Barua ya wazi kwa Mzee Jakaya Mrisho Kikwete: Hivi wakati unaweka ndani Masheikh wetu ulikuwa unafikiria nini?

Naona wachangiaji wanaconclude kuwa Masheikh ni Magaidi lakini leo wako ndani mwaka wa 8 na hakuna Ushahidi ulioletwa mahakamani wa kuwatia hatiani.

Hii precedence ya kukubali tu baadhi ya watu kumbikiziwa kesi za Ugaidi, kuwanyanyasa bila ushahidi wa uhusika wao, kamwe haitoishia kwa hawa waislamu, Wapo watu watakuja kubambikiziwa kesi za hivihivi na tutakosa moral authority ya kuwatetea kwa sababu zamani tulishaunga mkono raia wengine kubambikiziwa kesi za aina hii kwa sababu tu ya hisia za Udini wetu.

Leo tutanzaje kuwatetea akina Adamoo, wakati at the same time tunaunga mkono wengine kuwekwa ndani bila ushahidi wa ugaidi?
 
Mnama jamaa alishughulikiwa na watu wenye hasira kali baada ya kuleta michezo ktk mambo ya msingi,asilimia kubwa ya wanufaika wa huduma za afya ktk hospital za umma ni sis watu wa kipato cha chin anapotokea mtu anachagiza wahudumu wa hizo hosp wagome inamaana anatuumiza sis moja kwa moja kwa vyovyote vile mtu km huyo tutamchukulia km adui na hatuwez muonea huruma hata kimasikhara.
 
Raisi analaumiwaje kama mihimili mingine inafanya kazi kiufasaha?hao inawezekana walikamatwa hata raisi hajui,Wale Wa Uamsho tunajua walikua tishio kwenye suala la Muungano
 

Huduma za hospitali zilikuwa duni kwasababu ujira wao ulikuwa hauendani na kazi walizokuwa wanafanya. Jitiahada zao za mazungumzu na wakubwa zao kuhusu kuboresha mapato yao ziligonga mwamba hivyo ilibidi watumie njia ambayo ingefanikisha azma yao na pia ingewafanya madaktari wawahudumie wagonjwa kwa ari kubwa zaidi ya walivyokuwa wanafanya!!!
Adui wa wananchi ni yule aliyekuwa anatumia fedha za walipa kodi kuzurula dunia nzima na wapambe wake wakila bata badala ya kuzitumia fedha hizo kuboresha huduma za afya za hao unaowaita watu wa kipato cha chini.
 
Maneno matupu yale yale ya siku zote. Unaweza kusema kwa habari zako hizi ni kwanini Uamsho wameachiwa huru bila kumaliza kesi zao?

Watu waliokamatwa ni wale walioonekana kywa tishio kwa utawala wa ccm waliaminiwa kuwa ni watu wa dini hivyo hawapaswi kuwa wafuasi wa CUF.
 
Nakumbuka Mzee Mohamed Said aliwahi kueleza namna sheikh Ponda na wenzake walivyozunguka nchi hii kumpigania JK mwaka 2010........hii nchi dini na siasa zimejaa wasanii.
Mda wake uliisha pita, hawez kukumbuka waliompigania hapo ndipo utakumbuka TENDA WEMA UENDEZAKO wakina sheikh Ponda waliishamaliza kazi yao yakumnad malipo yao ndio hayo.
 

..Lissu aliwatetea mashekhe wa uamsho na answar sunna wakati wa kampeni za 2020.

..na alisema mashekhe wa answar sunna walioko rumande wanakadiriwa kuwa zaidi ya 160.

..inaelekea mashekhe walioachiwa ni wa uamsho toka Znz lakini wa answar sunna wanaendelea kushikiliwa.

..ni bahati mbaya kwamba kadhia ya mashekhe wa answar sunna haina wasemaji wengi kama ilivyokuwa kwa wenzao wa uamsho.
 
Sio ninaowaita wa kipato cha chini ni mim hapa mmoja kati wa kipato cha chin na kuhusu wanasiasa hilo lipo wazi dunia nzima kuanzia magharib mpaka mashariki wanasiasa ni watu wa kuish kianasa chini ya ulinzi mkubwa huyo mkwere unamuonea tu labda kwa vile taarifa zake unazipata kiwepes kuliko wanasiasa wengine lkn yule mshkaj alipata alichostahili
 
Wewe mtu wa mrima mambo ya Wanzibari yanakuhusu nini ? pambana wakimbizi haramu uko.
 
Mkuu Missile of the Nation nakuaminia sana kwa mada ila hili la Masheikh wa Uamsho liache lipite kama lilivyo. Hata wenyewe akina Sheikh Farid na Sheikh Mselem wamekubali kuwa kimya.

Bila busara na hatua madhubuti ambazo JK alichukua mwaka 2013, Tanzania ingegeuka Kismayu au Mogadishu nyingine.

Je uliwahi kusikia tena mapadre wameuliwa au makanisa yameungua moto baada ya kuwaweka rumande hao Uamsho?
 
Mimi nina declare masilahi kuwa ni Mkristu tena MKATOLIKI lakini sikubaliani kuhisisha UISLAMU na Ugaidi. Ni kweli mtu ana dini lakini tabia yake ni uhaidi, tusihusishe na dini yake. Na hawa watu wasijifiche kwenye kivuli ch uislamu
 
Nakumbuka kipindi cha kampeni, Lissu aliliongelea sana suala hili la Masheikh lukuki kuwa ndani miaka kibao.
Huu utawala wa CCM umejaa udhalimu wa kutisha!
 
Brother.
Hatuwatetei wahalifu, bali tunasema hivi, kama serikali ina ushahidi, basi sheria ichukue mkondo wake.

Lakini hawa watu unawaweka ndani miaka saba/nane na ushahidi wa kuwafunga haupo, sasa hapo unaendelea kuwashikilia kwa misingi ipi ya kisheria?

Kumhukumu mtu ugaidi na kumtreat kama Gaidi lakini at tje same time huna ushahidi wa kumuimplicate mahakamani hiyo ni mob justice, na wewe unafanya kosa hilohilo la kuwahukumu moja kwa moja kuwa hao ni magaidi. What if they are innocent?
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!! Usalama wa taifa ni wa muhimu kuliko chochote!! Kwanza rekebisha, hakuna mashehe waliowekwa ndani!! Waliowekwa ndani ni watunumiwaz wa ugaidi!! Hawakuwekwa ndani kwa ajili ya ushehe wao bali kwa ajili ya tuhuma zao. Nampongeza sana Kikwete kwa hilo!! Kama unabisha waulize nigeria kuhusu boko haram!! Amini usiamini mwelekeo ulikuwa ni huo!! Wakiachiwa wamshukuru Mungu !
 
Mmarekani mwenyewe hadi Biden anaingia madarakani Januari mwaka huu alikuwa na wafungwa 59 Guantanamo tangu miaka ya mwanzo ya 2000. Na hajawahi wafikisha Mahakamani.

Ugaidi usikie tu Afghanistan na Mogadishu lakini isiwe nchini mwako. I assure you hata wewe ungesoma ripoti aliyoiona JK na Shein, kama ungekuwa Rais wa Tz pengine ungechukua maamuzi makali kuliko haya. Trust the process
 
Marekani kawapeleka watuhumiwa wake Guantanamo sehemu ambayo US Law haiapply, angewaweka kwenye magereza ya ndani ya ardhi ya Marekani angepaswa kutumia sheria zote za Marekani.

Sasa sisi hapa kwetu, Masheilh wapo ndani ya ardhi yetu, na wanapelekwa katika mahakama hizihizi, kwa hiyo ni either serikali Ilete ushahidi kuwa kweli ni magaidi ili iwafunge AU kama hakuna ushahidi basi iwaachie huru!.

Ngoja nikuulize swali, tuliaminishwa kuwa Masheikh wa uamsho ni Magaidi, Mbona sasa serikali ilishindwa kuthibitisha ugaidi wao mahakamani, na mbona DPP alifuta kesi hiyo? —Ugaidi si ni kitu kibaya, kwa nini umfutie Gaidi Kesi kama kweli ni gaidi na ushahidi unao?
 
Kilichofanyika USA kwa kuwapeleka Guantanamo washukiwa wa ugaidi wa Alqaeda ni sawa na kilichowaleta Tanzania bara washukiwa wa ugaidi wa Uamsho. Mahakama ya Tanzania haina jurisdiction kwenye makosa yanayofanyika ardhi ya ZNZ kwa kuwa ZNZ ina Mahakama yake.

Mahakama ya Rufaa pekee ndiyo suala la Muungano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…