Barua ya wazi kwa Waziri Mkuu akiwa Kilindi Tanga

Barua ya wazi kwa Waziri Mkuu akiwa Kilindi Tanga

Nguva Jike

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2018
Posts
1,292
Reaction score
1,867
Hongereni kwa majukumu ya kazi za kila siku.
Barua hii kwa jina la Jamhuri ya muungano wa Tanzania imfikie mh Mwigulu Nchemba waziri mkuu wa Tanzania akiwa kilindi Tanga Leo tarehe 13.02.2026.

Kwakuwa kumuona mh.ana kwa ana ni ngumu tunaomba asome barua ya walimu wa kilindi Tanga inayohusu pesa za uhamisho.

Sisi walimu tuliohamishwa tangu 2023 mpaka Leo tunasota bila kulipwa stahiki zetu kwa wakati za uhamisho na Ded anatutishia kutufukuza kazi kwa kuwa tunadai mara kwa mara kwa kufuata ngazi yaani chain of command

Tumefika kwa Ded,DC,das,ras,rc,katibu mkuu tamisemi na waziri wa tamisemi nyaraka tunazo za sehemu hizo tulizopitia bila mafanikio mpaka sasa.Hivyo,tunakuomba Mh.Mwigulu Nchemba ulieapa kusikiliza kila mtanzania ikiwemo sisi watumishi utusaidie tulipwe pesa zetu ambazo zinaletwa lakini Ded anazibadilishia matumizi.

Mungu akubariki.
Kazi na utu.
 
Waziri Mkuu?

Endeleeni kusubiri miujiza kutoka kwa hao viongozi wenu mliowachagua.
 
MUARUBAINI WAKE UNAKUJA NDUGU KAA MKAO WA KULA

PIA KILIMANJARO BAADHI YA KATA KUNA TARIFA ZA KUKUSANYA MAJINA YA VIJANA KAMA NJIA YA KUUADAA UMA JUU YA MIKOPO KWA VIJANA HILO TUMESHALIJUA PIA WASIPOTEZE MUDA KWENYE HILO WATENDAJI WAZEMBE TUTAWAMULIKA
 
Back
Top Bottom