Barua ya wazi kwa Mzee Jakaya Mrisho Kikwete: Hivi wakati unaweka ndani Masheikh wetu ulikuwa unafikiria nini?


Brother hicho ulicho highlight ni matokeo ya operations za chini kwa chini na inform za mchunga kondoo....kuna mtu pia yuko jela Guantamo anaitwa KSM alishawahi kuwadokeza wakapuuza, dogo akaja na taarifa hizo hizo na akimtaja KSM ( ambaye tayari wanaye) baada ya hapo surveilance ndio ikaanza pamoja na hayo uliyohighlight hapo....amini hivyo usipate taabu.
 
Allah amsamehe Mzee Jakaya Kikwete katika yale aliyokosea. Amejitahidi mno katika nafasi aliyopata. Binafsi nampa udhuru na kumdhania kheri kuwa alifanya mambo yale kwa nia njema na kwa maslahi ya Waislam. Wakati wa zile harakati zilizofanywa na baadhi ya Waislam wakati ule (2010-2013), kiukweli kwangu mimi naona walifanya makosa mengi.

Nakumbuka jinsi walivyomsumbua Kikwete, jinsi Kikwete alivyotukanwa na kusemwa vibaya hadharani na baadhi ya hawa wanaharakati, nakumbuka maandamano yasiyokwisha. Usisahau na jinsi alivyopigwa vita na baadhi ya wasio Waislam.

Alikuwa na wakati mgumu sana, wakati huo bado nilikuwa mdogo, ila sasa nikifikiria hilo nagundua kwamba Jakaya alipata shida sana.

Allah amsamehe makosa yake.
 

Saga zima la kupatikana Osama bin Laden liko documented wazi wazi:

Manhunt for Osama bin Laden - Wikipedia

Mchunga kondoo?! Leta ushahidi.

Ninakazia mchawi siyo CCM, JK wala Samia. Mchawi wetu yuko hapa:

Kama CCM siyo adui -- mchawi wetu ni nani?
 
Umesahau hao masheikh walivoleta mpasuko wa kidini na mihadhara ya chuki au? waache wakae kwa kutulia.
 
Nakumbuka Mzee Mohamed Said aliwahi kueleza namna sheikh Ponda na wenzake walivyozunguka nchi hii kumpigania JK mwaka 2010........hii nchi dini na siasa zimejaa wasanii.
Nchi hii ni kubwa na ni zaidi ya interest za dini moja. Inashangaza sana wakati ule watu wanavamia vituo vya polisi na kuua hakuna aliyekuwa anasema kwanini wanafanya vile. JK aliapa kuilinda katiba. Angeisaliti, sababu ya ujinga wa kikundi cha watu wachache, unafikiri angeficha wapi uso wake? Tumuache JK apumzike. Sheria zipo. Tufuate taratibu za kisheria kuliko kuongozwa na jazba au fyoko fyoko kwenda haya mambo nyeti ya usalama
 
Kwa nini usiende kwa hao masheikh nao watakuambia kile walichokifanya hadi wamekaa ndani miaka zaidi ya 9.
Yaliyotokea MKIRU hayakuanzaia hewani.
 
Jee wakati wakifanya kampeni za kidini na kuchafua amani ya nchi na kueneza Al khaida na Islamic nation wewe ulitaka afanyeje ?
 
Hilo ni tatizo la dunia,dunia nzima inaamini kuna uhusiano kati ya uislam na ugaidi
 
Sawa usalama wa nchi una oparate kwa ushahidi sio kwa hisia au chuki huwezi kufunga mtu miaka 10 bila kumtia hatiani, walete ushahidi kwamba alikua hatari sio hearsays, hao watu wana familia, ni watanzania wana haki kamiri. Sio poa kutumia tishio la usalama wa Taifa kutesa watu.......JK wakati wa utawala wake hakua na mamlaka kamiri na na ma suala ya usalama ali laumiwa sana kwamba ana walea Magaidi, unakumbuka ma bomu ya mbagala paka leo report haijatoka kwa nini? Mlipuka mara mbili tena kipindi cha JK, kulikua na jambo nyuma yake ambao paka leo alija semwa........tafakari sana hayo mambo.
 
Asipo kujibu jiulize na yale makanisa na mapadri nani alikua anawaua na kuyachoma pia kuua watalii?
Na kwa nini walipokamatwa mauaji yaliisha ma utulivu ukalejea.

Je hao waliokufa kwa vitendo hivyo walikufa kwa haki au kwa dhurma?
 
Mkuu umenena.
Mkuu umenena. Huyu bwana alijisahau kabisa 😡😡
 
unaposema Jk hakuwa na Mamlaka kamili unakuwa unakusudia kumaanisha nini hasa?.

Ebu fafanua.
na yale mabomu ya mbagala unataka kusema yalilipuliwa makusudi kuua waislamu, ama?
 
Dr,Ulimboka alipata alichostahili hakuonewa hata chembe
 
Dr,Ulimboka alipata alichostahili hakuonewa hata chembe

Dr. Ulimboka alikuwa kiongozi wa madaktari waliokuwa wanadai haki ya kuongezewa stahili zao. Sasa mkwere kumtesa kwa kudai haki ndio stahili yake? Vasco Dagama has blood on his hands and he will live to pay up hapa hapa duniani!!
 
Dr. Ulimboka alikuwa kiongozi wa madaktari waliokuwa wanadai haki ya kuongezewa stahili zao. Sasa mkwere kumtesa kwa kudai haki ndio stahili yake? Vasco Dagama has blood on his hands and he will live to pay up hapa hapa duniani!!
Njia walioichagua kudai nyongeza ya marupurupu iligharimu maisha ya watu wengi sana wa kipato cha chini na ndio maana alipata alichostahili.
 
unaposema Jk hakuwa na Mamlaka kamili unakuwa unakusudia kumaanisha nini hasa?.

Ebu fafanua.
na yale mabomu ya mbagala unataka kusema yalilipuliwa makusudi kuua waislamu, ama?
Hapana sio hivyo sijaongelea wa Islamu, naomba utafari hili jambo kwa makini ondoa hisia.
 
Hapana sio hivyo sijaongelea wa Islamu, naomba utafari hili jambo kwa makini ondoa hisia.
Chief, angalia kuna alama za kuuliza katika koment yangu.
kwakuwa sijui ulikusudia kusema nini uliposema:, Jk hakuwa na mamlaka kamili", basi nifafanulie nini ulimaanisha.
 
Njia walioichagua kudai nyongeza ya marupurupu iligharimu maisha ya watu wengi sana wa kipato cha chini na ndio maana alipata alichostahili.

Hiyo ni sababu ya kujihami kwani Maisha ya watu hupotea kwa kukosa dawa na wadaktari wakiwepo!! Je baada ya hapo Kikwete aliongeza marurupu ya madaktari kama hiyo sababu unayotoa ina uhalisia? Wapi! Serikali haikuongeza kwasababu hela yote mkwere alikuwa anakomba kwa kusafiri na kuwahonga Wabunge!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…