Kalebejo
Member
- Sep 24, 2022
- 9
- 4
Natumaini u buheri wa afya.Kwanza nakupongeza sana Rais wangu Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa jitihada unazozifanya katika kuwaletea wananchi maendeleo,kwa kutafuta pesa nje na ndani ya nchi yetu Hongera sanaa kwa hatua hii nchi yetu inaendelea kupiga hatua za maendeleo.
Mhe.Rais,uliporithi mikoba ya urais kutoka kwa Hayati Magufuli uliahidi kuendeleza mambo mema aliyofanya, na hasa miradi ya kimkakati ikiwemo SGR. Lakini Jitihada zako Mhe,Rais zinazoloteshwa na watendaji wako ,kwa kipande kimoja kinachonisukuma kuandika barua hii kwako Mhe.Rais ni baadhi ya watendaji wako ambao amewapa mamlaka ya kusimamia mradi wa SGR kipande cha Mwanza
Kivuko cha Kamanga kipo karibu na bandari ya Mwanza kaskazini, kinavusha abiria na mizigo yao kutoka Mwanza mjini kwenda Kamanga-Sengerema.Kutokana na ufinyu wa eneo kwa upande wa Mwanza mjini kivuko kilitakiwa kiwe kimeamishwa kwenda eneo linanapostahili ambapo maeneo Yaliyotengwa na halmashauri ya jiji la Mwanza kwaajiri ya vivuko ni luchelele,awali kulikuwa na vivuko viwili kivuko cha SALAMA FERRY LTD na KAMANGA FERRY LTD, vivuko vyote hivi viliamriwa viamishe shughuli zao kutokana na unyeti wa eneo na kupisha mradi unao kuja wa SGR lakini ni kivuko kimoja tu cha SALAMA FERRY LTD ndio waliotii agizo hilo la kuhama na KAMANGA FERRY amekahidi agizo hilo hadi sasa .
Leo eneo la kivuko cha kamanga ferry mawaziri wawili wamesema eneo hilo ni hatari sana lakini mwekezaji huyu amekuwa akikahidi maagizo ya serikali amekuwa akitoa rushwa kwa baadhi ya wateule wako waliokwenye taasisi husika ili aendelee kufanya shughuli zake.
Kutokana na uwepo wa Kivuko cha Kamanga kuna athari kubwa za kimazingira,kiuchumi na kijamii zinaoendelea na hatua za haraka zinahitajika zichukuliwe ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea
i. Uchafuzi wa maji, huu unatokana na shughuli za kibinadamu zinazoendelea kwenye kivuko cha Kamanga Ferry kumwagika kwa sabuni kutoka kufua,kuoga, mama lishe kuosha vyombo na taka za plastiki kunasababisha eutrophication ya maji. Viumbe wa majini kama samaki wanakufa kutokana na uzuiaji wa kupita kwa kwa nuru na oksijeni hivyo inapelekea hasara kubwa kwa taifa letu kwasababu samaki hawazaliani na uchumi wa watu wa kanda ya ziwa unategemea shuguli za uvuvi
ii. Kelele zinazotokana na shughuli za kibinadamu, kelele za magari na kelele za wapiga debe, huyu mliliki wa kivuko amefanya kituo hicho kama stendi ya basi, abiria na mizigo yao na kivuko hicho kipo karibu kabisa na Mahakama ya wilaya ya Nyamagana,polisi na Kanisa la Aglikana, hivyo kupelekea usumbufu kwa huduma hizi za kijamii.
iii.Eneo hilo la kivuko sio salama kwa raia na mali zao kwasababu liko bararani na reli yaTRC inapita hapo na kunamwingiliano mkubwa kati ya wafanyabiashara wadogo wadogo(machinga),wauza samaki na shughuli za kivuko zimeziba njia za magari na watembea kwa Miguu hivyo kupelekea ajari za mara kwa mara.
iv.Mwekezaji huyu anazuia utalii usifanyike kwa upana wake kwasababu pale kuna kivutio cha utalii cha Bismack Rock na wageni wengi kutoka ndani na nje ya nchi hupendelea kutembelea kivutio hicho lakini kutokana na shughuli za kivuko hicho kumepelekea Kupungua kwa idadi ya watalii
v.Kufatia kuja kwa mradi unaoendelae sasa nchini wa reli ya kisasa wa SGR ambao utafika hadi bandari ya Mwanza kaskazini unaweza kukwamishwa na kivuko hicho kwasababu umbali kutoka reli ilipo sasa na kivuko kilipo haizidi mita 15 na umbali unaotakiwa ni mita 30 hivyo kwa vyovyote vile kutakuwa na mwingiliano kati ya SGR na kivuko cha Kamanga
Mhe.Rais kama umefanikiwa kusoma barua hii naomba uchukue hatua stahiki
Angalizo siku maafa makubwa yakitokea Kamanga ferry naomba serikali mfahamu kuwa janga hilo mmelitengeneza wenyewe hatutaki kusikia pole ,kwa kuwa fursa ya kuhakikisha kivuko cha kamanga ferry kinatoka mnayo ila rushwa zinawasumbua
Kazi iendelee