Barua ya wazi kwa Tundu Lissu kumuonya dhidi ya kutetea masikini na wapumbavu

Very well
 
Huwa naheshimu sana makala zako, lakini leo umeandika vumbi. Huna budi kuiomba wana JF msamaha kwa andiko hili ovu
Acha roho mbaya. Nyie miafrika kumsifia mtu sifa njema akiwa hai hamwezi.

Tundu Lissu anastahili sifa njema. Anaziishi
 
Aliyeumba hii dunia ndiye anataka dunia iwe hivi ilivyo, wapumbavu wahenyeke, wenye hekima wale bata. Masikini wachapike, matajiri wale upepo mwanana.
🤣🤣🤣we jamma.

Nyuzi za Lissu naona zinafufuliwa. Kwani kuna nini kimetokea?
 
Happy, kafufua uzi ambao hatukusoma tumesoma tumeelewa
 
Ukiweka bandiko hapa,kila mtu anasoma aliyemo humu na atatoa maoni kadri ajuavyo.

Kama ungetaka watu tusichangie ungemtafuta lissu inbox au ungeomba mawasiliano yake humu,wengine wanayo.

Maandiko ya biblia hujaelewa kabisa mleta Uzi wala Mungu humjui kiroho bali wamuelewa kiakili na ndiyo maana tafsiri yako unatumia akili.

Huyo Musa alikulia nyumba mfalme lakini alitorokea nchi ya Midian ili apate nafasi ya kutetea na kuwakomboa wanyonge ndugu zake.
Hakujali kitachompata.

Hakuna vema kuambatana na utajiri huku nduguze wakiteseka.
Kijana mleta Uzi nakuhurumia sana kwani huyaju matakwa ya Mungu kwako.
HEBU RUDI KWA MUNGU AKUFUNDISHE.

Nakufahamu kwa sehemu kupitia mabandiko yako mengi,huwa hupendi kukosolewa.
 
Nimewahi ona MATAJIRI wengi chini ya jua ambao ni WAPUMBAVU😀😀😀 Hasa ktk Nchi yangu.

Nimewahi pia kuona MATAJIRI wachache wenye AKILI.

UMASKINI ni ROHO na ni LAANA.

MASKINI ni MBONI ya JICHO la Mungu, ukiacha kutetea watu MASKINI, Mungu mwenyewe atawatetea.

Maskini ni MFUNGWA aliefungwa ktk Roho ya UMASKINI hivyo Si HAKI kuacha kumtetea.

Swali linabaki; Je nani wa kuwanyan'ganya Roho ya UMASKINI ulio ndani ya WATU maskini na kuwatilia UTAJIRI wa Ki Mungu?

Nadhani hoja Yako inahitaji NYAMA zaidi.
 

Unaelezea mchakato aliopitia na kuufanya Musa lakini hutaki kuelezea Matokeo ya kile alichokifanya.

Kuhusu kukosolewa hakuna sehemu nimekataa kukosolewa,

Pia hakuna sehemu nimesema Watu wasisaidiwe au wasitetewe isipokuwa Nimesema Watu Masikini na Wapumbavu ndio wasisaidiwe na kutetewa.

Mungu ninayemjua ni Yule aliyeumba Simba amle Swala,
Mkubwa amtawale mdogo,
Nuru ifukuze Giza,
Mwanaume amtawale mwanamke.

Huyo ndiye Mungu ninayemjua,

Mungu ninayemjua ni Yule anayeniambia hivi;
Mathayo 7:6
Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua.

Lisu alitupa Lulu mbele za Nguruwe akaishia kufanywa Kilema, na aliokuwa anawatetea wakamuita kiherehere, mropokaji n.k.

Yesu alikuja kukombia wanadamu kipi alichopata zaidi ya kuuawa,
Vipi kuhusu Musa, na vipi kuhusu mitume wengi wao matokeo yalikuwa mabaya zaidi.

Huenda Mungu ninayemjua Mimi na wako ni tofauti.
 

Mungu hatetei Masikini wapumbavu.
Hiyo haijawahi kutokea na haitakuja kutokea,

Yaani Masikini wasiotaka ukombozi, wasiotaka kutetewa Mungu ndio awatetee😀😀 hiyo haipo.

Kama Masikini wangesaidiwa na Mungu leo hii wasingekuwepo, Ila upumbavu na Kupenda uvivu, ubwanyenye, kutotaka kupigania Haki zao ndio kinawafanya waendelee kuumizwa.

Hata Mungu hapendi Masikini
 
Umeongea fact mkuu!

Mi mwenyewe Kuna mazezeta fulani nataka kuwadhulumu ardhi,maana hawajitambui
 
Umeongea fact mkuu!

Mi mwenyewe Kuna mazezeta fulani nataka kuwadhulumu ardhi,maana hawajitambui


😀😀😀
Usidhulumu Yatima na Wajane🏃🏃
Ila wapumbavu na malofa dhulumu tuu. Ila adhabu ipo.

Yakobo alimdhulumu Kaka yake Esau Kwa makubaliano.
Unampa mtu Debe la mahindi yeye anakupa Kipande cha dhahabu. Hiyo ni dhulma ya akili
 
Ahahaha, nimekusoma between the line na hii philosophical article yako ni nomaa, wasiokuelewa utaokota wengi tu hapa lakini kumbe unafikisha ujumbe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…