Dan Zwangendaba
JF-Expert Member
- Apr 25, 2014
- 5,814
- 8,118
Hata angetumbua DAWASA yote bado aliyesababisha Dar kuwa na uhaba wa maji hadi sasa ni yeye. Ujenzi wa bwawa la Kidunda ulipaswa uwe umekamilika siku nyingi all plans were already done. Kwa roho mbaya yake mradi ukayeyuka.Naunga mkono hoja ni aibu kwa miaka zaidi ya 60 bado kuwe na uncertain ya maji safi kwa wananchi haswa mji kama dsm.
Waliopo dawasa viatu haviwatoshi wavivue. Angekuwepo JPM ungesikia mtu katumbuliwa ili kutuma meseji kwa mainjinia wa maji wanaosubiri posho na vikao ila hawabuni miradi endelevu ya upatikanaji maji
Ajabu ni kwamba hata Mwanza kuna shida sana ya maji. Dar tunasingizia ukame mwanza je?
Sent from my Infinix X655 using JamiiForums mobile app
Kweli kabisa, ila haya mambo yanafikirisha sana,kwamba rais hajui kabisa kua Dar ni mji unakua kwa kasi na mahitaji ya maji ni Mengi? Dar ina shughuli nyingi sana kuliko mkoa wowote tz,na shughuli hizo zote zinahitaji maji na zinaongezeka kila siku.Tatzo la maji dsm litaendelea kuwa Sugu miaka ming sana, watu na mji unaongezeka kwa kasi sana huku chanzo cha maji kikiwa kile kile Mto Ruvu.. Nashauri Wizara ya Maji itafute chanzo mbadala mfano visima au kuchukua maji mito ya karibu na dsm kama Rufiji ambapo maji yanaingia meng Baharini bure tu
Tatzo la maji dsm litaendelea kuwa Sugu miaka ming sana, watu na mji unaongezeka kwa kasi sana huku chanzo cha maji kikiwa kile kile Mto Ruvu.. Nashauri Wizara ya Maji itafute chanzo mbadala mfano visima au kuchukua maji mito ya karibu na dsm kama Rufiji ambapo maji yanaingia meng Baharini bure tu
Leo nimeulizia lori la.maji lita 3000 inafika shiingi za kitanzania laki moja na hamsini. Wanadaiaji wanachota Mbezimwisho ndio kuna afueni yanatoka.
Wahusika hebu tokeni kwenye viyoyozi mje mseme maji yatapatikana lini
Siku hizi na wnyewe siku hizi,Wana inter breed na weusi,wanajitafutia matatizoš¤£Hivi wazungu nao wamelala? kwani hawawezi kufanya namna yoyote wakatuangamiza majitu meusi yote, naona tunawasumbua tu tunawamalizia hewa ya bure tu.