Barua ya wazi kwa members wenye chuki zisizo na msingi kuhusuya Id yangu!

Barua ya wazi kwa members wenye chuki zisizo na msingi kuhusuya Id yangu!

Hello members,

Kwanza kabisa, mimi sio mwanaume! kuna watu wananifahamu na ninaongea nao mambo mbalimbali ya kiimani na kibiashara! mimi sio malaya wala shoga! kukaa kwangu jf muda mwingi au kila siku sidhani kama inamuhusu mtu yoyote humu! mnaotaka kuni-babysit please sihitaji! yamekuja maparody na ids kibao kunijazia kunguni kila mahala, sitaki na ninaomba mniaiche! mara mtu akusalimie leo, kesho kajinunisha upumbavu, please!

Na kama kuna member yoyote ambaye nimewahi kuchat naye mambo ya pesa sijui umalaya ajitokeze na ushahidi! sijawahi kuomba pesa humu na wala sina hizo tabu ndogo ndogo kama mnavyonikadiria. Naona tuhuma zimekuwa nyingi si wame wala wake! mnanivamia sana kwenye comments na kukicha mnaongezeka! Hizo chuki zidi yangu zinawasaidia nini?

Inashangaza kuona jinsi baadhi ya watu wanavyotumia muda wao mwingi kutengeneza simulizi, tuhuma na hitimisho kuhusu kitu ambacho hawakifahamu kikamilifu. Wengine wamejigeuza wachunguzi, waendesha mashtaka na majaji kwa wakati mmoja, ilhali hawana ushahidi wala uelewa wa jambo lenyewe.

Kwa wale vijana mnaojitafuta na kunianzishia nyuzi zisizo na kichwa mimi huwa nahesabu kama utani na wengi wenu ni wadogo kwangu! nikisema niwe serious sana hapo tutazinguana sana halafu mimi ndio nitabaki kuonekana mjinga! Nyuzi nyingi haziko serious ila kuna hawa viumbe wenye nyota za mbwa wanaumia sana, mimi sijamtuma mtu kunianzishai nyuzi! kama kuna yoyote nachati naye nje ya uzi wake aje kunianika hapa!

Kuwa na maoni ni haki ya kila mtu, lakini kujenga chuki juu ya dhana, uvumi na hisia binafsi ni upungufu wa fikra, si hoja. Kama mngewekeza nguvu mnazotumia kunichunguza katika maisha yenu binafsi, huenda mngekuwa mbali zaidi kuliko mlipo sasa. Kama humjui mtu kwanini ujifanye unamjua? unapata faida gani kumchafua mtu? ukikaa kimya kuna biashara yako labda inaharibika?

Sina deni la kuwafurahisha wanaonichukia, wala sitabadilisha ukweli ili uendane na simulizi mnazozipenda. Ukweli hubaki kuwa ukweli hata kama hauwapendezi.

Kwa hiyo kabla ya kuhukumu, hakikisheni mnajua mnachokizungumzia. Vinginevyo, mnachobaki nacho si ukweli bali ni kelele za chuki zisizo na msingi.

Naruhusu maoni, chonde chonde leo sukari yangu iko juu!
Leo mtu akijichanganya, anazo za uso 😅
200w.gif
 
Ila kweli wamezidi. Mpaka wamekubatiza eti we Pawa Mabula. Hata sijui ni kwa nini. Pengine ni kwa vile umekuja na moto sana 24/7 uko active kila post upo tena inaonekana ni wale watu wanaojua kila kitu na matusi unaporomosha ikibidi. Sasa wenzio wanakuwa threatened hence the personal attacks. Au labda mmechukuliana mabwana humu. Wabongo sisi 🚮

IMG_6470.jpeg

Screenshot_20250420-213334.png

Ila JF hii haina mtaalamu aisee! Walikuwepo wengi waliokuwa na moto zaidi yako lakini wengi waliishia kwenye aibu wakaikimbia JF au kubadili ID. Walikuwepo akina Demiss. Akina Mbitiyaza. Akina Wangari Mathai. Akina Cutelove. Wengi tu. Hata wewe chukua tahadhari. Usijifanye mjuaji wa kila kitu na kuporomosha matusi. Mwisho wako hapa JF unaweza usiwe mzuri na usiwaone wenzio wametulia ukafikiri ni wajinga. But again you are you and you are free. Uko huru kufanya cho chote utakacho ali mradi tu huvunji sheria. Na jamii itakuelewa tu hatimaye. Vumilia! 👏👏👏👏

20260622_172951.png
 
sawa, kwanini mlundikano wa ids unahangaika na id yangu tu? ids zipo kibao kwanini mimi? sasa hivi uzushi wa kula sijui nauli na upumbavu kibao! unahisi kila mtu anapuuzia? kuna watu tunaheshimiana humu na tunaplan mambo makubwa, haya uaminifu haulegilegi?
Hamna sababu inayo kosa sababu, jaribu kuitafuta sababu.
Lakini pia jiulize kwa nini wewe kwa sasa na si wengine.
Pole tena , thats social network, ukizima data maisha yanendele kama kawaida so usiweke sana kipaombele artificial life ya kwenye social network.
 
Yaani unashindwa kuona kwamba hayo yote ni mzaha? Basi wewe ndo unajidanganya.

Kuna kamtindo humu, ID za kike zinakuja zinachangamka sana, zinaburudisha jukwaa mwishowe zinapotea. Kabla yako walikuja kina ephen_, leejay49, unique flower, figo 97 nafikiri na wengine wengi.

Itafika mahali utachoka tu, ule uchangamfu utaisha.
 
Ila kweli wamezidi. Mpaka wamekubatiza eti we Pawa Mabula. Hata sijui ni kwa nini. Pengine ni kwa vile umekuja na moto sana 24/7 uko active kila post upo tena inaonekana ni wale watu wanaojua kila kitu na matusi unaporomosha ikibidi. Sasa wenzio wanakuwa threatened hence the personal attacks. Sijui kama umeshawachukulia waume zao humu....

Ila JF hii haina mtaalamu aisee! Walikuwepo wengi waliokuwa na moto zaidi yako lakini wengi waliishia kwenye aibu wakaikimbia JF au kubadili ID. Walikuwepo akina Demiss. Akina Mbiti Yaza. Akina Wangari Mathai...Wengi tu. Hata wewe chukua tahadhari. Usijifanye mjuaji wa kila kitu na kuporomosha matusi. Mwisho wako hapa JF unaweza usiwe mzuri na usiwaone wenzio wametulia ukafiri ni wajinga. But again you are free. Uko huru kufanya cho chote utakacho ali mradi tu huvunji sheria. Na jamii itakuelewa tu hatimaye 👏👏👏👏

View attachment 3614798
View attachment 3614799
View attachment 3614800
Thanks kwa ushauri
 
Nimejiuliza sana muda mrefu sijapata majibu!
 
Yaani unashindwa kuona kwamba hayo yote ni mzaha? Basi wewe ndo unajidanganya.

Kuna kamtindo humu, ID za kike zinakuja zinachangamka sana, zinaburudisha jukwaa mwishowe zinapotea. Kabla yako walikuja kina ephen_, leejay49, unique flower, figo 97 nafikiri na wengine wengi.

Itafika mahali utachoka tu, ule uchangamfu utaisha.
Kwahiyo kumbe mnanisubiri nichoke? hakuna kazi zingine za kufanya? utani upi unaouongelea kwanza? mimi watu ninaotaniana nao nawajua wanatania!
 
Yaani unashindwa kuona kwamba hayo yote ni mzaha? Basi wewe ndo unajidanganya.

Kuna kamtindo humu, ID za kike zinakuja zinachangamka sana, zinaburudisha jukwaa mwishowe zinapotea. Kabla yako walikuja kina ephen_, leejay49, unique flower, figo 97 nafikiri na wengine wengi.

Itafika mahali utachoka tu, ule uchangamfu utaisha.
Unakuta labda ni haiba yake tu,
Mm naona anapenda sana kuchart
Hao wengine ukute majukumu yaliingilia kati
 
Ila kweli wamezidi. Mpaka wamekubatiza eti we Pawa Mabula. Hata sijui ni kwa nini. Pengine ni kwa vile umekuja na moto sana 24/7 uko active kila post upo tena inaonekana ni wale watu wanaojua kila kitu na matusi unaporomosha ikibidi. Sasa wenzio wanakuwa threatened hence the personal attacks. Sijui kama umeshawachukulia waume zao humu....

Ila JF hii haina mtaalamu aisee! Walikuwepo wengi waliokuwa na moto zaidi yako lakini wengi waliishia kwenye aibu wakaikimbia JF au kubadili ID. Walikuwepo akina Demiss. Akina Mbiti Yaza. Akina Wangari Mathai...Wengi tu. Hata wewe chukua tahadhari. Usijifanye mjuaji wa kila kitu na kuporomosha matusi. Mwisho wako hapa JF unaweza usiwe mzuri na usiwaone wenzio wametulia ukafiri ni wajinga. But again you are free. Uko huru kufanya cho chote utakacho ali mradi tu huvunji sheria. Na jamii itakuelewa tu hatimaye 👏👏👏👏

View attachment 3614798
View attachment 3614799
View attachment 3614800
Tena wangari mathari kabla yake alikua anajiita manengelo, pia kuna yule dada alie letwa kutoka mwanza kuja dar aklipwa mi sita sijui alikuja julikana.
Wapo wengi waliamua kupita mazima na I'd name zao , walio kubali kudhalikika leo hii wapo ila kwa tahadhari sana.

Mleta mada miezi sita mbele hamna aakae jua kama kuliwahibiuwa na mtu kama huyu hapa jf, maybe ajitoe sana ufahamu.
 
Back
Top Bottom