Barua ya mwaliko ili kupata passport

Barua ya mwaliko ili kupata passport

Barua ya utambulisho kutoka serikali ya mtaa wako

Cheti cha Kuzaliwa Mwombaji

Cheti/Kiapo cha Kuzaliwa Mzazi wa Mwombaji

Kitambulisho cha Taifa

Picha ya Mwombaji ya hivi karibuni yenye kivuli cha rangi ya buluu isiyokoza (Light blue Background)

Ada 150000.

Ushahidi wa Safari- hii ndio iliyomfanya aombwe mwaliko au kama ni safari ya masomo admission letter
 
Aisee Moja ya vigezo vyao ambavyo huwa vinaniudhi na kukera ni pamoja na hicho Cha barua ya mwaliko!!

Upumbavuu mtupu, yaani kuondoka hapa nchini mpaka nipate mwaliko huko ninakoenda??? Na je kama ninaenda kwa ajili ya kufanya exploration na kuangalia fursa za kiuchumi zilizoko huko???

Hivi hii nchi mbona Ina maudhi mengi kiasi hiki??? Ni lini tutatoka kwenye hizi bureaucracies za kipumbavvu kipumbavvu??

Haya nimepawa barua ya mwaliko, nikwambie Tena huyo mwenyeji wangu aambatanishe copy ya passport yake, hivi kwa dunia ya leo ilivyoharibika hii mtu anaweza akakupa tu copy ya nyaraka muhimu kama passport kirahisi rahisi hivyo???

Kwa hiyo wametengeneza mazingira ya makusudi hili karibu wote tufie humu humu nchini na wenye access ya kusafiri wawe wachache au?

Hakika siku nikiondoka kwenye hili jalala nitafurahi mno.
 
Mzee baba kwenye passport tu unalalama hivi, vipi ukikutana na figisu za kutafuta visa?

Lakini sio barua ya mwaliko. Tunajaza hizo form mara kwa mara
Logically ni kitu ki moja. Mfano unapojibu nimealikwa na mtu then toa mwaliko, kama utajibu unaenda masomoni utaombwa admission letter. Ilinitokea nlikuwa naenda exchange then waliomba ile barua ya kunialika kwenda kubadilishana uzoefu
 
Siku ya jana nimepeleka document zangu kwa ajili ya kupata passport lakini nimeambiwa inahitajika barua ya mualiko pamoja na copy ya passport ya mtu ninae kwenda kumtembelea.

Kama kuna mtu yuko na sample ya barua ya mualiko anisaidie nipate niweze kuedit kwa ajili ya kuitumia.
Uhamiaji wana masharti afadhali hata ya kwa mganga wa kienyeji
 
Barua ya utambulisho kutoka serikali ya mtaa wako

Cheti cha Kuzaliwa Mwombaji

Cheti/Kiapo cha Kuzaliwa Mzazi wa Mwombaji

Kitambulisho cha Taifa

Picha ya Mwombaji ya hivi karibuni yenye kivuli cha rangi ya buluu isiyokoza (Light blue Background)

Ada 150000.

Ushahidi wa Safari- hii ndio iliyomfanya aombwe mwaliko au kama ni safari ya masomo admission letter
Kwa hiyo kama Sina huo ushaidi wa safari siwezi kupata passport?

Na vipi kama nimeamua tu kutoka nchini kwa recreational purposes na Sina ndugu Wala rafiki huko ninakoenda siruhusiwi kusafiri au?

Kwamba wanatupenda sana na Wana hofu huko tunakokwenda kama hatuna mwenyeji tunaweza tukadhurika ndio maana wameweka mashariti ya namna hiyo au??? Yaani kwamba hii serikali inatupenda sana sisi raia wake?????

Haya Mimi mwakani Nina mpango wa kwenda Morocco kwenye michuano ya AFCON kusapoti taifa Stars, na huko Morocco Sina mwanyeji hata mmoja, je na penyewe wataniambia nitafute mwenyeji wa kuninadikia barua kutoka huko Morocco kabla sijaenda na endapo kama nikikosa mwenyeji huyo hawatoniruhusu kuondoka nchini kwenda kuisapoti taifa Stars??

Nchi hii Ina maudhi mengi sana..
 
Barua hiyo anakuandikia anayekualika anaweka anwani yake alipo.

Atapresent credential zake pia kama ile front page ya passport na kibali cha ukaazi huko aliko.
Kwanini lakini Inakuwa hivyo??

Mbona Rwanda hapo hawana mashariti ya kijinga kiasi gani?? Ni lini hili taifa litaanza kwenda sawa na ulimwengu?

Ulaya pacha umekuwa shida, haya hata passport nayo kupata mnaweka mashariti magumu na ya kipuuzi hivi? Daah
 
Kwa hiyo kama Sina huo ushaidi wa safari siwezi kupata passport?

Na vipi kama nimeamua tu kutoka nchini kwa recreational purposes na Sina ndugu Wala rafiki huko ninakoenda siruhusiwi kusafiri au?

Kwamba wanatupenda sana na Wana hofu huko tunakokwenda kama hatuna mwenyeji tunaweza tukadhurika au??? Yaani kwamba hii serikali inatupenda sana sisi raia wake?????

Haya Mimi mwakani Nina mpango wa kwenda Morocco kwenye michuano ya AFCON kusapoti taifa Stars, na huko Morocco Sina mwanyeji hata mmoja, je na penyewe wataniambia nitafute mwenyeji huko Morocco kabla sijaenda na nikikosa mwenyeji hawatoniruhusu kuondoka nchini kwenda kuisapoti taifa Stars??

Nchi hii Ina maudhi mengi sana..
Haya ndo ya kumwambia mgombea wako ayafanyanyie kazi akiingia ikulu.

U kweli ndio huo passport kwa Tanzania inachukuliwa kama starehe na sio hitaji la kila raia kama ilivyo NIDA
 
Kwanini lakini Inakuwa hivyo??

Mbona Rwanda hapo hawana mashariti ya kijinga kiasi gani?? Ni lini hili taifa litaanza kwenda sawa na ulimwengu?

Ulaya pacha umekuwa shida, haya hata passport nayo kupata mnaweka mashariti magumu na ya kipuuzi hivi? Daah
Walipa kodi kwa nini mnataka kutoroka😅😅😅
 
Mzee baba kwenye passport tu unalalama hivi, vipi ukikutana na figisu za kutafuta visa?
Kaka Kuna mambo mengi sana huwa yananiudhi na kuvuruga kabisa mzunguko wangu wa Damu Kila ninapoyaskia.. Moja wapo ni hili la kupata passport jinsi lilivyokuwa na milolongo mirefu isiyokuwa na kichwa Wala miguu.

Hilo la visa nimewahi kuliskia kwamba ndio hatari zaidi, Kuna nchi hasa zile ambazo raia wengi huwa wanakimbilia visa zake unaweza ukatafuta hata mwaka mzima
 
Siku ya jana nimepeleka document zangu kwa ajili ya kupata passport lakini nimeambiwa inahitajika barua ya mualiko pamoja na copy ya passport ya mtu ninae kwenda kumtembelea.

Kama kuna mtu yuko na sample ya barua ya mualiko anisaidie nipate niweze kuedit kwa ajili ya kuitumia.
ukikosa nitafute. sio bure. niandalie 20 nakutumia vyote. kama huamini, sio lazima.
 
Back
Top Bottom