May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Ili apotoshe uma mwingi?Wazee wetu kama nyinyi mlitakiwa kuwepo kwenye ya idara serikalini kwa kumbukumbu kama hizi ili zisiweze kupotea kirahisi, upate umri mrefu sana Mzee wetu Mohamed Said.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ili apotoshe uma mwingi?Wazee wetu kama nyinyi mlitakiwa kuwepo kwenye ya idara serikalini kwa kumbukumbu kama hizi ili zisiweze kupotea kirahisi, upate umri mrefu sana Mzee wetu Mohamed Said.
Huu ndio uongo wa kulaaniwa, ingawa Mleta uzi hasemi hivyo moja kwa moja ila ni dhahiri kuwa haya ndio anayopigania Watu waone ndivyo ilivyokuwa.UNO walimtaka Mkristo ndio akabidhiwe nchi kulikuwa na wasomi kama Said Fundikira aliehitimu Makerere kabla ya Mwl lakini hakufit
Gas...UNO walimtaka Mkristo ndio akabidhiwe nchi kulikuwa na wasomi kama Said Fundikira aliehitimu Makerere kabla ya Mwl lakini hakufit
Rudia kusoma mkuu. Nyerere aliutafuta utakatifu. Hata wewe pia utafute utakatifu. Tenda yale yanayompendeza Mungu.Mh!
Utakatifu?
basi hata Jiwe atakuja kuomba utakatifu
JK,Mohamed Said,
..inasemekana kuna barua ya Mwalimu Nyerere kwenda kwa Kanisa Katoliki akiwashutumu kujiingiza ktk mambo ya siasa. Nimeambiwa barua hiyo inapatikana ktk moja ya vitabu vinavyozungumzia mahusiano kati ya Kanisa na dola hapa Tz. Sijui kama una kitabu chenye barua hiyo, nitashukuru ukiweza ku-share na sisi. Yuko mkongwe mwenzetu Companero aliahidi kuileta hapa JF lakini naona amepotea siku hizi.
May Day,Ili apotoshe uma mwingi?
Mimi si Mtaalamu sana wa Kiswahili, na sijatumia neno 'muongo'.....nadhani kuna tofauti ya uongo na kupotosha, kwa maoni yangu muongo huweza kusema kisicho ukweli 100%, na anayepotosha huweza kusema yaliyo na ukweli ila akaongeza 'chumvi' au kupunguza kwa lengo la kufikia malengo yake. Ndio maana sikutaja moja kwa moja kama Muongo.May Day,
Kitabu leo kipo miaka 20 kimechapwa mara nne na hajatokea mtu yeyote kusema kuwa mimi ni muongo.
Kilichofanyika ni kuundwa jopo linaloongozwa na Prof. Issa Shivji akiwa na Prof. Saida Yahya na Dr. Kamatha ambao sasa wanaandika historia ya Mwalimu Nyerere ili angalau wapate kufahamu nafasi yake katika kuasisi harakati za kujikomboa kutoka ukoloni.
Jopo hili wamefanya mazungumzo na mimi nyumbani kwangu mara mbili na nimewapa picha na nakala za nyaraka kutoka Nyaraka za Sykes ambazo baadhi wamepata kuzionyesha katika Kavazi la Mwalimu Nyerere ambalo Prof. Shivji ni Mwenyekiti wake.
Marehemu Prof. Haroub Othman kaonana uso kwa macho na Mwalimu Nyerere kuhusu kitabu cha Ali Muhsin Barwani, ''Conflict and Harmony in Zanzibar,' Dubai (1997) na ''The Life and Times of Abdulwahis Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika, London (1998), vitabu viwili ambavyo Mwalimu katajika sana.
Kama ilivyokuwa kwako wewe Prof. Haroub alichomwa sana na historia hii niliyoandika akili yake ilikuwa inakataa kama yale anayosoma ni kweli.
Mimi nilizungumza na Prof. Haroub ambae ni mwalimu wangu na yeye ndiye aliyeniambia kuwa ameonana na Mwalimu na akamuomba na yeye aandike ili yapatikane majibu kwangu na kwa Sheikh Ali Muhsin.
Napenda kukufahamisha kuwa baada ya kuzungumza na mimi hakutosheka Prof. Haroub alikwenda kufanya mazungumzo na Ahmed Rashad Ali mtu aliyekuwa rafiki kipenzi na Abdul Sykes kutaka ukweli wa yale yeye alikuwa na mashaka.
Prof. Haroub aliondoka katika mazungumzo yake akiwa kichwa kainamisha.
Mimi sina sababu ya kuzua uongo.
View attachment 1221898
Kulia: Prof. Haroub Othman, Ahmed Rashad Ali na Ahmed Islam 1997
View attachment 1221902
Kulia: Prof. Issa Shivji, Prof. Saida Othman na Dr. Kamatha siku walipokuja kufanya mazungumzo na Mwandishi kuhusu kitabu cha Abdul Sykes
This strange and very interesting indeed.Mbona hata waasisi wa TAA Zanzibar nao walikuwa wakatoliki, na baadae wakawatafuta Waislamu ili waunde ASP na kutafuta Uhuru wa Zazibar?
View attachment 1221456
IT'S A STRANGE ATTITUDE OF EAST AFRICA POLITICS ENGINEERED BY BRITISH.
sawa, Mkuu.Tujitegemee,
Hiyo barua nimeletewa hivyo ilivyo.
May Day,Mimi si Mtaalamu sana wa Kiswahili, na sijatumia neno 'muongo'.....nadhani kuna tofauti ya uongo na kupotosha, kwa maoni yangu muongo huweza kusema kisicho ukweli 100%, na anayepotosha huweza kusema yaliyo na ukweli ila akaongeza 'chumvi' au kupunguza kwa lengo la kufikia malengo yake. Ndio maana sikutaja moja kwa moja kama Muongo.
Kama lengo la Makala zako ni kuwapamba/kuwatambulisha wale unaodhani wana ushiriki wao kwenye harakati za kupigania Uhuru, basi huna sababu ya kumuingiza/kumtaja Mwalimu ki hila hila na kumuonyesha kama Mtu 'aliyedandia' tu harakati zile.
Kufanya hivyo sio haki kabisa, kama huna taarifa za kutosha kumuhusu Mwalimu na chimbuko lake kwenye harakati ni bora ungebaki kuwaelezea hawa ambao una taarifa zao za kutosha na kusubiri watakaotafuta taarifa za Mwalimu ndio wamuelezee Mwalimu.
Sioni tatizo kwa yeyote kama Prof Haroub kushangazwa na baadhi ya mambo kwani huenda kweli hawakuyajua kabla, nadhani kitakachowasikitisha Wasomaji ni namna unavyotumia kupasha taarifa hizo kwa lengo la kupindisha mambo.
Sikuwahi kusema Mwalimu ndiye alipeleka TANU kwa kina Sykes.May Day,
Laiti ningeandika kwa nia ya kupindisha mambo ningelikiua hiki kitabu changu zamani sana.
Lakini kwa kuwa kitabu hiki nimekiandika kwa nia ya kusahihisha historia ambayo kwa hakika haikuwa historia ya kweli ya TANU, kitabu hiki leo miaka 20 baada ya kuchapwa tuko hapa tunakijadili na kipo toleo la nne.
Mimi napenda nikutaarifu kuwa nina taarifa za kutosha kuhusu Mwalimu Nyerere na historia yake katika TANU.
Mwalimu kafika Dar es Salaam 1952 kapokewa na wazee wangu na naweza kukutajia majina yao mmoja baada ya mwingine wake kwa waume na hawa ni watu mimi wameniona toka utoto wangu pale Mtaa wa Kipata, Gerezani.
Acha haya mimi nina taarifa za kutosha za Mwalimu Nyerere na TANU niilizosoma ndani ya Nyaraza za Sykes.
Nchi nzima hii hakuna mtu ana nyaraza kama hizi.
Nyaraza hizi zinaanza toka 1929 wakati African Association inaundwa nyumbani kwa Cecil Matola, Mtaa wa Masasi Mission Quarter.
Nyumba hii ipo hadi leo kwa hiyo usizungumze habari ya kuwa ati mimi simjui Nyerere au siijua historia ya TANU.
Hakuna hila yoyote katika historia niliyoandika.
La una ushahidi kuwa kuna hila tuwekee hapa hizo hila.
Wala hakuna popote niliposema Nyerere, chembelecho ''kadandia.''
Lakini ukweli utabakia kuwa Mwalimu aliikuta mipango ya TANU nyumbani kwa Abdul Sykes la kama una ushahidi kuwa yeye ndiye aliipeleka TANU kwa Abdul Sykes lete huo ushahidi.
Elewa kuwa huwezi kuandika historia ya Nyerere na TANU usimtaje Abdul Sykes.
Chuo Cha CCM Kivukoni kimejaribu na angalia balaa walilochuma hii leo baada ya mimi kuandikia historia ya TANU na kumtaja Abdul Sykes.
May Day,Sikuwahi kusema Mwalimu ndiye alipeleka TANU kwa kina Sykes.
Mwalimu mwenyewe alikiri kwamba jina TANU lililetwa na kina Sykes, na walikuwa nalo tangu wakiwa Burma...na nimeshawahi kusema hili...na kikubwa kilichofanyika pale ni kupitisha jina mbadala wa TAA, na hao waliokuja na TANU wakashinda, sioni kwa nini hilo mnalifanya ni 'big deal' kuliko hata maarifa ya harakati zenyewe.
Mwalimu alikwenda pale na 'road map' ambayo ndiyo muhimu kuliko hata kutunga jina la chama.
Mzee Said unaongozwa sana na dhana binafsi kiasi unamuondolea kabisa msomaji wako picha halisi ya Wazee walivyoendesha hizo harakati.
Haihitaji akili ya ziada sana kuelewa kuwa hao kina Syskes na wenzake walishanyoosha mikono juu, na Mwalimu kwao alikuwa ndiye mkombozi...na namna walivyoishi (m treat) inajieleza vizuri kuliko wewe unavyojaribu kuficha ficha...unaokoteza yale yanayowapamba Wazee wako zaidi.
Ingawa wewe unaonekana kuegemea zaidi kwa hawa 'Wazee wako' lakini Mwalimu amekuwa anawataja kundi la Wazee wa Dar es Salaam ambao walimuamini, kumuelewa na kumuunga mkono ndani ya muda mfupi tu....naona hujali sana michango ya wengine hao zaidi umeegemea kwa hawa 'Wazee wako' wachache.
JK,
Sina taarifa ya kitabu hicho.
UNO walimtaka Mkristo ndio akabidhiwe nchi kulikuwa na wasomi kama Said Fundikira aliehitimu Makerere kabla ya Mwl lakini hakufit