Barua ya ushauri: Freeman Mbowe omba msamaha ukajipange na maisha mengine

Barua ya ushauri: Freeman Mbowe omba msamaha ukajipange na maisha mengine

Hivi mnafuatilia kesi lakini......Je kwenye sheria zetu ni sheria gani inasema ukiomba msamaha tu kesi inaisha? ......vipi kuhusu muda na rasilimali zilizotumika gharama yake ataibeba nani?serikali ama Ndugu Mbowe.....Kuomba msamaha ni kukiri kosa kama nitakuwa nimekuelewa Ndugu MBOWE anapaswa akiri kosa ili asiendelee kuisumbua serikali juu ya kinachoendelea mahakamani kisha taratibu zingine za kimahakama zifuate....
 
Swila kaka na utamaduni gani tens mahakamani
 
Kuna watakaofaidika na Mbowe kukaa gerezani.
Maumivu ya Mbowe ni mtaji wa wengine.
Sioni Kwa Nini Mbowe anajitesa bila sababu.

Zito Kabwe alitumia busara TU kumwomba rais amwamuru DPP aondoe kesi ya Mbowe mahakamani lakini wanasiasa wanaofikiri kukaa gerezani Kwa Mbowe kutaiondoa CCM madarakani wakamtukana sana Zito.

Sasa sijui wanafikiri CCM ni Chama Cha siasa kilicho tayari kukabidhi nchi Kwa watu wasiotaka kukaa mezani na kuzungumza kisiasa. Nyerere hakuwa mjinga alipoamua kufuata masharti ya mkoloni na kujifanya kama vile ni mwenzao ili apate kwanza madaraka na uhuru wa bendera. Alipoona madaraka ni matamu Kwa kama bia Kwa walevi alijisahau lakini Jeshi likamkumbusha baada ya kutaka kupinduliwa. Tangu wakati huo Dola la Tanzania ni la kimapinduzi na linaongozwa kiraiakijeshi. Huwezi kuwatoa kirahisi bila kuwahakikishia usalama wa wanamapinduzi hao ambao wanaendesha nchi kidikteta chini ya utawala wa kijeshi uliojivika koti la Kiraia.
Wanajeshi waliovaa suti ndio wanaotawala nchi hii tangu 1964.

Kwa hiyo kujidanganya kuwa eti Mbowe akifungwa basi ndio Ukombozi ni kumuumi za TU Mmachame wa watu na familia yake.

Watanzania ni wanafiki sana.
Kwa mfano siku Pambalu akiona anakaribia utu uzima na anaachana na uenyekiti wa bavicha anakopata Heshima na maslahi ujue atakua anakaa mguu nje mguu ndani kama Katambi, ajira mtaani hakuna ,biashara ni Kodi tupu na ushuru na tozo tupu. Nani atakataa uteuzi. Wengine kama akina Sugu walishajilimbikizia Mali wakati wa JK na mabunge ya kiulaji yaliyopo.
Akina mdee wamejiongeza kuwa umri unakwenda na familia zinawategemea. Wote ni watanzania ,hakuna mkoloni Toka ulaya Karne hii ,wameamua kukaa meza Moja na wakoloni weusi ili kujenga maisha yao kama sio Taifa.


Niwashauri TU Chadema kama mtashindwa kukaa mezani na Dola wakati huu wa Mama Mh. Mkuu wa Machifu na Amiri Jeshi mkuu wa Majeshi na Rais wa JMT Suluhu ya matatizo ya Watanzania, mzanzibari asiye na makuu, mchaMungu,mnyenyekevu asiyejilimbikizia Mali, asiye na Makundi yake kimaslahi, mpenda haki na anayechukia dhulma, basi Tena msubiri siku Rais wa nchi hii akiwa Mwigilu, Nape, Kabudi,Polepole, Tulia Akson , January, Kigwangala, Paulo Makonda, Hapi. Ndugai n.k . Ndipo mtamkimbuka sana mama Samia kuwa alikua Rais mcha Mungu aliyewajali watanzania bila kujali vyama vyao.

Suala la Chadema wanamlaumu Mama Samia wakati watu wengi wako magerezani Kwa kubambikwa kesi na hao hao walimbambika Mbowe.
Na hali ilivyo Kwa Sasa bado lile kundi la wabambikaji wa kesi na waporaji ni kubwa sana ndani Kwa ndani. Ulikua ni mtandao na ndio uliotumika kuvuruga uchaguzi nchi nzima. Kuna Mapolisi wengi waligombea mpaka Ubunge kupitia CCM kinyume na katiba. Wakitumika kupora watu fomu za uchaguzi na kuumiza watu. Sio rahisi Kwa mama Samia kuwaingilia kesi iliyoasisiwa na genge kama Hilo kinalowaza maslahi yao ndani ya mifumo ya kodola. Ni lazima ajipange kwanza ukitegemea anatokea nchi mdogo ya Zanzibar. Watu kama hao bila kujipanga kimfumo wanaweza wakafanya matukio ya ajabu na ya kigaidi na nchi ikayumba wakasema tulikuambia ukatuona sisi ni wajinga . Matokeo yake unaonekana umeshindwa nchi.

Hivyo mama alipodanganywa kuwa Mbowe ni gaidi na wengine tayari walishalamatwa wapo gerezani asingeweza kukurupuka na kuwapinga kuwa sio Gaidi. Lakini Kwa Sasa amegundua na anasubiri TU washindwe kuthibitisha ili aweze kuwaweka pembeni na Kwa reference hiyo.
Akitoa kesi atashindwa kuwapata sababu ya kuwaambia Kwa wazi kuwa wanabambukizia watu kesi na ushahidi ni huu.
Ushahidi wa Kesi ya Mbowe unawashtua watu wengi mpaka sasa. Sio kwamba mama anaifurahia Bali anapata sababu ya kulipanga vyema Jeshi la Polisi.
Nadhani ni vizuri kesi hii ikiisha walifanya uovu huu Kwa Mbowe wakawekwa pembeni.
Ni vyema akamchagua CDF Toka JWTZ na Makamishna wanne wawe ni mameja General Toka JWTZ , Mapolisi wawe SITA. Hii itaondoa mitandao ya kifisadi na kibabaishaji ndani na nje ya Jeshi la Polisi.

Haina haja ya kuomba msamaha kwani kesi imeshaisha na Mbowe Hana hatia mpaka Sasa na majaji wanajua wazi kuwa kumfunga Mbowe itakua ni matakwa yao kweni Mama Kwa Imani yake na dini yake hawezi kimlazimisha Jaji atoe hukumu isiyo ya haki. Mama hawezi kushiriki dhulma kubwa kama hiyo kwani Urais wake ni Kutoka Kwa Allah Mwenyewe na yeye ndiye hakimu wa Haki Kwa wote.

Mila za Kiafrika na Kanuni za Machifu ni kusimamia haki za watu na kufanya matambiko ili yeyote anayedhulumu haki ya mtu mzimu imshughulikie.

Mbowe atatoka TU ,ila akitoka asimdharau Chifu Mkuu mana Kwa kweli amebadili hali ya nchi katika haki za watu na uhuru ukilinganisha na miaka mitano iliyopita. Hata Jaji anayesikiliza kesi sio Kama yule aliyeondolewa. Na Chifu Hangaya akiona kuwa yule Jaji anamawazo ya hofu na kidikteta ndio maana akampa kazi nyingine.
 
Back
Top Bottom