busha
JF-Expert Member
- Jan 21, 2019
- 1,712
- 2,577
Mzee nimekuelewa ila kama kuna kitu kipya hapa tena nimekiona
Ngoja kidoogo nikafanye marejeo mahala flani
Kisha nipitie na link ulizoweka hapa ili nipate kujua zaidi
itakua vema sana
Ngoja kidoogo nikafanye marejeo mahala flani
Kisha nipitie na link ulizoweka hapa ili nipate kujua zaidi
itakua vema sana
B...
Umekosea kumtaja Sheikh Hassan bin Ameir.
Sheikh Hassan hakuwa ameshika nafasi yoyote katika chama.
Wala Sheikh Hassan hakuwa na mwenzie katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.
Mwenzie kama alikuwepo ni Nyerere.
Sheikh Hassan alikuwa kiongozi bila ya kushika nafasi ya uongozi.
Wengi wenu hamjui nafasi ya Sheikh Hassan bin Ameir katika siasa za Tanganyika hadi Tanzania.
Sheikh Hassan bin Ameir alikuwapo katika mpango wa kuunda TANU toka mwaka wa 1950 akiwa mjumbe wa TAA Political Subcommitee.
Nakuwekea hapo chini mada niliyotoa Zanzibar University kuhusu Sheikh Hassan bin Ameir mpate kumjua.
Swali la pili kuwa Mwalimu awape nini waasisi wa TANU sijui kwa nini unauliza swali hili sidhani kama waasisi walikuwa wanataka kupewa kitu.
Hapa nawasemea waasisi ambao mimi nawajua vyema toka wako hai hadi walipofariki.
Sikupata kuwasikia wakisema kuwa hawakupewa kitu.
Nilichokisikia mara nyingi wakisema ni kuwa historia ya TANU inavurugwa na kupotoshwa.
Nakumbuka maneno ya Mzee Germano Pacha aliyoniambia katika mahojiano yetu wakati wa utafiti wa kitabu.
Mzee Pacha alisema kama si kuwapo ile picha ya waasisi wa TANU kungekuwa na waasisi wengi hivi sasa.
MUFTI SHEIKH HASSAN BIN AMEIR (1880 - 1979)
Seminar on The Role of Educated Youth to Muslim Society 27 th February – 4 th March 2004 ORGANISED BY ZANZIBAR UNIVERS...mohamedsaidsalum.blogspot.com