kuna ukweli juu ya hii taarifa au uzushi tu
- Tunachokijua
- Leo Machi 8, 2025 kwa mujibu wa ratiba ya ligi kuu ya NBC Tanzania umepangwa mchezo dhidi ya Simba sports club na Dar es salaam Young Africans katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es salaam.
Klabu ya Simba usiku wa kuamkia Machi 8, walitoa taarifa kwa umma kuelekea mchezo huo kuwa hawatoshiriki katika mchezo huo, kutokana na walivyoviita vitendo visivyo vya kiungwana dhidi ya timu yao kwa kunyimwa haki ya kufanya mazoezi katika uwanja wa Benjamini Mkapa kinyume na kanuni.
Madai
Kumekuwapo na barua inayosambaa inayoonesha kuwa bodi ya ligi kuu Tanzania (TPLB) wamejibu Taarifa kwa umma iliyotolewa na timu ya Simba Sporst Club, ambapo pamoja na mambo mengine barua hiyo ya bodi inaeleza kuwa imeona malalamiko ya Simba lakini wanaagiza mchezo huo uendelee kama ulivyopangwa kuheshimu ratiba ya ligi.
Uhalisia wa taarifa hiyo
JamiiCheck imefuatilia barua hiyo na kubaini kuwa si ya kweli na hivyo haijatolewa na bodi ya ligi Tanzania (TBLB). Ufuatiliaji umebaini mapungufu kadhaa katika barua hiyo ukilinganisha na barua rasmi zilizowahi kutolewa na bodi ya ligi.
Barua iliyotolewa ina mapungufu kadhaa ikiwemo kuchanganya aina zaidi ya moja ya mwandiko (Fonts), Mwandiko uliotumika katika kiini cha ujumbe (mainbody) ni tofauti na mwandiko uliotumika katika anuani na tarehe mwisho wa barua.
Ufuatiliaji wa kimtandao umebaini pia kuwa barua hiyo haijachapishwa katika kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya TFF.
Mwenyekiti wa bodi ya ligi kuu Steven Mguto alifanya mahojiano na kituo cha habari cha E-FM asubuhi ya Machi 8, 2025 amesema kuwa ameyasikia malalamiko ya Simba na hivyo anaitisha kikao cha dharura cha Saa 72 kujadili suala hilo na kisha watatoa taarifa, hii inaendelea kubainisha kuwa barua inayosambaa si rasmi
Bodi ya Ligi baada kufanya kikao chake cha saa walitoa barua rasmi na kueleza kuwa mchezo huo hautochezwa hadi itakapotangazwa tena.