Duuuuuh mlongo hebu tupe kisa kizima, nasubiri.
Achaa isingekua Kufahamiana na watu wakubwa zaidi yao shemeji yangu angeozea Jela,halafu chain ya askari ni moja huku chini kuanzia wakuu wa vituo vya Polisi,OCD na RPC wa zile wilaya za kipolisi lao moja tuu!ndo maana ameshindwa kusaidiwa!
Huyo mama anaitwa Mwadawa Lugongo alikuaga mtangazaji wa TBC enzi hizooo akatumbuliwaga kisa vyeti feki na magufuli yaani pale mtaani anawapelekesha balaa,anashirikiana sana na maaskari kukomoa watu pale mtaani,Sasa ni jirani na shemeji yangu ,walikuja watu wa viwanja kupima eneo wakamkuta mdogo wangu nje ,wakawa wanauliza mpaka mdogo wangu akaonesha mpk,baasi yule mwadawa kumbe alikua amemega sehemu ya ardhi kidogo ya nyumba ya mdogo wangu na mmewe baada ya kuona dogo ametaja mpk sahihi,akaanza kumsimanga,wale watu walivyoondoka alitukanaa matusi mazito kumtukana mdogo wangu!
Akaona haitoshi kila Siku matusi ,mdogo wangu hamjibu ikabidi amuambie mumewe dogo,baada ya kumuambia mwanaume akatoka uani akaanza kuongea kwa sauti kua hapendi tabia ya mkewe kutukana kila siku!hapendi Shari na anaheshimu kila MTU pale mtaani.Kuona vile bimkubwa yule kumbe alikua anatafuta sababu,akaenda Polisi kusema ametukanwa na ametishiwa kuuwawa,wakaja askari usiku wa manane wakamkamata shemeji,naskia walimpigaaa mpk akawa hawezi kutembea,wakamtia kwenye bajaji wakamkalia "jus imagine'kutoka Kongowe mpk Kizuani wakamfanya kiti,wamefika pale maturubai kipondo kikaendelea mpk asubuhi,shemeji mpk alizima ndo wakamuacha.
Ilikua usiku wa Alhamis kuamkia Ijumaa ,tukapigiwa simu tukaenda ndugu..kumbe tayari,yule mwadawa kashawaset maaskari pale " maturubai"mi mmefika pale Ijumaa mida ya saa nne, nkamuona ananingia akaenda kwa mkuu wa kituo msaidizi anaitwa afande hawa(we mama Mungu akulaani mpk siku unaingia kaburini)OC-CID ,na mi nkaingia nikamuambia afande mshtaki wangu nafikiri ni huyu ,shemeji yangu yuko humu toka Jana ,yule mama akajifanya kunikataa,mi nkatoka nkamuacha mwadawa na afande hawa mule ndani,nkaenda kwa mkuu wa kituo nako hakuna cha maana ,Yule afande hawa anasema live"nakuambia mtuhumiwa Fulani asidhaminiwe ng'oo kamtukana mwandishi wa habari Mwadawa Lugongo"kwa nguvu kituo kizima wanaskia.
In short nlikosa Msaada kwa OCD wa Wilaya ya mbagala maana nae walimset maana Mimi kuna mtu alinisadia namba ya RPC wa Ilala nafikir akaniambia amehamishwa hukoo ningekusaidia so alivyowapigia wakajua kua nna connections mtu wangu atatoka,nilivyompigia OCD wa mbagala akajifanya kumsapoti OCS(mkaka mdogo ila ana roho mbaya Mungu akulaani na washirika wengine. Hyo j1 tayari,ikabidi sasa tutumie mbinu za kivita,hapo mtaani yule mama anatamba kua shemeji hatoki mpk miezi mi3 anamkomesha na anadai amefurahi mnooo anadai kua amehonga kila sehemu kuhakikisha dogo hatoki.
Ikabdi sasa ajitokeze mtu mmoja ambae ana connection na Wakubwa zaidi ya hizo kenge,Kamishna Mussa ambae ni Msaidizi wa Simon Sirro(We baba pekee Mungu akubariki)akatuambia kesho twende kituoni askari yoyote tumpe simu aongee nae[emoji2][emoji2][emoji2]tulivofika simu ikapigwa tukamuambia Dada wa counter Kamishana Mussa anataka kuongea na wewe[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]weeee!aliruka kimanga akasema kata simu,kata simu ,mi naongea nini na Kamishna ,ona hapa (anaonesha beg)sina ht V moja ,mi bado mdogo sana jamani!walitafutana pale maturubai,wote walikataa kuongea nae!tukaambiwa chukueni mtu wenu!na hapo OCS aliandika "asidhaminiwe" wakaanza kuwaponda OCS na OC -CID wale makoplo kua wanapenda sana kunyanyasa watu halafu wao wa chini wanabeba mzigo.
Tukamchukua mtu wetu ,tukarui nyumbani,yule mama hakuamini macho yake alipagawa km anakata roho.Kesho yake j3 akaenda Polisi alivyofika 0CS akampa makaratasi aende mahakamani wakasema hatutaki tena mambo yako,wakaogopa.Mahakami kesi tulishinda maana hakua na hoja.
Ila sitakaa niwasamehe Mwadawa,maaskari walompiga shemeji maana walikua wanampiga kila siku,ametoka ht kusimama vzr hawezi,msaidizi na mkuu wa kituo wa kizuani na OCD wa Mbagala wale ni wanyama!pale ndani kuna mambo mazito yanandelea kuna watuhumiwa wamefungwa mule hawapelekwi mahakamani!miezi mi3,mi4 nk.kwa kesi za kukomoan tu!kisa mshtaki kawahonga.
Sent from my Infinix X559C using
JamiiForums mobile app