Barua ya wazi kwa maaskofu wa TEC: Baba zetu tuokoeni, nchi yetu inauzwa Uhuru wetu unamong'onyolewa

Barua ya wazi kwa maaskofu wa TEC: Baba zetu tuokoeni, nchi yetu inauzwa Uhuru wetu unamong'onyolewa

Unataka kubishana na msomi TL ambaye anajua historia ya nchi mikataba yote tangu mwaka 1929 unavamia ebu anzisha thread yako tuoneshe wapi TL wapi amepotosha
Kuna uzi ulishafunguliwa hapa. Upo page ya 12 utafute
 
Kwanza Nawasalimu kwa Jina la Kristu....
Hongereni sana kwa mjadala wa hekima ya Kina juu ya Mkataba wa Bandari yetu na DP WORLD.
Lkn hili la Bandari litumike kuwatoa usingizini maaskafu wetu wa Kikristu. Tunajua Ukristu na Unafiki ni mwiko lkn jiulizeni. Pamoja na Madhaifu yoooote ya Kiungozi yaliyopo mmewasikia Masheikhe wanavyo comment kuhusu Uongozi wa Nchi? Je Kuhusu Mkataba wa DP World? Je, Kuhusu haiba ya Mhe.Rais?
Mmesikia Maoni ya Sheikh Ponda kuhusu DP WORLD? Maaskofu mna kazi ya kufanya dhidi ya Waumini wenu wanaposhika Madaraka hasa URAIS.
Tumeona jinsi Viongozi wenzenu wanavyomlinda mfuasi wao kwa nguvu zote na kwa njia zote?
Maaskofu nyie tukirudi kwenu mlitumika sana kushambulia Kiongozi wa Nchi mfuasi wenu RIP JPM mkisoma takwimu za CORONA, Mkisoma Takwimu za Unyanysaji, mkisoma Idadi ya Uonevu wake. Bagonza, Mwamakula nk waligeuka kuwa mwiba kwa Mtawala Mfuasi wa Madhehebu yenu. Leo Mungu amejibu maombi yenu yule Mtawala mliyekesha mkiitisha Press Conference za Ubaya wake hayupo. Kawaletea mliyetaka na leo mnaendekeza Vilio vingine.
Bwana Awe Nanyi Viongozi wangu mnapaswa kukaa kimia tu maana mlipewa Upande wenu lkn mkageuka timu pinzani.
SALA YANGU IMEFIKA MWISHO..mimi Mkiristo nikiwa Kiongozi Askofu wangu anageuka Mpinzani wangu kwenye Madhabahu ya Bwana! Mjitafakari na Mtwambie Kiongozi wa BAKWATA hata mmoja tu anayekosoa Kiongozi wetu na Mikataba yake!
 
Samia achnanana huu mkataba Mara mojaa waambie ndugu zako kuwa tumegoma
 
Bila shaka mnatumwa na wafanyabiashara pamoja na wadau mnaonufaika na wizi hapo bandarini zama zenu zimefika mwisho lazima mifumo yote isomane tupate pesa mlizowea wizi pumbavu sana.
 
Umekosea ku-mention TEC peke yao ingeleta maana zaidi kama ungewajumuisha na BAKWATA.

Ukweli ni kwamba sisi kama nchi kuongozwa na mwanamke tena kutoka ng'ambo ya pili ni kosa la karne hakuna siku kama taifa tutaacha kulalamikia hata akiwa hayupo madarakani athari zake zitatuandama.
Bakwata wana uwezo wa kuchambua mkataba?
 
HAUHTAJI TENA KUFANYIWA UPASUAJI ILI KUPONA BAWASRI..............

Kama Umekua Ukitamani Kufahamu Njia Rahisi Na Za Haraka za Kupona Bawasiri Bila Upasuaji Basi Nina Habari Njema Sana Kwako..

Tumekuandalia Mafunzo Ya Bure Kabisa Kupitia WHATSAPP Ambapo Utajifunza Bure Jinsi Ya Kumaliza Changamoto Ya Bawasiri Bila Upasuaji

Hivyo .. Utaweza Kumaliza Kabisa Changamoto Ya Bawasiri Ukiwa Nyumbani Kwako, Bila Upasuaji....

Na Hii Ina Maana kua Utaweza Kuokoa Pesa Na Gharama Kubwa Ya Kufanyiwa Upasuaji

Na Hatimae Utaweza Kufurahia Maisha Yako Kama Kawaida

[ Gusa Hapa Kujiunga ]



Mafunzo Haya Ya BUREE Yanahitaji Watu 200 tu na Mpaka Sasa Zaidi Ya Watu 100+ Wamesha Jiunga na Darasa.

Hivyo Kabla Nafasi Hazijaisha Basi Jiunge Kwa Kugusa Link Hapa Chini

 
Kwenu baba zetu maaskofu.

Nawaandikieni nikiwa na hisia nzito iliyojaa huzuni kubwa juu ya mustakbali wangu na Taifa langu na vizazi vijavyo.

Baba zetu.
Siku zote Taifa letu linapokuwa katika mtanzuko mzito, hamjawahi kusita kusimama thabiti na kutoa muelekeo wenye kuponya ili kuwasaidia kondoo zenu.

Wakati, Utawala ulipokana Uwepo wa ugonjwa wa maangamizi wa Covid mlisimama kidete kuuambia wazi utawala kuwa Haiwezekani useme ugonjwa haupo, wakati watawa wenu wanafariki kwa ugonjwa huo.

Wakati utawala uliopita ulipominya Demokrasia, mlitoa waraka wa Kwaresma kukemea uminywahi huo wa haki.

Sasa leo mababa askofu, Bandari yetu, lango letu kuu la uchumi linapewa watu wa nje kwa mkataba ambao ni dhahiri siyo mzuri. Mkataba huu una mapungufu mengi sana ikiwemo:

1. Hauna ukomo.

2. Scope yake ni kubwa hadi kugusa bandari za kwenye maziwa yetu.

3. Mkataba hauelezei Share zetu zisipungue ngapi.

4. Mkataba hauelezi tunaweza kujitoaje pindi mwekezaji asipokidhi masilahi yetu.

5. Mkataba huu unavunja sheria ya bandari ya mwaka 2004 na ya rasilimali ya mwaka 2017 na hata katiba ya nchi kwenye suala la bandari maana bandari ni jambo la muungano.

6. Mkataba unatishia suala la muungano wetu maana ni bandari za upande mmoja tu wa muungano ndo zinaguswa ila za upande mwingine haziguswi. Hii inaibua hisia mbaya dhidi ya muungano.

7. Mkataba hauelezei chochote juu ya matakwa ya mwekezaji kulinda haki za binadamu.

8. Mkataba Unampa veto mwekezaji juu ya masuala yetu ya uwekezaji kwenye mambo ya bandari, maana yake Sovereignity yetu remote tumempa mgeni

Kwa hoja hizo hapo juu mababa askofu, mimi binafsi sina amani, nina wasiwasi na uhuru wangu na watoto wangu na watoto wa nchi hii. Kwa hivyo nakuombeni mababa zetu maaskofu.

1. Tusaidieni kuwaambia watawala kwa waraka mzito kuwa mnakataa vipengele vibaya katika mkataba huu na kwamba watawala wakae na mwekezaji wavirekebishe.

2. Nyie kama wachungaji wema Tunawaomba mfikishe ujumbe wa tahadhari kwa waumini wenu wote nchi hii ili wajue hatari ya mkataba huu.

3. Tunawaomba ikibidi muandae hata matembezi na makongamano ya amani ili kujenga awareness ya umma juu ya suala hili.

Asanteni sana.

CC Bishop Zacharia Kakobe
 
Back
Top Bottom