Barua ya wazi kwa Mrisho Gambo, ufisadi wako tunautambua

Joined
Feb 7, 2019
Posts
41
Reaction score
45
BARUA YA WAZI KWA MRISHO GAMBO

Asalaam Aleykum, Mheshimiwa mbunge wangu wa Arusha Mjini, kwanza nikupe pole kwa majukumu ya kututumikia wananchi wa Arusha mjini na pia najua utakua umechoka kwa ziara ya Mheshimiwa Waziri Mkuu hapa kwetu Arusha.

Mheshimiwa mimi ninayo machache ya kukwambia siku ya leo, Nimesikiliza kwa makini hoja zako ulizotoa mbele ya Waziri Mkuu juu ya Mkurugenzi wa jiji la Arusha Dr. John Maco Pima ambaye Kitaaluma, ni Mtafiti katika fani ya Sayansi ya Teknolojia ya Habari katika Nyanja za “Blended Learning”, Elimu Mtandao; “E-Government”; na “E-Records and Archival Management”.

Malalamiko yako juu ya Mkurugenzi huyu yalinirudisha nyuma na kuanza kujikuta nikitaka kufahamu ulipotoka kabla ya kufika Arusha,

Nimefahamu ulikua Mkuu wa wilaya ya Korogwe na kilichosababisha kuhamishwa toka Korogwe na kuletwa Arusha sababu ni mgogoro wako na mwanasheria wa Halmashauri hiyo hadi mkafikishana Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Na kupelekea Rais Kikwete Akutumbue.

Baada ulipokuja Arusha uliingia katika mgogoro na aliyekua Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dr. Maden sababu ikiwa ni fidia ya 1.9 Bilioni ambazo ulilazimisha zilipwe wakazi wa Oloresho, Kata ya Olasiti, ili kupisha ujenzi wa kituo cha mabasi.

Dr. Madeni alipokataa na kuunda tume ya kupitia malipo hayo na kugundua kuna zaidi ya milioni mia 8 zilikua zimezidishwa tofauti na kiwango halisi cha Milioni 40 kwa heka ambapo wewe na genge lako mliweka milioni 80 kwa heka ndio vita yako ikaanzia hapo na kusababisha Mheshimiwa Rais kuwatumbua wewe na Mkurugenzi huyo.

Nimejikuta nikijiuliza maswali na kupelekea kukuandikia barua hii ili kujua TATIZO LAKO NI NINI NA WATUMISHI WENZAKO?

Malalamiko yako ya leo yamenifanya nikuandikie barua hii kukukumbusha mambo machache ukiwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambapo nafasi hiyo uliipata kwa figisu uliyomfanyia aliyekua Mkuu wa mkoa wa Arusha Felix Ntibenda na tarehe 18, Agost 2016 uliteuliwa nafasi hiyo. (Hili tuliache sina uhakika nalo.)

Mheshimiwa Mbunge Unakumbuka ule Mradi wa bodaboda 2017 hadi 2020 wewe na kikundi chako mlikusanya pesa kutoka kwa wadau kwa ajili ya kununua pikipki 200 ambazo thamani ya kila pikipiki moja ni shilingi 2,100,000/- Je uliunda kamati kwa mujibu wa Sheria? Je fedha hizo zipo wapi? Unakumbuka wakati wa kampeni ulisema pesa zipo bank kwenye acc maalum iliyopo NMB na mpaka sasa kimya.

Je, unakumbuka Ajali ya Luck Vicent? Unakumbuka ulikusanya zaidi ya Milioni mia tatu? Je, ni kamati gani ilikusanya pesa hiyo?

Unakumbuka mkopo wa wanawake 600 wa kiasi cha laki 2 kila mmoja na fedha hizo ulisema ulichanga kutoka kwa wadau, Je ni kamati gani ilisimamia zoezi hilo? Je fedha hizo zipo wapi?

Unakumbuka ujenzi wa msikiti wa Murieti? Pesa ilitoka kwa wadau je Kamati gani ilisimamia zoezi hilo?

Unakumbuka ugomvi wako na DC wa Jiji la Arusha wakati ukiwa RC kuhusu ununuzi wa Mabati feki 200 pale Murieti?

Je tuhoji juu ya Shule ya Mrisho Gambo ? Ujenzi wake ulifuata utaratibu? Kuipa shule jina kulifuata utaratibu?

Unakumbuka ujenzi wa soko la Samunge? Au tukukumbushe?

Unakumbuka timu ya Arusha United? Michango ya timu hiyo, Jinsi ilivyouzwa?

Unakumbuka nyumba za Polisi ambazo Mheshimiwa Rais Magufuli alikataa kutoa vyeti vya pongezi kwa wadau waliochangia baada ya kugundua kuna upigaji? Je kamati ya Michango ya ujenzi iliundwa kwa mujibu wa sheria?

Mheshimiwa mbunge, Wewe ni mtu wa maslahi na usipokua kwenye maslahi unafanya fitna. Wewe ni mtu ambaye hutaki kuona vijana wakifanikiwa katika nyanja ya Siasa. Bila aibu umemsema Katibu Mkuu wa UVCCM na ulishawahi sema utamshughulikia.

Leo nimekuona ukiwa na Diwani wa wa Sombetini ndugu Msangi, Huyo diwani ndiye uliyemtuma leo kazi ya kupiga picha ambazo umemwambia Mheshimiwa Waziri unazo na pia ndiye kaandaa watu wa kukushangilia wakati unaongea. (Planning Presentation)

Una nini na vijana? Juzi bungeni ulimshambulia Mbunge kijana Mheshimiwa Asia Halamga Mbunge wa Viti Maalum Manyara kwa tiketi ya Vijana.

Katika barua hii nakushauri upunguze kiburi cha Madaraka na kutengeneza migogoro isiyo na Afya, Msaidie Rais Samia Suluhu Hassan kujenga nchi. Rais anahubiri Amani na Umoja. Anapambana kutafuta Mshikamano wa Kitaifa wewe unatengeneza Migogoro.

Wacha leo niishie hapa siku ingine tukionana nitakwambia kwa kirefu.

_Ni mimi mtoto wa Mama Ntilie
Wa soko Kuu Arusha_
 
Tanzania ni nchi ya ajabu sana.....yaani uchafu wa mtu unakemewa kwa kuibuliwa uchafu wa mtu huyo huyo........

Ukisema viongozi wa chama fulani Wana fanya ufisadi utasikia mbona kiongozi wa chama fulani anafanya..........

Kinachosikitisha zaidi kuna makundi ya watu wanaoshangilia hali hiyo.......mpaka unapata mashaka na utendaji kazi wa akili zao.....
 
Very unfortunate nation. Yaani ukitaka kujua kuwa Magufuli alikuwa mtu wa HOVYO angalia watu ambao aliwakumbatia kama wasaidizi wa karibu.

1. Daud Bashite aka Makonda
2. Lengai Ole Sabaya
3. Mrisho Gambo
4. Albert Chalamila

Hiyo mijitu yote ni takataka, miuaji, mijitu ya unyang'anyi na iliyokosa maadili. Still wapumbavu bado wanamuita Magufuli shujaa wao
 
BARUA YA WAZI KWA MRISHO GAMBO

Asalaam Aleykum, Mheshimiwa mbunge wangu wa Arusha Mjini, kwanza nikupe pole kwa majukumu ya kututumikia wananchi wa Arusha mjini na pia najua utakua umechoka kwa ziara ya Mheshimiwa Waziri Mkuu hapa kwetu Arusha.

Mheshimiwa mimi ninayo machache ya kukwambia siku ya leo, Nimesikiliza kwa makini hoja zako ulizotoa mbele ya Waziri Mkuu juu ya Mkurugenzi wa jiji la Arusha Dr. John Maco Pima ambaye Kitaaluma, ni Mtafiti katika fani ya Sayansi ya Teknolojia ya Habari katika Nyanja za “Blended Learning”, Elimu Mtandao; “E-Government”; na “E-Records and Archival Management”.

Malalamiko yako juu ya Mkurugenzi huyu yalinirudisha nyuma na kuanza kujikuta nikitaka kufahamu ulipotoka kabla ya kufika Arusha,

Nimefahamu ulikua Mkuu wa wilaya ya Korogwe na kilichosababisha kuhamishwa toka Korogwe na kuletwa Arusha sababu ni mgogoro wako na mwanasheria wa Halmashauri hiyo hadi mkafikishana Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Na kupelekea Rais Kikwete Akutumbue.

Baada ulipokuja Arusha uliingia katika mgogoro na aliyekua Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dr. Maden sababu ikiwa ni fidia ya 1.9 Bilioni ambazo ulilazimisha zilipwe wakazi wa Oloresho, Kata ya Olasiti, ili kupisha ujenzi wa kituo cha mabasi.

Dr. Madeni alipokataa na kuunda tume ya kupitia malipo hayo na kugundua kuna zaidi ya milioni mia 8 zilikua zimezidishwa tofauti na kiwango halisi cha Milioni 40 kwa heka ambapo wewe na genge lako mliweka milioni 80 kwa heka ndio vita yako ikaanzia hapo na kusababisha Mheshimiwa Rais kuwatumbua wewe na Mkurugenzi huyo.

Nimejikuta nikijiuliza maswali na kupelekea kukuandikia barua hii ili kujua TATIZO LAKO NI NINI NA WATUMISHI WENZAKO?

Malalamiko yako ya leo yamenifanya nikuandikie barua hii kukukumbusha mambo machache ukiwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambapo nafasi hiyo uliipata kwa figisu uliyomfanyia aliyekua Mkuu wa mkoa wa Arusha Felix Ntibenda na tarehe 18, Agost 2016 uliteuliwa nafasi hiyo. (Hili tuliache sina uhakika nalo.)

Mheshimiwa Mbunge Unakumbuka ule Mradi wa bodaboda 2017 hadi 2020 wewe na kikundi chako mlikusanya pesa kutoka kwa wadau kwa ajili ya kununua pikipki 200 ambazo thamani ya kila pikipiki moja ni shilingi 2,100,000/- Je uliunda kamati kwa mujibu wa Sheria? Je fedha hizo zipo wapi? Unakumbuka wakati wa kampeni ulisema pesa zipo bank kwenye acc maalum iliyopo NMB na mpaka sasa kimya.

Je, unakumbuka Ajali ya Luck Vicent? Unakumbuka ulikusanya zaidi ya Milioni mia tatu? Je, ni kamati gani ilikusanya pesa hiyo?

Unakumbuka mkopo wa wanawake 600 wa kiasi cha laki 2 kila mmoja na fedha hizo ulisema ulichanga kutoka kwa wadau, Je ni kamati gani ilisimamia zoezi hilo? Je fedha hizo zipo wapi?

Unakumbuka ujenzi wa msikiti wa Murieti? Pesa ilitoka kwa wadau je Kamati gani ilisimamia zoezi hilo?

Unakumbuka ugomvi wako na DC wa Jiji la Arusha wakati ukiwa RC kuhusu ununuzi wa Mabati feki 200 pale Murieti?

Je tuhoji juu ya Shule ya Mrisho Gambo ? Ujenzi wake ulifuata utaratibu? Kuipa shule jina kulifuata utaratibu?

Unakumbuka ujenzi wa soko la Samunge? Au tukukumbushe?

Unakumbuka timu ya Arusha United? Michango ya timu hiyo, Jinsi ilivyouzwa?

Unakumbuka nyumba za Polisi ambazo Mheshimiwa Rais Magufuli alikataa kutoa vyeti vya pongezi kwa wadau waliochangia baada ya kugundua kuna upigaji? Je kamati ya Michango ya ujenzi iliundwa kwa mujibu wa sheria?

Mheshimiwa mbunge, Wewe ni mtu wa maslahi na usipokua kwenye maslahi unafanya fitna. Wewe ni mtu ambaye hutaki kuona vijana wakifanikiwa katika nyanja ya Siasa. Bila aibu umemsema Katibu Mkuu wa UVCCM na ulishawahi sema utamshughulikia.

Leo nimekuona ukiwa na Diwani wa wa Sombetini ndugu Msangi, Huyo diwani ndiye uliyemtuma leo kazi ya kupiga picha ambazo umemwambia Mheshimiwa Waziri unazo na pia ndiye kaandaa watu wa kukushangilia wakati unaongea. (Planning Presentation)

Una nini na vijana? Juzi bungeni ulimshambulia Mbunge kijana Mheshimiwa Asia Halamga Mbunge wa Viti Maalum Manyara kwa tiketi ya Vijana.

Katika barua hii nakushauri upunguze kiburi cha Madaraka na kutengeneza migogoro isiyo na Afya, Msaidie Rais Samia Suluhu Hassan kujenga nchi. Rasi anahubiri Amani na Umoja. Anapambana kutafuta Mshikamano wa Kitaifa wewe unatengeneza Migogori.

Wacha leo niishie hapa siku ingine tukionana nitakwambia kwa kirefu.

_Ni mimi mtoto wa Mama Ntilie
Wa soko Kuu Arusha_
Doh! Mrisho kaisha
 
Mrisho Gambo..anauroho, tamaa na uchu wa madaraka kinachomsaidia ni uchawi, jeuri na kiburi.

Watu kama hao mnashindwaje kuwashughurikia kiumbe 1 kiwatese watu mamia..huo ni upumbavu hadi shetani anawashangaa.

Dawa ya moto ni moto.
 
Kuna kitu sijaelewa.
Unatska kusema hayo madudu yaliyoibuliwa na Majaliwa hayana ukweli?

Sijaelewa kusudi lako hasa ni nini?
Unataka Gambo aungsnishwe huko au unaona hakufaa kuwatuhumu sababu na yeye sio safi?
 
Kijiko anawacheki tu...huyu Mzee mlimfitini kwa kuwa alisimamia misingi ya UTAWALA BORA...najimbo likiwa chini ya CHADEMA.....

Mnafukuzana kwa kumvizia mwenye NYUMBA HAYUPO ngoja arudi KIWAKE....

None: Mkurugenzi huteuliwa na Prezidaa
 
Back
Top Bottom