Barua ya wazi kwa Mzee Bakhresa, Gharib wa GSM na Mo Dewji: Wakati mkiwekeza katika michezo, isaidieni jamii pia kwenye mambo mengine ya maana

Tafuta hela wewe acha kupangia watu watumieje pesa zao. Kwa taarifa yako Mo anafadhili mpaka wanafunzi vyuo vikuu.
 
Usikute we mwenyewe hata ukipata 10k hukumbuki kumtumia maza sukari hata ¼ au kumnunulia daftari 1 mtoto anaeishi mazingira magumu ila unatushauri matajiri jinsi ya kutumia pesa zetu wakati zako hutumii hivyo
 
Watu uliowataja wamewekeza sehemu nyingi sana,sema kwenye mpira Sasa ukiweka hata laki tu

Utajulikana umetoa
 
Je, sera za uwekezaji pamoja na usalama wa mali zao ukoje?
Ni sawa na kutumia muda mwingi kushangilia mipira na kuacha kujadili mambo ya muhimu zaidi
 
Daah we jamaa yale maviwanda ya bakhressa yako zaidi ya 3 dar pale tena yako barabarani tu na ajira zake waala sio kazi kupata na vijana kibao wako pale wanapiga job.
Wewe uko wapi huko unakosema hawa jamaa hawajawekeza kwenye sekta zinazowapa ajira watanzania. Wana magari na viwanda vilivyoajiri wajuzi na wasowajuzi, achana na huko hata hiyo sekta ya michezo watu kibao wamelamba kazi huko.

Wabongo tupunguze chuki kwa waliofanikiwa, hii kitu ni mbaya mno na inazidisha umaskini. Yaani huoni faida ya kitu mpaka kikuguse wewe moja kwa moja, unahisi hizo Billion 2 ni nyingi kuliko maviwanda, usafirishaji na biashara walizofungua hao jamaa.

Jifunze kuappreciate hata kama hizo pesa hutaramba hata mia kijana.
 
Ndugu Gharib, Mzee Bakhresa na Mo Dewji

Amani ya Mwenyezi Mungu iwe nanyi

Nichukue fursa hii kukupongezeni kwa jitihada zenu za kuinua michezo, hakika uwekezaji wenu utasaidia kuinua michezo nchini, kutoa ajira kwa vijana wetu wanaoshiriki ligi n. k

Lakini pamoja na hayo, naomba niongee na nyie mambo yafuatayo:

1. Hebu sasa isaidieni jamii kuwekeza kwenye mambo mengine ya msingi zaidi

Siwapangii namna ya kutumia pesa zenu, lakini je mnalionaje wazo la nyinyi kusaidia mambo ya maana zaidi kuliko hii mipiramipira?, Kwa mfano mnaonaje mkitengeneza makampuni ya uwezeshaji vijana wetu kwa kufinance startups zao?, kutengeneza funds mbalimbali za kusidia wenye uhitaji kama vile Yatima, Vikongwe n. k?

2. Saidieni Waislamu wajinyanyue kielimu

Nyinyi ni matajiri wa kiislamu, na jamii ya waislamu wenzenu iko nyuma sana kielimu, Takwimu zinaonyesha wazi katika madhehebu ya dini yanayoongoza kwa umiliki mdogo wa shule na mifumo ya huduma za jamii ni Waislamu, pia wako wachache vyuoni na katika ajira rasmi za serikali. Sasa nyie kama waislamu mliobarikiwa, Mnawasaidiaje Waislamu wenzenu kujikwamua kielimu?
Maana naona mipesa mingi mnaiingiza katika mpira. Je, vipi Waislamu wenzenu mnawasaidiaje? Na nyie tengenezeni Ahera yenu, pamoja na kuwekeza katika hii "michezomichezo" ya duniani, hebu wekezeni na ahera kwa kuinua waislamu wenzenu!

3. Ongezeni investment katika nyanja zinazoweza kutoa ajira zaidi kwa wananchi wa chini

Sina wasiwasi na uzalendo wenu, lakini naamini mna potential ya kuinvest kwenye sekta zinazoweza kugusa maisha ya wananchi wetu wengi, hii mipesa mnayomwaga kwenye mpira, kwanini msifikirie pia kufanya kilimo, tena kufanya kilimo. kwa kulenga watu wetu masikini? What if msianze kutafutia watu wetu masoko huko nje? What if msiweke dhamira ya kupanua ununuzi wa mazao ya wakulima zaidi? Nafahamu kuwa Mzee Bakhresa na Mo wanafanya kilimo ktk hatua kadha wa kadha, lakini hapa nazungumzia kilimo strategic kwa ajili ya kuwainua wakulima wadogowadogo na kutia ajira kwa vijana wetu.

Mwisho kabisa ningependa kumalizia kwa kusema kuwa, SIWAPANGII namna ya KUTUMIA PESA YENU lakini mimi kama mwanadamu na Mtanzania naona kuwa wakati mkiwekeza kwenye Mpira mbona hamuwekezi na kwenye mambo mengine ya maana zaidi kuliko mpira?

Ziko wapi universities, Au State of art schools, Au hospitali za maana mnazojenga nchini?

Ziko wapi investments za kumuinua mtu wa chini kwa kumjengea capacity?

Na pia mbona hamuinvest vya kutosha kusaidia waislamu wenzenu kielimu na kiuchumi?

Hayo tu!

Assalam aleikum
Gazeti reeefu halafu pumba tupu, hujui ulichokiandika wala hujafanya utafiti.

Matajili wa Tanzania ni waislamu hukuwahi kulijuwa hili kwa sababu unajuwa uislamu ni kuvaa makubanzi na kufuga mshipa tu.

Hospitali ya Agha Khan, shule za Agha khan na Diamond trust bank ni mali ya waislamu, nakupa mfano mdogo tu utoke usingizini maana ni kama umelewa kubeli.

Usidhani waislamu maana yake ni wale wahuni wa Bakwata kina Alhad Musa kila siku kiguu na njia kufukuzia minuso ya serikali na bahasha za kaki.
 
Daah we jamaa yale maviwanda ya bakhressa yako zaidi ya 3 dar pale tena yako barabarani tu na ajira zake waala sio kazi kupata na vijana kibao wako pale wanapiga job.
Wewe uko wapi huko unakosema hawa jamaa hawajawekeza kwenye sekta zinazowapa ajira watanzania. Wana magari na viwanda vilivyoajiri wajuzi na wasowajuzi, achana na huko hata hiyo sekta ya michezo watu kibao wamelamba kazi huko.

Wabongo tupunguze chuki kwa waliofanikiwa, hii kitu ni mbaya mno na inazidisha umaskini. Yaani huoni faida ya kitu mpaka kikuguse wewe moja kwa moja, unahisi hizo Billion 2 ni nyingi kuliko maviwanda, usafirishaji na biashara walizofungua hao jamaa.

Jifunze kuappreciate hata kama hizo pesa hutaramba hata mia kijana.
Hao GSM ukiacha maduka yao na uwekezeji mwingine ukiwa unasafiri kila dakika lazima upishane na truck za GSM, maana yake madereva wengi wamekula shavu hapo.
 
Ndugu Gharib, Mzee Bakhresa na Mo Dewji

Amani ya Mwenyezi Mungu iwe nanyi

Nichukue fursa hii kukupongezeni kwa jitihada zenu za kuinua michezo, hakika uwekezaji wenu utasaidia kuinua michezo nchini, kutoa ajira kwa vijana wetu wanaoshiriki ligi n. k

Lakini pamoja na hayo, naomba niongee na nyie mambo yafuatayo:

1. Hebu sasa isaidieni jamii kuwekeza kwenye mambo mengine ya msingi zaidi

Siwapangii namna ya kutumia pesa zenu, lakini je mnalionaje wazo la nyinyi kusaidia mambo ya maana zaidi kuliko hii mipiramipira?, Kwa mfano mnaonaje mkitengeneza makampuni ya uwezeshaji vijana wetu kwa kufinance startups zao?, kutengeneza funds mbalimbali za kusidia wenye uhitaji kama vile Yatima, Vikongwe n. k?

2. Saidieni Waislamu wajinyanyue kielimu

Nyinyi ni matajiri wa kiislamu, na jamii ya waislamu wenzenu iko nyuma sana kielimu, Takwimu zinaonyesha wazi katika madhehebu ya dini yanayoongoza kwa umiliki mdogo wa shule na mifumo ya huduma za jamii ni Waislamu, pia wako wachache vyuoni na katika ajira rasmi za serikali. Sasa nyie kama waislamu mliobarikiwa, Mnawasaidiaje Waislamu wenzenu kujikwamua kielimu?
Maana naona mipesa mingi mnaiingiza katika mpira. Je, vipi Waislamu wenzenu mnawasaidiaje? Na nyie tengenezeni Ahera yenu, pamoja na kuwekeza katika hii "michezomichezo" ya duniani, hebu wekezeni na ahera kwa kuinua waislamu wenzenu!

3. Ongezeni investment katika nyanja zinazoweza kutoa ajira zaidi kwa wananchi wa chini

Sina wasiwasi na uzalendo wenu, lakini naamini mna potential ya kuinvest kwenye sekta zinazoweza kugusa maisha ya wananchi wetu wengi, hii mipesa mnayomwaga kwenye mpira, kwanini msifikirie pia kufanya kilimo, tena kufanya kilimo. kwa kulenga watu wetu masikini? What if msianze kutafutia watu wetu masoko huko nje? What if msiweke dhamira ya kupanua ununuzi wa mazao ya wakulima zaidi? Nafahamu kuwa Mzee Bakhresa na Mo wanafanya kilimo ktk hatua kadha wa kadha, lakini hapa nazungumzia kilimo strategic kwa ajili ya kuwainua wakulima wadogowadogo na kutia ajira kwa vijana wetu.

Mwisho kabisa ningependa kumalizia kwa kusema kuwa, SIWAPANGII namna ya KUTUMIA PESA YENU lakini mimi kama mwanadamu na Mtanzania naona kuwa wakati mkiwekeza kwenye Mpira mbona hamuwekezi na kwenye mambo mengine ya maana zaidi kuliko mpira?

Ziko wapi universities, Au State of art schools, Au hospitali za maana mnazojenga nchini?

Ziko wapi investments za kumuinua mtu wa chini kwa kumjengea capacity?

Na pia mbona hamuinvest vya kutosha kusaidia waislamu wenzenu kielimu na kiuchumi?

Hayo tu!

Assalam aleikum
Mkuu wewe pigana nawe uwasaidie.na wewe ni binadamu. Usiwe unategemea kusaidiwa bali tegemea kusaidia na wewe ama wewe sio binadamu.
Pia Kama wewe ni mwafrika. Kuwa mjanja basi hujaelewa kuwa dini walieleta ili wakulainishe uwe mlaini unyonywe.
Si unajua mzungu alichofanya mwafrika na huku akamletea dini ama mwarabu alimuuza mwafrika utumwani na huku anamletea dini ya kumlainisha pia. Hebu amka basi jamaa wanaangalia mioyo Yao inataka Nini na sio kuwa wewe unataka Nini.
Wao wakijisikia kwenda kufanyiwa masaje na watt wa kilatino wanaenda Mana pesa Ipo wewe wa hapo mwananyamala tu wa 50k huwezi kuwamudu mkuu. Wanakula maisha Mana pesa ni Yao ama uliwasaidia kuitafuta
 
Inapendeza pia kuona wamewekeza katika huduma za kijamii unapita sehemu unakutana na Azam secondary school, Mo hospital, GSM University ilimradi lengo la huduma hizo ziwe ni huduma kwa wasio jiweza zisigeuzwe biashara.
 
Ni sawa!! lkn wewe mleta Mada labda humjui Bakhresa vizuri yaani unataka akusaidie wewe! ndo uone amefanya kitu kizuri! si ndiyo??

jamani huyu Mzee sijawahi ona roho nzuri ya kimalaika km huyu mzee!! mpaka kula jamani ana saidia watu, unatamani kulia kwa msaada wake mpaka sasa chozi linanitoka kwa wema wa huyu mtu!! sasa wewe unataka nini ndg? ......ajikatekate?
 
Hao GSM ukiacha maduka yao na uwekezeji mwingine ukiwa unasafiri kila dakika lazima upishane na truck za GSM, maana yake madereva wengi wamekula shavu hapo.
Naona pia GSM wanaingiza mabati yao sokoni
 
Hao kuwekeza kwenye michezo ni sawa na kwenda kulipia tangazo kwenye vyombo vya habari, sio kwamba wanasaidia michezo, ni wanainua biashara zao kupitia matangazo
Exactly, hapo ni mbinu ya kutangaza biashara zao.
 
Inapendeza pia kuona wamewekeza katika huduma za kijamii unapita sehemu unakutana na Azam secondary school, Mo hospital, GSM University ilimradi lengo la huduma hizo ziwe ni huduma kwa wasio jiweza zisigeuzwe biashara.
Wewe umeielewa vizuri mada hii.
Uwekezaji wa kiuchumi ni mzuri lakini si vibaya wakiwekeza kwenye huduma za jamii, Shule, vyuo, Mahospitali n. k. Wakifanya hivyo watakuwa wanagive back kwenye society kwa namna nzuri zaidi
 
Back
Top Bottom