Barua ya Adam Malima kumpinga Spika!

Barua ya Adam Malima kumpinga Spika!

Status
Not open for further replies.
As a matter of fact, Mengi asingepewa nafasi ya kusikilizwa kwenye suala hili kwani.

a. Malima hakumtaja kwa jina au chombo anachomiliki
b. Malima hakusema hayo ni maoni yake bali ni "habari" tu.. zinaweza kuwa za ukweli na uongo.
c. Suala alilozungumzia Malima lilikuwa ni kati yake ya Waziri wa Habari siyo yeye na Mengi!

Jambo hili lilikuwa complicated pale Sitta alipoamua kutaka ushahidi wa maneno ya Malima, kwani angeweza kukataa kabisa kumpa nafasi Mengi kwani hakutajwa wala kampuni yake kutajwa bungeni!
 
Kinachofuata sasa hivi ni kama standard iliyotumiwa dhidi ya Malima itatumiwa kwa kila atakayekuwa na "habari" kutakiwa alete ushahidi na wale wanaofikiriwa "ndio wao" kuleta malalamiko bungeni. Tusipoangalia mambo makubwa mawili yanaweza kutokea.

Moja, ni wabunge kuogopa kuzungumzia mambo fulani kwa kuogopa kuitwa na Kamati za Bunge kuleta ushahidi

Pili, raia wa kawaida wanapohisi ni "wao" wanazungumza kukimbilia Bungeni na kutoa malalamiko yao. Matokeo yake, Bunge litajikuta linageuka mahala pa malalamiko kila kukicha.. mtasikia "mbunge huyu alivyosema hivi, alinimaanisha mimi kwa vile ni mimi tu ndiye ninafit kwenye description hiyo, hivyo Mbunge amenikosoa aniombe radhi"... Na Mbunge atakimbilia na kusema "mimi sikumtaja na nilizungumza nikiwa na matumaini kuwa kinga yangu ya mazungumzo inanilinda, naomba chama kinitetee"... na gurudumu la hoja na hoja kinyume litaendelea kuzunguka!!
 
Mzee ES

Shukran kwa majibu yako murua.

Naomba kidogo punguza hasira, kauli kama "narudia tena niliyesema kuwa Malima ni mkurugezni katika kampuni za Manji ni mimi, FULL STOP", nadhani hapa mzee umekuwa mkali mno calm down dear.

Back to the issue, swali la mwanakijiji kwa Mh Malima kuhusu jambo hili limejibiwa vizuri tu Mh mwenyewe, naona kuna attempt za kupotosha ukweli Mh Malima kajibu hivi " Mimi nimewahi kufanyakazi na kuajiriwa na Benki of Tanzania to the best of my re-collection Bwana Manji hakuwa benki of Tanzania" Je kwa kauli hii anakubali au anakataa? Jamani kiswahili tu nacho taabu? In otherwords kama Benki of Tanzania inamilikiwa na Maji then its true aliajiriwa na Manji! simple is that!

Habari za wabunge kuwa wakurugenzi wa mashirika nakubali na wala si dhambi lakini katika hili mhusika anasema yeye hajafanyakazi huko, tukitaka ushahidi unasema piga simu watakwambia wenyewe!


Mzee ES kitabu sawa lakini ukweli upo palepale kesi iliyopo PCB ni madai ya rushwa ya Mzee Ndesamburo kama hutaki tawile! subiri kitabu cha Ndesamburo!
 
Mzee Masatu,

Heshima mbele, hayo uliyoninukuuu ni kwa sababu sioni sababu kwa nini ukweli unataka kupindishwa, wakati niliyesema ni mimi na sijakataa, nashangaa watu wengine kulaumiana kwa kitu nilichokisema ambacho ninajua kuwa ni ukweli, anyway nimekusikia mkuu,

Now back to the ishu, apmoja na kwamba sijui kama hiki kitabu kinaruhusiwa nitanukuu mahali ambapo Spika anasema kuipeleka hii ishu PCB,

"(Page:29).. ........Na kwa kuwa, kosa la jinai wabunge hatuna kinga yoyote, na kwakuwa kuna chombo mahususi cha kisheria cha kushughulikia uchunguzi wa rshwa, niliamua kumwagiza katibu wa bunge awasiliane kwa maandishi, na Mkurugenzi wa Tume ya kuthibiti Rushwa (TAKURU) ili uchunguzi ufanywe kubaini ukweli, na hatimaye kuachia sheria ichukue mkondo wake..........(Page:29)!

Mzee wangu Masatu, hii inasaidia au bado kwenye ile ishu ya Spika kuipeleka hii kesi kule, na hii ilikuwa baada ya Ndeasmburo kuipeleka huko hii kesi pia! Unless sikielewi vizuri hiki kipande niaona kuwa Spika habagui au ku-isolate ni kitu gani PCB wakichunguze, niaona ni kesi nzima kwa ujumla, au?
 
Mzee ES.. hicho kijitabu kinapatikana vipi....? kurasa 32 siyo nyingi kuna uwezekano wa kukiscan na kukiweka kwenye mtandao..?
 
Eeh bwana ngoja nihakikishe kuwa hakina noma kukitoa, nitakuarifu kwenye pm na kama ni waa nitakutumia kopi by the weekend, I promise! By kesho joni nitakuwa na jibu!
 
Jokakuu,

Unaposema kuwa Spika alizungumza kwa kirefu kesi hii ni sawa. Lakini swali je aliechunguza kesi na kutoa ripoti ni tume sio spika!. Sasa kama Spika alikuwa ana uwezo wa kufanya kazi ile vizuri zaidi kwanini aliipeleka kwenye kamati in the 1st place?

Inaonyesha una mashaka na maamuzi ya kamati, lakini ukweli utaendelea kubaki hivyo hivyo kuwa kamati imemuona Mh Malima hana hatia.

Itakuwa jambo la busara pia mbali na jambo hili kujadiliwa tena bungeni watu wa bunge wa post Hansard za proceedings za kamati kwenye web yao ili na sisi wananchi tuchambue pumba na mchele. Huu uamuzi wa Kamati based on what we will see ktk Hansard tutajua kama uamuzi wao ni questionable or what. Huu ni ushauri wa mjadala kuwa mpana zaidi na kuwaondoa wananchi mashaka.

Mungu Ibaraki Tanzania


Unajua tangu hii thread ianze umeuliza maswali ya msingi sana?

Pili ninamini kuwa kuna ripoti ya ili hatuioni na Mzee SIX kaamua tu kutoa yake anayoipenda na hii ni hatari kwani sika sasa anabehave like a dictator na cha ajabu hakuna aliye question hili

I hope hayo maswali uliyouliza hapo juu utajibwa

in the mean time na mie ngoja niende nikamalizie kiporo changu kwenye thread ya Zimbabwe maana huko nako kuna watu hawahitaji majibu mepesi mepesi

kwa hili naona masatu huku umeweka mambo very simple and clear
 
DrWho... kwanza kabla ya kukimbilia ya Wazimbabwe ungetake business uliyoiacha hapa....
 
Mzee ES.

Now back to the ishu, apmoja na kwamba sijui kama hiki kitabu kinaruhusiwa nitanukuu mahali ambapo Spika anasema kuipeleka hii ishu PCB,

"(Page:29).. ........Na kwa kuwa, kosa la jinai wabunge hatuna kinga yoyote, na kwakuwa kuna chombo mahususi cha kisheria cha kushughulikia uchunguzi wa rshwa, niliamua kumwagiza katibu wa bunge awasiliane kwa maandishi, na Mkurugenzi wa Tume ya kuthibiti Rushwa (TAKURU) ili uchunguzi ufanywe kubaini ukweli, na hatimaye kuachia sheria ichukue mkondo wake..........(Page:29)!

Mzee wangu Masatu, hii inasaidia au bado kwenye ile ishu ya Spika kuipeleka hii kesi kule, na hii ilikuwa baada ya Ndeasmburo kuipeleka huko hii kesi pia! Unless sikielewi vizuri hiki kipande niaona kuwa Spika habagui au ku-isolate ni kitu gani PCB wakichunguze, niaona ni kesi nzima kwa ujumla, au?


Mzee ES

Shukran kwa majibu yako murua,

Hii inasaidia SANA, lakini inasaidia kuthibitisha kile nilichokuwa ninakuambia! time and again. Im happy umethibitisha mwenyewe hapa kuwa madai yalipopelekwa PCB ni ya rushwa kama yalivyoletwa na Mh Ndesamburo.

Ninaanza kupata wasiwasi kama kweli unajua kazi za hiki chombo PCB au TAKURU, seriously Im casting a BIG doubt. Labda tu nikupe darasa kidogo, kesi mama ni Mengi Vs Malima na Malima Vs Mengi. Unapodai kesi hizi ndio zinapelekwa TAKURU una maana na wao wakajadili dakika? Mzee kazi za TAKURU unazijua kweli? the more u argue about this is the more u advertise ur own ignorance! It is spotless clear TAKURU wata deal na madai ya rushwa tu.

Hicho kifungo ulichokinukuu hapo juu umekianzia kati kama ungeanza mwanzo ungepata jibu lako. Kwa faida yako nakuletea nukuu ya toka mwanzo ktt rulling ya spika;


8.10 Tuhuma za “Wabunge kupewa rushwa” ni nzito na ukizingatia kuwa zimetolewa na Mbunge mtu mzima na mzoefu, haziwezi kupuuzwa hata kidogo. Kutokana na sababu hiyo, na kwa kuzingatia ukweli kuwa, kupokea au kutoa rushwa ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria za nchi;


8.11 Na kwa kuwa, kwa kosa la jinai Wabunge hatuna kinga yoyote, na kwa kuwa kuna chombo mahsusi cha kisheria cha kushughulikia uchunguzi wa rushwa, niliamua kumwagiza Katibu wa Bunge awasiliane kwa maandishi, na Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiti Rushwa (TAKURU) ili uchunguzi ufanywe kubaini ukweli, na hatimaye kuachia sheria ichukue mkondo wake.


8.12 Katibu wa Bunge aliandika barua tarehe 26 Januari, 2007 kukabidhi suala hili kwa TAKURU. Aidha, kwa nakala ya barua hiyo, Mhe. Ndesamburo amehimizwa kutoa ushirikiano kwa TAKURU, ili ukweli kamili ufahamike.


8.13 Aidha, nimemwagiza Katibu wa Bunge anipatie ushauri kamili wa uhalali au vinginevyo, wa Mhe. Ndesamburo akiwa mjumbe wa Kamati ya Bunge, kufanya mawasiliano yasiyo rasmi na mmoja wa wanaochunguzwa wakati uchunguzi unaendelea.


8.14 Ingewezekana kuiagiza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kufuatilia jambo hili, lakini nimeona si hekima kufanya hivyo kwa sasa. Nachelea kuchukua hatua zozote ambazo zitaonekana kumwekea vipingamizi Mhe. Ndesamburo, hasa kwa sababau tuhuma za rushwa anazielekeza kwa Waheshimiwa Wabunge wenzake.

Neno tuhuma za wabunge kupewa rushwa nime bold in red kukuthibitishia kuwa tuhuma zinapelekwa PCB za wabunge kupewa rushwa kama zilivyoletwa na Mzee Mh Ndesamburo.


Kama ulivyoelewa kuhusu suala la Mh Malima kuajiriwa na Manji na hili pia utaelewa lets go on...


Mungu Ibariki Tanzania
 
Ina maana humu ndani hakuna anayeng'amua mchezo unaochezwa? Achaneni na Malima na Mengiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii. Issue ni UNYANG'AU WA MANJI NA WENZIWE NSSF na PSRP.

Kuendelea kuongelea Mengi, Malima, Manji na genge lao ni kukubali kufanywa wajinga. HAMUELEWI????

Tanzanianjema
 
Mwanakijiji wrote:
As a matter of fact, Mengi asingepewa nafasi ya kusikilizwa kwenye suala hili kwani.

a. Malima hakumtaja kwa jina au chombo anachomiliki
b. Malima hakusema hayo ni maoni yake bali ni "habari" tu.. zinaweza kuwa za ukweli na uongo.
c. Suala alilozungumzia Malima lilikuwa ni kati yake ya Waziri wa Habari siyo yeye na Mengi!

Jambo hili lilikuwa complicated pale Sitta alipoamua kutaka ushahidi wa maneno ya Malima, kwani angeweza kukataa kabisa kumpa nafasi Mengi kwani hakutajwa wala kampuni yake kutajwa bungeni!

Mwanakijiji,
Mh.Malima hakumtaja kwa jina Reginald Mengi, but he was too elaborate kiasi kwamba kila mtu mwenye uelewa angejua kwamba anamzungumzia Raginald Mengi.

Hivi kuna ubishi kuhusu mmiliki yupi wa TV alitembelea Madrasa na alikuwa na malumbano na Sheikh wa Msikiti wa Kariakoo? Vilevile katika kupeleka ushahidi kwanini alipeleka ushahidi unaomhusu Mengi, if he was not talking about Mengi?

Malima anadai ati wabunge watatishika kutokana na hatua ya Spika. Mimi nasema hapana. Watakaotishika ni wale ambao wanataka kuzungumza bila utafiti, na kwa kutokuzingatia kanuni, na ustaarabu wa Bunge.
 
Ina maana humu ndani hakuna anayeng'amua mchezo unaochezwa? Achaneni na Malima na Mengiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii. Issue ni UNYANG'AU WA MANJI NA WENZIWE NSSF na PSRP.

Kuendelea kuongelea Mengi, Malima, Manji na genge lao ni kukubali kufanywa wajinga. HAMUELEWI????

Tanzanianjema

YOU CAN DO BETTER THAN THIS
 
Masatu, ES na wengineo,
Kesi hii ni nzito kuliko inavyodhaniwa na wengine, kwanza inamhusisha PM moja kwa moja, na ili uchunguzi ufanyike, basi ilikuwa inabidi PM anyang'anywe kwanza madaraka hata kwa muda. Kwa nini kwanza cell phone ya PM na ya Mengi, zilitakiwa zichukuliwe kufanyiwa utafiti, na pia hata cell phone za Manji, Malima na wabunge wa kamati, zote zilitakiwa zichukuliwe kufanyiwa utafiti kama mwasiliano hayo yalikuwa yanafanyika.

Sasa sijui kama hili limefanyika, au siasa zimeanza tena????
 
Mwanakijiji,
Mh.Malima hakumtaja kwa jina Reginald Mengi, but he was too elaborate kiasi kwamba kila mtu mwenye uelewa angejua kwamba anamzungumzia Raginald Mengi.

Hivi kuna ubishi kuhusu mmiliki yupi wa TV alitembelea Madrasa na alikuwa na malumbano na Sheikh wa Msikiti wa Kariakoo? Vilevile katika kupeleka ushahidi kwanini alipeleka ushahidi unaomhusu Mengi, if he was not talking about Mengi?
Malima anadai ati wabunge watatishika kutokana na hatua ya Spika. Mimi nasema hapana. Watakaotishika ni wale ambao wanataka kuzungumza bila utafiti, na kwa kutokuzingatia kanuni, na ustaarabu wa Bunge.

Hakuwa akimzungumziz Mengi halafu anapeleka tapes zinazoonyesha mengi na ITV duh!
 
huu mchezo wa bungeni na malima na manji ni mbimu tu,zogo liendelee huku wengine wanaendelea kutumbua pesa za mifuko ya hifadhi walizoiba,.

manji amefanya trick kubwa sana akisaidiana na associates wake..yaani kuhamishia attention ya watu kwenye....kufikiri hii kashafa ya nssf imeibuliwa kwa sababu za UDINI ili kuwamaliza yeye na wakurugenzi wa hayo mashirika ya hifadhi ambao ametumia kofia ya udini ili kuvuta hisia za wananchi kwamba wanaonewa.
pili hii hoja kupelekwa na kutolewa bungeni ni kati ya malengo ya kubadili akili za watu waamini suala la mabilioni ya manji na nssf,pspf..limezuliwa na mengi kwa kuzingatia chuki na wivu wa mengi dhidi yake kibiashara hasa kwa kuwa wote wameshawahi kushindania kuendesha michezo ya bahati nasibu,..

tatu manji ametumia michezo especially udhamini wake kwa YANGA kama moja ya kampeni zake za PR cleaning....haya mambo yakishasahauliwa YANGA wajue hawana mfadhili...afterall wanaomjua manji wanasema ni SIMBA mzuri tu ila STRATEGISTS wake walimshauri angeingilia simba asingekuja juu mapema kwa sababu kwa wakati huo simba walikuwa na mo na wengine ,ingekuwa ngumu kuwafunika ghafla.
 
Mzee Yomba Yomba,

Nimekusikia mkuu, una point nzito!

Mzee Masatu,


Mimi sitakujibu matusi, maaana huu mjadala kwangu ni muhimu sana,

PCB wanachunguza rushwa, iliyotolewa na nani na kwa sababu gani? Kwa hiyo ili kuhitimisha uchunguzi wao ni lazima PCB waangalie tepu zote kwa ujumla zilizotolewa kama kithibiti kwenye kamati iliyokaa kama mahakama,

Hivi mtu anahitaji kwenda shule kelewa hili? Kama kweli Malima alikuwa na convincing argument kwa nini Manji ilibidi ahonge jurors, na inaweza kusemwa on Mengi side pia kama alikuwa ni just a victim kwa nini ahonge jurors?

PCB wakimuonea Malima/Mengi akawa-sue, kisheria si atatakiwa kuonyesha sababu zote, na ni lazima tepu itabidi pia ziangaliwe au? Bado ninaamini kuwa Spika amewakabidhi PCB kesi nzima kwa ujumla, pamoja na kwamba kazi ya PCB ni rushwa tu, lakini ni lazima waangalie na sababu iliyopelekea rushwa kutolewa, kama ile sababu ni convincing mtu hawezi kutoa rushwa bila ya kuwa na sababu, kama Manji alitoa rushwa ina maana alijua kuwa hana kesi sasa PCB watathibitisha vipi kuwa hakuwa na kesi?

Hizi sababu na nyingine aidi zinanifanya niamini kuwa Spika ameikabidhi kesi kwa ujumla. PCB lazima watafute probable cause iliyosababisha kuwepo kwa rushwa!

Ahsante Mzee!
 
Mzee PM,

Sasa inaanza ku-make a sense kuwa kwa nini someone kwenye hii kesi ilibidi atoe rushwa kama ni kweli,

Tena ahsante sana kwa kuliweka sawa hili, ninayemuonea huruma ni ndugu yangu Malima, why put himself ni this, bado sipati jawabu?
 
true,

hata uamuzi wa spika kukataa kufuata mapendekezo ya kamati na kuamua kuja na maamuzi tofauti kabisa kwa kuzingatia busara,kwa kiasi kikubwa yalichangiwa na kamati kutuhumiwa kuhongwa na manji.so kwa namna yeyote hata ungekuwa wewe ni spika lazima ungetoa mapendekezo yasiyofungamana ,kwa sababu kukubali moja kwa moja mapendekezo ya kamati ,ingemaanisha kuwa manji amelinunua bunge akiwemo spika .
uamuzi aliotoa sitta alikuwa ni wa busara sana ,kwa kuwa umelenga maelewano,hakuna aliyeambiwa kashindwa ila wameombwa wakutane tu ofisini kwa spika japo kwa kikombe cha kahawa ..sasa wajameni hapo kuna ubaya gani?
ingemaanisha nini kwa wabunge kama malima anesimamishwa bungeni atubu? hata kama kweli alichemsha ,je heshima ya mbunge kusulubiwa na commoner tena bungeni ingezaa nini? au kama mengi angeombiwa atubu huku uraiani ...wananchi hawangejenga hisia ya manji kununua bunge lote?

spika kiwango!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom