Barua ya wazi kwa maaskofu wa TEC: Baba zetu tuokoeni, nchi yetu inauzwa Uhuru wetu unamong'onyolewa

Mwenye akili timamu hawezi kuwa wewe unayesema mradi wa bandari hauna uhusiano na IGA iliyopita bungeni!!.

Anayoyafanya Samia yana uhusiano wa moja kwa moja na ilani ya CCM. Nchi yetu haina wa kuiuza kwa yoyote yule ni uelewa wetu mdogo katika masuala ya kisasa ya uendeshaji wa bandari, ndio tatizo letu.
 
IGA ya bandari ni moja tu unayoifahamu wewe, unajua IGA nyingine zinazoendesha miradi mingine zinafanana vipi?.

Na hiyo bandari ina magati manne yanayokwenda kuendeshwa na DP World, unafahamu nini kitaandikwa kwa mwendeshaji anayekwenda kupewa magati namba nane mpaka kumi na moja?.

Tafuteni maarifa ili mpunguze lawama zisizo na msingi wowote.
 
Tatizo lenu mnachagua kipengele kipi cha kusoma na kipi cha kuacha. Mnatafsiri kile ambacho mnadhani kinawapendelea katika kujenga hoja zenu lakini ukitaka kuelewa kwa kina mkataba mzima una maana gani basi muusome wote kwa ukamilifu wake.
 
TPA haiwezi kuendeshwa kwa mbinu zile zile za kizamani halafu ikaongeza tija kwenye uchumi mkuu wa hazina, tambua hilo.

Hakuna maendeleo kwa kuwa na kiongozi mwenye kujifungia tu humu ndani ni lazima atoke nje kutafuta kitu cha kuongezea kile kinachopatikana kwenye mzunguko wa pesa za ndani.

Ule ujeuri wa marehemu JPM uliifika mahali ukatukwamisha. Kumbuka kwamba mfumo wa ujamaa tatizo lake ni kufika mahali nchi ikakosa pesa za kuendesha miradi haswa ile mikubwa, makusanyo pekee ya kodi hayatoshi kujenga reli ya SGR ukaimaliza.

Makusanyo pekee ya kodi hayatoshi kuanzisha miradi ikasimamiwa mpaka ikamalizika. Ni lazima rais awe na hulka ya kujichanganya kimataifa kwa faida ya upatikanaji wa pesa zinazoweza kusaidia kumalizia miradi mikubwa aliyoachiwa na mtangulizi wake.

Nyumba nayolala mimi haina uhusiano wala mfanano na masuala ya nchi yenye watu milioni 64.

DP World yupo Uingereza, na huko anataka kuwafanya waingereza kuwa vijakazi wa waarabu?, Yupo India pia na huko anataka kuleta mawazo ya kitumwa tena?.

Maono na uelewa wa dunia ya kisasa ni tatizo la wasomi wengi tulioanoa akiwemo Kalamu, mnaitazama dunia katika jicho lile lile la mwaka 1985.
 
Nimekwisha kuelimisha vya kutosha, sasa unaharisha tu bila kuelewa unachoandika humu kina maana au la;. mradi uonekane unaandika kitu basi.
 
TPA haiwezi kuendeshwa kwa mbinu zile zile za kizamani halafu ikaongeza tija kwenye uchumi mkuu wa hazina, tambua hilo
Kwa nini unataka TPA waendeshe bandari kwa mbinu hizo hizo; hiyo amri unaitoa wewe kwa sababu zipi?
Nyumba nayolala mimi haina uhusiano wala mfanano na masuala ya nchi yenye watu milioni 64.
Unaona hivyo kwa sababu ya ufinyu wa upeo ulio nao.
DP World yupo Uingereza, na huko anataka kuwafanya waingereza kuwa vijakazi wa waarabu?, Yupo India pia na huko anataka kuleta mawazo ya kitumwa tena?.
Uingereza hakuna vilaza na mawakala kama wewe na huyo SSH, kila mara ninakukumbusha hili, lakini najua akili yako haina uwezo wa kupambanua tofauti zilizopo.
Ule ujeuri wa marehemu JPM uliifika mahali ukatukwamisha. Kumbuka kwamba mfumo wa ujamaa tatizo lake ni kufika mahali nchi ikakosa pesa za kuendesha miradi haswa ile mikubwa, makusanyo pekee ya kodi hayatoshi kujenga reli ya SGR ukaimaliza.
Haya sasa, mnaanza kujifunua wenyewe juu ya unafiki mnaouficha. Mara muimbe uzuri wa Magufuli na "Kazi Iendeleee", kumbe nyinyi ni FISI mliokuwa mnasubiri aanguke chini mle mzoga wake!
Magufuli alikuwa na mapungufu mengi sana kama kiongozi, lakini hakuthubutu hata mara moja kuisaliti Tanzania kama mnavyofanya nyinyi. Ndiyo maana hatma yenu imekwisha andikwa. Hamuwezi kuisaliti nchi hii mkabaki salama.
Maono na uelewa wa dunia ya kisasa ni tatizo la wasomi wengi tulioanoa akiwemo Kalamu, mnaitazama dunia katika jicho lile lile la mwaka 1985.

Katika hili la "maono na uelewa wa dunia ya kisasa" sioni popote kutoka kwako kinachonionyesha hata kiduchu tu cha mambo hayo. Ninachokiona toka kwako ni ulafi, ufisadi, uhujumu na mengine ya hovyo tu. Genge lenu haliitakii mema Tanzania. Maono yako ni kuwaona waTanzania kuwa vijakazi wa wajomba zenu waarabu. Hili halitatokea hata siku moja.
 
Tatizo lenu mnachagua kipengele kipi cha kusoma na kipi cha kuacha. Mnatafsiri kile ambacho mnadhani kinawapendelea katika kujenga hoja zenu lakini ukitaka kuelewa kwa kina mkataba mzima una maana gani basi muusome wote kwa ukamilifu wake.
Mabaya yaliyomo ndani ya mkataba huo yanaharibu kila jema unaloliona wewe ndani ya mkata wenyewe.
Uelewa wako huo mdogo ndilo tatizo linalokusumbua.
 
Nilisha kwambia, hii siyo IGA ya kwanza kwa Tanzania; lakini ni IGA ya kwanza mbovu kabisa kuliko zingine zozote zilizowahi kuandaliwa na kuwepo hapa nchini.
Ni IGA ya kipuuzi kabisa, mliyo andaliwa na hao wajomba zenu, wakijua nyinyi ni mbumbumbu hamuwezi kuhoji chochote.
Mkaileta hapa, na kutaka kuifanya siri kubwa muipitishe kwa siri. Wazalendo wa nchi hii wakakataa na kutoa hiyo siri.

Tangia hapo unakomalia "siri siri"; lakini uhaini wenu siyo siri tena.
Wewe ni mtu mmoja mwovu sana kwa maslahi ya nchi hii na watu wake.
 
Usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Hiyo ni mojawapo tu ya IGA nyingine zinazowezesha miradi mingi ifanyike hapa nchini.

Ingekuwa ni mbovu leo hii pale TPA pasingetangazwa tender za uendeshaji wa magati namba nane mpaka kumi na moja, mmlivamia suala ambalo linawazidi uwezo na mkalisambaza bila ya kuwa na uelewa wa nini mnachojadili.

Uhaini ni maneno yako ya chuki baada ya nia yako ya kutaka serikali ikamwe!, utaumia sana moyoni kwani mengi unayotaka yatokee yanaishia kutokea kwenye ndoto zako tu.
 
Mabaya yaliyomo ndani ya mkataba huo yanaharibu kila jema unaloliona wewe ndani ya mkata wenyewe.
Uelewa wako huo mdogo ndilo tatizo linalokusumbua.
Wewe ndiye mwenye uelewa mdogo unayejitwisha nia ovu ya kuifanyia fitina serikali ya SSH, IGA ile ile iliyopitishwa bungeni ndio hii imetengeneza Commercial Agreements zilizosainiwa pale Dodoma.
 
Hakuna usaliti wowote kwa maslahi mapana ya Tanzania, muda wa uwekezaji unaofika ni lazima ufanyike kwa maslahi mapana ya ushoroba huu tulioano.

Tukiachana na DP World yeye atakwenda zake Msumbiji na Angola na kufanya biashara kule, itakuwa imekula kwetu.

Narudia tena kukwambia usikariri suluhisho lenye kulingana na miaka ya 80 na 90 ukadhani linaifaa Tanzania ya miaka 2010. Ondokana na hizo dhana za kukariri uendeshaji wa TPA wa kizamani.

Mahitaji ya kidunia ya kiuchukuzi yanabadilika kwa kasi sawa na dunia inavyobadilika. Ondokana na fikra mgando za kijamaa ambazo hazina nafasi katika dunia ya 'end to end logistics', Sayansi imepiga hatua kubwa na sisi ni wajibu wetu kwenda nayo sambamba ili tusibakie nyuma.
 
Nimekwisha kuelimisha vya kutosha, sasa unaharisha tu bila kuelewa unachoandika humu kina maana au la;. mradi uonekane unaandika kitu basi.
Nina uhakika wa asilimia mia moja kwamba IGA ile ndiyo imezaa commercial agreements zilizosainiwa Dodoma mbele ya Rais SSH.

Waliyofanya kazi nzima ya kutengeneza zile documents zilizosainiwa ni watu wangu wa karibu sana.
 
Ingekuwa ni mbovu leo hii pale TPA pasingetangazwa tender za uendeshaji wa magati namba nane mpaka kumi na moja, mmlivamia suala ambalo linawazidi uwezo na mkalisambaza bila ya kuwa na uelewa wa nini mnachojadili.
Huo ulikuwa mpango kazi wa TPA hata kabla ya uchafu wenu wa IGA kuzaliwa. Usifanye kama hiyo IGA ndiyo ilikuwa inaendesha bandari zetu toka miaka yote.
Akili yako ni mbovu. Huwezi kufikiri sawasawa.
Uhaini ni maneno yako ya chuki baada ya nia yako ya kutaka serikali ikamwe!, utaumia sana moyoni kwani mengi unayotaka yatokee yanaishia kutokea kwenye ndoto zako tu
Wewe bado huoni mlivyojiweka kitanzi wenyewe?
 
Nchi imemomomonyoka sana kimaadili!
Kila anaeteuliwa anatanguliza umimi!
Kila mmoja amekuwa mkwapuaji!
Wanashindana kuuza raslimali za taifa kama zao binafsi.
Watoto wao ndio wamekuwa makuwadi wa mali zetu!
 
Wewe dunia yako inaanzia DP World, na kuishia DP World. Sasa mtu wa aina yako utakuwa na lipi la kuwaeleza wengine?
 
Huo ulikuwa mpango kazi wa TPA hata kabla ya uchafu wenu wa IGA kuzaliwa. Usifanye kama hiyo IGA ndiyo ilikuwa inaendesha bandari zetu toka miaka yote.
Akili yako ni mbovu. Huwezi kufikiri sawasawa.
Wewe bado huoni mlivyojiweka kitanzi wenyewe?
Bandari ya Dar inakwenda kuendeshwa na TPA pamoja na kampuni nyingine mbili, hii ni hatua kubwa sana ya kimaendeleo.

Hapo hatujaongelea bandari za Bagamoyo na Tanga. Maendeleo ni hatua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…