Barua ya wazi Kwa wanawake: Usiolewe na mwanaume mpumbavu na mwoga!

Barua ya wazi Kwa wanawake: Usiolewe na mwanaume mpumbavu na mwoga!

Ikitokea Kwa mfano ndugu zako wanne wanasafili bahati mbaya wakapata ajali mmoja akafariki watatu ni walemavu na wanapata matibabu na kipato chako Kwa siku ni TSH 10,000 .ikatokea ukawauguza miaka Kumi .je kama haujajenga na hauna kitu bado utakuwa mpumbavu .?
Chizi huyo.
 
USIOLEWE NA MWANAUME MPUMBAVU NA MWOGA!

Kwa Mkono wa RObert Heriel.

Leo nitakaanga wapumbavu wote na waoga bila kupepesa. Iwe ni Mimi mwenyewe, wewe au Yule. Andiko hili halitamkwepa mwanaume yeyote Mpumbavu na mwoga bila kujali nafasi yake, hadhi yake, na umri wake.

Aidha andiko hili natanguliza tahadhari ikiwa moyo wako ni mwepesi hautavumilia maonyo haya ni Bora uishie kusoma hapahapa. Endapo utakaidi ukaendelea kusoma basi nisihesabike wala nisipewe lawama Kwa madhara yatakayokupata.

Niite Taikon wa Fasihi, mkaangaji.

Mwanaume yeyote asiyemjali mke wake ni Mpumbavu.
Mwanaume yeyote asiyejali familia yake ni Mpumbavu.
Mwanaume yeyote asiyefanya kazi ni Mpumbavu.
Mwanaume yeyote asiyeweza kujitetea jamii yake ni mshenzi na Mpumbavu.
Mwanaume yeyote anayedhalilisha wanawake ni Mpumbavu.
Mwanaume yeyote anayeharibu watoto wa wenzake ni mshenzi na Mpumbavu tuu!

Enyi kina Dada, mabinti na wanawake wote, kamwe usiolewe na Mwanaume Mpumbavu.
Usimuendekeze Mpumbavu.
Usifikiri atabadilika, wapumbavu ni ngumu kubadilika.


Mwanaume yeyote mwenye aibu ya kufanya kazi ni Mpumbavu.
Usikubali hata akuongeleshe, akikufuata mtemee mate, akikuzingua mlete Polisi hapa tutakusaidia kukupa mawakili afikishwe mahakamani afungwe, apeleke upumbavu wake Jela huko.

Uliona wapi mwanaume akasikia aibu kufanya kazi. KAZI ndio inampa hadhi mwanaume yeyote.
Mwanaume habagui kazi ILIMRADI ni halali.
Mwanaume anayechagua kazi asikuoe IPO siku mtalala njaa.

Ogopa mwanaume aliyeiweka akili yake kwenye kazi moja. Mkimbie Kama ukoma. Huyo lazima akufanye uwe masikini dunia ingalipo.

Mwanaume mwoga usikubali akuoe.
Mwanaume mwoga hataweza kukulinda.
Kumbuka kuna woga na Heshima.
Kama Mwanaume woga anauita heshima mtemee mate kisha ukimbie, akikukimbiza akupige mlete kwetu tumfundishe adabu ili siku nyingine zimkae sawia.

Mwanaume anayedhulumiwa huyo usikubali akuoe. Huo ni mkosi katika familia yenu.
Usikubali kuolewa na Mwanaume anaemuchia Mungu. Mtakuwa Masikini, mtaonewa, watoto wako watateseka.

Usiolewe na Mwanaume asiyeweza kuwa hata na nyumba au Shamba, huyo atakuachia Mateso Duniani, atatesa watoto wako. Atawaacha watoto wako pasipo Urithi. Likikutongoza limwanaume la namna hiyo liliulize swali linashamba au kiwanja, Kama halina liulize utaishije na Mimi kama huna Shamba au kiwanja. Likikujibu bado linahangaika au mjini viwanja bei ghali liambie likuonyeshe Shamba au kiwanja huko kijijini. Halina litemee mate kisha toka nduki.
Usicheke na limwanaume lipumbavu litakutia mikosi na kukuzalisha Matoto ya hovyo hovyo.

Olewa na Mwanaume sio uolewe na mtu mwenye Cover/motherboard ya kiume alafu ndani ni jike jenzako.

Hakuna cha huruma hapa!
Usiolewe na Mwanaume anayependa kuhurumiwa hurumiwa, huyo ni mpuuzi.
Wanaohurumiwa ni watoto, wanawake na Wazee.
Ukiolewa na Mwanaume apendaye kuhurumiwa utaishi maisha ya kutia huruma mpaka unye mavi Kwa upuuzi wako.

Olewa na Mwanaume ambaye anapambana Kama Mwanaume. Akikosa mjini basi apate shambani. Akikosa shambani apate mjini. Sio limwanaume lililokosa bara na Pwani. Hilo usikubali kuolewa nalo. Ni ishara ya mwanaume Mpumbavu asiyeweza tumia akili yake vizuri

Usiolewe na Mwanaume anayekuhonga laki tano alafu halina hata kiwanja, utateseke wewe mpaka ukome. Huyo Hana akili nzuri no mwehu tuu anaweza fanya hivyo.
Labda umtumie kumchuna pesa zake ili lifilisike litie Akili.

Nasisitiza usikubali kuolewa na Mwanaume asiye na uwezo wa kuacha Urithi Kwa watoto atakaokupa. Utazaa mitoto itakayohangaika hapa Duniani mpaka ikome.

Lazima uchague mwanaume anayejua nyakati, na mazingira. Akiona mjini vitu bei ghali basi akanunue nje ya mji huko kijijini vilipo rahisi.
Sio limwanaume linalong'ang'ania kujenga mjini linakusanya pesa zisizojaa, mwisho linakosa bara na Pwani.

Usiolewe na Mwanaume anayejipenda kimwili kukushinda, yaani mtanashati kukushinda wengi uwezo wao wa kufikiri ni mdogo, wengi ni wabinafsi, utashindia kanga moja Kama Sanda ya maiti, vitoto vyako vitavaa marapurapu wala Baba Yao halitajali.
Wanaume watashanashati kupitiliza wanatabia ya aidha ubinafsi au ushoga Kati ya hizo tabia lazima moja umkute nayo.

Hujawahi ona limwanaume limependeza lakini mkewe na Watoto wamevaa hovyo?? Ndio matokeo ya kuolewa na wanaume wapumbavu.

Usiolewe na Mwanaume Mlafi, na mwenye kujipenda mwenyewe. Huyo hawezi kujitoa kafara Kwa ajili ya Familia. Huyu anaweza kuwalisha Dagaa wa chukuchuku wewe na watoto lakini lenyewe linakunywa Bia na supu huko nje. Haya unayakuta yamenenepa na kukuza vitambi alafu wake zao dhoofu ilhali.


Usilivumilie! Likimbie! Hata Kama halijakufukuza ndani ya ndoa liache hapo, usiishi na Mwanaume Mpumbavu ndani ya nyumba.

Mara nyingi nawasema wanawake wapumbavu kuwa tusiwavumilie lakini leo nasi wasituvumilie.

Wewe jitu likulishe Dagaa miezi nenda Rudi aalafu lenyewe linakula nje na kunenepeana bado unalichekea.
Hakuna kulirekebisha, hiyo sio kazi yako, Kama halikurekebishwa na wazazi wake huko basi liende kanisani au msikitini huko ndio wanalipwa zaka na Sadaka Kwa kazi za namna hiyo. Hakuna kuchekeana na wapumbavu.

Mwanaume atakayekupiga bila sababu zile kubwa kubwa Kama kukutwa unataka ku-cheat, au ukiwa una-cheat, au mwanamke mwenyewe kutaka kupigwa maana wapo wanawake wanakuwaga wanawashwa washwa.

Lakini jitu limekukosea unaliambia Kwa adabu alafu linakupandia na kukupiga. Usilichekee. Piga chini. Usicheke na Mwanaume Mpumbavu.
Yaani lije limechelewa nyumbani, linanuka pombe, linatukana hovyo hovyo, ukiliuliza imekuwaje linajibu kipumbavu "hapa ni kwangu" na majibu ya mengine ya hovyo. Kisha likakojoe huko chooni au kutapika hovyo hovyo, bado likupige, loooh! Hakika ukiishi na Mwanaume WA hivyo nawe ni Mpumbavu tuu.

Kupenda upumbavu ni Dalili ya kichaa.

Mimi huwaga nawaambia Dada zangu na pia nitawausia binti zangu hayo wasiyachekee. Wasicheke na Kima, mwanaume Mpumbavu hachekewi muwashie Moto mpaka aone dunia chungu. Usimuhofie, akizingua mlete kwetu tumnyooshe kisheria.

Ewe binti usiyaogope maisha ikiwa unamikono na miguu na akili timamu. Ni Bora uishi mwenyewe kuliko kuishi na Lofa na lipumbavu likakuchosha mwili na Akili.

Mtu Kama hakuheshimu wa nini?
Mtu Kama hajiheshimu Kwa nini umheshimu?
Mwanaume sio Mungu, Ila ni mungu mdogo endapo atafanya wajibu wake Kwa hekima na akili.

Usitishwe na Motherboard yake Kama ndani yake ni Mwanamke.

Binti zangu, msitishwe na wanaume wapumbavu wasiojielewa. Bali Tishweni na wanaume wema, wenye akili na hekima, wanaojiheshimu na kuwaheshimu, wanaomheshimu Mungu. Hao wakiwaoeni hao watiini na kuwasujudia ikibidi Kwa maana HAO ni Kama mungu kwenu.

Lakini hawa Mbuzi wasiojielewe msipoteze muda nao. Msiwakawize, wawashieni moto mpaka waelewe.

Kama nilivyowaandikia na Kuwafunza ndivyo mtakavyofanya.

Mimi Baba Yenu,

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa, MBEZI BEACH, DAR ES SALAAM
Umesahau moja, wasiolewe na wanaume waongeaji sana kama wewe, hawatatoboa.
 
Pale inapotokea kupendwa na mpenzi wako na akakupa mahaba na kusahau yote sasa ole akusaliti na akupe maumivu yale ambayo hata dawa yake haijagunduliwa we eee asikwambie mtu utaimba bia taam na kuja kuedit ulichooandika na kutafuta gunia la mkaa [emoji23][emoji23][emoji23] maisha hayaa

Ila ubarikiwe alie juu tunakungojachiniView attachment 2024325
Kama ana akili timamu na komavu, hata akipatwa na majanga hataweza kuedit chochote hapo kwasababu alichoandika ni ukweli mtupu, kumbuka "uongo unakupa ushindi kwa siku moja, ukweli unaishi milele moja kwa moja" Thanks Nako for this piece of wisdom!
 
Kama ana akili timamu na komavu, hata akipatwa na majanga hataweza kuedit chochote hapo kwasababu alichoandika ni ukweli mtupu, kumbuka "uongo unakupa ushindi kwa siku moja, ukweli unaishi milele moja kwa moja" Thanks Nako for this piece of wisdom!
Haya mkuu hata mimi naona ana ukomavu
 
Ikitokea Kwa mfano ndugu zako wanne wanasafili bahati mbaya wakapata ajali mmoja akafariki watatu ni walemavu na wanapata matibabu na kipato chako Kwa siku ni TSH 10,000 .ikatokea ukawauguza miaka Kumi .je kama haujajenga na hauna kitu bado utakuwa mpumbavu .?


Jenga nyumba kulingana na kipato chako.

Kama huna kipato Jenga pasipo na kipato.

Jenga nyumba ya matope, au piga tofali ezeka nyasi. Usifikiri kuna kuonewa huruma hapa.

Be a Man not like a man.

Akili na Afya ni zaidi ya kipato Mkuu
 
Kuna

Mpumbavu kama wewe zamani alikuwa akiamini kila aliyepo jela ni kibaka au jambazi.

Basi miaka ikaenda ikatokea short ofisini akajikuta Polisi, fasta mahakamani then gerezani keko.

Sina haja ya kuandika mengi nimekuonesha tu upumbavu wako.


Wapi nimesema kila aliyeko jela ni kibaka?
Mbona unanilisha maneno?
 
Mkuuu ,Naomba kwanza nikukosoe .Uzi wako ni nzuri Mno Ila kuna Mambo matatu umeshindwa kuyatambua 1.Binadamu anabadilika kulingana na mazingira ( Human being is dynamic not sysmatic)) 2.mwanaume yeyote ili awe na Maisha yaliyonyooka Kwa asilimia Mia ni lazima awe na mke na watoto ( familia Kwa ujumla ) 3.hakuna binadamu anaependa Kuishi Maisha ya kipumbavu ila hii ni dunia tunaishi katika mazingira yafuatayo a.folish age b.umaskini ndani ya familia c.ukosefu WA elimu ( fikra na maradhi ) na mwisho Ni elimu dunia kututawala....NI mtazamo wangu
We unaongea nini, et hakuna mtu anapenda kuishia maisha ya kipumbavu, hivi kila siku tunavyosema kuna watu ni wavivu husikiagi au unadhani sio kweli, tunavyosema kuna watu ni wazembe unadhani hayo maneno yanatoka hewani, watu wanavyosema kuna watu wanachagua kazi unafikiri hayo maneno wanaropoka kama hayawani? Kuna vitu mtoa post kavisema na mimi nitaongezea kingine, watu wamekuwa na tabia za ubinafsi (narcissism) watu kama hawa wakishinikizwa na kukemewa it is possible kuondokana na hiyo shida, thanks God kuna religious leaders and motivational speakers hii tabia mtu akiondokana nayo familia lastly inaonja equality and equity. Watu tumekuwa na tabia ya kuridhika(satisfaction), mtu akioa akipata watoto akiweza kuleta chochote kinywani anaona it's enough lakini under pressure na kwa kutambua kuwa wakati fulan it's better and possible to fight for more tunaweza kuwa na maisha bora na yanayoweza kutukimu kwa kujitosheleza, remember poverty mostly causes sadness and distress so think of it the opposite way! Actually there is a lot of things humankind needs to change positively but with perseverance and hard endeavor to attain community and individual progress for the perfect world, we are having every resource at hand, time is now to take action. But in all these I strongly believe that knowledge is power!

It's not easy, but it's possible!
Let's take action, let's press on!
 
Huu ni ukweli japo ni mchungu lakin wanaume inatakiwa tupambane hakuna atakae pambana kwaajili ya maisha yako kama mwanaume unachagua kazi na hautaki kupambana tafuta mwanaume mwenzako akuoe ili apambane kwaajili yako ili wewe uendelee na tabia yako ya kuvaa soksi na malapa na earphones zako maskion

Hizi tabia za kujilegeza na kuchagua kazi ndo zinasababisha ushoga uongezeke mitaani, vijana hatutaki kazi za kuchafuka tunataka tule kiulaini, kama unataka kula kiulaini anza kuish kama hamisa mobetto.
 
We unaongea nini, et hakuna mtu anapenda kuishia maisha ya kipumbavu, hivi kila siku tunavyosema kuna watu ni wavivu husikiagi au unadhani sio kweli, tunavyosema kuna watu ni wazembe unadhani hayo maneno yanatoka hewani, watu wanavyosema kuna watu wanachagua kazi unafikiri hayo maneno wanaropoka kama hayawani? Kuna vitu mtoa post kavisema na mimi nitaongezea kingine, watu wamekuwa na tabia za ubinafsi (narcissism) watu kama hawa wakishinikizwa na kukemewa it is possible kuondokana na hiyo shida, thanks God kuna religious leaders and motivational speakers hii tabia mtu akiondokana nayo familia lastly inaonja equality and equity. Watu tumekuwa na tabia ya kuridhika(satisfaction), mtu akioa akipata watoto akiweza kuleta chochote kinywani anaona it's enough lakini under pressure na kwa kutambua kuwa wakati fulan it's better and possible to fight for more tunaweza kuwa na maisha bora na yanayoweza kutukimu kwa kujitosheleza, remember poverty mostly causes sadness and distress so think of it the opposite way! Actually there is a lot of things humankind needs to change positively but with perseverance and hard endeavor to attain community and individual progress for the perfect world, we are having every resource at hand, time is now to take action. But in all these I strongly believe that knowledge is power!

It's not easy, but it's possible!
Let's take action, let's press on!
Mleta Uzi na wewe pastory kimaryo .soon naomba niwaone mkiwa leval za dangote au bilgate
 
Cha msingi mimi naona hakuna sababu ya mwanaume unakuja kuandika hapa kwa kujihurumisha ili ionekane kwamba mambo ni magumu na hayawezekani, waafrika huko Misri miaka mingi B.C walijenga pyramids kubwa na hakukuwa na technology halafu mtu anakuja hapa anaanza kutetea kulalalala. Sikilizeni hakuna kitu ambacho hakiwezekani ila ni ngumu (it's not easy but it's possible), sasa chagueni mlale muishi kama mlivyozoea au tupige kazi afu tuishi kama wafalme, the choice is yours lakin mimi hata nikiwa kiwete nitasimamia ukweli kwa nguvu na akili zangu zote na wala sitaona aibu wala kujihurumia.
Cha msingi elimu ni kila kitu, elimu ni muhimu katika kurahisisha maisha (knowledge is power).
Mungu yupo, let's pray!
 
Kwa hyoo unategemea Mali za Baba yako mkubwa ?
Ngoja nikuwekee logic: baba angu mkubwa ana hela nyingi, no matter how hard I hustle i cannot attain even ⅛ of his wealth but I will have some, why the hustle then?
Remember, knowledge is power!
 
Hakuna mwanaume asiyekuwa na Mali Ila upumbavu ndio unatufanya kukosa Mali.

Hivi Kama Ndege na sisimizi wanapata Mali sembuse binadamu??

Mimi mwenyewe nimepitia hayo yote unayoyasema na niligundua ninayapitia hayo Kwa sababu ya upumbavu wangu au wazazi wangu.

Labda uamue kuutetea upumbavu lakini utakuwa unajisumbua Kwa sababu upumbavu hautetewi na huwezi kuutetea.

Unakosaje nyumba na Dunia bado haijajaa?
Unakosaje Shamba wakati dunia bado ni kubwa?

Kitakachotufanya tukose ni kung'ang'ania kuishi sehemu ambazo hatuwezi kuzimudu.
Nimekuelewa vizuri Mkuu...
Jambo moja ambalo nadhani hukulipa nafasi katika uzi wako ni kwa huyu mwanamke asisamehe mwanaume hata pale ambapo mwanaume ametafakari na kugundua kuwa amefanya makosa, na kuamua kubadili mwenendo wake...
Najaribu kuwaza hapa siku moja ambapo tulitoka na wife halafu baada ya kurudi home nikatapika sana...hivi angeniacha siku ile kwa sababu ya huo upumbavu...leo hii watoto wetu wangeishia wapi????
 
Back
Top Bottom