Barua ya Julius Nyerere ya kujiuzulu ualimu St. Francis College Pugu 1955

Barua ya Julius Nyerere ya kujiuzulu ualimu St. Francis College Pugu 1955

Nimeletewa barua ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kujiuzu kazi ya ualimu, aliyeniletea bila shaka akidhani siijui barua hii.

Nimeamua kumwandikia kumpa fikra zangu na kumweleza historia nzima ya barua hii ambayo inaitwa ''Uamuzi wa Busara.'':

''Hii barua ni maarufu ila kilichopungua ni vipi Mwalimu Nyerere alifikia katika uamuzi mgumu kama huu wa kuacha kazi na kuamua kuwa mtumishi wa TANU chama kichanga cha siasa kilichoasisiwa miezi minane tu iliyopita.

Chama ambacho kilikuwa kikiendeshwa kutoka fedha za wafadhili wake wanne: John Rupia, Waziri Dossa Aziz na ndugu wawili Abdulwahid na Ally Sykes.

Bahati mbaya barua aliyoandikiwa Mwalimu na mwajiri wake hapa haipo lakini nayo pia ni barua maarufu.

Toka alipochaguliwa kuwa Rais wa TAA tarehe 17 April 1953 mkakati uliokuwa umepangwa na Hamza Mwapachu na Abdul Sykes ilikuwa ni kuunda TANU na kudai uhuru wa Tanganyika.

Sasa haikutegemewa kuwa Rais wa TANU atadai uhuru wa Tanganyika akiwa mfanyakazi wa Kanisa.

Huu ulikuwa muhali mkubwa na hili viongozi wa TANU wakilijua na Abdul na Nyerere walishalizungumza kabla na ukweli ni kuwa kabla ya safari ya kwanza ya UNO Februari 1955, Nyerere alitaabika sana na fikra ya kuacha kazi.

Ujasiri wa kuacha kazi Mwalimu hakuupata kwa kule kuzingirwa na watu wenye uwezo hawa viongozi na wahisani wakubwa wa TANU.

Ujasiri wa kuacha kazi aliupata siku aliporudi UNO na akapokewa na umma ambao ulikuwa haujapatapo kuonekana Dar es Salaam.

Siku ile ndiyo Nyerere alitambua kuwa ana watu wanaomuunga mkono na wana mapenzi ya kweli na yeye na TANU na wanataka kuwa huru na wamemkubali yeye kama kiongozi wao.

Kwa upande wa serikali ya Gavana Edward Francis Twining walitanabai ule ukweli kuwa sasa siku zao Tanganyika zilikuwa zinahesabika.

Kwa upande wa mwajiri wa Mwalimu Nyerere, yaani Kanisa iliwadhihirikia kuwa mtumishi wao alikuwa amewasababishia mgongano mkubwa sana wa maslahi kwani Kanisa na Serikali walikuwa na ushirikiano mkubwa katika kuitawala Tanganyika.

Kubwa zaidi lililowashangaza ni kuwa ni ile jamii waliyokuwa wameinyima elimu kwa hila za ukoloni za wagawe uwatawale.

Waislam wameunda chama na kumweka kiongozi Mkatoliki aongoze mapambano ya kuikomboa Tanganyika.

Mkakati huu ulikuwa na maana gani?

Mwalimu alikuwa alama ya umoja na alama ya kuwaita walio mfano wa yeye kuingia TANU na kuunga mkono juhudi za kudai uhuru wa Waafrika wa Tanganyika.

Barua ile aliyoandikiwa Nyerere na mwajiri wake ilisomwa na Abdul Sykes mtu aliyekuwa karibu sana na Nyerere na Abdul alisisitiza kuwa Nyerere aache kazi lakini barua ile akapendekeza ijadiliwe na Halmashauri Kuu ya TANU chini ya Mwenyekiti Clement Mohamed Mtamila na ilikuwa nyumbani kwake Mtamila ndipo barua ile ilipojadiliwa na uamuzi ukawa Nyerere aandike barua ya kujiuzulu kazi.

Nyerere aliandika barua ya kujiuzulu na akaja mjini Dar es Salaam sio mwalimu wa shule tena na kwa muda akaishi nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Aggrey na Sikukuu.

Katika Halmashauri Kuu ya TANU mmoja kati ya wajumbe wale alikuwa Tatu bint Mzee.

Yapo mengi sana katika historia ya TANU na historia ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo wengi hawayajui.

Picha ya kwanza juu ni barua ya Mwalimu Nyerere na picha ya pili hapo chini ni wa kwanza kulia ni Bi. Tatu bint Mzee akifuatiwa na Bi. Titi Mohamed na wa kwanza kushoto ni Bi. Chiku bint Said Kisusa wakimsindikiza Julius Nyerere Uwanja wa Ndege safari ya kwanza UNO.

nafiki hapa umechanganya maamuzi ya Nyerere: kinachoitwa Uamuzi wa Busara katika historia ya nchi yetu ni ule wa Tabora wa kukubali Uchaguzi wa Kura Tatu. Uamuzi wa Nyerere kuacha kazi ya ualimu unajulikana kama "Uamuzi Mgumu." Kuna kitabu kiliandikwa na Barongo mwanzoni mwa miaka ya sitini mara tu baada ya uhuru kinaitwa "Mkiki mkiki wa siasa Tanganyika"
 
"Waislam wameunda chama na kumweka kiongozi Mkatoliki aongoze mapambano ya kuikomboa Tanganyika."

Angalieni huyu mzee alivyojaa hila na maandishi yake yenye malengo ya kipuuzi!!

Anaendelea kupanda mbegu ya hila na kuipalilia!! Watanzania leo wanafundishwa kuwa TANU ilikuwa ya waislamu sio watanganyika kwa umoja wao!
 
Kiliwakuta nini hao waislamu waliounda Chama afu nchi akachukua mkristo?
Nadhani ni kuonesha umoja tu ingawa huyo mkristo alibebeshwa maono na wenye maono. Pana siri kubwa hapo. Kwa tabia ya waislam ya kujiona dini bora kuliko nyingine, ilikuwa si rahisi kumsimika kafiri kwenye nafasi hiyo.

Uhuru wa Tanganyika bila Mwl Nyerere ilikuwa vigumu sana. Siri hii ndiyo usalama wetu had leo.

Washukuriwe wenye maono na mbeba maono pia. Natamani familia ya Sykes wangepewa tunu fulani. Walikuwa na hela lakini hawakuwa na tamaa ya madaraka kama akina Makamba na Nnauye wa sasa, wenye kujiona bila wao nchi haina uongozi.
 
Hua nasema Mungu alitupendelea sana kutupa Mwl Nyerere kama baba wa Taifa,kuna viongozi flani flani hua nawaza kama wao ndio wangekua waasisi wa Taifa sijui tungekua na hali gani kwa kweli.
Ikulu ingekuwa ukumani.
 
UNO walimtaka Mkristo ndio akabidhiwe nchi kulikuwa na wasomi kama Said Fundikira aliehitimu Makerere kabla ya Mwl lakini hakufit
Sina uhakika, lakini nadhani kale kashirika ka kijasusi ka kikatoliki ndiko kalikuwa kakizishauri nchi za Afrika kuelekea uhuru.
Tanganyika ni mojawapo. Ushirika wao ulipitia kanisani ili kuwakwepa watawala wa kikoloni.
Ilikuwa ni vita baina ya majasusi.
 
May Day,
Kitabu leo kipo miaka 20 kimechapwa mara nne na hajatokea mtu yeyote kusema kuwa mimi ni muongo.

Kilichofanyika ni kuundwa jopo linaloongozwa na Prof. Issa Shivji akiwa na Prof. Saida Yahya na Dr. Kamatha ambao sasa wanaandika historia ya Mwalimu Nyerere ili angalau wapate kufahamu nafasi yake katika kuasisi harakati za kujikomboa kutoka ukoloni.

Jopo hili wamefanya mazungumzo na mimi nyumbani kwangu mara mbili na nimewapa picha na nakala za nyaraka kutoka Nyaraka za Sykes ambazo baadhi wamepata kuzionyesha katika Kavazi la Mwalimu Nyerere ambalo Prof. Shivji ni Mwenyekiti wake.

Marehemu Prof. Haroub Othman kaonana uso kwa macho na Mwalimu Nyerere kuhusu kitabu cha Ali Muhsin Barwani, ''Conflict and Harmony in Zanzibar,' Dubai (1997) na ''The Life and Times of Abdulwahis Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika,'' London (1998), vitabu viwili ambavyo Mwalimu katajika sana.

Kama ilivyokuwa kwako wewe Prof. Haroub alichomwa sana na historia hii niliyoandika akili yake ilikuwa inakataa kama yale anayosoma ni kweli.

Mimi nilizungumza na Prof. Haroub ambae ni mwalimu wangu na yeye ndiye aliyeniambia kuwa ameonana na Mwalimu na akamuomba na yeye aandike ili yapatikane majibu kwangu na kwa Sheikh Ali Muhsin.

Napenda kukufahamisha kuwa baada ya kuzungumza na mimi hakutosheka Prof. Haroub alikwenda kufanya mazungumzo na Ahmed Rashad Ali mtu aliyekuwa rafiki kipenzi na Abdul Sykes kutaka ukweli wa yale yeye alikuwa na mashaka.

Prof. Haroub aliondoka katika mazungumzo yake na Mzee Rashad akiwa kichwa kainamisha.
Mimi sina sababu ya kuzua uongo.

View attachment 1221898
Kulia: Prof. Haroub Othman, Ahmed Rashad Ali na Ahmed Islam 1997

View attachment 1221902
Kulia: Prof. Issa Shivji, Prof. Saida Othman na Dr. Kamatha siku walipokuja kufanya mazungumzo na Mwandishi kuhusu kitabu cha Abdul Sykes 2013

May Day,
Unaweza kutaka kumjua Ahmed Rashad Ali ni nani katika historia ya Tanzania.
Tafadhali ingia hapo chini:

Nimependa ushahidi wa maneno na picha unanivutia hayo maelezo
 
Unazo, Sheikh wangu, kama sikosei umekinukuu hicho kitabu ndani ya kitabu chako cha Abdulwahid Sykes cc: Joka Kuu
Companero,
Simkumbuki kuwa kipo kitabu kinachoeleza kuwa Nyerere alilikaripia Kanisa Katoliki nami nikaeleza hilo katika kitabu cha Sykes.
 
nafiki hapa umechanganya maamuzi ya Nyerere: kinachoitwa Uamuzi wa Busara katika historia ya nchi yetu ni ule wa Tabora wa kukubali Uchaguzi wa Kura Tatu. Uamuzi wa Nyerere kuacha kazi ya ualimu unajulikana kama "Uamuzi Mgumu." Kuna kitabu kiliandikwa na Barongo mwanzoni mwa miaka ya sitini mara tu baada ya uhuru kinaitwa "Mkiki mkiki wa siasa Tanganyika"
Kichuguu,
Sijakusudia uamuzi wa busara kitabu.

Mie pia nimeandika kitabu kinaitwa, "Uamuzi wa Busara," (2007).

1570077492382.png

Katika waandishi wote walioandika historia ya Kura Tatu ni mimi ndiye niliyeeleza yale ambayo wengine labda kwa kutoyajua hawakuyaandika.

Mimi nina sura nzima katika kitabu cha Sykes inaitwa, "Mkakati wa Tanga," sura hii inaeleza mkutano wa siri uliofanyika Tanga kati ya Hamisi Heri, Abdallah Rashid Sembe, Julius Nyerere na Amon Kissenge.

Mipango iliyosukwa na viongozi hawa wa TANU ndiyo iliyosababishwa kushindwa kwa wapinzani wa Kura Tatu wakiongozwa na Sheikh Suleiman Takadiri Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU.
 
Mimi si Mtaalamu sana wa Kiswahili, na sijatumia neno 'muongo'.....nadhani kuna tofauti ya uongo na kupotosha, kwa maoni yangu muongo huweza kusema kisicho ukweli 100%, na anayepotosha huweza kusema yaliyo na ukweli ila akaongeza 'chumvi' au kupunguza kwa lengo la kufikia malengo yake. Ndio maana sikutaja moja kwa moja kama Muongo.

Kama lengo la Makala zako ni kuwapamba/kuwatambulisha wale unaodhani wana ushiriki wao kwenye harakati za kupigania Uhuru, basi huna sababu ya kumuingiza/kumtaja Mwalimu ki hila hila na kumuonyesha kama Mtu 'aliyedandia' tu harakati zile.

Kufanya hivyo sio haki kabisa, kama huna taarifa za kutosha kumuhusu Mwalimu na chimbuko lake kwenye harakati ni bora ungebaki kuwaelezea hawa ambao una taarifa zao za kutosha na kusubiri watakaotafuta taarifa za Mwalimu ndio wamuelezee Mwalimu.

Sioni tatizo kwa yeyote kama Prof Haroub kushangazwa na baadhi ya mambo kwani huenda kweli hawakuyajua kabla, nadhani kitakachowasikitisha Wasomaji ni namna unavyotumia kupasha taarifa hizo kwa lengo la kupindisha mambo.
Unaonaje basi ukituletea hiyo histoaria yako isiyo na chembe ya upotoshaji?! Yaani nongwa kwako wewe ni kutajwa wale ambao hawakutajwa kwenye vitabu vingine vya historia ambavyo bila shaka unaona ndivyo havijapotosha? Hebu tuelezee hapa hiyo Road Map ya Mwalimu ili watu tujifunze!
 
"Waislam wameunda chama na kumweka kiongozi Mkatoliki aongoze mapambano ya kuikomboa Tanganyika."

Angalieni huyu mzee alivyojaa hila na maandishi yake yenye malengo ya kipuuzi!!

Anaendelea kupanda mbegu ya hila na kuipalilia!! Watanzania leo wanafundishwa kuwa TANU ilikuwa ya waislamu sio watanganyika kwa umoja wao!
Mimi nimwelewa tofauti! Nilichomwelewa ni kwamba, Wakoloni walikuwa wanajaribu kutugawa kwa dini zetu! Na mbinu hii wakoloni waliitumia kote barani Afrika! Lakini waasisi wa TANU katika kuwaonesha "sisi, kwa maana ya Watanganyika Wakristo na Waislamu ni wamoja" ndipo waasisi wa chama kilichoundwa Waislamu, wakampa Mkristo Uenyekiti wa chama! Huo ulikuwa ni ujumbe tosha kwa Wakoloni kwamba wasingeweza kutugawa!!
 
Kiufupi stori za Mzee Said zimejaa hila kuliko uhalisia.

Mtu akieleza ukweli uliofichwa katika historia basi watu wabaya watajitokeza kumuita kwa majina mabaya na kuhafifisha ukweli huo , lakini historia itabaki kuwa historia licha ya hila zilizokuwepo na zilizopo za kutaka kuificha historia. Tunayohamu ya kujua historia kutoka kwa mtu awaye yeyote hata akiwa si Mtanzania ilimuradi azungumze UKWELI tu.🤔
 
Nimependa ushahidi wa maneno na picha unanivutia hayo maelezo
Mkuu wa Kijiji,
Ahsante sana.

Siku zote mimi hujiuliza ingekuwaje laiti kama Kleist Sykes asingeleiandika maisha yake na katika mswada ule asingelieleza historia ya African Association.

Nani leo angelijua historia ya TAA na historia ya Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika vyama viwili ambavyo vilikuja kutoa uongozi katika TANU na kuingiza wanachama wengi wa mwanzo.

Wazee wetu wametuachia picha nyingi sana za harakati za uhuru na hizi nimeziweka hapa mara nyingi tu kwa faida ya wasomaji.
 
Mimi nimwelewa tofauti! Nilichomwelewa ni kwamba, Wakoloni walikuwa wanajaribu kutugawa kwa dini zetu! Na mbinu hii wakoloni waliitumia kote barani Afrika! Lakini waasisi wa TANU katika kuwaonesha "sisi, kwa maana ya Watanganyika Wakristo na Waislamu ni wamoja" ndipo waasisi wa chama kilichoundwa Waislamu, wakampa Mkristo Uenyekiti wa chama! Huo ulikuwa ni ujumbe tosha kwa Wakoloni kwamba wasingeweza kutugawa!!
Myplusbee,
Nimeeleza hapa mara nyingi kuhusu mkutano uliofanyika Nansio Ukerewe nyumbani kwa Hamza Mwapachu kati ya Abdul Sykes, Ali Mwinyi Tambwe na Mwapachu kuhusu Nyerere kuingizwa katika uongozi wa TAA katika uchaguzi uliokuwa unakaribia April 1953.

Swali kubwa lilikuwa Abdul akitaka kauli ya Hamza Mwapachu kuwa ampishe Nyerere katika kiti cha urais wa TAA na 1954 waunde TANU kudai uhuru wa Tanganyika.

Kauli ya Mwapachu ilikuwa yeye anaamini Nyerere ndiye anafaa zaidi kuchukua uongozi wa TAA 1953 na 1954 waunde TANU Nyerere akiwa rais na aongoze harakati za kudai uhuru.

Hamza akamwambia Abdul kuwa yeye Abdul kama Muislam itatia dosari harakati za uhuru kwa Waingereza kuja na propaganda kuwa TANU ni vurugu nyingine za Waislam kama zile walizofanya dhidi ya Wajerumani na kuanzisha Vita Vya Maji Maji.

Yako mengi ya kueleza.
 
Mimi nimwelewa tofauti! Nilichomwelewa ni kwamba, Wakoloni walikuwa wanajaribu kutugawa kwa dini zetu! Na mbinu hii wakoloni waliitumia kote barani Afrika! Lakini waasisi wa TANU katika kuwaonesha "sisi, kwa maana ya Watanganyika Wakristo na Waislamu ni wamoja" ndipo waasisi wa chama kilichoundwa Waislamu, wakampa Mkristo Uenyekiti wa chama! Huo ulikuwa ni ujumbe tosha kwa Wakoloni kwamba wasingeweza kutugawa!!
Pole sana
 
Sina uhakika, lakini nadhani kale kashirika ka kijasusi ka kikatoliki ndiko kalikuwa kakizishauri nchi za Afrika kuelekea uhuru.
Tanganyika ni mojawapo. Ushirika wao ulipitia kanisani ili kuwakwepa watawala wa kikoloni.
Ilikuwa ni vita baina ya majasusi.
Mkuu hivi unajuwa kanisa ndio ukoloni na ukoloni ndio kanisa huwezi tenganisha hata siku moja so mkoloni/kanisa alisuggest mtu wa kupewa nchi lazima awe na jina la kizungu
 
Sio sahihi kuwa UNO ndio walimchagua Nyerere ingawa walikuweo wengine kama Said Fundira, Tewa Said Tewa na wakina John Keto. Nyerere alichaguliwa kwasababu ya kukubalika kwake na wale aliokuwa anawaongoza!
Nyerere sio wa kwanza kwenda UNO kwa taarifa tu, Sykes alishaenda huko na kupewa masharti hayo aliporudi akawajulisha wazee then wakakaa kujadili watampata wapi huyo muRC ndipo Fundikira alipowaambia kuna dogo mmoja nimemuacha kule Makerere nadhani atafaa.
 
Gas State,
Hakuna Sykes aliyekwenda UNO.
 
Mimi nimwelewa tofauti! Nilichomwelewa ni kwamba, Wakoloni walikuwa wanajaribu kutugawa kwa dini zetu! Na mbinu hii wakoloni waliitumia kote barani Afrika! Lakini waasisi wa TANU katika kuwaonesha "sisi, kwa maana ya Watanganyika Wakristo na Waislamu ni wamoja" ndipo waasisi wa chama kilichoundwa Waislamu, wakampa Mkristo Uenyekiti wa chama! Huo ulikuwa ni ujumbe tosha kwa Wakoloni kwamba wasingeweza kutugawa!!
Myplusbee,
Nitaongeza kitu kingine kueleza juhudi walizofanya wazee wetu katika kujaribu kuiongoza TANU kiwe, ''a nationalist-secularist party.''

Ndani ya TANU kama chama cha siasa kulikuwa na ''symbols'' nyingi sana za Uislam kwanza kuanzia wanachama wenyewe, mavazi ya kanzu, kofia hadi mila na tabia zao kwa wanaume na kwa wanawake kulikuwa na mabaibui na mitandio na mikutanoni wakijitenga mbali na wanaume.

Inasemekana ilikuwa katika mkutano wa TANU Bagamoyo mbele ya Sheikh Mohamed Ramiyya Bi. Titi baada ya kuona uzio wa makuti uliokuwa unawatenganisha wanawake aliamuru uzio ule wa makuti uvunjwe.

Hii ikaonekana kama vile inajenga dhana ya ubaguzi ndani ya chama kiasi cha kudhani TANU ni chama cha Waislam peke yao na wengine hawana nafasi.

Turudi nyuma katika historia ya African Association ilipoanzishwa mwaka wa 1929.

Katika mswada wake alioandika kabla ya kuariki kwake mwaka wa 1949 Kleist Sykes anasema kuwa waasisi wa AA wengi wao walikuwa Waislam kwa kuwa Wakristo walikuwa wakionywa na viongozi wao wa kanisa kutojihusisha na siasa.

Lakini hii si kama iliwazuia kabisa Wakristo kutojihusisha na siasa la hasha,

Wako Wakristo wengi hasa baada ya WW II walijiingiza katika siasa za TAA na wakawa viongozi lakini kwa ujumla wake Waislam ndiyo waliotawala uwanja wa siasa.

Mwaka wa 1955 ukaitishwa mkutano Mtaa wa Pemba kujadili hali hii ndani ya TANU na hatua zipi zichukuliwe ile kupunguza ule Uislam ndani ya chama.

Katika viongozi waliohudhuria mkutano huu alikuwa Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Nurdin Hussein, Sheikh Abdallah Chaurembo, Rajab Diwani na waumini wengine.

Ndipo hapo ikaagizwa kuacha kutumia salam ya Kiislam ya, ''Asalaam Aleikum,'' na badala yake TANU ikaja na salimu ya ''Ahlan Tabu.''

Ndiyo kipindi hiki ikawa sasa Surat Fatha na dua iliyokuwa inafungua mikutano yote ya TANU ikaachwa kusomwa.

Angalia picha hiyo hapo chini ya mkutano wa kwanza wa TANU mwaka wa 1955 uliofanyika Ghandhi Hall Dar es Salaam ona kofia zilivyotanda.

Historia hizi leo zikielezwa zinawatisha wengi na akili zao zinakataa kukubali hii ndiyo historia ya TANU.

1570112591233.png
 
Back
Top Bottom