Mzee ES.
Now back to the ishu, apmoja na kwamba sijui kama hiki kitabu kinaruhusiwa nitanukuu mahali ambapo Spika anasema kuipeleka hii ishu PCB,
"(Page:29).. ........Na kwa kuwa, kosa la jinai wabunge hatuna kinga yoyote, na kwakuwa kuna chombo mahususi cha kisheria cha kushughulikia uchunguzi wa rshwa, niliamua kumwagiza katibu wa bunge awasiliane kwa maandishi, na Mkurugenzi wa Tume ya kuthibiti Rushwa (TAKURU) ili uchunguzi ufanywe kubaini ukweli, na hatimaye kuachia sheria ichukue mkondo wake..........(Page:29)!
Mzee wangu Masatu, hii inasaidia au bado kwenye ile ishu ya Spika kuipeleka hii kesi kule, na hii ilikuwa baada ya Ndeasmburo kuipeleka huko hii kesi pia! Unless sikielewi vizuri hiki kipande niaona kuwa Spika habagui au ku-isolate ni kitu gani PCB wakichunguze, niaona ni kesi nzima kwa ujumla, au?
Mzee ES
Shukran kwa majibu yako murua,
Hii inasaidia SANA, lakini inasaidia kuthibitisha kile nilichokuwa ninakuambia! time and again. Im happy umethibitisha mwenyewe hapa kuwa madai yalipopelekwa PCB ni ya rushwa kama yalivyoletwa na Mh Ndesamburo.
Ninaanza kupata wasiwasi kama kweli unajua kazi za hiki chombo PCB au TAKURU, seriously Im casting a BIG doubt. Labda tu nikupe darasa kidogo, kesi mama ni Mengi Vs Malima na Malima Vs Mengi. Unapodai kesi hizi ndio zinapelekwa TAKURU una maana na wao wakajadili dakika? Mzee kazi za TAKURU unazijua kweli? the more u argue about this is the more u advertise ur own ignorance! It is spotless clear TAKURU wata deal na madai ya rushwa tu.
Hicho kifungo ulichokinukuu hapo juu umekianzia kati kama ungeanza mwanzo ungepata jibu lako. Kwa faida yako nakuletea nukuu ya toka mwanzo ktt rulling ya spika;
8.10 Tuhuma za Wabunge kupewa rushwa ni nzito na ukizingatia kuwa zimetolewa na Mbunge mtu mzima na mzoefu, haziwezi kupuuzwa hata kidogo. Kutokana na sababu hiyo, na kwa kuzingatia ukweli kuwa, kupokea au kutoa rushwa ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria za nchi;
8.11 Na kwa kuwa, kwa kosa la jinai Wabunge hatuna kinga yoyote, na kwa kuwa kuna chombo mahsusi cha kisheria cha kushughulikia uchunguzi wa rushwa, niliamua kumwagiza Katibu wa Bunge awasiliane kwa maandishi, na Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiti Rushwa (TAKURU) ili uchunguzi ufanywe kubaini ukweli, na hatimaye kuachia sheria ichukue mkondo wake.
8.12 Katibu wa Bunge aliandika barua tarehe 26 Januari, 2007 kukabidhi suala hili kwa TAKURU. Aidha, kwa nakala ya barua hiyo, Mhe. Ndesamburo amehimizwa kutoa ushirikiano kwa TAKURU, ili ukweli kamili ufahamike.
8.13 Aidha, nimemwagiza Katibu wa Bunge anipatie ushauri kamili wa uhalali au vinginevyo, wa Mhe. Ndesamburo akiwa mjumbe wa Kamati ya Bunge, kufanya mawasiliano yasiyo rasmi na mmoja wa wanaochunguzwa wakati uchunguzi unaendelea.
8.14 Ingewezekana kuiagiza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kufuatilia jambo hili, lakini nimeona si hekima kufanya hivyo kwa sasa. Nachelea kuchukua hatua zozote ambazo zitaonekana kumwekea vipingamizi Mhe. Ndesamburo, hasa kwa sababau tuhuma za rushwa anazielekeza kwa Waheshimiwa Wabunge wenzake.
Neno tuhuma za wabunge kupewa rushwa nime bold in red kukuthibitishia kuwa tuhuma zinapelekwa PCB za wabunge kupewa rushwa kama zilivyoletwa na Mzee Mh Ndesamburo.
Kama ulivyoelewa kuhusu suala la Mh Malima kuajiriwa na Manji na hili pia utaelewa lets go on...
Mungu Ibariki Tanzania