Barua ya wazi kwa maaskofu wa TEC: Baba zetu tuokoeni, nchi yetu inauzwa Uhuru wetu unamong'onyolewa

Hilo la mkataba andikeni maumivu, mtalalamika mpaka siku mnakwenda kaburini, mchezo ndio umeshatoka tena hakuna atakayerudi nyuma.

Badala ya kuumiza vichwa katika kufikiria namna za kufaidika kibiashara ndio kwanza akili ya kimaskini inawaza juu ya siasa nyepesi za uanaharakati!.

Tuna ujinga mwingi sana vichwani mwetu.
 
Chuki hizi mtakwenda nazo kaburini, Hakuna mwenye dawa ya kuponya nafsi zenu.

SSH hajawaleta yeye kama yeye hawa DPW, wameletwa na ilani ya CCM inayotaka uwepo ushirikiano wa kibiashara kati ya serikali na waendeshaji binafsi wenye uwezo.

Kuna wapumbavu wakikusoma wanakuunga mkono kwa kufuata hoja za chuki ulizonazo, hawawezi kuangalia mbali zaidi ya rangi za SSH, Mungu anatulinda lakini.
 
Mungu ndiye anayepanga nani awe rais na nani asiwe. Ukiandika kwa kufikiria sana juu ya mapenzi ya Mungu unakuwa unamkufuru Muumba huyo huyo.

Wakati wewe unalialia humu jukwaani huko mikoani watanzania wengi tu wanakula matunda ya huyu huyu mwanamke. Chunga mdomo wako.
 
Swali moja lenye mantiki ndani yake, Ni vipi bandari hiyo hiyo iliyouza nchi kwa mkataba huu wa DP World inaweza kutangaza tender nyingine kadhaa za uendeshaji wa bandari zetu nyingine?.

Kama ni kweli tumejifunga kupitia hiyo IGA, imewezekana vipi kwa mamlaka hiyo hiyo ya TPA kutangaza tender za uendeshaji wa bandari ikiwemo hiyo hiyo ambayo DP World wataendesha magati namba nne mpaka namba saba?.

Utawapata wajinga wachache wenye upeo mdogo.
 
Tatizo la ujinga wetu ni kuliweka suala la DP World katika mitazamo duni ya kidini wakati ni suala la kiuchum lenye kufuata misingi yote ya uchumi. Huku ni kufilisika vichwani.

DPW anakwenda kufungua hoteli kule Njombe, itakuwa ni ya kitalii, anakwenda kuifungua Iringa kwani kuna uwanja wa ndege pale wenye kukidhi viwango vya kimataifa. Tujiulize hoteli ile inakwenda kusaidia wangapi kwa maana ya wakristo wenzetu, tujiulize mzunguko wa pesa wa mkoa ule utakuwa katika hali gani.

Tujifunze kuitazama dunia katika mitazamo chanya sio kila kitu tuwe tunakijadili kwa kuchangia mawazo hasi tu, mawazo ya kupinga hata kile ambacho hatukifahamu vizuri.
 
Haya yote nilisha kueleza; lakini kwa vile una kichwa cha panzi huwezi kuelewa.

"Chuki", kama ni chuki juu ya nchi yetu kunajisiwa na watu wa hovyo kama nyinyi, hiyo chuki siijutii hata mara moja, na Mungu ataona roho yangu juu ya hili.
Kwa hiyo, nikueleze kwa mara ya mwisho, chuki ya kuchukia anayoifanyia Tanzania Samia na genge lote lililomshikilia, hii chuki nitakuwa nayo sana, na nitawahimiza waTanzania wenzangu wote wenye mapenzi na nchi yao kuwa na chuki juu yenu nyote.

Unajionyesha kuwa mtu wa hovyo kabisa asiye elewa chochote, kwa kudai kuwa "...DPW wameletwa na ilani ya CCM..." Ni wapi Ilani ya CCM imewataja DPW kwa jina, na ni lini iliagiza pawepo na IGA ya kijinga aina ile.
Kuwepo kwa ilani ya CCM ikitaka pawepo na ushindani, haina maana ya Samia kuichukulia kuwa nafasi ya kwenda kuhujumu nchi anayoiongoza na kwa kweli kushiriki katika uhaini wa nchi.
Kama akili yako haiwezi kutofautisha haya, ni kwamba nyote kwenye hilo genge, akiwemo na Samia mwenyewe akili zenu hazifanyi kazi vizuri. Mnaliangamiza taifa letu.

Mwisho, Mungu kamwe hawezi kulinda watu wenye nia mbaya kwa waTanzania kama nyinyi. Tutawakabiri tu.
 
Mkumbuke mwarabu huyu huyu ameshapewa Uwanja wa ndege wa Kia, misitu yetu yote, shirika la posta, loliondo.

Sultani anarudishwa kidogo kidogo.
Mpaka anarudishwa sisi tumeshindwa vipi kuiendesha KIA?. Tuna wepesi mwingi sana wa kuja kulia mitandaoni, tunafanya kipi cha maana katika kujitafutia maendeleo?.

Kuna wengi huko mitaani wanaitazama dunia halisi na wanapambana nayo kila kukicha, wapumbavu wachache wa humu JF kazi yao ni kudhani kuwa mchawi wa jitihada zao ni mtu mwingine wanayemuona. Adui yako ni yule unayemuona kila unapojitazama kwenye kioo.
 
Kila mara ninakueleza juu ya hili, na bado akili yako imelala.
Mikataba hii haitangazwi chini ya mpango wenu huo wa kifisadi wa IGA; lakini wewe umekomalia IGA IGA, IGA. IGA ilikufa kifo cha kibudu.

Hizi shughuli zote zinazoendelea hazina uhusiano wowote na ile GA yenu.
 
Jibu la kipumbavu kabisa hili.
Hiyo mistari miwili ya mwanzo, huoni uhusika wa hao viongozi, kama huyo SSH katika kushindwa kwao kuwa viongozi wa wananchi na kusimamia shughuli za wananch hao? Badala yake unakimbilia kulaumu wasiohusika!

Halafu unasema "kuna wengi huko mitaani wanaotazama dunia halisi..." dunia halisi kwa maoni yako ni kutawanya na kugawa mali za taifa kwa mataifa mengine, bila ya kuhakikisha zinaleta manufaa kwa wananchi?

Sasa ni dhahiri kabisa adui wa nchi hii hasa ni nani. Ni watu kama nyinyi, na SSH mnaotafuta kuturudisha tena katika utmwa mambo leo. Hili kamwe hatutalikubali.
 
Mpuuzi tu wewe dada. Samia kila anapokwenda huko nje ni kwa faida ya kutafuta pesa zinazojenga zahanati na utanuzi wa barabara, Kwa kifupi huwezi kukwepa uwekezaji.

Haipo namna ambayo Tanzania inaweza kuishi ikifanana na kisiwa fulani, binadamu tumeumbwa ili tutegemeane, ni akili na mawazo ya kijamaa siku zote pale tunapodhani kwamba ni sisi tu tunaoibiwa utajiri wetu!. Mawazo ya kichoyo na kishamba sana haya.

Mwekezaji kaja ili tija ya bandari iongezeke, ikishaongezeka maana yake pato la nchi limeongezeka, na linapokuwa limeongezeka maana yake pesa za kuhudumia sekta za afya, maji, umeme na zenyewe zinaongezeka.

Tujitahidi tuwe na maono hayo, sio kubakia na akili za kudhani tunaibiwa sisi tu siku zote, pathetic mindsets.
 
Hujui unaloliandika na kwanini hujui hilo jibu unalo mwenyewe. Kinachofanyika bandarini muda huu kimezaliwa kutokana na IGA iliyopita bungeni ndio imezaa hizi commercial agreements zilizosainiwa mbele ya rais pale Ikulu Dodoma.

Sitachoka kukuelimisha kuhusiana na hilo.
 
Uhujumu na uhaini upi alioufanya Samia kwenye mradi wa DP World?.

Unajua kwamba bandari ilimshinda marehemu JPM kuiendesha?. Makelele mengi kutoka kwa TEC na kwa wengine ni baada ya kugundua kuwa mirija yao inakwenda kukatwa mazima.

DP World amekuja kwa vigezo vinavyotokana na ilani ya CCM kukubaliana na biashara ya ubia kati ya serikali na waendeshaji mahiri na wenye mitaji na uzoefu wa mashirika ya kimataifa.
 
Mpuuzi tu wewe dada. Samia kila anapokwenda huko nje ni kwa faida ya kutafuta pesa zinazojenga zahanati na utanuzi wa barabara, Kwa kifupi huwezi kukwepa uwekezaji.
Ninaposema upeo wako ni mdogo sana, usifikiri natania au nina bahatisha.

Anakwenda nje ya nchi kutafuta wawekezaji wa kutujengea Zahanati? Hivi kweli unazo akili timamu wewe na unaelewa unacho kiandika humu?
Hatuna hata uwezo wa kujenga Zahanati, hadi Samia aende huko nje kutafuta wawekezaji?

Hatuwezi kujenga barabara zetu, hadi wawekezaji anao watafuta Samia wapatikane? Hivi hii nchi mnaoinaje nyinyi watu? Hivi miaka yote hii mlikuwa mmejificha wapi, na mara hii kuibuka na mambo ya ajabu namna hii?

Hiyo nyumba unamo lala wewe na familia yako, kakujengea nani? Ulikwenda kutafuta mwekezaji?

Mnataka kutufanya waTanzania kuwa vijakazi tu wa ndugu zenu mnao waleta hapa watutawale tena?
Hilo sahau, halitatokea tena.
 
Kila mara unakimbia swala husika, toka mwanzo. Ni mara ngapi umeambiwa humu tatizo siyo uwekezaji, tatizo ni nyinyi mawakala mnaotumia uwekezaji huo kuwa mbaya kwa mikataba mibaya kama huo wa IGA.

Unarukia mambo yasiyo husika. Nani kakwambia hataki Tanzania ishirikiane na mataifa mengine.
Kushirikiana na mataifa mengine au kuleta uwekezaji haina maana ya kutojitahidinasi tuwe na uwezo kama hao wanaokuja kuwekeza hapa.

Hao DP World, hawakuwepo, na hawakuwa na lolote kabla ya 1999. Kwani wao kufanikiwa hadi kuwa walivyo sasa katika miaka hii michache, walisubiri watu wengine wawafanyie kazi, ndipo wapate mafanikio ya kuwafikisha hapo walipo?

Ninakueleza yote haya, lakini ni kama namueleza tu mbuzi asiye kuwa na utambuzi wa lolote.

Weka maslahi yako pembeni kwanza, yatazame maslahi ya nchi hii kwa upana wake.

Ukweli ni kuwa mnaudhi sana watu wa aina yako na huyo mama yako.
 
Sasa ni dhahiri kabisa uliitegemea sana hiyo IGA katika mipango yenu ovu kwa nchi hii. IGA haihusiki na chochote kinacho fanyika sasa hivi.
Mlitaka kubadili sheria zinazolinda mali zetu ili huo uovu wenu kwenye hiyo IGA utimie. Hapo mkakwaa kisiki.
Lakini nia ya uovu wenu kwa nchi yetu umekwisha jifunua, lililobaki ni kuwafurumsha tu. Subiri yanayo kuja.
 
Uhujumu na uhaini upi alioufanya Samia kwenye mradi wa DP World?.
Kutaka kutuingiza katika mkataba ule wa kitumwa, IGA, tena akijua wazi na kushiriki moja kwa moja katika hujuma hiyo.

Hakuna kiongozi yeyote anaye ipenda nchi yake anayo iongoza anaweza kudiriki na kutaka kuiingiza nchi yake katika utumwa ule uliowekwa ndani ya ile IGA.
 
Unajua kwamba bandari ilimshinda marehemu JPM kuiendesha?. Makelele mengi kutoka kwa TEC na kwa wengine ni baada ya kugundua kuwa mirija yao inakwenda kukatwa mazima.
Angalia usivyokuwa na akili timamu. Maslahi gani wanayo TEC katika lile swala la bandari?
Halafu hata hukumbuki uliyo kwish andika mwenyewe humu!
Umeandika mara kadhaa kuwa huo mpango wa DP World ulikuwepo toka enzi za Magufuli, na kwamba hiyo DP World walishawekwa ndani ya ilani ya CCM, halafu sasa hivi unapiga mengine kivyako, ujuavyo mwenyewe!

Hii kazi ya uwakala wa kuiuza nchi yetu msidhani inaweza kuwaacha salama.
 
Sasahiv anaitwa mama wa taifa.
 
Sasahiv anaitwa mama wa taifa.
Hao wanaoimba hizo nyimbo ni unafiki tu na uchawa. Atakapo enguliwa hapo utawasikia hao hao wanamwimbia nyimbo huyo atakayekuwepo kwenye nafasi hiyo. Makundi ya aina hii huwa hayana uzito wowote.

Hawa siyo wafuasi, hawa ni watafuta fursa tu basi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…