Barua ya wazi kwa Rais Samia kuhusu Katiba Mpya (Sehemu ya kwanza)

MWAISEMBA CR

Member
Joined
Apr 21, 2014
Posts
87
Reaction score
81
🇹🇿BARUA YA WAZI KWA RAIS WANGU MAMA SAMIA SULUHU HASSAN

(SEHEMU YA KWANZA)

🔵KUTOKA KWA : Shujaa Charles Richard Mwaisemba (©️®️Ⓜ️

Tabata,Dar es salaaam

stmwaisembac@gmail.com

♨️YAH: OMBI JUU YA KURUHUSU KUENDELEA KWA MCHAKATO WA KUPATA KATIBA MPYA

Shikamoo mama,Pole na majukumu mazito ya kuongoza nchi yetu ya Tanzania na hongera kwa kutimiza mwaka mmoja tangu uapishwe kama Rais wa awamu ya sita wa Tanzania.

Nimeona Vyema nitumie nafasi hii ya haki yangu ya kikatiba kama Raia wa Tanzania, kukushauri mambo makuu matatu(3️⃣) ya msingi ya kuyafahamu unapoendelea na uongozi wako kuiongoza nchi yetu ambayo ikiwa utayazingatia na kuyafuata yakusaidia sana katika safari yako ya uongozi na utakuwa ni miongoni mwa marais bora sana watakaokumbukwa kwa vizazi vyote vilivyopo na vitakavyokuja na ambapo itakujengea heshima kubwa sana katika nchi yetu ya Tanzania.

1️⃣HEKIMA YA KIUONGOZI KUTOKA KWA MUNGU KWA WANANCHI

Moja ya jambo la msingi na la maana kwa Kiongozi yeyote anayeongoza watu chini yake, analopaswa kuwepo nalo na Kumuomba Mungu ni HEKIMA YA KIUONGOZI.Mfalme Suleiman kabla ya kuwa mfalme alianza kwanza Kumuomba Mungu ampatie Hekima ya kuwaongoza na kuwaamua wananchi anaoenda kuwatawala na kuwaongoza , Ndipo Mungu nae si tu alimpatia hekima bali ndiye alimfanya kuwa tajiri na mfalme aliyeandikwa katika historia ya Israel kwa Kujenga Hekalu kubwa la wayahudi linalojulikana kama HEKALU LA SULEIMAN

♨️{1 WAFALME 3:9,11-13}

"[9]Kwa hiyo NIPE MIMI MTUMWA WAKO MOYO WA ADILI NIWAHUKUMU WATU WAKO, na kupambanua mema na mabaya; maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako walio wengi?

[11]Mungu akamwambia, Kwa kuwa umeomba neno hili, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi; wala hukutaka utajiri kwa nafsi yako; wala hukutaka roho za adui zako; BALI UMEJITAKIA AKILI ZA KUJUA KUHUKUMU;

[12]basi, tazama, nimefanya kama ulivyosema. Tazama, nimekupa MOYO WA HEKIMA NA AKILI; hata kabla yako hapakuwa na mtu kama wewe, wala baada yako hatainuka mtu kama wewe.

[13] NA MAMBO YALE USIYOYAOMBA NIMEKUPA, mali na fahari, HATA HAPATAKUWA NA MTU KATIKA WAFALME KAMA WEWE,SIKU ZAKO ZOTE.

Mama malengo ya kukuandikia barua hii ya wazi, ni kutaka kukupa ushauri utakaoweza kukufanya nawe si tu uwe na hekima ya kiuongozi bali uwe ni Rais bora ambaye hajawai kutokea katika nchi yetu ya Tanzania.Na sitaki hasa nikupe ushauri wangu kama ushauri wangu kwani unaweza ukatafsirika ni ushauri wa kibinadamu au wa kisiasa bali leo nitatumia Maandiko matakatifu kukupa Ushauri wa Mshauri wa ajabu,Yesu Kristo hasa katika eneo hilo la Kujua hekima ya kufanya na kuamua katika kuwaongoza watu ambayo itakufanya si tu kupendwa bali itakufanya kuacha historia kubwa katika nchi yetu....

Mama , kabla ya kukueleza utumie hekima gani au ufanye nini, Ninaomba nikupe historia fupi ya Maongozi ya Mungu kwa wanadamu ambayo itakupa picha ya nini unatakiwa kufanya kwa upande wako katika kuwaongoza wananchi wako

Mungu tangu kuumbwa kwa dunia mpaka sasa, pamoja na nguvu zake zote, na uwezo wake wote na ufalme wake wote lakini kamwe hajawai kumtawala mwanadamu kwa manguvu au mabavu (Kidicteta) au hajawai kulazimisha wanadamu wamkubali au kuwafanya wamuamini hata kama wao hawataki kumuamini au kumkubali, yaani kwa maana rahisi na ya kueleweka ni kwamba MUNGU NI MUNGU AU BABA WA DEMOCRASIA, nikiwa na maana amempa kila mwanadamu uhuru wa kuchagua ni nani anayetaka kumtumikia? YOSHUA 24:15 .Mungu ndiye amempa mwanadamu utashi wa kuchagua Mema au mabaya, yaani kufanya kitu kwa uhuru au hiyari yake mwenyewe .Na Hapo ndipo tunapoanza Kuona Mungu akijenga misingi ya Democrasia kwa mwanadamu

Lakini pamoja na yote,Kwa wakati fulani bado Mungu alitaka kuendelea kuwa Mfalme wa Taifa lake aliloliita Israel ambalo kwa miaka Mingi halikuwa na Mfalme mwanadamu aliyekuwa analiongoza na kuliamua, isipokuwa Mungu ndio alikuwa mfalme wao.Lakini kutokana na ule utashi aliouweka ndani ya wanadamu hao hao, ilifika mahali hata hao watu wake(Taifa lake israel) nao wakaona watumie haki yao ya kutafuta democrasia yao au uhuru wao, kwa kutaka nao wajipatie mfalme mwanadamu kama mataifa mengine wanavyofanya sio kuendelea kuwa chini ya maongozi ya kiutawala ya Mungu

Lakini kutokana na kuwepo na shinikizo kubwa la watu waliokataa Mungu asiwe mfalme wao bali wajipatie Mfalme mwanadamu kama wao, bado Mungu ambaye pia ni Baba wa Democrasia hakung'ang'ania Ufalme wake bali aliwaachia uhuru wao waliojitakia, kwa kuwapa ruhusa ya ombi lao la kufanya mabadiliko ya kikatiba na kisheria juu ya utawala wa kisiasa waliokuwa nao {Soma 1SAMWELI 8:6-7,19-20,22}

Kwa Msingi wa historia hiyo, tungeweza kusema hao wananchi wa Israel walikuwa hawataki Maongozi ya kikatiba aliyoyaweka Mungu ya kuwaongoza hivyo waliomba MABADILIKO YA KATIBA MPYA ambayo itawaruhusu Kupata Mfalme mwanadamu wa kuweza kuwaamua wao kwa wao sio ile katiba ya zamani ya kiutawala aliyoiweka Mungu. Lakini pamoja na yote bado Mungu ambaye ni mtawala wa democrasia, hakuwazuia wala kuwakatalia pamoja alikuwa na uweza huo.Maanake Ombi la Mabadiliko ya Katiba ya Israel ikaandikwa upya, na ndipo kwa mara ya kwanza ndipo akapatikana Mfalme wa kwanza wa Israel aliyejulikana kama Sauli, akafuata Daudi na ndipo akaja Mfalme Suleiman.Wafalme wote hao maarufu walipatikana baada ya MABADILIKO YA KATIBA YA ISRAEL.

Mama, baada ya kuangalia kwa ufupi historia fupi ya mabadiliko ya kwanza ya katiba ya Israel yalivyopatikana baada ya Mungu kuwakubalia Ombi lao Wana israel ya kupata mfalme,Nilitamani ujifunze kitu kimoja tu hapo.

Kwanza, Ili uwe ni mtawala bora atakayependwa na watu, basi unashauriwa kuwapa uhuru,Democrasia ya kweli wananchi unaowaongoza hata kama unafikiri wewe ndio unajua zaidi yao.Mungu hakuwakatalia Israel ombi lao la kupata Katiba Mpya itakayowawezesha kupata Mfalme mwanadamu, sio kwasababu wao walikuwa wanajua zaidi ya Mungu au sio kwasababu Mungu hakutaka kuendelea na ule ufalme wake kwao ,ila Mungu alikuwa anajua madhara ya wao kujiongoza wenyewe lakini bado aliamua kuheshimu Ombi la watu hao la kutaka mabadiliko ya katiba

Vivyo hivyo mama, wewe kama Rais wetu, tunakuomba unaposikia Kelele za WATANZANIA wanaomba KATIBA MPYA, hata kama unafikiri wao hawapo sahihi kuomba katiba hii kwa sasa au hata kama unaona haina manufaa kwao kwa sasa,Nakushauri wasikilize sauti zao,Usiwakatalie wala kuwapinga

Mama, ikiwa utakubali kufuata hekima ya Mungu katika kuwaongoza watu kama hii kwa kusikiliza sauti yao ya MADAI YA KATIBA MPYA, basi itakupa sifa kubwa sana.Kumbuka Mungu alipowakubalia wanaisrael ombi lao,halikumfanya Mungu asiwe Mungu,Vivyo hivyo nawe ukiwakubalia watanzania Ombi la kupata katiba Mpya ,halitakufanya wewe usiwe Rais wa Tanzania bali litakupa kibali kikubwa sana hata huko mbele ya kuwa Rais bora zaidi kuliko marais wote

Mama,kubali kuwa Rais unayesikiliza wananchi wako wanataka nini? , kubali utawala wa democrasia kwa kuruhusu uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kuabudu,uhuru wa kujieleza,uhuru wa kukosoa au uhuru wa kufanya mikutano ya kisiasa n.k lakini zaidi sana ruhusu Mabadiliko ya Mfumo mzima wa kikatiba wa nchi yetu maana katiba ya sasa iliandikwa katika wakati wa Tanzania ikiwa nchi ya chama kimoja ila sasa ni nchi ya vyama vingi na mazingira na mambo mengi yamebadilika

Mama, Kumbuka Kelele na sauti hizi za mabadiliko ya Katiba Mpya hazijaanza leo tu, Tangu wakati wa Tume ya nyalali mpaka wakati huu wa Tume ya Jaji Warioba ambapo, wewe mama ulikuwa Makamu mwenyekiti wa bunge la katiba.Kumbuka kama ni swala la watu kufahamu na elimu kutolewa, jambo hilo lilikwishafanyika kwa vipindi vyote hivyo ndio Maana hata wakati ule Rais Kikwete aliweza kuliruhusu Kuanza kuelimisha watu,kukusanya maoni ya watu nchi nzima ,kuanza kuandikwa kwa Rasimu ya kwanza ya katiba mpaka likafikia kwenye mkwamo kule bungeni si kwa wananchi kwamba hawakuwa hawana uelewa juu swala uhitaji wa katiba mpya.

Hivyo mama,nilichotaka kukushauri ni kwamba usitumie hekima za wanadamu au hekima za wanasiasa ambao wanaangalia tu maslai ya Chama ya leo ila hawaangalii maslai ya Tanzania ya kesho au usitumie hekima ya washauri wako ulio nao wanaokutisha na kukuogopesha kutokusiliza Sauti za watanzania wanaopiga kelele juu ya Kuendelea kwa Mchakato wa kupata Katiba Mpya, ndio maana nimeanza kwa kukupa hekima ya KiMungu aliyofanya pale aliposikia kelele za namna kama hizi kwa Taifa lake juu ya mabadiliko ya katiba yao ya namna ya kumpata Mfalme mwandamu kama wao.Mungu alikubali kuwasikiliza wananchi wanataka nini, na wewe mama nakushauri sikiliza hekima hii ya KiMungu itakupa kukumbukwa na vizazi vyote vya Tanzania ya sasa na ijayo kwani ndiye utakayekuwa ni Rais wa Kwanza kubadilisha Katiba Mpya inayoendana na Mfumo wa kidemocrasia tulio nao sasa...

Sipo kukushauri kama wanasiasa wanavyoshauri ila nakushauri kwa kupitia Neno la Mungu kuwa Wasikilize wananchi wako wanataka nini ? Kumbuka ukiruhusu kuendelea kwa Mchakato huu wa katiba mpya ndio kutawafanya watu wengi kukupenda zaidi. Sio wananchi wote wanaohitaji katiba mpya, eti wanahitaji kwa sababu za kisiasa tu, Katiba imebeba mambo mengi sana mbali ya kisiasa.Sio wananchi wote ni wanasiasa wala katiba sio ya wanasiasa peke yao bali ni ya watanzania wote, inawezekana inaonekana ni wanasiasa ndio wanaongelea sana kwasababu tu ya nafasi walizo nazo lakini Je kweli, wewe mama ina maana huoni uhitaji wa kufanya mabadiliko haya ya katiba mpya mpaka tusubiri baada ya mwaka 2025? .

Maboresho ya sheria mbalimbali tutakayoyafanya hakufanyi katiba iliyopo iwe mpya, kwani vilaka vimekuwa vingi sana na katika iliyopo imechakaa bali inapaswa tutengeneze kitu kipya kinachoendana na mazingira ya sasa, tutengeneze mifumo mipya katika kila eneo ili tuijenge Tanzania mpya kwa kuwa na Dira mpya itakayomuwezesha mtawala yeyote atakayeingia kuwa mzalendo, mwana democrasia na atakayezingatia utawala wa kisheria na utawala bora....

Asante mama, Hili ni jambo la kwanza kati ya 3 niliyotaka kukushauri.....Nitaendelea kukueleza hayo mambo 2 yaliyosalia katika mwendelezo wa barua yangu hii ya wazi kwako Rais wangu Mama Samia Suluhu Hassan...Mungu akubariki

Wako mtiifu

🔵Na:Shujaa©️®️Ⓜ️

0712054498/0785248997
 
Mama!. Kabla hujafanya lolote. Hebu jiulize.. Aliyenitangulia asingekufa, Swali hili lingeulizwa? Lingeulizwaje? Maamuzi ninayofanya sasa yangefanyikaje? Na Yangekuwa na impact gani kwa nchi yangu?
 
Barua imekaa vyema. Mtumishi wa Mungu Barikiwa sana
 
Maboresho ya sheria mbalimbali tutakayoyafanya hakufanyi katiba iliyopo iwe mpya, kwani vilaka vimekuwa vingi sana na katika iliyopo imechakaa bali inapaswa tutengeneze kitu kipya kinachoendana na mazingira ya sasa, tutengeneze mifumo mipya katika kila eneo ili tuijenge Tanzania mpya kwa kuwa na Dira mpya itakayomuwezesha mtawala yeyote atakayeingia kuwa mzalendo, mwana democrasia na atakayezingatia utawala wa kisheria na utawala bora....
Sahihi
 
Vivyo hivyo mama, wewe kama Rais wetu, tunakuomba unaposikia Kelele za WATANZANIA wanaomba KATIBA MPYA, hata kama unafikiri wao hawapo sahihi kuomba katiba hii kwa sasa au hata kama unaona haina manufaa kwao kwa sasa,Nakushauri wasikilize sauti zao,Usiwakatalie wala kuwapinga
Barikiwa Sana Richard.

Ni nani mwanaye akimuomba Samaki atampa nyoka? ama akimuomba Mkate atampa jiwe??
 
Katika ni nini? Uandishi wa hovyo kabisa, shuleni ulienda kusomea ujinga? haya majitu ndiyo yanaleta vurugu huko dayosisi ya Konde yakishirikiana na Shoo
 
Back
Top Bottom