PreGE2025 Barua ya CHADEMA ikimjibu Lembrus Mchome kuhusu malalamiko ya kupitishwa kwa viongozi kinyume na katiba ya chama

PreGE2025 Barua ya CHADEMA ikimjibu Lembrus Mchome kuhusu malalamiko ya kupitishwa kwa viongozi kinyume na katiba ya chama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
YAH: MALALAMIKO YA KUTHIBITISHWA/KUPITISHWA KWA VIONGOZI KINYUME NA KATIBA YA CHAMA
​
Nakiri kupokea barua yako yenye Kumb. Na. KM/CDM/A-B/2025 ya tarehe 18 Februari 2025 kuhusu somo tajwa hapo juu. Baada ya kupitia kumbukumbu za mahudhurio ya kikao cha Baraza Kuu cha tarehe 22 Januari, 2025, ninapenda kujibu madai yako kama ifuatavyo:

1. Kwamba idadi ya wajumbe halali wa Baraza Kuu waliohudhuria kikao hicho ni 234, ambayo ni sawa na asilimia 56.8 ya wajumbe wote.

2. Kwamba kwa mujibu wa Katiba yetu ya Chama ibara ya 6.2.2(a), kikao halali cha ngazi ya kawaida, kama vile Baraza Kuu, kinahitaji akidi ya asilimia 50 ya wajumbe wote wa kikao hicho:

3. Kwamba, Kikao halali cha maamuzi ya kisera, au cha uchaguzi, au cha kurekebisha Katiba ya Chama, kama vile Mkutano Mkuu wa Chama Taifa, kinahitaji akidi ya asilimia 75 ya wajumbe wote wa kikao hicho;

4. Kwamba, Kikao cha Baraza Kuu unachokilalamikia hakiwezi kuwa kikao cha maamuzi ya kisera au kikao cha uchaguzi au cha kubadilisha Katiba bali kilikuwa kikao cha kawaida cha Baraza Kuu kwa ajili ya kutekeleza majukumu ya kawaida ya Baraza Kuu yaani kuthibitisha jina la Katibu Mkuu, Manaibu Katibu Wakuu na wajumbe wa Kamati Kuu walioteuliwa na Mwenyekiti wa Chama:

5. Kwamba, Bi. Lilian Masiaga na Eng. Dr. Nyamatari Anselm Tengecha, unaodai walikuwepo ndani ya ukumbi wa kikao cha Baraza Kuu sio wajumbe na hawapo kwenye orodha ya mahudhurio ya wajumbe wa Baraza Kuu. Kwa hiyo kuwepo au kutokuwepo kwao hakuwezi kuathiri akidi ya kikao cha Baraza Kuu wala kubatilisha maamuzi yaliyofanyika. katika kikao tajwa.

6. Kwamba, kwa mujibu wa kumbukumbu za kikao cha Baraza Kuu unachokilalamikia, wewe mwenyewe hukuhudhuria kikao hicho. Kwa hiyo, inaelekea malalamiko yako yametokana na maneno ya kuambiwa ama ya kuhisi, lakini yasiyokuwa na ukweli au msingi wowote:

7. Kwamba, ingependeza sana kama mwanachama na kiongozi wa chama kama ungetafuta ukweli wa jambo hili kwenye ofisi yangu kwanza kabla ya kuandika na kusambaza uzushi huu mitandaoni na kwenye vyombo vya habari na hivyo kuleta taharuki ya bure kwa wanachama na wananchi;

8. Kwamba, kwa sababu zote nilizozitaja hapo juu, malalamiko na maombi yako yote hayana ukweli wala msingi wowote.

Wako katika demokrasia na maendeleo.
John Mnyika
KATIBU MKUU
1747143646317.png

1747142902034.png
 
Angalia tarehe basi shida unapenda kukurupuka
hata mwaka muandaa hiyo script ya barua angeweza kuandika 2020 gentleman,
kwani tarehe nini, na mbona hiyo barua hakupewa mchome tarehe hiyo? :pedroP:
 
YAH: MALALAMIKO YA KUTHIBITISHWA/KUPITISHWA KWA VIONGOZI KINYUME NA KATIBA YA CHAMA
​
Nakiri kupokea barua yako yenye Kumb. Na. KM/CDM/A-B/2025 ya tarehe 18 Februari 2025 kuhusu somo tajwa hapo juu. Baada ya kupitia kumbukumbu za mahudhurio ya kikao cha Baraza Kuu cha tarehe 22 Januari, 2025, ninapenda kujibu madai yako kama ifuatavyo:

1. Kwamba idadi ya wajumbe halali wa Baraza Kuu waliohudhuria kikao hicho ni 234, ambayo ni sawa na asilimia 56.8 ya wajumbe wote.

2. Kwamba kwa mujibu wa Katiba yetu ya Chama ibara ya 6.2.2(a), kikao halali cha ngazi ya kawaida, kama vile Baraza Kuu, kinahitaji akidi ya asilimia 50 ya wajumbe wote wa kikao hicho:

3. Kwamba, Kikao halali cha maamuzi ya kisera, au cha uchaguzi, au cha kurekebisha Katiba ya Chama, kama vile Mkutano Mkuu wa Chama Taifa, kinahitaji akidi ya asilimia 75 ya wajumbe wote wa kikao hicho;

4. Kwamba, Kikao cha Baraza Kuu unachokilalamikia hakiwezi kuwa kikao cha maamuzi ya kisera au kikao cha uchaguzi au cha kubadilisha Katiba bali kilikuwa kikao cha kawaida cha Baraza Kuu kwa ajili ya kutekeleza majukumu ya kawaida ya Baraza Kuu yaani kuthibitisha jina la Katibu Mkuu, Manaibu Katibu Wakuu na wajumbe wa Kamati Kuu walioteuliwa na Mwenyekiti wa Chama:

5. Kwamba, Bi. Lilian Masiaga na Eng. Dr. Nyamatari Anselm Tengecha, unaodai walikuwepo ndani ya ukumbi wa kikao cha Baraza Kuu sio wajumbe na hawapo kwenye orodha ya mahudhurio ya wajumbe wa Baraza Kuu. Kwa hiyo kuwepo au kutokuwepo kwao hakuwezi kuathiri akidi ya kikao cha Baraza Kuu wala kubatilisha maamuzi yaliyofanyika. katika kikao tajwa.

6. Kwamba, kwa mujibu wa kumbukumbu za kikao cha Baraza Kuu unachokilalamikia, wewe mwenyewe hukuhudhuria kikao hicho. Kwa hiyo, inaelekea malalamiko yako yametokana na maneno ya kuambiwa ama ya kuhisi, lakini yasiyokuwa na ukweli au msingi wowote:

7. Kwamba, ingependeza sana kama mwanachama na kiongozi wa chama kama ungetafuta ukweli wa jambo hili kwenye ofisi yangu kwanza kabla ya kuandika na kusambaza uzushi huu mitandaoni na kwenye vyombo vya habari na hivyo kuleta taharuki ya bure kwa wanachama na wananchi;

8. Kwamba, kwa sababu zote nilizozitaja hapo juu, malalamiko na maombi yako yote hayana ukweli wala msingi wowote.

Wako katika demokrasia na maendeleo.
John Mnyika
KATIBU MKUU
View attachment 3332759
View attachment 3332741
Kama hao waliotajwa hawakuwa Wajumbe halali, walikuwa na shughuli gsni huko ndani?
 
Uhalali wa Baraza Kuu na Uteuzi-1 (1).jpg



Uhalali wa Baraza Kuu na Uteuzi-1 (1)-2.jpg


Chama cha Demoktasia na Maendeleo (Chadema) kimesisitiza kuwa kikao cha Barza Kuu kilichoketi Januari 22, 2025 na kuwathibitisha baadhi ya viongozi walioteuliwa na Mwenyekiti Tundu Lissu kilikuwa halali.
Soma zaidi: Msajili atengua uteuzi wa wajumbe

Hatua hiyo inafuatia taarifa za Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kubatilisha viongozi walioteuliwa na kikao hicho leo Mei 13, kutokana na malalamiko yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro, Lembrus Mchome anayedai kuwa kikao hicho hakikuwa halali kwa kuwa akidi haikutimia.

Viongozi wanaolalamikiwa na msajili ameamua kuwaweka kando hadi Baraza kuu jingine liitishwe ni Katibu Mkuu, John Mnyika, Amani Golugwa (Naibu Katibu Mkuu – Bara) na Ally Ibrahim Juma (Naibu Katibu Mkuu – Zanzibar).

Wengine ni wajumbe wa kamati kuu walioteuliwa na kuidhinishwa na Baraza Kuu, Godbless Lema, Rose Mayemba, Salma Kasanzu, Hafidh Ally Saleh na Dk Rugemeleza Nshala ambaye pia aliteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa chama hicho.
Soma zaidi
Kupitia barua iliyosainiwa na Katibu Mkuu, John Mnyika ya Februari 20, 2025 kwenda kwa Lembrus Mchome aliyekiandikia chama hicho Februari 18, 2025, chama hicho kimesisitiza kuwa kikao kilifuata Katiba ya chama.

Barua hiyo imesambazwa kwenye vyombo vya habari leo Mei 13 na chama hicho kikienedelea kusisitiza msimamo wake kuhusu hatua iliyochukuliwa na Msajili wa Vyama vya Saisa.

Mnyika amesema idadi ya wajumbe halali wa Baraza Kuu waliohudhuria kikao hicho ni 234, ambayo ni sawa na asilimia 56.8 ya wajumbe wote, ambapo kwa mujibu wa Katiba ya Chadema ibara ya 6.2.2(a), kikao halali cha ngazi ya kawaida, kama vile Baraza Kuu, kinahitaji akidi ya asilimia 50 ya wajumbe wote wa kikao hicho:

“Kikao halali cha maamuzi ya kisera, au cha uchaguzi, au cha kurekebisha Katiba ya Chama, kama vile Mkutano Mkuu wa Chama Taifa, kinahitaji akidi ya asilimia 75 ya wajumbe wote wa kikao hicho, kikao cha Baraza Kuu unachokilalamikia hakiwezi kuwa kikao cha maamuzi ya kisera au kikao cha uchaguzi au cha kubadilisha Katiba bali kilikuwa kikao cha kawaida cha Baraza Kuu kwa ajili ya kutekeleza majukumu ya kawaida ya Baraza Kuu yaani kuthibitisha jina la Katibu Mkuu, Manaibu Katibu Wakuu na wajumbe wa Kamati Kuu walioteuliwa na Mwenyekiti wa Chama,” ameeleza Mnyika katika barua hiyo.

Ameendelea, “Bi. Lilian Masiaga na Eng. Dr. Nyamatari Anselm Tengecha, unaodai walikuwepo ndani ya ukumbi wa kikao cha Baraza Kuu sio wajumbe na hawapo kwenye orodha ya mahudhurio ya wajumbe wa Baraza Kuu. Kwa hiyo kuwepo au kutokuwepo kwao hakuwezi kuathiri akidi ya kikao cha Baraza Kuu wala kubatilisha maamuzi yaliyofanyika katika kikao tajwa.

“Kwa mujibu wa kumbukumbu za kikao cha Baraza Kuu unachokilalamikia, wewe mwenyewe hukuhudhuria kikao hicho. Kwa hiyo, inaelekea malalamiko yako yametokana na maneno ya kuambiwa ama ya kuhisi, lakini yasiyokuwa na ukweli au msingi wowote:

“Ingependeza sana kama mwanachama na kiongozi wa chama kama ungetafuta ukweli wa jambo hili kwenye ofisi yangu kwanza kabla ya kuandika na kusambaza uzushi huu mitandaoni na kwenye vyombo vya habari na hivyo kuleta taharuki ya bure kwa wanachama na wananchi. Kwa sababu zote nilizozitaja hapo juu, malalamiko na maombi yako yote hayana ukweli wala msingi wowote,” ameeleza Mnyika.
 
Walisha andika na Mnyika aliweka mpaka press muda umepita ! Naona CCM badala ya kujadili hoja sasa ni shika shika ! Hii haitabadilisha wananchi. Msingi mkubwa huwezi kuuwa hoja kwa Polisi
kwahiyo barua inajibiwa na press confrence gentlema, right? :pedroP:
 
Sijui nimetigwa na mawazo mengi au nini. Kule katiba yao haikufuatwa kabisa na sajili jumba kavaa tinted huku katiba haikufuatwa lakini wanasema mlalamikaji hakuwepo kikaoni sajili jumba kavaa kiona mbali
 
Mapolisi, Kitengo, ofisi ya msajili, nk. nk. Lakini CHADEMA iko IMARA.
Maua kwa CHADEMA💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐

Kama Mama BP inataka kufanya yake kwanini asiombe serikali ya mpito ya mseto ambayo itakaa mpaka tupate KATIBA MPYA TUME HURU halafu after three years tufanye general election.
 
Back
Top Bottom