalance, lakini tunataka kuona jitihada za kujenga serikali inayoakisi sura ya watu wa nchi yetu
 
Back
Top Bottom