Naomba kwa ruhusa yako niandike kwa kifupi mambo muhimu kutoka kwenye waraka wako kwa manufaa ya Watanzania wote,kama nimekosea mtanirekebisha;
[emoji637]Mahakama kurudishiwa mamlaka yake
[emoji818]Hapa kama ulikuwa na kesi na huridhishwi na mwenendo wake,ukifungua kesi kukosoa mwenendo wa shauri,kesi itafutwa na utakamatwa upya na kushtakiwa kwa kesi hiyohiyo,maana yake kama ulikaa miaka minne jela,kesi itaanza upya kwakuwa shauri ni jipya.
[emoji638]Makosa yasiyo na dhamana yapitiwe upya
[emoji818]Hali ilivyo , watu hukaa gerazani hata miaka 10 baadae huonekana hawana makosa,hapa tutumie mfumo wa "peleleza-kamata-shtaki"
[emoji639]Kuweka kikomo cha muda kwenye upelelezi
[emoji818]Hapa hata kama makosa yana ukomo wa muda wa upelelezi,mtuhumiwa atakamatwa na kushtakiwa upya,na hukaa gerezani au mahabusu wakisubiri upelelezi ukamilike
[emoji640]Watuhumiwa kushikiliwa vituo vya polisi zaidi ya muda wa kisheria
[emoji818]Wapo ambao hukaa hata mwezi mmoja lakini hawaadikwi kwenye taarifa za mahabusu(occurance book)
[emoji641]Kesi za kubambika na mashtaka ya hila
[emoji818]Hapa vita vya kiuchumi,madawa ya kulevya ,wakosoaji wa serikali ndio hutumika kama sababu ya kubambika kesi
[emoji818]Wanaotuhumiwa hapa ni ofisi ya mashtaka ya taifa (NPS)na Jeshi la polisi(task force)
[emoji642]Mateso katika vituo vya polisi
[emoji818]Hapa watu hulazimishwa kukiri makosa kwa mateso kama kuingiziwa spoku kwenye uume nk
[emoji643] Makubaliano ya kukiri kosa( Plea bargain)
[emoji818]Hii imegeuka mbadala wa upelelezi katika makosa ya uhujumu uchumi.Ili umalize kesi lipa uendelee na shughuli zako.(hapa hakuna majadiliano).Zoezi hili lifanyike kwa uwazi.
[emoji644]Mahakam kutoa huduma kwa mfumo wa TEHAMA
[emoji818]Hapa shabaha ilikuwa kurahisisha ila kutojiandaa vema kumesababisha uahirishaji wa kesi kwa sababu ndogondogo kama mtandao kufeli,umeme nk.
[emoji645]Watoto,wenye ulemavu na wageni
Pamoja na kuwepo mahabusu na mahakama za Watoto bado unakuta Watoto katika magereza ya watu wazima(hatari ya kuathirika na ulawiti)
[emoji818]Mahabusu wenye matatizo ya akili kuendelea kushikiliwa gerezani badala ya kupatiwa matibabu hospitalini.
[emoji818]Wakimbizi na wageni wasio na hatia kuendelea kushikiliwa magerezani
[emoji647]Marufuku ya Taulo za kike Magerezani
[emoji818]Huu ni ukatili dhidi ya utu wa mwanamke
[emoji818]Wenye ulemavu,wajawazito wapo hatarini kupata magonjwa kutokana na mazingira.
[emoji637][emoji637]Kutofuatwa kwa sheria magerezani
[emoji818]Ukaguzi magerezani ni zoezi linalodhalilisha utu(kuvuliwa nguo) bila kuzingatia rika,kupigwa,matusi,kulazimishwa kujisaida na kuleta kinyesi nk
[emoji637][emoji638]Huduma duni za afya na msongamano
[emoji818]Gereza la kuhifadhi wafungwa 800 kuhifadhi zaidi ya 2000
[emoji818]Malazi yasiyoridhisha(godoro la futi 3 kwa sita kulaliwa na mahabusu zaidi ya wawili nk.