SI KWELI Barua ya bodi ya ligi kuwaambia Simba mchezo upo kama kawaida, Kariakoo Derby Machi 8, 2025

SI KWELI Barua ya bodi ya ligi kuwaambia Simba mchezo upo kama kawaida, Kariakoo Derby Machi 8, 2025

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
kuna ukweli juu ya hii taarifa au uzushi tu
1741421505245.png
 
Tunachokijua
Leo Machi 8, 2025 kwa mujibu wa ratiba ya ligi kuu ya NBC Tanzania umepangwa mchezo dhidi ya Simba sports club na Dar es salaam Young Africans katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es salaam.

Klabu ya Simba usiku wa kuamkia Machi 8, walitoa taarifa kwa umma kuelekea mchezo huo kuwa hawatoshiriki katika mchezo huo, kutokana na walivyoviita vitendo visivyo vya kiungwana dhidi ya timu yao kwa kunyimwa haki ya kufanya mazoezi katika uwanja wa Benjamini Mkapa kinyume na kanuni.

Madai

Kumekuwapo na barua inayosambaa inayoonesha kuwa bodi ya ligi kuu Tanzania (TPLB) wamejibu Taarifa kwa umma iliyotolewa na timu ya Simba Sporst Club, ambapo pamoja na mambo mengine barua hiyo ya bodi inaeleza kuwa imeona malalamiko ya Simba lakini wanaagiza mchezo huo uendelee kama ulivyopangwa kuheshimu ratiba ya ligi.

Uhalisia wa taarifa hiyo

JamiiCheck imefuatilia barua hiyo na kubaini kuwa si ya kweli na hivyo haijatolewa na bodi ya ligi Tanzania (TBLB). Ufuatiliaji umebaini mapungufu kadhaa katika barua hiyo ukilinganisha na barua rasmi zilizowahi kutolewa na bodi ya ligi.

Barua iliyotolewa ina mapungufu kadhaa ikiwemo kuchanganya aina zaidi ya moja ya mwandiko (Fonts), Mwandiko uliotumika katika kiini cha ujumbe (mainbody) ni tofauti na mwandiko uliotumika katika anuani na tarehe mwisho wa barua.

Ufuatiliaji wa kimtandao umebaini pia kuwa barua hiyo haijachapishwa katika kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya TFF.

Mwenyekiti wa bodi ya ligi kuu Steven Mguto alifanya mahojiano na kituo cha habari cha E-FM asubuhi ya Machi 8, 2025 amesema kuwa ameyasikia malalamiko ya Simba na hivyo anaitisha kikao cha dharura cha Saa 72 kujadili suala hilo na kisha watatoa taarifa, hii inaendelea kubainisha kuwa barua inayosambaa si rasmi

Bodi ya Ligi baada kufanya kikao chake cha saa walitoa barua rasmi na kueleza kuwa mchezo huo hautochezwa hadi itakapotangazwa tena.
Huwa nachunguza maandishi, hasa font type na font size. Nikiona ndani ya barua moja kuna mahali vimetofautiana, najua sio waraka halisi

1000024190.jpg
 
YAH: TAARIFA YA SIMBA SPORTS CLUB KUHUSU MCHEZO WA LIGI KUU NBC DHIDI YA YANGA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea barua ya malalamiko kutoka Simba Sports Club kuhusu changamoto zilizojitokeza kabla ya mechi ya Ligi Kuu NBC dhidi ya Yanga. Tumechukua hatua za haraka kufanya uchunguzi wa tukio hilo.

Pamoja na hayo, tunapenda kuwajulisha kwamba kwa mujibu wa Kanuni ya 15(10) ya Kanuni za Ligi Kuu Bara", timu yoyote inayoshiriki Ligi Kuu ina wajibu wa kushiriki michezo yote iliyoratibiwa na kuandaliwa na TFF bila kukosa, isipokuwa kutakuwepo na sababu maalum zilizoidhinishwa rasmi na Shirikisho.

Aidha, kukosa kushiriki mchezo husika kunaweza kupelekea adhabu kulingana na Kanuni ya 16(1) inayohusu maamuzi dhidi ya timu zisizotii ratiba za ligi.

Pia, kwa mujibu wa Kanuni ya 17(45) inayotaja haki ya kufanya mazoezi uwanjani, tunahakikisha masuala hayo yanafuatiliwa kwa kina, na hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya wahusika wa uvunjifu wa kanuni hizo.

Hivyo basi, kwa kufuata kanuni za Shirikisho, tunawaagiza kuendelea na mchezo kama ulivyopangwa ili kuheshimu ratiba ya Ligi Kuu NBC na kuzingatia maslahi ya mashabiki, wadhamini, na ligi kwa ujumla. Malalamiko kuhusu changamoto zilizojitokeza yatafanyiwa kazi kwa wakati unaofaa.

TFF inaendelea kujitahidi kuhakikisha ligi inaendeshwa kwa haki na uwazi kwa kuzingatia kanuni zilizopo. Tunasihi mshirikiane kwa dhati ili kuhakikisha mchezo huu unachezwa kwa amani na kufanikisha ligi bora zaidi.

Idara Ya Habari Mawasiliano
Bodi Ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB)
Machi 8, 2025
 
Hao Bodi ya Ligi walikuwa wapi kuhakikisha kanuni na taratibu zinafuatwa za Timu mwenyeji kufanya mazoezi?
 
TFF haina uwezo wa kufanya maamuzi magumu kwenye hii derby iwapo Simba au Yanga zitagomea mchezo.

Hawawezi kumpa mtu point 3 mezani tena zikiwa zinapishana alama chache hivyo.

Karia ataambiwa alete vitambulisho vya kuzaliwa vya babu na bibi yake!

Kuna wanasiasa nyuma ya maamuzi ya hizi timu.
 
Back
Top Bottom