Barua ya wazi kwa Waziri wa OR-Menejmenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Barua ya wazi kwa Waziri wa OR-Menejmenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Mapato55

Member
Joined
Feb 7, 2015
Posts
12
Reaction score
7
kwako Mheshimiwa Waziri;Jenister Mhagama,

Hongera kwa kuendelea kuaminiwa na kushika nyadhifa muhimu katika Kutenda maamuzi muhimu ndani ya serikali yetu ya JMT,
dhumuni la Ushauri huu ni kuelezea mambo muhimu ili kuleta ufanisi kwenye utendaji na utoaji wa huduma kwa wananchi pasi na kuweka gharama na urasimu usio wa wazima,

Mheshimiwa Waziri; Unalojukumu la kuhudumia watanzania kwa kushirikiana na wataalamu ulio wakuta hapo wizarani ninapendekeza uunde dawati la ufuatiliaji ndani ya wizara na aidha liwe na email au namba ya simu ambapo wananchi wataweza kuwasilisha kero au matatizo yao na kutapa ufumbuzi au mrejesho sahihi wa nini hasa kinacho endelea kwa tatizo wanalo lifuatilia na siyo kama ilivyo hivi sasa inamlazimu mwananchi kutoka Udinde Songwe asafiri hadi Dodoma kufuatilia Jambo ambalo ni upotevu wa raslimali muda na Fedha.

Mheshimiwa Waziri; Nina pendekeza uwajibikaji na uwazi miongoni mwa maafisa wa ngazi za juu hapo wizarani , kwani siku zote kuwapo kwa ufanisi katika nyanja yoyote ile inategemea sana uwajibikaji na uwazi kwa walengwa watendao suala husika.

Mheshimiwa Waziri; Ninapendekeza kuundwa kwa Task Force kitakacho fuatilia utendaji na uwajibikaji wa maafisa wote wa ngazi za halmashauri ili waweze kuwajibika kwa wakati bila kuonea wala kupindisha haki za watumish katika ngazi husika.

Mheshimiwa Waziri; ;Ninapendekeza umoja na mshikamano miongoni mwa watumishi wa Halmashauri/Wizara hii ili wawe mfano bora kama ambavyo jina la wizara linavyo jinasibu.

Mheshimiwa Waziri; Ninakutakia utekelezaji Mwema na Mungu Akubariki.
 
Back
Top Bottom