EMANUEL JOHN JOHN
JF-Expert Member
- Jul 31, 2018
- 502
- 461
Taikon wa fasihi,wewe unasoma vitabu au ni by nature# BIG UP sana.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nakuelewa btn the lines.Mungu hatetei Masikini wapumbavu.
Hiyo haijawahi kutokea na haitakuja kutokea,
Yaani Masikini wasiotaka ukombozi, wasiotaka kutetewa Mungu ndio awatetee😀😀 hiyo haipo.
Kama Masikini wangesaidiwa na Mungu leo hii wasingekuwepo, Ila upumbavu na Kupenda uvivu, ubwanyenye, kutotaka kupigania Haki zao ndio kinawafanya waendelee kuumizwa.
Hata Mungu hapendi Masikini
Mi maskini unatakiwa uifanyie Kama Magufuli alivyo ifanyia. Unaiibia kwa kuwapa vitambulisho feki vya machinga unaiambia mtafanya biashara popote yenyewe inalipa hela huku ilikenua meno Kama mazuzu halafu wew unachukua pesa zile unakula bata na kujijengea uwanja wa ndege nyumbani kwako. Halafu ukifa Ile Ile mimaskini uliyo idhulumu itakusifu sana na kukuita wew ulikuwa shujaa wao.BARUA YA WAZI KWA TUNDU LISU
Na, Robert Heriel
Taikon wa Fasihi,
S.L.P 9977, JIBI,
Kutoka Nyota ya Tibeli.
30, 07. 2020.
YAH: KUKUONYA DHIDI YA KUTETEA MASIKINI NA WAPUMBAVU.
Ndugu Mhe Lisu, Kichwa cha habari hapo juu cha husika.
Ninafuraha kubwa kukuandikia barua hii ya wazi ambapo najua watu wengi wataisoma nawe itakufikia. Utanisamehe ikiwa njia hii niliyoitumia pengine isikufurahishe lakini ni katika hali ya kukupa ujumbe wenye manufaa wewe na wale wote wenye tabia kama zako, mimi nikiwa mmoja wao.
Mhe. Lisu, nimekufuatilia kwa miaka saba sasa, sisemi nakufahamu lakini angalau ninachakusema kidogo kukuhusu. Umejipambanua kama mtu apendaye haki, mtu apendaye utawala wa sheria, mtu apendaye demokrasia. Lisu umekuwa mstari wa mbele kukemea maonevu uyaonayo ndani ya nchi yako, umejigeuza kama msemaji wa wanaoonewa, kutetea wanyonge wanaonyimwa haki zao. Upo sawa, lakini umekosea jambo moja; nalo ni kushindwa kujua unatetea watu wa aina gani. Hilo ndilo kosa lako kuu.
Huwezi tetea haki za masikini ukabaki salama, huwezi tetea haki za wapumbavu ukabaki salama. Huwezi tetea watu wasiojielewa, huwezi tetea watu wasiojua unapigania nini kwao, huko ni kujitafutia matatizo makubwa ambayo hao unaowatetea hawatakusaidia kitu kwa sababu wao ni wapumbavu na masikini.
Kikawaida masikini ni watu wasiojithamini, watu wasio na shukrani, watu wasiojitambua, wengi wao ni wachawi, wanga, watu wasio na fadhila, masikini ukimsaidia huyo huyo ndio atakuja kukusema unajidai, ukimtetea masikini au mpumbavu huyo huyo ndio atakuambia unakihere here. Kamwe nakusihi acha mara moja kuhangaika na masikini.
Masikini unachoweza kuwasaidia ni kuwadhulumu hata kile kidogo walichonacho, kuwabagua, kuwatenga, kuwadharau, hicho ndicho wakipendacho masikini. Lakini ukijifanya unawapenda, unawajali nakuhakikishia unajiingiza mkenge, utaumia, utasagika na hakika utamalizika.
Nikukumbushe Ndugu Mhe. Lisu, hakuna aliyewahi kuwatetea masikini, na kuwapigania masikini akabaki salama. Wote waliojiingiza katika harakati hizo walikufa vifo vibaya, wengine walipewa adhabu kali za kuliwa na mamba, kuliwa na simba, kuchomwa moto, wakapotea na kuangamia.
Katika Dini, wapo Manabii walikuja kutetea haki za wanyonge, haki za masikini lakini wote waliuawa, tena wakazomewa na hao hao masikini. Nakupa mifano ya watu katika dini waliokuwa wanaharakati kama wewe, Musa, ndiye yule Mlawi aliyewatoa waisrael Misri, naye aliwapigania watumwa wale na kutaka kuwa uhuru wao. walichomlipa wote tunajua, walianza kulalamika kuwa bora warudishwe utumwani Misri kuliko kuwa huru Kanaani katika nchi yao. Mungu alitaka kuwaua lakini Kihere here cha Musa akawatetea, siku zilizofuata wakataka kumuua Musa wasijue huyo ndiye aliwatetea wasiuawe na Mungu. Musa alipowashtaki kwa Mungu, Mungu akamuambia, wewe si uliwatetea hao masikini, watumwa, wapumbavu wasiojielewa. Acha wakuue ili uwe na akili. Musa akabaki katumbua macho. Biblia inasema, Mungu aliwafyeka wote njiani, akambakiza Joshua na Kalebu. Huwezi kukomboa masikini, huwezi komboa watumwa, huwezi komboa wapumbavu ukabaki salama. Kuwatetea wapumbavu ni kutaka kutofika kanaani, usishangae kwa nini Musa hakufika Kanaani, aliwaendekeza wapumbavu wale.
Yesu naye walimuua, wakamsulubisha, na kumtemea mate. Na wale aliokuwa anawatetea ndio hao hao waliomtukana, walioimba asulubiwe. Huwezi Mkomboa masikini hata siku moja. Huwezi komboa mtu mpumbavu ukasalimika.
Hata kwenye maisha ya kawaida, wale unaowasaidia ndio hao hao watakaogeuka maadui zako. Hao hao ndio watakao kuteta.
Mhe Lisu, naomba nikuonye, na ikikupendeza fuata ushauri wangu. Acha kutetea haki za wapumbavu, haki za masikini, haki za wanyonge sijui upuuzi gani. Mungu mwenyewe atahangaika na watu wake. Ikiwa yeye kaacha watu waonewe wewe unakuja kuwatetea huoni unatafuta maneno.
Masikini ni kama swala au digidigi mbugani, huwezi mgeuza digidigi akawa simba alafu ukabaki salama. Ili mbuga iwe na amani ni lazima swala aliwe, kumtetea swala ni kuchafua amani ya mbugani.
Nature inataka dunia iende hivyo, wote waliojifanya kutetea tabaka la chini walipotezwa, na uhakika ni kuwa watazidi kupotezwa.
Nakushauri; tetea watu wenye akili, watu matajiri, watu wenye nguvu, hao utapata ulinzi, hao hawana unafiki, hao utapata cheo, na utaishi kwa amani.
Matajiri ukiwatetea wanajua thamani ya kile unachokifanya, hivyo nawe watakutetea siku yakikukuta yako. Lakini masikini ukiwatetea kwanza wao wenyewe hawajui thamani yao iweje wajue thamani ya kile ukifanyacho, zaidi sana watakutelekeza siku yakikupata kisha watakuambia ulikuwa unakihere here.
Watu wenye akili ukiwatetea watakulinda, kwa maana wanajali kile ukifanyacho, watakulipa hisani na fadhila. Lakini wapumbavu ukiwatetea hao hao watakuwa wakwanza kukusnitch na kukuuza kwa bei ya kutupwa, mwisho utauawa na kuangamizwa.
Wenye nguvu ukipendekeza kwao, watakulinda. Wao wanajua na kuthamini mchango wako kwao. Lakini sio kwa watu wanyonge na fukara. Wanyonge wataishia kukusengenya na kukuloga, ukiwa mbele yao wanakushangilia ukitoka wanakusema. Wataachaje kukusema ikiwa hawana kazi, kazi yao ni kusengenya watu vijiweni.
Mhe. Lisu, acha kupoteza muda wako. Hutapata zawadi popote pale iwe huku duniani au kwa yule aliyeiumba hii dunia.
Aliyeumba hii dunia ndiye anataka dunia iwe hivi ilivyo, wapumbavu wahenyeke, wenye hekima wale bata. Masikini wachapike, matajiri wale upepo mwanana.
Namna bora ya kumsaidia masikini ni kumdhulumu na kumuonea. Namna bora ya kumsaidia mpumbavu ni kumfundisha upumbavu,.
Kufikia hapa Mhe, Lisu niseme ni matumaini yangu barua hii utakuwa umeielewa. Na utaifanyia kazi.
Wako katika majukumu
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
robertheriel99@gmail.com
Nakala moja kwa
1. Tundu Anthipas Lisu
2. Wanaharakati wote
3. Wanamageuzi
Nakala nyingine nitabaki nayo.
Nakuelewa btn the lines.
Bt nasikitika kusema, Ikitokea Lissu akaacha utume wake,
Mungu atawaleta akina Lisu zaidi ya 100 kuendelea na utume huo.
Mungu aliwaumba wote, maskini na matajiri Ili wasaidiane Si wahujumiane.
Na Hali ya kutojitambua ikiendelea na MATAJIRI WAPUMBAVU wakibweteka, itatokea Ugomvi kati ya matajiri, Bado hapatatulia.
Tuandike maoni yetu, bt tusivuke mpaka na kujiona tuna uelewa kuliko MUUMBA na kupitiliza kuwa WAPUMBAVU.
Ameeen.
Mungu anaetetea maskini, anawapenda maskini ila ANACHUKIA UMASKINI na Upumbavu ulio ndani ya MASKINI.Mungu hatetei Masikini wapumbavu.
Hiyo haijawahi kutokea na haitakuja kutokea,
Yaani Masikini wasiotaka ukombozi, wasiotaka kutetewa Mungu ndio awatetee😀😀 hiyo haipo.
Kama Masikini wangesaidiwa na Mungu leo hii wasingekuwepo, Ila upumbavu na Kupenda uvivu, ubwanyenye, kutotaka kupigania Haki zao ndio kinawafanya waendelee kuumizwa.
Hata Mungu hapendi Masikini
Mungu anaetetea maskini, anawapenda maskini ila ANACHUKIA UMASKINI na Upumbavu ulio ndani ya MASKINI.
Ndomana nakushauri usijitutumue sana ukaelekea Kuwa MPUMBAVU sababu ya SHIBE, maana nimesema wapo MATAJIRI WAPUMBAVU wengi mno ktk Nchi yangu.
Mungu ndo huweka roho ya utume juu ya mission Fulani ndani ya mtu, LISSU Kuna wakati pia hujishangaa imekuwaje anafanya ayafanyayo.Amina!
Tatizo ni Ile Hali ya kumtetea mtu asiyetaka kutetewa, unaweza kimpeleka punda mtoni kunywa Maji lakini huwezi mlazimisha Anywe maji.
Lisu na wengine Kama yeye, wanapaswa wasubiri uhitaji wa Watu kutaka kusaidiwa.
Mimi naamini kuwa Leo hii Lisu akiulizwa kuhusu Yale aliyoyafanya atafurahi na kujivunia lakini atasikitishwa na matokeo ya aliowapigania.
Inauma Sana umtetee mtu alafu akuambie hakukutuma kumtetea, kumsaidia au kumkomboa,
Musa aliagizwa na Mungu kuwakomboa Waisrael baada ya Kilio Chao kufika mbinguni,
Inamaana Bila ya kilio kufika mbinguni Mungu wala asingemtuma huyo Musa.
Msaidie mtu anayehitaji msaada lakini kamwe usimsaidie mtu ambaye hajakuomba msaada hata kama unamuona anahitaji kusaidiwa.
Ninaweza nisieleweke, wengine wakaniona nina roho mbaya, lakini nikisemacho ndio nature inavyotaka
Mungu ndo huweka roho ya utume juu ya mission Fulani ndani ya mtu, LISSU Kuna wakati pia hujishangaa imekuwaje anafanya ayafanyayo.
Yote Yana faida na hasara zake Ili Mapenzi ya Mungu yatimie.
Nimesema UPUMBAVU na UMASKINI ulio ndani ya MASKINI Hauna tofauti na MFUNGWA aliyepigwa pingu za minyororo mikononi na miguuni.Ni kweli Kabisa.
Kupitia tukio la Lisu watu wengi wamejifunza ukuu wa Mungu lakini pia wamejifunza kuwa Unaweza kutaka kumkomboa mtu lakini mkombolewa akakataa.
Hata sasa maandiko yanadai kuwa Yesu alikuja kuukomboa ulimwengu lakini walimwengu tumemkataa. Ndivyo ilivyo
Na kweli. Watanzania wa hovyo sanaHuwezi tetea haki za masikini ukabaki salama, huwezi tetea haki za wapumbavu ukabaki salama. Huwezi tetea watu wasiojielewa, huwezi tetea watu wasiojua unapigania nini kwao, huko ni kujitafutia matatizo makubwa ambayo hao unaowatetea hawatakusaidia kitu kwa sababu wao ni wapumbavu na masikini.
Na kweli. Watanzania wa hovyo sana
Yupo sahihi sanaHongera kwa makala ya kimasikini na kipumbavu ..duuh kweli duniani Kuna mambo
Ook ndiyo maana mweusi akiitwa mweusi huko ulaya anachukia sana(kumbe ni kweli ni mweusi).Lakini mweupe akiitwa mweupe wala hakina NGO inayojitokeza kupigiza kelele."Mlete mdhunguu" wala siyo shida ila "mlete mweusii".... noma!Wapo matajiri wapumbavu ndio Ila mada inawahusu Masikini Mkuu.
Tatizo la dunia haipendi ukweli hasa likiguswa kundi au tabaka la chini.
Ni Kama vile uwaseme wanawake utaambiwa unawadhalilisha au kuwanyanyasa kisa kuwaambia ukweli
Ook ndiyo maana mweusi akiitwa mweusi huko ulaya anachukia sana(kumbe ni kweli ni mweusi).Lakini mweupe akiitwa mweupe wala hakina NGO inayojitokeza kupigiza kelele."Mlete mdhunguu" wala siyo shida ila "mlete mweusii".... noma!
Nafurahi kwa maandiko yako hapa Jamvini, hakika unatutendea haki.
Lakini ni haki kuwaacha tu haya makundi? Ama tuendelee tu kutoa elimu.
Maana iliandikwa watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.
Sasa, watu hawa nani anapaswa kuwapa maarifa hata kama wao hawaoni haja ya kutafuta.
Lissu hawezi elewa hii, mpk siku atakapozikwa pale Ikungi na masikini wake
Taikon wa fasihi,wewe unasoma vitabu au ni by nature# BIG UP sana.
By nature + vitabu.By nature