Barua ya Adam Malima kumpinga Spika!

Barua ya Adam Malima kumpinga Spika!

Status
Not open for further replies.
Nafikiri hiki itabu cha Ndesamburo, ambacho nasikia tayari Spika anakipiga vijembe kabla hakijatoka, kitakata mzizi wa fitina,

Hivi katika sheria zetu hakuna inayombana Spika kuwa akiyavulia maji nguo lazima ayaoge? Maana kuipeleka ishu kwenye kamati ya bunge na kuitangazia public ni kitendo kizito sana kitaifa kwamba I am lost kuwa at the end aliamua kutumia busara?

Na hivi hatuna sheria ya special prosecutor ambaye ni independent kama wanavyofanya huko majuuu, ambaye at this point ilitakiwa ndiye apewe hii kesi? kama vile mzee Ken Star?

Halafu ninaomba msaada wakati Malima, anatoa maelezo ya kesi yake mbele ya kamati ya bunge, alikuwa amekula kiapo? Maana kama alikula kiapo halafu ikagundulika kuwa alilidanganya bunge under oath si kuna kesi ya perjury hapo au?

kwa kweli hii kesi ni very interesting sana!
 
huu mchezo wa bungeni na malima na manji ni mbimu tu,zogo liendelee huku wengine wanaendelea kutumbua pesa za mifuko ya hifadhi walizoiba,.

manji amefanya trick kubwa sana akisaidiana na associates wake..yaani kuhamishia attention ya watu kwenye....kufikiri hii kashafa ya nssf imeibuliwa kwa sababu za UDINI ili kuwamaliza yeye na wakurugenzi wa hayo mashirika ya hifadhi ambao ametumia kofia ya udini ili kuvuta hisia za wananchi kwamba wanaonewa.
pili hii hoja kupelekwa na kutolewa bungeni ni kati ya malengo ya kubadili akili za watu waamini suala la mabilioni ya manji na nssf,pspf..limezuliwa na mengi kwa kuzingatia chuki na wivu wa mengi dhidi yake kibiashara hasa kwa kuwa wote wameshawahi kushindania kuendesha michezo ya bahati nasibu,
..
Hili Lina ukweli kwa kiasi kikubwa na hata ktk Bunge letu wapo washiriki wa hili na maokeo yake ndiyo hali tunayoiona sasa.
tatu manji ametumia michezo especially udhamini wake kwa YANGA kama moja ya kampeni zake za PR cleaning....haya mambo yakishasahauliwa YANGA wajue hawana mfadhili...afterall wanaomjua manji wanasema ni SIMBA mzuri tu ila STRATEGISTS wake walimshauri angeingilia simba asingekuja juu mapema kwa sababu kwa wakati huo simba walikuwa na mo na wengine ,ingekuwa ngumu kuwafunika ghafla.
Hapa kidogo pana utata Manji alijiingiza Yanga kwa kuendeleza vita yake dhidi ya Mengi......................kama unakumbuka mengi ndiyo aliyekuwa msuluhishi wa mgogoro wa Yanga yaani makundi yote matatu ya Yanga yaliyokuwa yanatofautiana na kilifikia kipindi karibu angefanikiwa hilo, hapa ndipo Manji alipoingia na kuongeza mitafaruku ktk hatua za mwisho za Yanga kufikia Makubaliano na katika kikao amabcho ni cha mwisho kufanyika Klabuni cha wanachama wa wote wa klabu ya Yanga na Mengi akiwepo Hapa ndiyo Manji aliwanunu kundi la Yusuph Mzimba (Yanga asili Likafanya vujo)Na Mengi kushindwa kulimaliza Gogoro na Kuondolewa Chini ya Ulizni Mkali Kutoka Klabu Ya Yanga pale jangwani hapo ndipo mengi alipopata akili na siku hiyo hiyo alitangaza kujivua na kutoendelea tena na usuluhishi.Hapa ndipo kina mzimba wakafanikisha kazi waliyotumwa na Manji,sasa Manji kwa kutaka kujionyesha yeye ni zaidi kuliko Mengi akaingiza Jeshi na kupenyeza Rupia kwa wingi NA Kuwamwagia mapesa zaidi wote wenye njaa na vyazno vikuu vya migogoro na akafanikiwa kuwasuluhisha na Akaendelea na kuchukua udhamini.(Hapa PR ya Manji ).Ndiyo maana leo Hii UNASIKIA Mzimba Yupo Tunis na Yanga..............Anakula matunda ya Manji,Zitakapo ota mbawa basi watarudi kule kule Lakini so far so good for Yanga.
Sasa itakapotokea Migogoro ya Manji na Mengi Kumalizika Basi ni kweli Yanga wahesabu hawana mdhamini na pengine si hilo tu kwani kwa Historia ya Manji huenda tayari akawa na shares hata za kuinunua Yanga Kampuni Nzima na kuleta mtafaruku wa kisheria.Kwani Huyu huwa hawekezi bure kwenye sehemu yeyote ile...........................!
 
Phillimon mikael. a.k.a Chief marreale.

ZEE LA UKABILA NA UDINI UMERUDI? au ULIENDA KUFANYIWA OPERATION YA MAKENGEZA YAKO?
STAY TUNED.
 
Mzee ES,

Shukran kwa majibu yako Murua,

Umesema kuwa ktk majibu yako hotujibu matusi, hii ina maana mimi nimekutukana? Naomba unifahamishe mahala nilipokutukana (if any) ili tuwekane sawa kwani hata mimi mjadala huu kwangu una umuhimu mkubwa.

Katika majibu yako umesema mtu ahitaji kwenda shule kuelewa hili, naam! nakubaliana na wewe kabisa, kwani itakuwa ni kioja cha mwaka Spika apeleke kesi PCB at the same time aipeleke bungeni kujadiliwa! I know off late standards of our speaker have slipped in the last few occassions, but for lawyer like him to do that will be a joke of the year if not century!

Pia umedai kuwa kama Malima alikuwa na convicing arguments kwanini Manji awahonge Jurors? Hapa tukubaliane tu kuwa haya ni madai na yataendelea kuwa madai mpaka itapokuwa proved otherwise.

Naona ushatoa hukumu kuwa kamati imehongwa which i think is not fair. Hii ni kwa sababu mtu mwingine nae atakuja na madai Mengi kamhonga Ndesamburo, maana Mzee Ndesa kakiri walikuwa wanawasiliana na Mengi time to time.

Mzee Philemon Mikael,

Unadai hii ni zuga tu kuficha uovu ktk uendeshaji wa mifuko ya hifadhi. Baadae ukadai ni UDINI. Kama kuna je udini umeletwa nani? maana ktk kesi hii spika ambae ni mkristo kayafanyia kazi madai ya Mengi ambae ni Mkristo kwa kuyapeleka ktk kamati yenye uwiano karibu sawa wakristo na waislamu na kamati hiyo ndio iliyomuona Bw Malima hana hatia.

Inaonyesha hapa kuna mchezo wa kuigiza inapozungumzwa kamati suala sio udini suala linakuwa rushwa, anapozungumzwa Manji suala linakuwa udini huu sasa ni usanii unaotaka kutuletea Bw. PM

Unadai uamuzi wa spika ni wa busara sana, unadai isingekuwa vizuri kwa Mh Malima kusimamishwa bungeni na kutubu! Hivi huna habari kuwa wabunge kadhaa wameshaombwa kufuta kauli zao? sio tu wa upinzani bali wa CCM. Why not Malima? Who is he? Ndugu Mikael milioni 100 zetu zilizotumika huna huruma nazo na kuzifananisha na kunywa kikombe cha kahawa ofisini kwa Spika!

Mungu Ibariki Tanzania
 
huu mchezo wa bungeni na malima na manji ni mbimu tu,zogo liendelee huku wengine wanaendelea kutumbua pesa za mifuko ya hifadhi walizoiba,.manji amefanya trick kubwa sana akisaidiana na associates wake..yaani kuhamishia attention ya watu kwenye....kufikiri hii kashafa ya nssf imeibuliwa kwa sababu za UDINI ili kuwamaliza yeye na wakurugenzi wa hayo mashirika ya hifadhi ambao ametumia kofia ya udini ili kuvuta hisia za wananchi kwamba wanaonewa.pili hii hoja kupelekwa na kutolewa bungeni ni kati ya malengo ya kubadili akili za watu waamini suala la mabilioni ya manji na nssf,pspf..limezuliwa na mengi kwa kuzingatia chuki na wivu wa mengi dhidi yake kibiashara hasa kwa kuwa wote wameshawahi kushindania kuendesha michezo ya bahati nasibu,..

tatu manji ametumia michezo especially udhamini wake kwa YANGA kama moja ya kampeni zake za PR cleaning....haya mambo yakishasahauliwa YANGA wajue hawana mfadhili...afterall wanaomjua manji wanasema ni SIMBA mzuri tu ila STRATEGISTS wake walimshauri angeingilia simba asingekuja juu mapema kwa sababu kwa wakati huo simba walikuwa na mo na wengine ,ingekuwa ngumu kuwafunika ghafla.




PHILEMON MICHAEL

Mbona unatia aibu? si lazima kila topic ujibu kwani inaonekana kuwa una hamu sana ya kutafuta matatizo kule NSSF lakini naona hupati. Sasa wewe unajua una mchezo unaitwa Character Assassination na hii ni hatari. Nakushauri nex time kama huna data basi wewe unaweza ukawa LURKER tuuu humu ndani kwani italinda heshima yako

huko nyuma ulisema hivi:

kuhusu propaganda nilisema nilihisi kwamba mswahili anapiga sana propaganda dau...kiasi kwamba hamtyendei haki ...ni sawa na kumuharibia ..dau bado ni kijana na nauwezo wa kufanya zaidi sasa kama atahusishwa na mswahili itafanya mbele ya safari akose SIFA ZA KITAIFA...kama anafanya kazi watu wanaona ,hakuna haja ya kumpigia mayowe,wakurugenzi wa mashirika ya umma wapo wengi wanaofanya vizuri...

wakurugenzi waliotangulia wa NSSF kama sikosei mkullo mustapha ,ndie aliyejenga investments nyingi...zikiwemo hosteli za chuo ...sasa kama ujenzi ulipoisha alishastaaafu ..hilo sijui...ni kama uwanja wa taifa mpya utakapoisha mwezi wa saba ,..je tutasema umejengwa na kikwete au mkapa..kwa kifupi maendeleo ya taasisis yoyote ni TEAM WORK na sio ONE MAN SHOW...anaepokea kijiti anakuwa muendelezaji ....

http://www.jamboforums.com/showthread.php?p=24289&highlight=NSSF#post24289


kisha siku chache baadae ukaendelea kusema hivi:

kuhusu NSSF naona hakuna tofauti kati ya dau na mkullo au mattaka...tena sanasana DAU bado hajafanya vivid investment kulinganisha na enzi ya kina mkullo au mattaka [hata mkimsema ..jamaa ni kichwa ]....ila aendelee kujitahidi ..na nafikiri ni mtu anayetumia sana propaganda chini chini..natambua ni PAN AFRICA mzuri na mtoto wa mjini ,,,but we want more results...


http://www.jamboforums.com/showthread.php?p=24278&highlight=NSSF#post24278

na mimi nilikuuliza maswali ambayo mpaka leo HUJAJIBU hata moja ku back up arguments zako. na leo ninarudia kukuliza tena hayo maswali na ukiyajibu then tutaendelea kujadiliana based on hoja katika majibu yako


Je,Dr DAU aliingia NSSF lini?

Alikuta makusanyo pale NSSF chini ya MKULO yalikuwa kiasi gani?

Sasa hivi yako kiasi gani?

Je Kulikuwa na investments za kiasi gani?

Sasa hivi investments zimefikia kiasi gani?

Na ni Propaganda zipi anazitumia kuendesha shirika kubwa la wanachi la NSSF?

Na imekuwaje ameweza kusurvive pale muda wote huo tangu MKAPA amuweke pale?

Kuna udini gani kule NSSF? naomba at least ushahidi wa newsclip.
 
MZEE ES,

HII NIMEITOA KTK KABRASHA LETU, SIJUI ITASAIDIA KUKUPA MWANGA KIDOGO....

Ndesamburo apelekwa PCB


Mengi, Malima uso kwa uso kwa Spika


Mbunge wa Mosho Mjini (CHADEMA), Philemon Ndesamburo


Mbunge wa Mkuranga (CCM) , Adam Malima


Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi

Habari Kamili

Na Epson Luwagho, Uhuru Publications.

MBUNGE wa Moshi Mjini (CHADEMA), Philemon Ndesamburo, ametakiwa kuisaidia Taasisi ya Kuzuia Rushwa (PCB) juu ya tuhuma alizozitoa kuwa Wabunge walihongwa na mfanyabiashara mmoja maarufu wa Dar es Salaam.

Uamuzi huo umefikiwa kufuatia madai aliyoyatoa mwezi uliopita jijini Dar es Salaam wakati wa kusikilizwa kwa shauri la Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi na Mbunge wa Mkuranga (CCM), Adam Malima

Kuhusu suala la Mengi na Malima, Spika wa Bunge, Samuel Sitta, ameamua kulimaliza kwa njia ya usuluhishi kwa kuwa suala hilo limeingia katika suraya ukabila, udini na ubaguzi wa rangi.

Akitoa uamuzi juu ya suala hilo, aliousoma kwa dakika 57, Sitta alisema matamshi ya Ndesamburo ni mazito na yanastahili kufanyiwa uchunguzi na hatimaye kufikishwa katika mkondo wa sheria.

Sitta alisema katika kauli zake kwa nyakati tofauti, Ndesamburo alitoa kauli zilizokuwa zikiashiria kuwa kulikuwepo na vitendo vya rushwa katika kushughulikia suala la Mengi na Malima.

Kwa mujibu wa Spika, Mbunge huyo alisema Mengi alimweleza kwamba Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, isingemtendea haki mfanyabiashara huyo kwa kuwa kulikuwa na vitendo vinavyoashiria kuingiliwa na
serikali.

"Pia alisema alikuwa na taarifa ya ushahidi kuwa Mengi aliitwa na Waziri Mkuu ambaye alimshauri ajitoe katika 'kesi' hiyo kwa kuwa Wabunge wamehongwa na Manji, hivyo asingeshinda.

Spika alisema kauli hiyo ya Ndesamburo ilijikanganya kutokana na maelezo aliyoyatoa, kama ni kamati ndiyo iliyohongwa au Wabunge na pia alishindwa kueleza mtu aliyewahonga Wabunge kama ni mfanyabiashara Yusuf Manji au Manji mwingine.

Kwenye uamuzi huo, Sitta alinukuu barua ya Mbunge huyo iliyosema: "...Sijamtaja Yusuf Manji aliyenitukana magazetini. Mimi nimemtaja Manji tu ambaye anamjua Bwana Mengi na huenda siyo Yusuf Manji."

Kuhusu madai ya rushwa, Spika alisema kwa kuwa yametolewa na mtu mzima, na mzoefu, hayawezi kupuuzwa na kwamba suala la kutoa au kupokea rushwa ni kosa la jinai, hivyo ameamua suala hilo lishughulikiwe na vyombo husika.

Alisema tayari ofisi yake imeshawasiliana na PCB kwa ajili ya kuanza kufanya uchunguzi. Spika pia alisema amemuomba ushauri Katibu wa Bunge juu ya sualala Ndesamburo kufanya mawasiliano na mmoja wa watu wanaochunguzwa katika suala husika.

Kwa upande wa suala la msingi la Mengi na Malima, Sitta alisema matamshi ya Malima yamemuathiri Mengi kwa vile yamemgonganisha na viongozi wakuu wa nchi kama alivyodai Mengi anapewa muda mwingi katika vyombo vyake vya habari kuliko Rais na Waziri Mkuu.

Vile vile alisema matamshi ya Mengi, kupitia vyombo vya habari yamemuathiri Malima kwa sababu Mengi hakutumia utaratibu katika kuelezea malalamiko yake na pia alitumia lugha ya matusi.

Pamoja na kwamba wote waliathirika katika suala hilo, alisema Malima alikiuka kanuni ya 50 (i) ya Bunge kwa kusema uongo kuwa Mengi alipewa muda katika televisheni ya ITV wa dakika 10, kuzungumza na watoto wa madrasa ya Msasani na pia wanafunzi wa Zanzibar walipotembelea, ilhali Rais na Waziri Mkuu walipewa dakika 1.30 kila mmoja.

Hata hivyo, Spika alisema ameamua kutumia busara kulimaliza suala hilo kwa njia ya usuluhushi na kwamba atafanya kazi hiyo Dar es Salaam wakati muafaka watakaona wahusika unafaa.

Katika Bunge la Mkutano wa Bajeti mwaka jana, Malima alilalamika kuwa Mengi alipewa muda mwingi katika vyombo vyake vya habari kuliko viongozi wakati uchunguzi umebaini kuwa siyo kweli.
__________________
 
Can anyone makes sense of this nonsense .I have only one question --is this Adam Malima not the son of Kigoma Malima?Where is all the money his father's stole . Can someone please HELP
 
Mzee Masatu,

Heshima mbele mkuu, kwangu the big picture ni mjadala wa the legal strengh na weaknesses katika hii kesi, wewe umesema nini na mimi nimesema nini sio muhimu sana kwangu,

Anyway ninaheshimu elimu ninayoipata kutoka kwako na wengine wote kwenye huu mjadala, kwenye haka kakitabu ka-Spika kuna article mbili za wabunge waliokwenda kinyume na wenzao, naona maoni yao kuwa ni muhimu sana kisheria maana hata wao wanaashira kuamini kuwa kuna rushwa ilitolewa,

Sendeka alimwambia el uso kwa uso kuwa amepokea rushwa pia, Mama Anna, kamati ilipoanza kikao hakuwepo alikuwa nje ya nchi, aliporudi siku ya kwanza kukaa kwenye kamati hakuamini aliyokuwa akiyasikia na yeye pia kuonyesha wasi wasi wake na rushwa ndani ya kamati, so far hatujasikia kuwa Mengi ametoa rushwa, wote waliotamka wanamuandama Manji,

Ndesamburo alijitoa kwa sababu alidai kuwa Manji amewahonga wabunge, gazeti moja nchini lilikuwa na kichwa cha habari kuwa el amesema Manji amehonga wabunge, sasa unaamini hawa wote walikuwa wanamuhukumu Manji? Kwenye hili la rushwa Malima hayumo kabisaa hili ni deal la Manji, kwa hiyo mimi sijamuhukumu mtu ila ninafuatilia mawazo ya awali ya wabunge,

Ila ndugu yangu bado ninahangaika kujua kama hawa wote waliohusika ni hiii kesi walikuwa under oath, na bado ninamsikitia ndugu yangu Malima kwa kujiingiza kwenye hii mess!
 
next week will be a very interesting week... nasubiri kusikia Makamba akiirudisha barua ya malalamiko ya Malima kwa Kamati ya Wabunge wa CCM... na hapo patakuwa patamu.
 
Mzee Masatu,

Heshima mbele mkuu, kwangu the big picture ni mjadala wa the legal strengh na weaknesses katika hii kesi, wewe umesema nini na mimi nimesema nini sio muhimu sana kwangu,

Anyway ninaheshimu elimu ninayoipata kutoka kwako na wengine wote kwenye huu mjadala, kwenye haka kakitabu ka-Spika kuna article mbili za wabunge waliokwenda kinyume na wenzao, naona maoni yao kuwa ni muhimu sana kisheria maana hata wao wanaashira kuamini kuwa kuna rushwa ilitolewa,

Sendeka alimwambia el uso kwa uso kuwa amepokea rushwa pia, Mama Anna, kamati ilipoanza kikao hakuwepo alikuwa nje ya nchi, aliporudi siku ya kwanza kukaa kwenye kamati hakuamini aliyokuwa akiyasikia na yeye pia kuonyesha wasi wasi wake na rushwa ndani ya kamati, so far hatujasikia kuwa Mengi ametoa rushwa, wote waliotamka wanamuandama Manji,

Ndesamburo alijitoa kwa sababu alidai kuwa Manji amewahonga wabunge, gazeti moja nchini lilikuwa na kichwa cha habari kuwa el amesema Manji amehinga wabunge, sasa unaamini hawa wote walikuwa wanamuhukumu Manji? Kwenye hili la rushwa Malima hayumo kabisaa hili ni deal la Manji, kwa hiyo mimi sijamuhukumu mtu ila ninafuatilia mawazo ya awali ya wabunge,

Ila ndugu yangu bado ninahangaika kujua kama hawa wote waliohusika ni hiii kesi walikuwa under oath, na bado ninamsikitia ndugu yangu Malima kwa kujiingiza kwenye hii mess!

Ninaona kuwa mtazamo wako kweli una mantiki. Wengi wanakimbilia swala la demokrasia ya wengi wape hata kama kuna ushahidi otherwise. Pamoja na mapungufu yake spika, sidhani kuwa uamuzi wake ulikuwa nje ya madaraka yake. (a) Kanuni za bunge zinampa spika mamlaka ya kubypass maamuzi ya kamati yoyote; alitumia mamlaka hayo. (b) Spika alishaona kuwa kuna reasonable doubt kuhusu impartiality ya kamati hiyo kutokana na kuwepo kwa madai ya rushwa. Kwa hiyo, kwa vile jukumu la kuthibitisha rushwa linashughulikiwa na chombo vingine, spika alitakiwa asubiri hadi kukamilika kwa upelelezi wa madai hayo ya rushwa kabla ya ripoti ya kamati hiyo kupokelewa bungeni. Badala ya kusubiri muda wote huo, yeye aliamua kutumia madaraka yake kuibypass kamati na kuwapatisha Mengi na Malima akidhani kuwa kwa kufanya hivyo mambo yataisha; hilo ndilo kosa alilofanya lakini uamuzi wake huo ulikuwa chini ya mamlaka yake.
 
Mzee Wangu,

Unafikiri ni kwa nini wakati zingine tumeziona? Makamba atakuwa anaficha nini? Lakini tutailalia macho hiyo barua tutaipata tu!

Mzee Kichuguuuu,

Heshima mbele mkuu, nafikiri ni very important hiyo hoja kwamba Spika angesubiri kwanza matokeo ya uchunguzi wa PCB, ndipo atoe uamuzi kwa sababu matokeo ya mambo aliyoyafanya kienyeji amefungua mianya kwa Mengi na Manji kwenda mahakamani at anytime wakihisi kutoridhika na maamuzi ya huko mbele, au ya sasa!

Ninaanza kuwa na wasi wasi na role ya Spika kwenye hii kesi nzima, kutokana na hizi facts zinavyojitokeza!
 
next week will be a very interesting week... nasubiri kusikia Makamba akiirudisha barua ya malalamiko ya Malima kwa Kamati ya Wabunge wa CCM... na hapo patakuwa patamu.

Jumanne tarehe 10 baada tu ya kiipindi cha maswali na majibu...........kahistoria kadogo kuandikwa juu ya uhuru wa Bunge kwa mujibu wa ibara za katiba 8, 63 na 100. Pia sheria na.3 ya mwaka 1988 na kanuni za Bunge. Fuatila kwa makini............................
 
Mzee Wangu,

Unafikiri ni kwa nini wakati zingine tumeziona? Makamba atakuwa anaficha nini? Lakini tutailalia macho hiyo barua tutaipata tu!

Mzee Kichuguuuu,

Heshima mbele mkuu, nafikiri ni very important hiyo hoja kwamba Spika angesubiri kwanza matokeo ya uchunguzi wa PCB, ndipo atoe uamuzi kwa sababu matokeo ya mambo aliyoyafanya kienyeji amefungua mianya kwa Mengi na Manji kwenda mahakamani at anytime wakihisi kutoridhika na maamuzi ya huko mbele, au ya sasa!

Ninaanza kuwa na wasi wasi na role ya Spika kwenye hii kesi nzima, kutokana na hizi facts zinavyojitokeza!

Mzee Es, salamu mzee
unataka Spika aache kazi zake mpaka PCB wamalize kazi yao? PCB wanachunguza rushwa na waendelee. Spika anaendesha Bunge na lazima alinde hadhi ya Bunge. Tusubiri Jumanne
 
Jumanne tarehe 10 baada tu ya kiipindi cha maswali na majibu...........kahistoria kadogo kuandikwa juu ya uhuru wa Bunge kwa mujibu wa ibara za katiba 8, 63 na 100. Pia sheria na.3 ya mwaka 1988 na kanuni za Bunge. Fuatila kwa makini............................

Hiyo itakuwa maada au semina?Na kama ni mada mtoaji ni nani?au mimi sijaelewa kitakachojiri baada ya hicho kipindi cha maswali?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom