Barua ya wazi kwa Tundu Lissu kumuonya dhidi ya kutetea masikini na wapumbavu

Aisee nakwenda kuihibiri hii madhabuhi kanisaniii ila sitaiweka ktk mlengo wa Ki Lisu bali kwa wapumbavu na wajinga. Najua watakuwepo watapasuka mbavu tu kwa vicheko.
 
Fikira Fikirini
Wazo Wazeni
Ubongo umesizi
Akili imedoda
Nimechoka

Bazazi
 
bora kufa kwa kutetea unacho kiamini mkuu kuliko kufa kwa malaria by the way kila mtu alipozaliwa tiyari kifo chake kilisha pangwa ni mazingira gani utapia kufa so lazima alima utetee kile unachokiamin never give up mkuu , ila nikili kwenye hayo magroup yako mi simo mkuu
 
Mleta mada umeandika ukweli mtupu kwani tunaona hata kwenye mtandao huu wale wanaotetewa ndio hao hao wanaokula buku saba na kuendelea kumtukana humu.Hawathamini kabisa alichowafanyia kuwasaidia wao na kwamba ndicho hicho kilichomletea adha yote anayopata. Ni kumwombea tu Mungu amsaidie !!!
 
Hii ni mojawapo ya hekima kubwa iliyowahi kuwakilishwa vyema hapa jukwaani kuhusiana na wale wenye kutambulika kama wanyonge ndani ya taifa letu. Hii ni sura halisi ya watu hao, na hata kuweza kuthibitika wazi ktk maisha yetu ya kila siku.

Umaskini ni kama laana tu, mtu maskini ni vigumu sana kuaminika, tunaona hata viongozi wetu wote waliowahi kuliongoza Taifa, wenye kuhusudu sera za kijamaa zenye kukumbatia sera za umaskini wa pamoja na kuchukia mafanikio ya mtu mmoja mmoja jinsi ambavyo wamefeli.
 
Sasa nimekuekewe wewe kweli n taikon wa Fasihi few will catch you
 
Huu ni mtazamo kwa wanyama porini ambapo mwenye nguvu ndio anaishi (survival for the fittest). Ukitaka wanadamu waishi hivyo ni kuwataka waishi kama wanyama pori. Sina uhakika kama unafurahia kuona mtu akiibiwa au kudhulumiwa na mwenye nguvu zaidi. Siku za kuishi mawazo yako ni zama za kale kabla hata watu hawajavumbua moto. Mwanadamu amebadilika sana na anaendelea kupata hekima ya juu zaidi. Mambo mengi sana yamebadilika kuhusu haki na ustaarabu, hata mimi kijana nimeshuhudia mengi mno yakibadilika kijijini kwangu ukilinganisha na miaka ya tisini. Tundu Lissu anafanya kazi adhimu kabisa ya kuwatetea wanyonge ili wasidhulumiwe na wadhalimu. Hili ni jambo la juu sana na linawahusu wenye fikra na upeo mkubwa na ndio maana wengi hawawezi. Ni rahisi kutetea matumbo na hisia binafsi. Tundu Lissu anayafanya ya akina Yesu, Nyerere, Mandela, n.k na hata akifa, angali bado anaishi. Akina Idd Amin, Mobutu, Bokassa na wengine wamekufa na wamekufa kweli.
 
Narudia kusoma Tena na Tena nimegundua kitu kimoja kwako. Wewe Ni mwandishi wa fasihi. Tundu Lissu wewe endelea na harakati ndio maana Mungu alikuponya ukanusurika kifo. Kufa utakufa tu hata wewe mwandishi siku ikifika hakuna namna. Sote tutakabiliana na kifo kwahiyo tusihofu kutenda mazuri.
Talanta ziko nyingi, Kuna wengine wamepewa ya uongo, ukarimu, upole, ukatili, huruma nk. Hatuwezi kulingana wote Ni lazima kila mmoja wetu aitendee talanta yake haki inayostahili.
 
Kwani mkuu, hujawahi kusoma "aliyenacho ataongezewa na asiyenacho atanyang' anywa" jamaa kaongea ukweli unaochomachoma!
Ni kweli Mkuu ila hii issue iko subjective maana humohumo wameandika katka 3Yohana 1:2
"Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote............."
 
Huyu ndugu Heriel yuko sahihi sana. In a philosophical point of view, hamaanishi moja kwa moja binadamu tusisaidiane. Kusaidiana viumbe hai ni natural. We are living symbiotically. Kila kiumbe kinamtegemea kiumbe mwingine ili uhai/uzima na maisha yaendelee. Kusaidiana ili maisha yaendelee kuna sura na ni kwa aina nyingi.
SASA unatakiwa umakini mkubwa linapofika suala la kusaidiana.
Kwa ujumla, kumsaidia maskini kuliko kuzuri ni kule kwa aina inayochukuliwa na kuonekana kama kumnyonya, kumdhurumu, kumdhalilisha, na kadhalika.
Kwa kweli ni hatari sana kwa mtu mwenye maono ya maendeleo kuwa karibu na mtu maskini. Uhusiano wenu uwe ktk kumtumikisha huku ukihakikisha 99% ya faida inabaki kwako ili aendelee kukutumikia.
Kwa kweli, umaskini ni kitu kibaya. Ni mojawapo ya laana Bwana Yesu Kristo alikuja kutuponya wanadamu (2Wakorintho 8:9).
Ila tusiache kusaidiana kwa kadiri na kwa mujibu wa imani zetu (Mambo ya Walawi 25:35; Ayubu 29: 12; Wagalatia 6:10, n.k.).
Umaskini unaandamana na taabu, mateso, adha, msongo wa mawazo, sonona; mara nyingi hutawaliwa na moyo wa kulipa kisasi hususani kwa watu wenye ukwasi, hivyo, huwa mwepesi kufanya Uovu. "Wajumbe" wengi ni maskini, si mmeshuhudia ktk maeneo mengi walilolifanya lililo kinyume na Wananchi wengi? Wamewapigia kura nyingi wale waliowapatia pesa.
Umaskini ni kitu kibaya hakika. Na maskini ni mtu wa hatari all together.
 
Umeandika kwa kutumia fasihi maridadi sana....

Kwa ubunifu wa lugha uliyoitumia kuandika, wengi wanaisoma bila kutafakari, wameshindwa kukuelewa...

Binafsi nimekuelewa vizuri. Ujumbe unaokusudia kumpa Tundu Lissu, actually siyo kwamba aache harakati zake za kutetea hawa masikini, wajinga na wapumbavu...

Maudhui ya andiko hili yamejikita kwenye taahadhari zaidi kwa Tundu Lissu kwamba, lipo tatizo ktk uelewa wa wengi wa watu anaowatetea ambao kiuhalisia hawajui hata kama huyu mtu anawatetea wao, anaumia kwa ajili yao, amemwaga damu kwa ajili yao, amevuliwa ubunge wake kwa ajili yao, amepigwa risasi kiasi cha kutwaa uhai wake kwa ajili yao....

Haya mambo ndivyo yalivyo. Siku zote hakuna watetezi wa haki na uhuru wa watu malofa, masikini na wapumbavu (kama ulivyowaita) wamewahi kuungwa mkono na malofa wote. Na sababu ni moja tu, UFAHAMU na UELEWA duni....

Lakini jambo moja ni hakika. Wengi wa wapumbavu, malofa na masikini hawa wasioelewa, hufa ama hufyekelewa nbali lakini MBEBA MAONO HUWA HAFI mpaka maono yake ama kusudi alilopewa na Mungu Yehova limetimia....

Umewatolea mfano MUSA MLAWI na YESU KRISTO, MNAZARETHI...

Hawa walikuwa wajumbe maalumu waliobeba VISION na MISSION ya Mungu juu ya watu wa dunia hii ambao wengi ni malofa na masikini na wajinga na wapumbavu....

Hawa walilindwa na Mungu mwenyewe kwa nguvu zote. Hakuna aliyekufa japo walipitia kwenye dhahama kubwa ya mateso ya kufa na kupona...

Pamoja na hayo, mpango wa Mungu siku zote na milele huwa hakuna binadamu awaye yeyote anaweza kuuzuia usifanikiwe japo watajitajidi kutaka kuukwamisha...

Ndivyo ilivyokuwa kwa Musa dhidi ya kuwakomboa wana wa Israel toka Misri kwenda Kanaani nchi ya maziwa na asali. Musa hakufa. Musa alitwaliwa hai na Mungu mwenyewe....

Ndivyo ilivyokuwa kwa Yesu Kristo. Alitumwa na Mungu mwenyewe kuukomboa ulimwengu. Kumkomboa mwanadamu toka ktk utumwa wa dhambi na mauti kwa njia ya KIFO CHA MSALABA...

YESU KRISTO hakuuwawa kifo cha kawaida ili watesi wake wajitangazie ushindi. Kifo cha Yesu Kristo kiliruhusiwa na Mungu mwenyewe kama njia ya kuishinda nguvu ya mauti...

Hii haikujalisha hawa malofa na masikini na wajinga na wapumbavu wanamfikiriaje huyu mpigania haki na uhuru wao yaani YESU KRISTO...

Wakati mwingine, siyo lazima lofa, masikini na mjinga huyu aone na kutambua kuwa anakombolewa yeye. Atatambua baadaye na wakati mwingine hatatambua kabisa mpaka anakufa. Thamani ya ukombozi utafurahiwa na kizazi chao kinachofuata....

Tundu Lissu ni mbeba maono ya nchi hii. Ni mkombozi wa malofa na masikini na wapumbavu na wajinga wa nchi hii. Hajuti sasa. Hatajuta baadaye. Hahitaji kutambuliwa sasa. Atatambuliwa baadaye. Hahitaji uungwaji mkono wa hili Kundi ingalau kwa sasa...

Kumbuka, MBEBA MAONO ama KUSUDI FULANI la MUNGI diku zote huwa HAFI na wala kamwe HAJUTI hadi kusudi limetimizwa....!!
 
Umeongea ukweli unaochoma
Ndio maana Mkapa aliwaita wapinzani marofa na wapumbavu, Lisu huyu alikuwa anawatetea mabwenyenye akina accacia Kwa vitisho vikali, mala tutanyorewa kipara bila maji, ho, madini yote sio yetu, mala tutaperekwa miga mchi ifirisiwe,. Hiyo tuwaache mabwenyenye waendelee kutuibia, harafu huyu ndiye anataka nchi hawatetee masikini. Kawadanganye marofa wenzio huko
 
Kitambo tulishaandika humu... ngumu sana "malofa na wapumbavu" wenzetu kuelewa PUNDA YAKE FIMBO NA MZIGO!!

Nilipoandika hayo nilitarajia tungeshinikiza KATIBA MPYA KUPITIA VYAMA VYETU AU MAHAKAMA... TUNACHOWAZA SISI SIO WAWAZACHO WAO...
 
Hiki ni kiswahili au kikabila?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…