PreGE2025 Barua ya CHADEMA ikimjibu Lembrus Mchome kuhusu malalamiko ya kupitishwa kwa viongozi kinyume na katiba ya chama

PreGE2025 Barua ya CHADEMA ikimjibu Lembrus Mchome kuhusu malalamiko ya kupitishwa kwa viongozi kinyume na katiba ya chama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
YAH: MALALAMIKO YA KUTHIBITISHWA/KUPITISHWA KWA VIONGOZI KINYUME NA KATIBA YA CHAMA
​
Nakiri kupokea barua yako yenye Kumb. Na. KM/CDM/A-B/2025 ya tarehe 18 Februari 2025 kuhusu somo tajwa hapo juu. Baada ya kupitia kumbukumbu za mahudhurio ya kikao cha Baraza Kuu cha tarehe 22 Januari, 2025, ninapenda kujibu madai yako kama ifuatavyo:

1. Kwamba idadi ya wajumbe halali wa Baraza Kuu waliohudhuria kikao hicho ni 234, ambayo ni sawa na asilimia 56.8 ya wajumbe wote.

2. Kwamba kwa mujibu wa Katiba yetu ya Chama ibara ya 6.2.2(a), kikao halali cha ngazi ya kawaida, kama vile Baraza Kuu, kinahitaji akidi ya asilimia 50 ya wajumbe wote wa kikao hicho:

3. Kwamba, Kikao halali cha maamuzi ya kisera, au cha uchaguzi, au cha kurekebisha Katiba ya Chama, kama vile Mkutano Mkuu wa Chama Taifa, kinahitaji akidi ya asilimia 75 ya wajumbe wote wa kikao hicho;

4. Kwamba, Kikao cha Baraza Kuu unachokilalamikia hakiwezi kuwa kikao cha maamuzi ya kisera au kikao cha uchaguzi au cha kubadilisha Katiba bali kilikuwa kikao cha kawaida cha Baraza Kuu kwa ajili ya kutekeleza majukumu ya kawaida ya Baraza Kuu yaani kuthibitisha jina la Katibu Mkuu, Manaibu Katibu Wakuu na wajumbe wa Kamati Kuu walioteuliwa na Mwenyekiti wa Chama:

5. Kwamba, Bi. Lilian Masiaga na Eng. Dr. Nyamatari Anselm Tengecha, unaodai walikuwepo ndani ya ukumbi wa kikao cha Baraza Kuu sio wajumbe na hawapo kwenye orodha ya mahudhurio ya wajumbe wa Baraza Kuu. Kwa hiyo kuwepo au kutokuwepo kwao hakuwezi kuathiri akidi ya kikao cha Baraza Kuu wala kubatilisha maamuzi yaliyofanyika. katika kikao tajwa.

6. Kwamba, kwa mujibu wa kumbukumbu za kikao cha Baraza Kuu unachokilalamikia, wewe mwenyewe hukuhudhuria kikao hicho. Kwa hiyo, inaelekea malalamiko yako yametokana na maneno ya kuambiwa ama ya kuhisi, lakini yasiyokuwa na ukweli au msingi wowote:

7. Kwamba, ingependeza sana kama mwanachama na kiongozi wa chama kama ungetafuta ukweli wa jambo hili kwenye ofisi yangu kwanza kabla ya kuandika na kusambaza uzushi huu mitandaoni na kwenye vyombo vya habari na hivyo kuleta taharuki ya bure kwa wanachama na wananchi;

8. Kwamba, kwa sababu zote nilizozitaja hapo juu, malalamiko na maombi yako yote hayana ukweli wala msingi wowote.

Wako katika demokrasia na maendeleo.
John Mnyika
KATIBU MKUU
View attachment 3332759
View attachment 3332741
Mnyika anasumbuliwa na njaa
 
Unacho tia shaka ni pale wewe ambaye ni mwana CCM kindakindaki unahangaika na barua za CHADEMA wakati nyie CCM bado hamjamalizana na huyo aliye jipitisha Dodoma na mnaogopa hata kuhoji,ila mna manung'uniko mioyoni mwenu.
relax gentleman na kuzingatia hoja zangu kitaalamu, sio kuropoka tu 🐒
 
Aisee, mh Lissu kakata mirija mingi iliyokuwa inanyonya chama kupitia mwenyekiti mbowe.
Sasa warudi tu kitaa waishi maisha halisi ya watanzania wa kawaida tunayoishi.
Njaa ni mbaya sana.
Inawezekana aisee, maana si kwa malalamiko haya ,daaah!! Kila mtu anaoiga kelele mpaka unajiuliza why????? Na nafikiri mrija mkubwa ni wa FAM sasa hawa wengine ni walikua wana vi sub-mirija kwenye main-mrija
 
Back
Top Bottom